"Mwaka 2016 nilipoteza kazi niliyokuwa nimeajiriwa kwa makosa ambayo sikuhusika, lakini upepelezi ulipokuja kufanyika nilionekana ni kama na mimi nilihusika kwenye huo wizi ingawa ukweli sikuhusika.
Sikujua chochote na wala sikula hata sh 100.
Wanasema siku ya kusurubiwa kwako manabii wa uongo watakuja ili kukutolea ushahidi wa uongo lengo uangamie, ndio kilichonitokea mimi.
Baadae ya kupoteza kazi Mungu alinipa ujasiri sana maana sikuwahi kujutia kupoteza kazi bali nilianza kuwaza naishije kwa sasa na nafanya nini ili maisha yaende?.
Sikuweza kupata kitu cha haraka haraka cha kufanya ili kiniingizie kipato cha kujikimu maisha. Michongo haikuwa rahisi kupatikana.
Nikapata wazo jingine, nilichowaza ni kuchukua mafao yangu na nijiendeleze kielimu.
Niliamua kusoma QT kwa ajili ya kidato cha tano na sita maana nilikuwa na alama nzuri tu nilizopata kidato cha nne.
Nakumbuka nilianza kusoma kwa kuchelewa mwezi wa tisa mwaka 2017 na mwezi wa tano, 2018 nilifanya mtihani wa kidato cha sita.
Licha ya kusoma kwa muda mfupi sana, Mungu alisaidia nikapata ufaulu mzuri ulionifanya nikaingia chuo kikuu.
Nashukuru mwaka huu namalizia chuo kikuu na mimi rasmi niwe na degree yangu.
Nimejifunza unaweza kupoteza kitu na kujilaumu lakini kumbe kupoteza hicho kitu inaweza Kuwa njia ya kubadili mfumo wako wa maisha na kupata kitu kingine bora zaidi.
Bila kupoteza kitu cha mwanzo, mimi nisingekuwa hapa nilipo". Mzalendo, Mwanza. #WatuNiStory
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
"Nimetokea kwenye familia maskini sana na kibaya zaidi ilidharaulika sana, tena kwa pande zote mbili yaani upande wa baba na mama.
Nimekuwa huku kauli za kejeri zinasikika na kuishi masikioni mwangu.
Hilo kwangu ndio lilikuwa tatizo kubwa. Niliwachukia sana jamaa zangu mpaka nimekua mkubwa sikuwahi kuomba msaada wa aina yoyote kwao.
Hadi wazazi wangu niliwahi kuwakataza, niliwaambia shida zote na huduma wanibebeshe mimi.
Kuwaeleza shida zetu, ilikuwa kama kuwalilia njaa kwao.
Leo Mungu amesaidia tunakula kwa muda sahihi na tunalala pazuri. Kiukweli sitamani hata kuwapigia simu. Sasa hivi wamenibadilisha jina wanasema mimi ni jeuri.
"Mwaka 2005 nilihitimu chuo cha ualimu Kabanga kilichopo mkoani Kigoma. Sikukaa muda mrefu mtaani, mwaka 2006 nilifanikiwa kupata ajira wilayani Moshi.
Nilifundisha pale miaka mitatu nikakutana na jamaa mmoja tukawa marafiki. Kumbe alikuwa mganga wa kienyeji.
Katika harakati zake, akanishawishi nikawa chawa wake. Siku zilivyoenda nikajikuta na mimi nimetamani kuwa mganga.
Sikuwa na majini ila kutokana na ukaribu wetu na nilivokua naona watu wengi wenye shida wanakuja kwake wanamuachia hela nyingi kiasi kwamba hela ambayo alikuwa anaipata ilikua inazidi mshahara wangu kama mwalimu.
Nikashawishika kuacha kazi ya ualimu na nikawa mganga.
“Wakati naanza mwaka wa kwanza pale IFM nilimpa mimba mpenzi wangu. Nilikua naye toka mimi nikiwa Form 5. Bahati mbaya alifeli Form 4 akaishia hapo hapo.
Aliniambia mimba ni yangu na nilikubali nikaanza kuilea ile mimba. Japo tulisumbuana sana kwenye pesa za matumizi kwa sababu
sikua na pesa za kutosha kila kitu kwa wakati huo.
Chuki kwangu ikazidi balaa. Sikuiweka moyoni niliamini ni mimba inamsumbua.
Alienda kwao kujifungua mkoa mwingine. Na akajifungua mtoto wa kiume. Baada ya siku tatu akaniambia mtoto amefariki na baada ya hapo hakupokea simu
zangu tena wala za mama yangu. Mama yangu alilia sana.
Tayari tulishanunua vitu kibao vya kwake na vya mtoto. Kuna namna niliamini huu ni mchezo nimechezewa ila nilikaza maisha yakaendelea. Nikasonga na maisha mapya.
Baadae nikapata mwanamke mwingine na tulipendana sana japo
“Nakumbuka nikiwa shule ya msingi maisha hayakua mazuri. Biashara ya mama yangu ya bagia ikawa ndio inaendesha maisha yetu. Mimi ndio mkubwa na ndiye mtoto wa kiume kwetu. Kwa kipindi hicho mdogo wangu wa kike alikua bado mdogo sana.
Ilinibidi nisaidiane na mama kuuza bagia.
Nikitoka shule nakuta zimeshatayarishwa nabeba sufuria natembeza mpaka vijiji vya jirani. Nahakikisha zimeisha ndipo narudi nyumbani.
Utaratibu ulikua ni huo huo tangu darasa la tatu hadi form three. Nakumbuka wenzangu walikua wananicheka. Nilikosa marafiki.
Kila mtu alikua ananitenga na kunidhihaki kwamba mtoto wa kiume nabebaje sufuria na kwenda kuuza bagia. Walisema ni kazi za kike.
Ilifika muda nikikuta wenzangubwanapiga stori nikifika tu wote wanatawanyika. Nabaki mnyonge.
“Hii siri nitaitunza mpaka lini? Nibaki nayo au nijisalimishe?
Nilikuja Dar kutokea kijijini kupambania ugali. Mungu mwema mitikasi ilikubali. Kama unavyojua tena jiji la Dar wanawake warembo kila kona. Ni kama nilikua na ngekewa kila nilipotupa ndoano ilinasa. Nilijichanganya
nilitembea na kila aina ya mwanamke niliyemtamani.
Katika haya mahangaiko nilikutana na dada mmoja wa Songea. Huyu dada alikuja kunieleza amepata mjamzito. Ila akawa ameenda kwao Songea. Nilikua nikituma matumizi ila ilifika mahali mawasiliano yalikufa. Sikumpata tena. Ni miaka
mitano sasa sina mawasiliano yoyote sijui alipoteleaga wapi.
Maisha yaliendelea huku Dar nikakutana tena na mwanamke kutoka Kahama. Na yeye akapata ujauzito. Alirudi kwao Kahama pia ila mawasiliano yaliendelea kuwepo.
Ulifika muda nikaona hii njia sio sahihi. Nikabadilika