JAPHET MATARRA Profile picture
Jul 27, 2021 37 tweets 25 min read Read on X
FAHAMU MVUMBUZI WA TELEVISION (📺)

#Yes_____&&
#Thread|story🕐
Any sufficiently Advanced Technology is indistinguishable from MAGIC!! Binafsi huwa nasema Technology Is the Great ant💉dote to the Poison of Enthusiasm and Superstition💣
📋Asili ya TV
📋Historia yake
📋Uvumbuzi n.k
Televisheni (TV) au Runinga ni kifaa chenye kioo ambacho kinapokea mawasiliano kutoka kituo cha televisheni na kuyabadilisha kuwa picha na sauti.

Neno "Televisheni" linatokana na maneno mawili:
(i)Tele (Kigiriki)-kwa mbali sana na
(ii)Visio (Kilatini)-mwono.

RT @omari_manyama
kwa pamoja yanaunda neno la Kiingereza #Television limetoholewa kwa lugha ya Kiswahili "Televisheni".

Ugunduzi wa TV📺 ni kazi iliyofanywa na watu wengi mwishoni mwa karne ya 19.Karne ya 20 Watu mmoja-mmoja na makampuni yalishindana kuunda chombo kilichopiku teknolojia ya awali.
Wengi walisukumwa kuwekeza mitaji ktk ugunduzi huo na kupata faida huku wengine wakitaka kuubadili ulimwengu kwa njia ya teknolojia ya mawasiliano ya kuona na kusikia kwa wkt mmoja. Hayupo mtu mmoja wa kupewa sifa pekeake kwa uvumbuzi wa 📺, kila mmoja alifanya kwa uwezo wake.!!
Wazo hilo lilikuwa likizunguka muda mrefu kabla teknolojia haijawahi kutokea, na wanasayansi na wahandisi wengi walitoa michango yao ambayo ilijengwa kwa kila mmoja hatimaye kutoa kile tunachojua kama Runinga ya leo.
Asili ya TV inaweza kufuatiwa hadi miaka ya 1830's na 1840's, wakati SAMUEL F.B. MORSE alipotengeneza mfumo wa kutuma ujumbe uliotafsiriwa kwa sauti (Telegraph) ktk uzi au waya. ALEXANDER BAIN ndiye aliyeanzisha mtambo wa kutengeneza kivuli cha picha baina ya mwaka 1843/46.
Mfumo wa kwanza wa kivuli cha picha kufanyiwa kazi kwa mistari ya telegrafu uliendelezwa na kuingizwa kazini na Giovanni Caselli kuanzia mwaka 1856 na kuendelea. Willoughby Smith akatengeneza mkondo wa picha wa kifaa cha selenium mwaka 1873.
Hatua nyingine muhimu mbele ilikuja mnamo 1876 ambapo Alexander Graham Bell alitengeneza mtambo wenye kama mfumo wa simu ambayo iliruhusu sauti ya mwanadamu kusafiri kupitia waya kwa umbali mrefu zaidi
Alexander Bell na Thomas Edisons waliamua juu ya uwezekano wa kutengeneza kifaa kama simu ambacho kinaweza kusambaza picha na sauti. Baadae mtafiti mmoja wa Ujerumani ndiye aliyechukua hatua iliyofuata kuelekea kukuza teknolojia iliyowezesha runinga.
Rt @balozi_twita @Kiganyi_
Mnamo 1884, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ujerumani, Paul Julius Gottlieb Nipkow akiwa na umri wa miaka 23, alibuni na kutengeneza kitu km sahani iliyoitwa "Nipkow disk" iliyokuwa na mfumo wa kutuma picha kupitia diski inayozunguka ktk waya, akaiita "Electronic telescope"
Hii ilikuwa ni santuri ya kuzunguuka ikiwa na matundu ya duara ndani yake, kila tundu likifanya mstari wa picha. Japo yeye hakujenga modeli ya utendajikazi ya mfumo huo lakini aina mbalimbali za santuri ya Nipkow zikawa mashuhuri mno.
Constatin Perskyi ndiye aliyebuni neno #Television katika andiko lililowasilishwa ktk Mkutano wa Umeme wa Kimataifa kwenye maonesho ya kimataifa mjini Paris, Agosti 25, 1900. Andiko la Perskyi lilipitia upya teknolojia zilizokuwepo za nguvu ya umeme wa mitambo.
RT @Vet_doctor87
Mwanzoni mwa 1900, mwanafizikia wa Kirusi Boris Rosing na mhandisi wa Uskoti Alan Archibald Campbell-Swinton walifanya kazi kwa kujitegemea kuboresha mfumo wa Nipkow kwa kubadilisha diski zinazozunguka na kuwekwa ktk kiwambo cha Cathode tube.
Teknolojia hiyo iliboreshwa zaidi na mwanafizikia wa Ujerumani #Karl_Braun.

