Utakubali kuhudumiwa na Muuguzi Roboti Hospitalini?
UVIKO-19 umebadilisha sana mwenendo wa maisha yetu ndani ya miaka 2 iliyopita. Nani aliwaza kwamba leo hii kufanya kazi kutoka nyumbani ingekuwa ni kitu kinachopewa kipaumbele hivi?
🧵
Katika jitihada za kuokoa maisha ya watu wengi zaidi duniani, tumeona uundaji wa roboti ambao wanachukua nafasi za wauguzi katika hospitali.
Kampuni ya Hanson huko Hong Kong imekuja na roboti huyu mwenye muonekano wa kibinadamu.
Amepewa jina la "Grace".
Hanson robotics kwa wale msioifahamu, ni kampuni ile ile ambayo ilimtengeneza Sophia. Roboti mmoja maarufu sana duniani.
Sophia alipewa uraia wa Saudi Arabia. Na sasa Hanson robotics wanatuletea Grace.
Grace atahusika zaidi kutoa huduma kwa wagonjwa wa UVIKO-19 hospitalini.
Grace ameunda kutoa huduma kwa wagonjwa waliopo karantini, hasa wazee. Amepewa uwezo wa kuongea lugha zaidi ya moja.
Miongoni mwa hizo lugha ni English, Mandarin na Cantonese. Pia anaweza endesha mazungumzo ya kumfanya mtu ajiskia vizuri na kuchora picha pia.
Kwa sasa Hanson Robotics wanategemea kuanza kumtengeza Grace kwa wingi zaidi na kuanza kumuuza huko China.
Gharama yake inatemewa kuto tofautiana sana na zile za gari za starehe, ambayo ni kati ya Tsh. 100mil na Tsh. 300mil.
Iwapo siku utafika muhimbili kupata matibabu na ukapewa Roboti huyu akuhudumie. Je, utakubali kupewa huduma yake?
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
African Network Information Centre (AFRINIC) taasisi ambayo toka mwaka 2005 ilipewa mamlaka ya kusambaza anawani za kimtandao (IP addresses) barani Afrika ipo hatarini kushindwa kuendelea kufanya kazi.
Kutaka kutupia PC ni ili kuboresha ufanisi wa kazi na kuongeza spidi ya kufanya kazi.
Bahari mbaya Windows huwa si rafiki kwetu siku zote katika hili. Unaweza hitaji kukamilisha kazi haraka, lakini windows ikakufedhehesha.
Somo la leo ni jinsi ya kuongeza spidi ya win10.
UZI
Windows 10 imeboreshwa sana ukilinganisha na matoleo ya nyuma ya Windows. Inafanya vizuri sana kwa PC ambazo zimekidhi vigezo, shida huwa kwa PC za kizamani.
PC hizi hazina uwezo mzuri kubeba hii OS, hivyo mara nyingi watumiaji wake huwa wakilalamika kuhusu ubora wa Win10.
Twende moja kwa moja kuangalia ni kwa namna gani tunaweza ongeza spidi ya Win10.
MUHIMU: Hacks hizi ni zile anazoweza fanya mtu yeyote.