Kutaka kutupia PC ni ili kuboresha ufanisi wa kazi na kuongeza spidi ya kufanya kazi.
Bahari mbaya Windows huwa si rafiki kwetu siku zote katika hili. Unaweza hitaji kukamilisha kazi haraka, lakini windows ikakufedhehesha.
Somo la leo ni jinsi ya kuongeza spidi ya win10.
UZI
Windows 10 imeboreshwa sana ukilinganisha na matoleo ya nyuma ya Windows. Inafanya vizuri sana kwa PC ambazo zimekidhi vigezo, shida huwa kwa PC za kizamani.
PC hizi hazina uwezo mzuri kubeba hii OS, hivyo mara nyingi watumiaji wake huwa wakilalamika kuhusu ubora wa Win10.
Twende moja kwa moja kuangalia ni kwa namna gani tunaweza ongeza spidi ya Win10.
MUHIMU: Hacks hizi ni zile anazoweza fanya mtu yeyote.
1. Ondoa "Startup Programs"
Hizi ni zile programu ambazo huanza kufanya kazi pale PC yako inapowaka (Hazikuhitaji wewe uziruhusu kuanza).
Unaweza kuwa unafurahia kuona program fulani ikianza yenyewe unapowasha Win10 PC yako, lakini hii inapelekea PC yako kuwaka pole pole sana.
Namna ya kuziondoa
. Minya button hizi kwa pamoja ctrl + shift + esc.
. Chagua sehem ya "Starup". Angalia program ambazo zina "High impact" kwenye kipande cha "Startup impact".
. Right click kwenye hiyo program kisha chagua "disable".
restart PC yako.
2. Ondoa "Background Apps"
Kuna program hufanya kazi nyuma ya pazia. Vitu kama email zinahitaji kufanya kazi nyuma ya pazia, lakini sio apps zote zinahitaji kufanya hivyo.
Kuzizima hizi fata hatua hizi.
.Fungua settings kisha chagua "Privacy"
.Shuka chini na chagua "Background Apps". Hapo "Disable" application zote zisizo na muhimu kufanya kazi in background.
3. Zuia Apps kuanza baada ya kufanya restart
Hizi ni tofauti na zile background apps na Startup apps. Windows 10 inaruhusu baadhi ya apps kuanza zenyewe na kurudi pale zilipofungwa mara ya mwisho.
Lakini apps hizi huaribu ufanyaji kazi wa Win10 yako na kuifanya kuwa slow sana.
Kuzuia fanya hivi
.Minya button ya windows, kisha andika hivi "Restart apps after signing in"
.Chagua jibu la kwanza, kisha ndani yake zima tu sehem ya "Restart apps" (Frame II).
4. Ondoa faili Takataka (Junk files)
Hizi ni vyema ukaondoa mwenyewe na sio kutumia third-party apps. Huwa hazizingatii ufanyaji kazi wa OS yako, zinaweza futa files zinazohitajika kwa muda huo.
Baada ya kusema hivyo tumalize jinsi ya kuzitoa.
.Minya button ya windows + r kisha andika "temp" kisha minya "Enter".
.ikikuomba ruhusa chagua "Continue". Ndani ya folder itakayo funguka, chagua kila kitu kilichomo alafu minya delete.
.Ikileta ujumbe (pichani) chagua skip.
5. Usitumie Antivirus zaidi ya moja.
Katika vitu ambavyo sio vizuri kwenye windows ni kutumia Antivirus zaidi ya moja.
Kwanza italeta mkanganyiko katika system, na ni kitu ambacho sio kizuri.
Jibu hapa ni kutumia Windows Defender yenyewe inayokuja na Windows au ukichagua kutumia Antivirus nyingine basi ongeza moja tu inatosha.
Njia nyingine zipo nyingi sana, lakini kwa leo hizi zinatosha.
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
African Network Information Centre (AFRINIC) taasisi ambayo toka mwaka 2005 ilipewa mamlaka ya kusambaza anawani za kimtandao (IP addresses) barani Afrika ipo hatarini kushindwa kuendelea kufanya kazi.
Utakubali kuhudumiwa na Muuguzi Roboti Hospitalini?
UVIKO-19 umebadilisha sana mwenendo wa maisha yetu ndani ya miaka 2 iliyopita. Nani aliwaza kwamba leo hii kufanya kazi kutoka nyumbani ingekuwa ni kitu kinachopewa kipaumbele hivi?
🧵
Katika jitihada za kuokoa maisha ya watu wengi zaidi duniani, tumeona uundaji wa roboti ambao wanachukua nafasi za wauguzi katika hospitali.
Kampuni ya Hanson huko Hong Kong imekuja na roboti huyu mwenye muonekano wa kibinadamu.
Amepewa jina la "Grace".
Hanson robotics kwa wale msioifahamu, ni kampuni ile ile ambayo ilimtengeneza Sophia. Roboti mmoja maarufu sana duniani.
Sophia alipewa uraia wa Saudi Arabia. Na sasa Hanson robotics wanatuletea Grace.
Grace atahusika zaidi kutoa huduma kwa wagonjwa wa UVIKO-19 hospitalini.