Mfumo huo wa Swinton, ndio ambao uliweka mirija ya cathode ndani ya kamera iliyotuma picha iliyokuwa inafanana na ile inayotolewa na mpokeaji, na kimsingi huu ndio ulikuwa mfumo wa kwanza wa televisheni
Hata hivyo, waliendelea kupambana ili kitu cha maana zaidi ktk mawasiliano na mnamo mwaka 1907, maendeleo ya teknolojia ya mtambo wa kukuza sauti yalipofikiwa na Lee de Forest ambapo Arthur Korn pamoja na wengine walifanya muundo huo kuanza kazi
Kuonekana kwa mawasiliano rasmi ya picha kulifanywa kwa mara ya kwanza na Rignoux na A. Fournier mnamo mwaka 1909. Mpangilio (matrix) wa vibetri vidogo vidogo vipatavyo 64, kila kimoja kikiwa kimeunganishwa waya katika mtambo endeshi ndivyo vilivyofanya kazi kama retina ya jicho.
Katika kipokezi, aina ya kibetri cha Kerr cell ndicho kiliratibu mwanga na milolongo ya vioo mbalimbali vya pembeni vilivyoambatanishwa na ukingo wa sahani inayozunguka (santuri) ikigagamiza mwangaza hadi ndani ya kioo cha luninga.
Mfumo maalum wa umeme ndio ulioratibu utendajikazi wa pamoja wa chombo hicho. Kioo cha ukubwa wa nane kwa nane katika mtambo huo wa runinga kilitosha kuwasilisha herufi za maneno pamoja picha ilionekana mara kadhaa kwa kila sekunde.
Mnamo mwaka 1911, Boris Rosing na mwanafunzi wake Vladmir Zworykin walibuni mfumo ambao ulitumia kigagamizi cha ngoma ya kioo ambacho, kwa maneno ya Zworykin, kilileta picha chafu sana kwa waya uliounganishwa na muanzi wa mwangaza ndani ya kipokezi.
Huyu Vladimir Zworykin alizaliwa Urusi na alikuwa akifanya kazi kama msaidizi ktk kampuni ya Boss wake Boris Rosing kabla ya wote kuhama kufuatia Mapinduzi ya Urusi.
Baadae Zworykin aliajiriwa katika kampuni ya utengenezaji vifaa vya kielektroniki na umeme huko Pittsburgh Westinghouse, miaka ya 1923 ambapo aliomba hati miliki ya kwanza ya runinga, kwa "Iconoscope," ambayo ilitumia mirija ya cathode ray kusambaza picha.
Kufikia 1920's, TV ilianza kufanya kazi, mgunduzi wa nchini Scotchland Bw. John Logie Baird alitumia santuri ya Nipkow ktk mifumo yake ya video.
Alitengeneza aina yake ya santuri huko Santa Cruz (Trinidad Islands). Pia aliyeanza utundu wa kubuni televisheni ya kwanza ya rangi.
Mnamo Machi 25, 1925, Baird alitoa onesho la kwanza la picha za kutembea za televisheni Jijini London. Kwa kuwa nyuso za wanadamu zilikuwa zinaoneka vizuri ktk mfumo huo duni alitengeneza sisira la kuzunguka ambalo lilitengeneza muonekano au sura yake ya mtu.
Mnamo 1929, Zworykin alionyesha mfumo wake wa elektroniki kwenye maonyesho ya wahandisi wa redio. Mojawapo waliohudhuria ktk maonyesho hayo ni David Sarnoff, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Redio la Amerika (RCA), kampuni kubwa ya mawasiliano ya taifa wakati huo.
Mnamo Januari 26, 1926, alionesha picha ya uso. Hii ndiyo inayohesabiwa kama Televisheni ya kwanza ya kuonesha picha nzuri katika historia. Na mwaka 1929, Zworykin alionyesha mfumo wake wa elektroniki kwenye maonyesho ya wahandisi wa redio.
