UNASHINDWA KUANDIKA CAPTION NZURI KATIKA POST ZAKO?

Kama una Brand au unaendesha biashara yako kupitia Mitandao ya kijamii...

... basi utakuwa unafahamu ni ngumu kiasi gani kuja na mawazo ya kuandika kila siku katika kila post unayoweka kwenye ukurasa wako.
Kutokana na jinsi unavyotaka watu wakutazame kupitia Brand/biashara yako...

...Unaweza kuchagua Tone ya sauti unayotaka watu wakutambue nayo.

Kupitia Caption zako, unaweza kuonekana Mcheshi, Mpole, au serious kiasi.

Sasa Social Media Entrepreneurs wengi ni WAVIVU mno...
katika uandishi wa Caption.

Unakuta mtu amepost Picha ya Viatu au Handbag, then kaandika tu

"Kiatu kama hiki ni Tsh 65,000/= Piga namba hii 0712 312XXX"

Come on! Hapo unaweza kusema umemshawishi mteja wako kununua?

Usichukulie poa, unazungumza na Mteja kupitia Caption yako!
Hapo ndipo unapomshawishi akufuate DM kuuliza zaidi au kununua kabisa.

Katika Uhalisia, unapaswa kufikiria namna ya kuandika caption ya kumshawishi mteja wako, kuliko hata picha ya product unayotaka kupost.
Caption yako ni lazima izungumze na mteja wako, na kumshawishi afanye kile unachomwaambia.

Sasa, unawezaje kuandika Caption nzuri katika post yako?

Are you ready?

Good, Tuendelee.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA UANDISHI WA CAPTION YAKO.

▶Chagua Tone ya Sauti, itakayokutambulisha.

Unapojenga community ya wateja mtandaoni, utatambulika kutokana na namna unavyoandika au tone of voice unayotumia katika uandishi wako.
Ninaposema "tone of voice", ni aina ya lugha unayotumia katika uandishi wako.

Je, serious sana? Mcheshi kiasi? Unahamasisha? Mpole mpole?

Mfano: Kama ni Brand ya Afya, basi unaweza kutumia lugha ya kuhamasisha na upole zaidi katika uandishi wako.
Mfano: Ukiangalia tu Uandishi wa mdogo wetu☺ @mafolebaraka unajua kabisa huyu ni mpole kiasi😎

Ukiangalia Uandishi wa @NyandaAmosi utagundua huyu ana u-serious zaidi🤭

Wewe pia, ni muhimu uchague tone utakayotumia katika uandishi wako, kwa kuzingatia watu unaozungumza nao.
▶Usiogope kutumia Emojs☺

Unaweza kuweka Emoj katika kila mwisho wa Caption yako ili kuonyesha hisia zako juu ya kile ulichopost...

...au unaweza kutumia emoj katika sentence zako kama mbadala wa neno.

Mfano: "Kiatu kama hiki unaweza kukipata dukani kwetu tu!😎
▶Andika kama unazungumza na mteja wako Ana kwa Ana.

Fikiria kama upo na Mteja wako ana kwa ana, na anataka kuchagua bidhaa au huduma yako...

Utamwambia nini? Maneno gani utayatumia ili kumshawishi aweze kununua?

Andika hayo maneno katika Caption yako.
▶Hashtags ni Rafiki yako wa Faida✊

Unapotaka kufikia watu wengi kwa haraka, basi huwezi kuacha kutumia Hashtags.

Matumizi mazuri ya Hashtags, yanaweza kukusaidia kupata Followers na kuonekana kwa watu wengine wengi wasiokufahamu.
Lakini sasa, hakikisha unatumia Hashtags zinazoendana na kile unachokifanya.

Kama unauza Cosmetics, basi hakikisha unatumia Hashtags zinazoendana na Cosmetics.

Unaweza kuziandika mwisho wa caption yako au katika comment section ya kila post yako (Kwa Instagram).
Uandishi wa Caption inaweza kuwa changamoto kubwa kwako. Lakini, kupitia tips hizi chache naamini umeshafahamu ni wapi pa kuanzia.

So, what's next?🤔

Kanuni yetu ya UPENDO ni ile ile...

RETWEET ili na wengine wapate Maarifa haya.

See you soon!

Your Friend
Ansey.

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Anselmo

Anselmo Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @CoachAnsey

14 Oct
UNATESEKA KUPATA MAUZO KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII?

Inawezekana una Bidhaa nzuri, una Huduma bora kabisa, una post kila siku kwenye account zako, lakini huoni ukipata faida yoyote kupitia mitandao ya kijamii unayotumia

Nina Habari njema sana kwako siku ya leo

Are you ready?🤔
Kabla haujafanya uamuzi wa kufuta post zako, au kufunga kabisa kurasa za biashara yako...

Nataka kukuonyesha Hatua 5 muhimu sana zinazoweza kukusaidia ili kupata matokeo mazuri.

Twende wote taratibu sasa...
1. Anza kwa kuweka Malengo Maalumu.

Inawezekana unafeli sehemu kubwa kwa sababu haujui ni nini unataka kutimiza kila siku, week au mwezi.

Anza kupanga Malengo maalumu kila siku. Haya yatakuwa kama...
Read 13 tweets
18 Aug
MBINU 5 ZITAKAZOKUSAIDIA KUKUZA BIASHARA YAKO KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII.

Inawezekana hapo ulipo umekwama, huoni maendeleo yoyote ya biashara yako, wakati huo huo unaona wapinzani wako wanaendelea kupiga hatua.

Upo katika hali hiyo?
Usiwe na wasiwasi, kila mfanyabiashara au mjasiriamali kama wewe, amewahi kupitia hali kama hiyo.

Kama umeshindwa leo, haina maana utaendelea kushindwa kila siku.

Au unasemaje Brother @mafolebaraka ?
Siku zote SILAHA kubwa katika biashara na MAARIFA!

Maarifa ndio silaha yako kubwa, ndio maana leo unapaswa kunisikiliza kwa makini kwa sababu ninaenda kukupa MAARIFA (Mbinu) takazokusaidia kufufua tena matumaini yako.
Read 21 tweets
16 Aug
JINSI YA KUTENGENEZA MAUDHUI (CONTENTS) YENYE KUONGEZA USHAWISHI KWA MTEJA.

Mara nyingi katika kutengeneza Maudhui, tunatumia mawazo, Ideas na ushawishi wetu binafsi...

..lakini, kuzingatia muonekano na aina ya Maudhui yanayoandikwa ni jambo muhimu mno.
Ni rahisi sana kutengeneza mawazo na topic mbalimbali kwa ajili ya wateja wako...

..Lakini, kama muuzaji, ni lazima uwe na uelewa mkubwa wa namna ya kuwasilisha mawazo hayo kwa mteja wako.
Ndio maana ni muhimu sana kufahamu namna mbalimbali ya kuandika maudhui yanayokidhi mahitaji ya mteja wako.

Kupitia mchanganyiko huu wa maudhui, itakusaidia kuongeza wafuasi wako zaidi, kufikia wateja wapya, na kutengeneza mazingira rafiki ya kuuza Bidhaa au huduma yako.
Read 13 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(