Afrika Bila Internet kwa muda usiojulikana.

African Network Information Centre (AFRINIC) taasisi ambayo toka mwaka 2005 ilipewa mamlaka ya kusambaza anawani za kimtandao (IP addresses) barani Afrika ipo hatarini kushindwa kuendelea kufanya kazi.

UZI 🧵
#habarinews
Kila kifaa kinachotumia mtandao kina anwani iitwayo IP Address. Anwani hii inakutambulisha wewe mtandaoni.

Anwani hizi ndizo ambazo zinatambulika mtandaoni na si jina la simu, website au PC unayotumia.
website kama ya @RednetCompany unaweza ifikia kwa kutafuta rednet.co.tz lakini computer yako inapoingia mtandaoni itatafuta 162.214.100.22.

Namba hii ni anwani ambayo mtandao inatambua kama ni miliki ya @RednetCompany
Simu yako pia unapotumia internet inapewa anwani inayoendana na hiyo lakini namba tofauti.

Anwani hizi zipo za aina mbili IPv4 na IPv6. Kwa sasa tunatumia IPv4. Ambazo kwa ujumla zipo anwani 4,294,967,296 (Hiyo ni 4.294 Bilioni).

AFRINIC ana mamlaka ya kusambaza hizi anwani...
kwa watumiaji wake ili waweze pata internet. Endapo AFRINIC atashindwa kusambaza anwani hizi, maana yake ni kwamba tutashindwa pata internet Afrika nzima.

Nini kilitokea mpaka kufikia hapa?
Wakati kila bara lina taasisi yake inayosambaza anwani hizi, kuna sheria moja...
inayotumika haijawahi kuwekwa katika maandishi. Sheria hii inasema "Anwani ambazo kila taasis imepewa zitatumika katika bara husika tu."

Shida ilianzia wapi?
Kampuni ya Cloud Innovation ya China ilivunja sheria hii baada ya kununua anwani 6 mil kwa AFRINIC na kwenda kuzitumia
China. Kati ya hizi 6 mil ni 1 mil tu ndizo walizitumia Afrika.

Kwanini wasingenunua kwa taasisi ya Asia?
Walishindwa kwa sababu Asia inawatumiaji wengi. Anwani zilizobaki hazitoshi mahitaji yao.

Kampuni hii iliweza pata hizi anwani baada ya kusajili kampuni nyingine...
chini yao huko Seychelles.

AFRINIC kutambua ukiukwa huu wa makubaliano waliwapa Cloud Innovation siku 90 kurekebisha makosa yao.

Badala yake Cloud Innovation waliwashtaki AFRINIC katika mahakama za Mauritius.

Kumbuka sheria wanayosimamia AFRINIC haukuwahi andikwa wala...
kuidhinishwa katika mkataba wowote.

Haya yalikuwa ni makubaliano ya nia njema kati ya AFRINIC na watumiaji wake. Bahati mbaya Cloud Innovation si waungwana kama tulivyo Afrika.

Kwa sababu hiyo AFRINIC walishinda kesi na wakaendeleza mashtaka kudai malipo ya uharibifu.
Mahakama iliwakubalia mashtaka yao na kuwachaji AFRINIC faini ya USD $50 mil.

Hiki ni kiasi cha pesa ambacho AFRINIC hawawezi kulipa na akaunti zao hazina kiasi hicho cha pesa.

Hii imepelekea akaunti zote za kibenki za AFRINIC kufungwa.
AFRINIC kwa sasa hawawezi lipa mishahara wafanyakazi wao, wala kufanya malipo ya nje ya kuendesha kampuni.

Kwahiyo, hapa ndipo tulipofikia. Hali ikiendelea hivi kuna uwezekano mambo yote yanayohitaji mtandao yatashindwa kwenda.
AFRINIC karata anayotakiwa kucheza hapa ni kukaa chini na kufanya mazungumzo na Cloud Innovation waweze fikia makubaliano yenye faida kwa wote.

Bahati nzuri Cloud Innovation wapo tayari kufanya mazungumzo, lakini AFRINIC wanasuasua.
AFRINIC inabidi awetayari kwa hili na wafanye yafuatayo.
1. Waweke katika maandishi kwamba kampuni yoyote itakayonunua anwani kutoka kwao ni lazima zitumike Afrika tu.

2. Kuongeza kasi ya kupitishwa kwa IPV6.
3. Kuweka njia wanazotumia kusambaza anwani hizi. Bado haijulikani Cloud Innovation walipataje anwani nyingi hivyo wakati kampuni kama SEACOM na Liquid zimepewa anwani chache kulinganisha na zile za Cloud Innovation.