Mojawapo waliohudhuria ktk maonyesho hayo ni David Sarnoff, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Redio la Amerika (RCA), kampuni kubwa ya mawasiliano ya taifa wakati huo.
Sarnoff alizaliwa ktk familia masikini ya Kiyahudi huko Minsk, Urusi, baadae akaenda New York akiwa mdogo na akaanza kazi za telegraph.
Ktk usiku wa janga meli ya #Titanic alikuwa kazini, lkn alishindwa kuratibu ujumbe wa sauti uliotumwa na meli za karibu kuomba msaada wa uokoaji
Sarnoff alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kufanikisha maendeleo ya Televisheni ya sasa ambapo baadae alimwajiri Zworykin ktk kampuni yake kukuza na kuboresha teknolojia ya runinga kwa kampuni hiyo.
Zworykin alikutana na Philo Farnsworth kijana mmoja mporipori aliyekuwa akifanya kazi RCA (kampuni ya Sarnoff) kitengo cha Television, akampa wazo la kuweka bomba la utupu ambalo litagawanya picha kuwa mistari, kisha kusambaza mistari hiyo na kuigeuza kuwa picha.
Wamarekani huamini Farnsworth ndiye mtu wa kwanza kuvumbua TV kwasababu mnamo 1927, akiwa na miaka 21, alitengeneza kitu chenye mfano wa mfumo wa kwanza wa runinga wa elektroniki unaofanya kazi kabisa. Lakini ukweli ni kuwa sio yeye maana hata ujuzi aliotumia ni wa Paul Nipkow.
Kutokana na wazo lake lile inaaminika miaka ya karibuni alijikuta akiingia kwenye mgogoro wa kisheria kwa muda mrefu na kampuni ya RCA, ambayo ilidai uvumbuzi wa Aawali wa Zworykin wa mwaka 1923 ndio ulichukuliwa kipaumbele kuliko uvumbuzi wa Farnsworth.
Rt @chapo255 @funjojr
Serikali ya Marekani iliamua mgogoro huu kwa kumpendelea Farnsworth (Mmarekani) na kipaumbele kwamba mnamo 1934 alisaidia kuwa sehemu muhimu na mvumbuzi wa television tena akiwa mdogo hivyo Sarnoff mwishowe alilazimishwa kumlipa Farnsworth US$ 1M km ada ya leseni.
Ingawa alitazamwa na wanahistoria wengi kama mwanzilishi wa runinga, lkn Farnsworth hakupata faidi zaidi kutokana na uvumbuzi wake, na alikuja kushtakiwa baada RCA kukata rufaa. Baadaye aliendelea na taaluma za utengenezaji wa silaha za nyuklia na alifariki dunia 1971 akiwa deni.
Sarnoff na kampuni yake mauzo, alitambulisha TV yenye muundo mpya na kubwa kuliko zote ktk maonyesho ya ulimwengu huko New York City mnamo 1939. Chini ya mwavuli wa RCA, kampuni ya utangazaji ya kitaifa (NBC). Alifanya ufunguzi, kisha na Rais Franklin D. Roosevelt alihutubia.
Baada ya hapo kumekuwepo na miundo mbalimbali ya TV na imekuwa ikibadilika siku hadi siku, muongo baada ya muongo mmoja, teknolojia ya Runinga imeendelea kwa kasi. Muonekano mzuri wa rangi ilivumbuliwa ktk miaka ya 1960, ikifuatiwa na cable miaka ya 1970's na VCRs miaka ya 1980's
Maendeleo zaidi ya Televisheni yenye picha angavu zaidi kwa mfumo wa High definition (HDTV) ilikuja mwishoni mwa miaka ya 90. Ktk karne ya 21, watazamaji wana uwezekano wa kutazama vipindi kwenye simu za rununu (smartphones), kompyuta ndogo km vile unavyoona ktk 📺 ya kawaida.
Leo hii kuna Televisheni za kisasa ambazo ni kubwa sana na zenye picha angavu sana.

