UNATESEKA KUPATA MAUZO KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII?
Inawezekana una Bidhaa nzuri, una Huduma bora kabisa, una post kila siku kwenye account zako, lakini huoni ukipata faida yoyote kupitia mitandao ya kijamii unayotumia
Nina Habari njema sana kwako siku ya leo
Are you ready?🤔
Kabla haujafanya uamuzi wa kufuta post zako, au kufunga kabisa kurasa za biashara yako...
Nataka kukuonyesha Hatua 5 muhimu sana zinazoweza kukusaidia ili kupata matokeo mazuri.
Twende wote taratibu sasa...
1. Anza kwa kuweka Malengo Maalumu.
Inawezekana unafeli sehemu kubwa kwa sababu haujui ni nini unataka kutimiza kila siku, week au mwezi.
Anza kupanga Malengo maalumu kila siku. Haya yatakuwa kama...
Ngazi ya kukusukuma kwenda mbele.
Hakikisha malengo yako ni SMART.
Yaani
📍Specific - Maalumu
📍Measurable - Unaweza kutrack maendeleo yake
📍Attainable - Una uhakika unaweza kuyafikia.
📍Relevant - Yanaendana na uhalisia wako
📍Time - Bound - Unaweka Deadline yake.
Badala yake, sema "Nataka kuongeza followers wangu twitter, kutoka 30 Mpaka 50 Ndani ya Mwezi huu."
Umeona tofauti hapo?
Hebu jaribu na wewe sasa katika angle nyingine...
2. Wasome wateja wako
Mtambue mteja wako ni nani kwa kufanya Research ndogo, sio kutumia mawazo yako.
Usiwe mvivu hapa!
Usipotambua nani anahitaji huduma au bidhaa yako, utaishia kujaribu kuuza kwa kila mtu.
Mwisho wa siku, hutauza kabisa!
Jihangaishe, ufahamu mteja wako ni mtu wa aina gani.
Anapenda maudhui ya aina gani, mahitaji na matamanio yake ni yapi?
Njia Rahisi ya kuanzia ni kuingia katika Magroup ya Facebook, Whatsapp, page za watu wanaofanya biashara au bidhaa kama yako nk.
Huko unaweza kupata...
Data za kuanzia ili kumsoma mteja wako kwa undani.
Wakati mwingine unaweza kutengeneza Survey ndogo na kuzituma kwa watu (Hasa watumiani wa huduma yako), ili kutambua mahitaji yao halisi na nini wanatamani kupata.
3. Usiwafumbie macho washindani wako.
Hakikisha unajua nani ni mshindani wako kibiashara.
Fuatilia anavyofanya. Angalia ubora na udhaifu wake.
Kwa namna yoyote tafuta Fursa kupitia yeye. Fanya zaidi ya ubora wake, na tumia udhaifu wake (Kibiashara tu) kama faida kwako.
4. Unahitaji maboresho katika Kurasa zako za kibiashara.
Katika Lugha ya kwetu, tunaita "Social Media Audit"
Chunguza effort zako, kisha jiulize
▶Ni wapi unafanya vizuri na wapi unahitaji kuongeza jubudi zaidi?
▶Ni watu gani wanatembelea sana ukurasa wako?
▶Mtandao upi unatumiwa sana na Wateja wako?
▶Unatumiaje Fursa ya kuwepo mtandaoni, ukilinganisha na washindani wako?
Hakikisha kila week unaangalia maendeleo yako, fursa ulizotumia na zile zilizokupita.
Mtandaoni hakuhitaji mtu MVIVU! Lazima ukubali kuchakarika kweri kweri😎
5. Hakikisha account yako inavutia na Kushawishi.
Kuandika jina tu na username yako, bado haitoshi.
Ukurasa wako unapaswa kuwaambia watu...
▶Wewe ni nani?
▶Unatoa huduma gani?
▶Wanawezaje kupata huduma yako?
Angalia mifano👇👇
Bado una mawazo ya kukata tamaa na kufunga ukurasa wako wa biashara?
Unaweza kuanza tena, and this time...It's going to be juust fine!
Kanuni yetu ya UPENDO bado ni ile ile...
RETWEET ili na wengine wapate Maarifa haya.
Your Friend
Ansey.
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
Siku zote SILAHA kubwa katika biashara na MAARIFA!
Maarifa ndio silaha yako kubwa, ndio maana leo unapaswa kunisikiliza kwa makini kwa sababu ninaenda kukupa MAARIFA (Mbinu) takazokusaidia kufufua tena matumaini yako.
JINSI YA KUTENGENEZA MAUDHUI (CONTENTS) YENYE KUONGEZA USHAWISHI KWA MTEJA.
Mara nyingi katika kutengeneza Maudhui, tunatumia mawazo, Ideas na ushawishi wetu binafsi...
..lakini, kuzingatia muonekano na aina ya Maudhui yanayoandikwa ni jambo muhimu mno.
Ni rahisi sana kutengeneza mawazo na topic mbalimbali kwa ajili ya wateja wako...
..Lakini, kama muuzaji, ni lazima uwe na uelewa mkubwa wa namna ya kuwasilisha mawazo hayo kwa mteja wako.
Ndio maana ni muhimu sana kufahamu namna mbalimbali ya kuandika maudhui yanayokidhi mahitaji ya mteja wako.
Kupitia mchanganyiko huu wa maudhui, itakusaidia kuongeza wafuasi wako zaidi, kufikia wateja wapya, na kutengeneza mazingira rafiki ya kuuza Bidhaa au huduma yako.