“Nakumbuka nikiwa shule ya msingi maisha hayakua mazuri. Biashara ya mama yangu ya bagia ikawa ndio inaendesha maisha yetu. Mimi ndio mkubwa na ndiye mtoto wa kiume kwetu. Kwa kipindi hicho mdogo wangu wa kike alikua bado mdogo sana.
Ilinibidi nisaidiane na mama kuuza bagia.
Nikitoka shule nakuta zimeshatayarishwa nabeba sufuria natembeza mpaka vijiji vya jirani. Nahakikisha zimeisha ndipo narudi nyumbani.
Utaratibu ulikua ni huo huo tangu darasa la tatu hadi form three. Nakumbuka wenzangu walikua wananicheka. Nilikosa marafiki.
Kila mtu alikua ananitenga na kunidhihaki kwamba mtoto wa kiume nabebaje sufuria na kwenda kuuza bagia. Walisema ni kazi za kike.
Ilifika muda nikikuta wenzangubwanapiga stori nikifika tu wote wanatawanyika. Nabaki mnyonge.
Basi nilizoea ile hali nikajikuta naishi maisha bila marafiki. Lakini huwa nashukuru juu ya hili jambo kwa sababu ilinifanya nipambanie ndoto zangu mwenyewe. Huenda ningekua na marafiki nisingefika hapa nilipo.” Frank, Iringa. #WatuNiStory
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
“Wakati naanza mwaka wa kwanza pale IFM nilimpa mimba mpenzi wangu. Nilikua naye toka mimi nikiwa Form 5. Bahati mbaya alifeli Form 4 akaishia hapo hapo.
Aliniambia mimba ni yangu na nilikubali nikaanza kuilea ile mimba. Japo tulisumbuana sana kwenye pesa za matumizi kwa sababu
sikua na pesa za kutosha kila kitu kwa wakati huo.
Chuki kwangu ikazidi balaa. Sikuiweka moyoni niliamini ni mimba inamsumbua.
Alienda kwao kujifungua mkoa mwingine. Na akajifungua mtoto wa kiume. Baada ya siku tatu akaniambia mtoto amefariki na baada ya hapo hakupokea simu
zangu tena wala za mama yangu. Mama yangu alilia sana.
Tayari tulishanunua vitu kibao vya kwake na vya mtoto. Kuna namna niliamini huu ni mchezo nimechezewa ila nilikaza maisha yakaendelea. Nikasonga na maisha mapya.
Baadae nikapata mwanamke mwingine na tulipendana sana japo
“Hii siri nitaitunza mpaka lini? Nibaki nayo au nijisalimishe?
Nilikuja Dar kutokea kijijini kupambania ugali. Mungu mwema mitikasi ilikubali. Kama unavyojua tena jiji la Dar wanawake warembo kila kona. Ni kama nilikua na ngekewa kila nilipotupa ndoano ilinasa. Nilijichanganya
nilitembea na kila aina ya mwanamke niliyemtamani.
Katika haya mahangaiko nilikutana na dada mmoja wa Songea. Huyu dada alikuja kunieleza amepata mjamzito. Ila akawa ameenda kwao Songea. Nilikua nikituma matumizi ila ilifika mahali mawasiliano yalikufa. Sikumpata tena. Ni miaka
mitano sasa sina mawasiliano yoyote sijui alipoteleaga wapi.
Maisha yaliendelea huku Dar nikakutana tena na mwanamke kutoka Kahama. Na yeye akapata ujauzito. Alirudi kwao Kahama pia ila mawasiliano yaliendelea kuwepo.
Ulifika muda nikaona hii njia sio sahihi. Nikabadilika
"Wakati nakutana na mpenzi wangu ambaye kwa sasa ni mchumba wangu na tutaoana sio mda mrefu, nilimwambia kabisa mimi sina mapenzi ya maonyesho.
Sinaga habari za mitoko wala kupostiana kuandikiana caption za makopakopa. Wewe ukitaka kutoka, toka na rafiki zako. Wala sitajalii.
Me nifanyie vitu vya kawaida tu kabsa nitafurahi sana.
Nina amini katika mahusiano ya siri na yenye staha. Kupostiana watu huleta chuki na maneno ambayo hayapo.
Wengine wana vijicho, wanataka mazuri unayopata wewe na yeye ayapate. Mpenzi wako anakupost kwa mapenzi tu ila unakuta mtu wivu unamshika anaanza kujipendekeza kwake.
Na wanaume sio wa kustahimili vishawishi na hapo ndoa ndio inaanza kuwa ngumu.
Baada ya kumaliza shule nilimpata binti niliyeamini atakuwa wa maisha yangu alikuwa anaitwa Mwajuma, hapo ndio kwanza nilikuwa ninaanza kuingia katika ulimwengu wa mapenzi.
Sikuwa ninaelewa kabisa kuhusu maana ya neno penzi, watu waliotabiri mwisho wangu na Mwajuma niliamini kuwa ni wanafiki na walikuwa na malengo mabaya dhidi yetu.
Siku zilivyozidi kusonga penzi letu lilizidi kustawi kama bustani iliyokuwa inasimamiwa vizuri, tulipanga hadi kutambulishana kwa wazazi.
"Tulifanya interview kutafuta mtu wa finance katika kampuni yetu. Tulipokea maombi mengi, watu tano ndio walifanikiwa kupigiwa simu na kuitwa kwa ajili ya usahili.
Wote walifika. Kila mtu alipangiwa muda wake.
Nakumbuka kuna kijana alikuja amependeza, yuko smart na alikuwa na vigezo vyote vya kupata ajira.
Alikuwa na madaha na majivuno ya hapa na pale wakati tunafanya nae interview. Alitaka mshahara wake usishuke si chini ya milioni moja na laki tano.
Alisema bila mshahara huo hawezi kutoka kwenye kampuni anayoifanyia kazi.
Hatukuwa na hiyo hela. Hivyo tulimchagua mtu mwingine ambaye tulielewana nae.
1/10 “Naitwa William Adam Lukoo ,mzaliwa wa mkoa wa Morogoro. Mwaka 2003 familia yetu ilihamia jijini Tanga kwa ajili ya harakati za kimaisha. Haikua rahis kwa sababu ya ugeni lakini wazazi walipambana kuhakikisha napata elimu bora. Licha ya kutoka kwenye familia ya kimaskini...
2/10 ..nilihakikisha nafanya vizuri kwenye masomo kiasi cha kuwavutia walimu na kujizolea umaarufu shuleni. Nilifanikiwa kuhitimu mwaka 2010 shule ya msingi Majani Mapana wilayani Tanga mjini. Mwaka 2011 nilianza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Usagara..
3/10 ..lakini kutokana na ugumu wa maisha, wazazi wangu wote hawakuwa na kazi. Ikawalazimu kufikia hatua ya kuuza vitu vya ndani ili kuweza kunilipia ada. Maisha yalikuwa magumu mno nyumbani kiasi cha kufikia hatua ya kushindwa kupata chakula na kodi.