4. Wafanya linalowezekana kuhoji namna kampuni itatumia...
anwani inazouziwa na AFRINIC.

Baadhi ya mamlaka zinazohusika na kusambaza anwani hizi ndani ya nchi zikitegemea huduma kutoka AFRINIC zimekuwa na machache ya kusema.

Moja wapo ni yetu hapa tanzania Tanzania Internet Service Provider Association (TISPA). Taarifa yao (pichani)
Taarifa ya African Internet Exchange Association (IXP)
taarifa ya Angola ISPA.
Internet Association nao walikuwa na lao la kusema.
Tutegemee miujiza au kutakuwa na suluhisho?

Nitaendelea kuwajuza yanayojiri katika vikao vya bodi ya AFRINIC. 😁Mkitaka kuja nipiga sawa lakini mimi siko bodi ya AFRINIC.

Huwa wanatoa kwa ufupi makubaliano ambayo bodi imefikia kupitia kurasa hii afrinic.net/board/meeting/…
Taarifa hii imeletwa kwenu kwa ushirikiano wa @HabariTech pamoja na @AlphaOlomi

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with HabariTech

HabariTech Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @HabariTech

8 Sep
Websites zilizojificha kwenye 60,000,000,000 TB za data kwenye internet.

Internet ni kijiji kimoja kikubwa sana kinachozidi kukua kila sekunde. Kama unavyojua maisha yetu kijijini ni ujamaa.

Kuna hizi website kadhaa ni muhimu sana zinaweza boresha uwepo wako mtandaoni.

🧵
1. Soap2Day

Huwa una bando la kutosha na unaweza vumilia matangazo yasiyo na mpangilio? Tumia hii website ya soap2day kuangalia movies mtandaoni.

Hapa hauna haja ya kumiliki akaunti ya netflix ni mwendo wa ski ads na press and play.

wvw.ssoap2day.to
2. Temp Mail

Kuna huduma unahitaji kujaribu kama inakufaa, lakini hutaki kutumia email yako ya kila siku?

Tempmail ipo kukupa email utakayo tumia kwa muda mfupi kukamilisha zoezi hilo.

Ukiingia kwenye page hii utakuta email ipo tayari kwa ajili yako.

temp-mail.org/en/
Read 6 tweets
1 Sep
Utakubali kuhudumiwa na Muuguzi Roboti Hospitalini?

UVIKO-19 umebadilisha sana mwenendo wa maisha yetu ndani ya miaka 2 iliyopita. Nani aliwaza kwamba leo hii kufanya kazi kutoka nyumbani ingekuwa ni kitu kinachopewa kipaumbele hivi?

🧵
Katika jitihada za kuokoa maisha ya watu wengi zaidi duniani, tumeona uundaji wa roboti ambao wanachukua nafasi za wauguzi katika hospitali.

Kampuni ya Hanson huko Hong Kong imekuja na roboti huyu mwenye muonekano wa kibinadamu.

Amepewa jina la "Grace".
Hanson robotics kwa wale msioifahamu, ni kampuni ile ile ambayo ilimtengeneza Sophia. Roboti mmoja maarufu sana duniani.

Sophia alipewa uraia wa Saudi Arabia. Na sasa Hanson robotics wanatuletea Grace.

Grace atahusika zaidi kutoa huduma kwa wagonjwa wa UVIKO-19 hospitalini.
Read 6 tweets
31 Aug
Kutaka kutupia PC ni ili kuboresha ufanisi wa kazi na kuongeza spidi ya kufanya kazi.

Bahari mbaya Windows huwa si rafiki kwetu siku zote katika hili. Unaweza hitaji kukamilisha kazi haraka, lakini windows ikakufedhehesha.

Somo la leo ni jinsi ya kuongeza spidi ya win10.

UZI Image
Windows 10 imeboreshwa sana ukilinganisha na matoleo ya nyuma ya Windows. Inafanya vizuri sana kwa PC ambazo zimekidhi vigezo, shida huwa kwa PC za kizamani.

PC hizi hazina uwezo mzuri kubeba hii OS, hivyo mara nyingi watumiaji wake huwa wakilalamika kuhusu ubora wa Win10. Image
Twende moja kwa moja kuangalia ni kwa namna gani tunaweza ongeza spidi ya Win10.

MUHIMU: Hacks hizi ni zile anazoweza fanya mtu yeyote.
Read 14 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(