#The End_______&&

If u Read this #Uzi kindly
JUST RETWEET and FOLLOW ME
kwa Ajili ya Kupata #Nyuzi bin #Nyuzi Everyday..!!

Thanks 🙏🙏

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with JAPHET MATARRA

JAPHET MATARRA Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @Eng_Matarra

Oct 19, 2021
NANI ALIYEMUUA SOKOINE?

#UZI

🔲Mnamo April 12, 1984 ilikuwa ni siku mbaya sana ktk Taifa letu na haitosahaulika kwa Watanzania. Siku hiyo tulimpoteza kijana makini aliyekuwa Waziri Mkuu EDWARD MORINGE SOKOINE, aliyefariki kwa ajali mbaya ya gari eneo la Wami-Dakawa (Morogoro). ImageImageImage
🔲SOKOINE mmoja wa viongozi bora nchini amefariki miaka 37 iliyopita akiwa na miaka 46. Ikiwa ulizaliwa kpnd hicho sasahv ushakuwa na watoto na pengine unaelekea wajukuu.

🔲Ingawa historia tumesoma ndio, ILA #chanzo cha kifo chake bado kuna utata kuna maswali YasiYo na majibu. Image
🎤Nimeamua tufukue makaburi najua hukuambiwa haya💣⤵️

🔲Hv NANI HASA ALIYEMUUA SOKOINE?

🔲ILIKUWAJE AKAGONGWA NA GARI La "Private" #KATIKATI Ya MSAFARA na kupelekea kifo chake (Tujuavyo msafara wa VIP unakuwaga na ulinzi wa usalama, hakuna gari linaruhusiwa kutembea hadi upite) Image
Read 111 tweets
Sep 26, 2021
PUTIN ANAVYOPINDUA VIONGOZI WA AFRIKA KUJIIMARISHA

#UZI:

💨Rais Alpha Conde (Guinea) alipinduliwa kwa msaada wa USA & Ufaransa, lkn kwa ASSIMI GOÏTA (Mali) alisaidiwa na Urusi.Pia mauaji ya IDRIS DÉBY (Chad) yalifanywa na URUSI
👩‍💻𝐌𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐌𝐚𝐳𝐢𝐭𝐨 𝐓𝐮𝐬𝐢𝐲𝐨𝐲𝐚𝐣𝐮𝐚👇
Mnamo Aprili 20, 2021 majira ya jioni zilianza sherehe huko La Brasserie Kiss, umbali wa 100M kutoka ktkt ya mji wa Bangui (Afrika ya Kati). Kila aliyepita huo mtaa aliona magari kadhaa yamepaki mbele ya nyumba moja ya Ghorofa 3, jumba ambalo ni kivutio kikubwa sana ktk jiji hilo
Jengo hili lipo nje kidogo ya mtaa maarufu wa DU COLONEL CONUS na ikifika usiku hupendeza sana kutokana na mng'ao wa taa ulioizunguka. Kulingana na saa kule ilikuwa mida ya saa 2 usiku hivi na kwa wenyeji wa mji huo, ni muda ambao amri ya kutotembea usiku huanza kutumika.
Read 17 tweets
Sep 18, 2021
𝐂𝐈𝐀 ILIVYOTUMIA MWANAMUZIKI ARMSTRONG KUMUUA PATRICE LUMUMBA (Congo)

#Thread

Mnamo Sept 19, 1960, Mkuu wa CIA huko Leopoldville (sasa Kinshasa) alipokea SMS kupitia chombo cha siri kutoka wakuu wake huko Washington. Mtu aliyejiita 'Joe from Paris' ndiye aliyepiga simu na ..
kumwambia angefika Congo kwa ajili ya Operation maalum.

Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa. Baadae mkuu huyo alionywa kutozungumzia ujumbe huo na mtu yeyote. Wiki 01 baadae 'Joe' aliwasili nchini humo.

