"Katika harakati za kutafuta maisha,wanaume huwa tunapitia mambo mengi kweli. Mengine yanabaki mioyoni na kuwa siri zetu.

Nakumbuka baada ya kukosa mishe na harakati za kuingiza hela, nilijikuta naingia kwenye kuuza bangi. Naweza kusema tabia yangu ilisanifu kazi yangu.
Maana nilikuwa mbabe sana na mtu mwenye matukio mengi sana mtaani.

Ilikuwa ni ngumu sana kwangu kupitisha wiki na sijafanya tukio lolote la kibabe au kuogopwa. Hayo ndio yalikuwa maisha yangu.
Kama unavojua hii kazi huwezi kwepa kufuatiliwa na jeshi la polisi, yaani kila muda wanakutamani.

Mimi nimekamatwa na kushtakiwa mara tatu kwa kuuza bangi.
Mara ya kwanza niliwashinda tu kizimbani kwa kuongea na kujieleza, mara ya pili walinikamata na baada ya kukaa mahabusu walikosa uthibitisho na kuachiwa.

Mara ya tatu ndio nilipatikana, tena baada kuchomwa na shemeji yangu yaani mke wa mdogo wangu.
Yaani aliwapa ramani ya home na kila sehemu zaga zangu zinakaa.

Siku wanakuja kufanya msako nyumbani, shemeji aliwapa ushirikiano wa kutosha na nikadakwa. Hili nililishuhudia kwa macho yangu.

Ilikuwa hakuna namna ya kuchomoka kwenye ile kesi, nilihukumiwa jela miaka mitano.
Baada ya mwezi mmoja nilihamishwa kutoka hapa na kupelekwa jela moja ipo huko Ludewa.

Achana na hii story, nikikusimulia na story za huko hatutamaliza. Ila nachoweza kukwambia jela sio sehemu nzuri.

Ila nashukuru ilinifundisha. Kule sikuwa mbabe tena.
Nilikuwa nafuata mambo yao kama wanavyotaka. Ni ishu ya kwenda na muda na kufuata ratiba zao, hapo kidogo utakuwa salama.
Baada ya miaka mitatu ya tabia nzuri ndani ya jera, nimeruhusiwa na sasa natumikia kifungo cha nje. Kila asubuhi naenda kufanya usafi ofisi za Halmashauri na majengo ya hospitali. Nikisaini vitabu vyao ndio naondoka.
Mtaani hawanielewi na wananishangaa sana. Imekuaje mtu wa matukio nimekuwa mpole hivi, wasichojua mwenzao nina kifungo cha nje yaani kosa lolote hata la kusingiziwa likifika polisi, naweza rudishwa jela.
Na nikikumbuka maisha ya kule, naona bora niwe mpole tu. Hata shemeji yangu yule aliyeni-snitch haamini kama nimekuwa mpole hivi". - Anonymous, Babati.
#WatuNiStory

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with WatuNiStory

WatuNiStory Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @watunistory

30 Oct
"Tangu naanza Shule Ya Msingi, O level na A level Mungu alinijalia Uwezo Mkubwa Darasani. Nikafanikiwa kumaliza kidato cha Sita Vizuri na kuweza kuchaguliwa kujiunga na Chuo kikuu Cha Afya Muhimbili. Image
Ndipo nilipo anza kuonja joto la kufeli masomo semester ya kwanza nikakamatwa kwenye moja ya somo gumu (Anatomy), second semester Nikapita vizuri, nikarudi October kuja kusapua.

Kutoka na maandalizi duni nikafeli tena nika carry.
Nikaingia mwaka wa pili semester ya Kwanza nikanasa tena kwenye somo moja konk (Micro 1 and 2).
Presha ikanianza kwamba semester inayofuata nikishikwa tena ndo disco.

Semester ya pili nikanasa tena kwenye somo konk (Pharmacology 1 and 2) Ila siku Disco.
Read 9 tweets
27 Oct
"Kuna story ambayo baba yangu Mzazi (Mzee Eugeni) alinisimulia kuwa kipindi cha nyuma akiwa kijana alikuwa anaishi mwanza kufanya kazi ndogo ndogo katika harakati zake alioa Mwanamke ambaye anaitwa Maria na alipata naye watoto wawili. Image
Mtoto wa kwanza wa kike alikuwa anaitwa Agnes (Eugeni)alizaliwa 1979 na mtoto wa Pili alikuwa anaitwa Ana(Eugeni) alizaliwa 1983.

