Nilipokua chuo mwaka 2018 nikisomea course ya IT nilibahatika kupata mdada ambaye niliishi nae kama mchumba na kumpa mahitaji yote na tulikubaliana tuzae.
Basi nikampa kweli ujauzito huku nikimhudumia kwa kila kitu bila wazazi wangu kujua na hakuwahi kukosa kitu alichohitaji kwangu japo sikuwahi kuomba msaada kwa mtu, ila niliendeleza life langu kwa mishe zangu za kitaani(kwa wanaoelewa IT huwa hatukosi mishe za hapa na pale).
Ilipofika mwezi mmoja na nusu kabla ya binti kujifungua alisema anaenda jifungulia nyumbani.
Sikumkataza kwa vile na mimi niliona sitaweza ghaili masomo nisaidie malezi. Hivyo nikamruhusu aende na kumpatia vitu vyote muhimu alivyohitaji kwa ajili ya safari na mambo mengine.
Basi yule binti akaanza safari mpaka akafika. Siku zikakata mpaka akajifungua.
Mwisho wa siku nakuja pata habari kuwa alienda kujifungua kwa mwanaume wake aliyempa ujauzito. Nilishtuka ikanibidi nifunge safari mpaka alipo kwenda kumuona,
cha ajabu mtoto nusu anafanana na mimi nusu anafanana na huyo anayesemekana ni baba yake.
Sikuelewa. Nilipoomba nikapime DNA na mtoto nilikataliwa.
Ikanibidi niwaache na maisha yao nikapiga moyo konde nikaanza safari ya matumaini. Walibahatika kuoana pia baada ya mtoto kuzaliwa
Maisha yameenda na cha ajabu yule binti ananisumbua mpaka hii leo anahitaji turudiane huku akidai kuwa mtoto ni wangu licha ya kuwa aliwahi nikana kuwa sio mtoto wangu hapo awali.
Kiukwel nampenda sana ila tatizo ni kuwa ameshaolewa na hajaachwa kwa talaka ila wamepishana kauli tu na mumewe tangu mwaka jana mwezi wa saba. Najiuliza nirudiane nae? na itakuaje kwa mtoto? haitaleta utata zaidi?". Anonymous, #WatuNiStory
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
"Ipo hivi, mimi ni kijana wa miaka 25, nilikuwa na mpenzi wangu ana mtoto sio wangu. Kipindi nipo nae nilikuwa sina kazi na tulikuwa tumepanga tunaishi pamoja lakini yeye alikuwa na kazi. Sasa hakutaka kubeba mimba yangu akihofia hali ngumu ya maisha ambayo ninapitia.
Kile kitendo kikaniumiza sana, nikaja Dar kutafuta maisha, ikawa kila baada ya miezi mitatu narudi nyumbani kumtembelea.
Sasa mwezi wa tisa nikashindwa kwenda kwa wakati, lakini tulikubaliana kwakuwa mkataba ulikuwa karibu kuisha, nimalizie mkataba ndio niende nyumbani.
Kweli, nikaenda mwezi wa 12 ila cha ajabu namkuta na mimba ya mwezi na ananieleza kuwa aliempa mimba hakuwa na mahusiano nae na hamtaki tena.
Kwa hasira nikaondoka, nikamwacha. Ety katoa mimba ananiomba msamahe na turudiane.
"Ilikuwa Jumapili weekend moja nimekaa ghetto kwangu nimefulia mbaya. Simu yangu inaita, kucheck alikuwa mwanangu.
Kupokea ananiambia ana msala inabidi nimsaidie kuu-solve. Inakuaje? nikauliza.
Ndio ananiambia amempa mimba binti wa kidato cha nne hivyo anaomba aje kwangu kufanya harakati za kuitoa. Ashaongea na dokta, na dogo yupo tayari bado eneo la tukio tu sababu hawawezi kufanyia hospital.
Daah!nikicheck ni mwanangu sana. Na kwao ana mke na mtoto.
"Kuna demu mmoja nina urafiki nae kiasi kwamba binafsi nikiwa na shida yoyote ananisaidia. Mara nyingi huwa anakuja home hata nguo zangu huwa anafua na usafi anafanya. Chochote nitakachomwambia anafanya.
Alishaniweka wazi kuwa ana ngoma na mambo yake yote huwa hanifichi hata awe na mahusiano basi ataniweka wazi kwa kila kitu hata akalale na huyo mwanaume.
Tatizo linakuja sehemu moja, hatujawahi kuongelea swala la kuwa na mahusiano. Mimi na yeye huwa ni stori za kawaida tu.
Mimi nina mahusiano na demu mwingine na anamfahamu hata nikikosana na demu wangu anakuwa wa kwanza kutusuluhisha. Alishawahi kuolewa wakaachana na mume wake kisa huyo mwanaume alimwambia aache mazoea na mimi akakataa.
"Miaka kadhaa iliyopita Vijana mtaani kwetu waligundua kuwa Kuna mama huwa anaacha wazi madirisha ya nyumba yake pindi akiwa anabadilisha nguo. Ni mama mgeni ambae alikua kahamia miezi michache tu iliyopita.
Alikua akifanya hivyo kila siku mida ya saa moja na nusu usiku akitoka kuoga.
Yule mama MashaAllah alijaliwa shape. Yani alikua na shape moja ya ukorofi sana. Alienda hewani.. huko nyuma ni kama pembe la ng'ombe tuu.. halifichiki.. hatari sana.
Basi Vijana ndo ukawa mchezo wao.. Taarifa ziliponifikia nikawa natamani nikamwambie yule mama kuna raia wanamla chabo maana alikua ni jirani yangu na ananifahamu vizuri tunaheshimiana halafu alikua mwalimu wa shule ya msingi.
"Tangu naanza Shule Ya Msingi, O level na A level Mungu alinijalia Uwezo Mkubwa Darasani. Nikafanikiwa kumaliza kidato cha Sita Vizuri na kuweza kuchaguliwa kujiunga na Chuo kikuu Cha Afya Muhimbili.
Ndipo nilipo anza kuonja joto la kufeli masomo semester ya kwanza nikakamatwa kwenye moja ya somo gumu (Anatomy), second semester Nikapita vizuri, nikarudi October kuja kusapua.
Kutoka na maandalizi duni nikafeli tena nika carry.
Nikaingia mwaka wa pili semester ya Kwanza nikanasa tena kwenye somo moja konk (Micro 1 and 2).
Presha ikanianza kwamba semester inayofuata nikishikwa tena ndo disco.
Semester ya pili nikanasa tena kwenye somo konk (Pharmacology 1 and 2) Ila siku Disco.