Leo nikiwa nasoma kitabu cha 𝐖𝐡𝐢𝐭𝐞 𝐌𝐚𝐥𝐢𝐜𝐞 (Author: SUZAN WILLIAMS)
kilichotoka Agosti 20, 2021, nimejikuta nikiumia sana nafsi baada ya kufahamu jinsi Marekani ilivyomuua Waziri Mkuu wa kwanza wa DR-Congo, mzalendo wa kweli, kijana mdogo mrefu, mwembamba miaka 36, kwasababu tu USA iliogopa Umoja wa Kisovieti (USSR) ikaamua kumuua.
Read 120 tweets
Sep 13, 2021
FULL OPERATION MAPINDUZI YA RAIS (GUINEA)

#Thread

Baada ya TALIBAN nchin Afghanistan, habari sasa ni MAMADY DOUMBOUYA kiongozi wa kijeshi huko Guinea, kumpindua rais na kuchukua madaraka #Unadhani kikosi kidogo cha SFG kiliwezaje kudhibiti kambi za kijeshi na kumkamata rais?👇
Yes, mwanajeshi wa zamani wa Ufaransa (French Legionnaire) aliyerudi nyumbani miaka 03 iliyopita na kuaminiwa na Rais ALPHA CONDÉ, ndiye aliyemsaliti na kumuondoa madarakani baada ya kutaka kuongoza nchi kwa muhula wa 03

MAMADY DOUMBOUYA ambaye ana cheo cha Kanali alionekana..
kwenye kituo cha Radio-Télévision Guinéenne(RTG), mnamo 5 Septemba majira ya saa 2 usiku, akiwa amevalia kofia nyekundu (Red Beret) ameweka bendera ya taifa hilo begani mwake, na kuzungukwa na wanajeshi wanane, akatangaza kuwa jeshi limechukua madaraka ya nchi.
Read 147 tweets
Sep 9, 2021
MAPINDUZI YA GUINEA TZ🇹🇿 YA SAMIA INACHAKUJIFUNZA

#UZI

Ilianza kama utani Mzee Condé hakuamini kijana wake mwenyewe aliyemlea, mwenye masters ya vita na cheo akampatia alipomwambia "simama juu hlf ukae chini" Unadhani ilikuwa rahisi kumpindua? Naam It's #Guinea:1958-Present👇
Sikuweza kuandika Uzi yalipotokea mapinduzi ktk nchi nyingine mbalimbali, lkn kwa yaliyotokea jumapili nchini Guinea nimeona niandike ili Watanzania tuone km kuna lolote la kujifunza. Nitaangazia upande wa kisiasa tu. Nitachambua kila kitu kuanzia uhuru hadi kutokea mapinduzi.
Maswali nayotaka kukujibu km ulijiuliza ni haya:👇

💨Historia ya Guinea ikoje?

💨Kwnn mpk mapinduzi?

💨Col. Doumbouya ana nguvu gani

💨Kwann wananchi wamefurahia?

History repeats itself, 1st as Tragedy, second as Farce.
Just retweet 🔄 huenda siku
Uzi huu ukakukumbusha kitu
Read 211 tweets
Aug 18, 2021
WHO is '𝐓𝐀𝐋𝐈𝐁𝐀𝐍'? WANATAKA NINI HASA AFGHANISTAN?

#𝕿𝖍𝖗𝖊𝖆𝖉:
Ifahamike, walikuwa yatima ktk kambi za wakimbizi Pakistan.
Je, wana uhusiano na AL-QAEDA? #Tragedy:UINGEREZA & URUSI kuchezea kipigo cha Mbwakoko.
✴️Chimbuko
📡Walio nyuma yao?
📋Tofauti yao na MUJAHIDINA..
Vita vya Marekani nchini Afghanistan vimedumu kwa takribani miaka 20. Nimeona watu wengi wakitoa maoni juu ya Jeshi la TALIBANI kuchukua nchi Lkn wengi hawana historia juu yake. Wengine wanasema Rais wa Marekani @JoeBiden mefanya 'makosa' kuondoa majeshi yake.
BIG NO __Hapana.
Wengi tusichojua ni kwamba, huu ulikuwa ni uhalifu wa kivita na DICK CHENEY, aliyekuwa Vice President wa G. W BUSH na DONALD RUMSFELD, Kiongozi Mkuu wa Ulinzi kipindi cha Vita ya IRAQ (alishafariki), ndio walioiingiza Marekani kwenye shida hii unaiona Leo, kisa wanamtafuta OSAMA
Read 114 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us!

:(