Mwaka 1984 baba alisafiri kusalimia Nyumbani kwake alipozaliwa ambapo ni Kilimanjaro.
Kutokana na maisha ya kipindi kile alishindwa kurudi Mwanza ilimlazimu yeye kubaki Kilimanjaro ambapo alioa mwanamke mwingine ambaye ni mama yangu mzazi.
Read 6 tweets
24 Sep
"Nimetokea kwenye familia maskini sana na kibaya zaidi ilidharaulika sana, tena kwa pande zote mbili yaani upande wa baba na mama.

Nimekuwa huku kauli za kejeri zinasikika na kuishi masikioni mwangu.
Hilo kwangu ndio lilikuwa tatizo kubwa. Niliwachukia sana jamaa zangu mpaka nimekua mkubwa sikuwahi kuomba msaada wa aina yoyote kwao.

Hadi wazazi wangu niliwahi kuwakataza, niliwaambia shida zote na huduma wanibebeshe mimi.
Kuwaeleza shida zetu, ilikuwa kama kuwalilia njaa kwao.

Leo Mungu amesaidia tunakula kwa muda sahihi na tunalala pazuri. Kiukweli sitamani hata kuwapigia simu. Sasa hivi wamenibadilisha jina wanasema mimi ni jeuri.
Read 4 tweets
23 Sep
"Mwaka 2005 nilihitimu chuo cha ualimu Kabanga kilichopo mkoani Kigoma. Sikukaa muda mrefu mtaani, mwaka 2006 nilifanikiwa kupata ajira wilayani Moshi.

Nilifundisha pale miaka mitatu nikakutana na jamaa mmoja tukawa marafiki. Kumbe alikuwa mganga wa kienyeji.
Katika harakati zake, akanishawishi nikawa chawa wake. Siku zilivyoenda nikajikuta na mimi nimetamani kuwa mganga.
Sikuwa na majini ila kutokana na ukaribu wetu na nilivokua naona watu wengi wenye shida wanakuja kwake wanamuachia hela nyingi kiasi kwamba hela ambayo alikuwa anaipata ilikua inazidi mshahara wangu kama mwalimu.

Nikashawishika kuacha kazi ya ualimu na nikawa mganga.
Read 5 tweets
22 Sep
"Mwaka 2016 nilipoteza kazi niliyokuwa nimeajiriwa kwa makosa ambayo sikuhusika, lakini upepelezi ulipokuja kufanyika nilionekana ni kama na mimi nilihusika kwenye huo wizi ingawa ukweli sikuhusika.

Sikujua chochote na wala sikula hata sh 100.
Wanasema siku ya kusurubiwa kwako manabii wa uongo watakuja ili kukutolea ushahidi wa uongo lengo uangamie, ndio kilichonitokea mimi.
Baadae ya kupoteza kazi Mungu alinipa ujasiri sana maana sikuwahi kujutia kupoteza kazi bali nilianza kuwaza naishije kwa sasa na nafanya nini ili maisha yaende?.
Read 7 tweets
21 Sep
"Tulikuwa kwenye mahusiano miaka saba. Katika uhusiano wetu nilibahatika kupata mimba yake.

Aliikataa kabisa sio mimba yake. Niliumia sana. Ikabidi nilee mimba mwenyewe, hadi najifungua sikujua alipo na sikuwahi kumuona. Image
Mtoto alipokuwa na mwaka na nusu nilipost picha yake Facebook. Alimuona na akaanza kunifuatilia.

Badae alinitafuta akaja hadi nyumbani na kwa ndugu zangu, akaomba msamaha. Hatukuwa na hiyana nae, tulimsamehe.
Tukalea mtoto mpaka akanunua uwanja. Alianza kujenga na nyumba ilipoisha akanimbia nijiandae tufunge ndoa tumlee mtoto pamoja.

Gafla akaanza kubadilika na mwaka huu akaanza kuniambia kwao ndugu zake hawanitaki hivyo nitafute bwana na anioe na mtoto anamchukua.
Read 6 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(