Dr. Badi Profile picture
Feb 12 9 tweets 2 min read
Barabarani, unakutana na mwanamke mchuuzi masikini mwenye *mtoto mgongoni,* unashusha kioo cha gari lako na kumuuliza kwa sauti ya kijeshi:

"Unauza bei gani hivyo vitunguu na hizo ndizi?" Muuzaji masikini *kwa upole anakujibu "shilingi elfu moja kwa kichane cha ndizi,....
na elfu moja kwa fungu la vitunguu."* Kwa kiburi unamwambia unahitaji kichane cha ndizi kwa shilingi mia tano na fungu la vitunguu kwa shilingi mia tano, au vinginevyo haununui.

Muuzaji masikini anakubaliana na hali na kukujibu, *"Chukua tu kwa bei unayotaka,........
sijauza chochote tangu asubuhi,* walau sasa nipate cha kununulia watoto chakula cha usiku."

*Amepata hasara, lakini zaidi anaenda kukununulia pia mfuko wa kuweka bidhaa hizi ulizo nunua.* Unamwagiza afanye haraka vinginevyo utabadili mawazo........
. Anaomba msamaha, na *kwa tabasamu anakukabidhi bidhaa zako, anakubariki pia kwa kumuungisha.*

Unamrushia hela na kuchomoka kwa kasi na kumwachia wingu la *vumbi na moshi linalomfunika yeye na mtoto. Anakohoa wakati anaweka vizuri fedha kidogo alizopata.*........
Umaskini haujamwachia uchaguzi.

Umefika sasa kwenye hoteli ya nyota tano, ambapo utakutana na rafiki zako. Unawaambia *waagize chakula na vinywaji kadiri wanavyotaka.* Wanaagiza vyakula vya gharama kubwa, na mabaki ya chakula ni mengi kuliko chakula walichokula.......
. *Gharama nzima inakua shilingi laki tano. Unalipa bila kuomba upunguziwe,* unampa mhudumu tip ya shiligi elfu kumi shukrani kwa chakula alichowahudumia ambacho hamkula hata nusu yake.

Tukio hili linaweza kuonekana la kawaida kabisa kwako, *lakini sio la kibinadamu.*.....,,,,
Point ni kwamba:-
Kwanini kila mara tunaonyesha tuna nguvu ya kubishania bei wakati tunaponunua kutoka *kwa maskini?*
Kwanini tunakua wakorofi tunaponunua *kwa maskini?*
Kwanini tunakua wachoyo tunaponunua kwa wahitaji?

Kwanini tunaonyesha ukarimu kwa wale ambao wala......
*hawahitaji ukarimu wetu?*
Kwanini tunaonyesha *upole na utu* tunaponunua kwa watu matajiri ambao wanaona hela yetu kama chenchi ndogo tu?
Kwanini tunaelekeza *fedha zetu kwenye bahari ya fedha?*.....
*#Tafadhali nunua vitu rahisi kwa watu mskini kwa bei ya haki*
#Wakati mwingine, makusudi lipa na ziada unaponunua kutoka kwao.. Kua na UTU wakati mwingine BARAKA zinatoka kwa watu Masikini. MUNGU NIWETU SOTE ...

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Dr. Badi

Dr. Badi Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @DrBadiBoy

Feb 12
hujapata wala kutimiza malengo yako. Ukitafakari unaona hujawahi kufurahia maisha, wala kufanya starehe yoyote. Watoto wako wanaishi kwa shida, hujawahi hata kuvaa nguo ya laki au kuvaa kiatu cha elfu 50, miaka yote umeishi kwenye nyumba ya kupanga..mke wako amekukimbia sababu ya
umasikini wako...aaahh. 😢😢 Unawaza hadi moyo unataka kupasuka, unatamani kufa, unajiuliza nakosea wapi? Mbona vijana wa juzi tu wanafanikiwa haraka, wanamiliki majumba, magari na vitu vya thamani?

Nikutie nguvu mzee mwenzangu, kila mtu hapa duniani anafungu lake,........🤲
amini fungu lako bado. Endelea kupambana jibidishe wala usikate tamaa, tena usidhani umekuja duniani kusindikiza wengine lah.
Nikukumbushe kitu👇
Miaka yako yote hujawahi kuumwa wewe wala watoto wako na unakumbuka siku ile mnaenda mnadani gari ikapata ajali wenzako......👇
Read 9 tweets
Feb 9
Laki tano, Mshahara wa Teller wa Benki hapa mjini Laki Tano, Bei ya IPHONE 6 ya kujishebedulia Snapchat na Istagram Laki Tano, Bajeti ya Mafuta ya SUBARU mwezi Mzima Laki Tano , Bajeti ya HEINEKEN 100 KWA wanywaji wa Pomb HELA FLANI YA MBOGA TU• ....
@nyuki_malkia ANAANDIKA✍🏼
Lakini ,Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji.

Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua SIMTANK la lita 5000 ( ndoo 250 za lita 20) ambazo zinaweza....
kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila SIMTANK unalouza.

Laki tano hii hii inaweza kulima Ekari 2 za Maharage pale Simanjiro na baada ya Miezi Minne ukavuna si chini ya Million 3 ambazo zitaexpand kilimo chako MARA 6..
Read 11 tweets
Feb 8
Msichana aitwae Aida, mwanafunzi wa darasa la tano shule moja ya msingi ilioko huko Ludewa Njombe alikuwa akichukiwa sana na mwalimu wake wa darasa. Aida alikuwa akijitahidi kufanya kila jambo kumfurahisha mwalimu wake lakini mwalimu alizidi kumchukia kuliko wanafunzi wake wote..
Siku moja wamisionari tokea Marekani walitembelea shule ya wakina Akida na wakataka kuwachukua watoto watatu waliopo darasa la tano ili waende nao Marekani wakasome huko na kuwafadhili masomo yao mpaka chuo kikuu....
Kwa kujua hili mwalimu wa darasa la wakina Aida alimweka Aida mwishoni kabisa mwa darasa akae huko ili watakapoingia wale wafadhili wasipate kumchagua.

Wamisionari walipoingia darasani, waliongea na wanafunzi na mmoja wao akaenda nyuma ya darasa.
Read 9 tweets
Feb 8
TAFAKARI LEO

Mwenye degree asiye na ajira kuna wakati huwa anaona bora angeishia form four na angefanya shughuli nyingine... Na aliyeishia darasa la saba kutokana na hali ya maisha aliyonayo kuna wakati anaona alipaswa kufika chuo kikuu ili awe na maisha mazuri...
...HUO NDIYO UTAMU WA MAISHA... Uzuri ni kwamba maisha huwa hayana formula maalum...aliyesoma maskini, wakati asiyesoma ni tajiri, na kuna asiyesoma maskini wakati aliyesoma ni tajiri... Mwenye pesa anaumizwa na mapenzi mpaka anatamani kuwa Single....
na asiye na pesa anaachwa kwa sababu hana kipato cha kumudu gharama za mwenzi wake... Unawaza kuacha shule ili ufanye biashara kwa sababu watu wengi wanafanikiwa na kuna mwenzako anawaza kuacha biashara kwa sababu biashara hailipi ili arudi shule akimaliza akaajiriwe.....
Read 8 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

:(