"Kuna demu mmoja nina urafiki nae kiasi kwamba binafsi nikiwa na shida yoyote ananisaidia. Mara nyingi huwa anakuja home hata nguo zangu huwa anafua na usafi anafanya. Chochote nitakachomwambia anafanya.
Alishaniweka wazi kuwa ana ngoma na mambo yake yote huwa hanifichi hata awe na mahusiano basi ataniweka wazi kwa kila kitu hata akalale na huyo mwanaume.

Tatizo linakuja sehemu moja, hatujawahi kuongelea swala la kuwa na mahusiano. Mimi na yeye huwa ni stori za kawaida tu.
Mimi nina mahusiano na demu mwingine na anamfahamu hata nikikosana na demu wangu anakuwa wa kwanza kutusuluhisha. Alishawahi kuolewa wakaachana na mume wake kisa huyo mwanaume alimwambia aache mazoea na mimi akakataa.
Watu mtaani wanahisi mimi nina mahusiano nae, kitu kitu ambacho si cha kweli. Wazazi wake walishampiga marufuku kuhusu mimi lakini kagoma kabisa maana yule aliyemuoa alienda kushtaki. Akitongozwa mie ndio mtoa maamuzi, akubali au akatae.
Kila boy anayekuwa nae wanaachana baada ya muda mfupi, ukiuliza sababu ni yeye kuwa karibu na mimi.

Baadhi yao wananichukia kuwa nawachukulia demu wao kitu ambacho sio kweli.
Hata demu wangu huwa anahisi hivyo lakini hajawahi kuona tupo mazingira ya kumfanya aamini tuna mahusiano ya chinichini.

Anasema hakuna wa kuja kunitenganisha urafiki nae hata iweje na mtu atakaekuja kumuoa akubali kwanza kuhusu mimi ndo wataelewana.
Na kama unavyojua wanaume walivyo na wivu. Akikuta watu wananiongelea vibaya ni kesi, alishawahi lala polisi kapiga mtu kisa kuniongea vibaya.
Nilishamweleza kuwa akae mbali na mimi nisije fanyiwa kitu kibaya na watu wake, lakini hayupo tayari na alishajaribu kujiua kwajili ya kumwambia hivyo.
Alinambia siku moja kwamba mimi na yeye kamwe hatuwezi kuwa na mahusiano maana itatokea siku tutagombana na atanikosa na urafiki wetu utaishia hapo. Anachotaka tuwe na urafiki tu.
Ana kazi yake ya ususi, sasa nashindwa nifanyeje maana nazidi kuongeza maadui tu kuhusu yeye na hayupo tayari kukaa mbali na mimi. Sielewi nifanye nini". Anonymous #WatuNiStory

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with WatuNiStory

WatuNiStory Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @watunistory

28 Dec
"Miaka kadhaa iliyopita Vijana mtaani kwetu waligundua kuwa Kuna mama huwa anaacha wazi madirisha ya nyumba yake pindi akiwa anabadilisha nguo. Ni mama mgeni ambae alikua kahamia miezi michache tu iliyopita.
Alikua akifanya hivyo kila siku mida ya saa moja na nusu usiku akitoka kuoga.

Yule mama MashaAllah alijaliwa shape. Yani alikua na shape moja ya ukorofi sana. Alienda hewani.. huko nyuma ni kama pembe la ng'ombe tuu.. halifichiki.. hatari sana.
Basi Vijana ndo ukawa mchezo wao.. Taarifa ziliponifikia nikawa natamani nikamwambie yule mama kuna raia wanamla chabo maana alikua ni jirani yangu na ananifahamu vizuri tunaheshimiana halafu alikua mwalimu wa shule ya msingi.
Read 9 tweets
30 Oct
"Tangu naanza Shule Ya Msingi, O level na A level Mungu alinijalia Uwezo Mkubwa Darasani. Nikafanikiwa kumaliza kidato cha Sita Vizuri na kuweza kuchaguliwa kujiunga na Chuo kikuu Cha Afya Muhimbili.
Ndipo nilipo anza kuonja joto la kufeli masomo semester ya kwanza nikakamatwa kwenye moja ya somo gumu (Anatomy), second semester Nikapita vizuri, nikarudi October kuja kusapua.

Kutoka na maandalizi duni nikafeli tena nika carry.
Nikaingia mwaka wa pili semester ya Kwanza nikanasa tena kwenye somo moja konk (Micro 1 and 2).
Presha ikanianza kwamba semester inayofuata nikishikwa tena ndo disco.

Semester ya pili nikanasa tena kwenye somo konk (Pharmacology 1 and 2) Ila siku Disco.
Read 9 tweets
29 Oct
"Katika harakati za kutafuta maisha,wanaume huwa tunapitia mambo mengi kweli. Mengine yanabaki mioyoni na kuwa siri zetu.

Nakumbuka baada ya kukosa mishe na harakati za kuingiza hela, nilijikuta naingia kwenye kuuza bangi. Naweza kusema tabia yangu ilisanifu kazi yangu.
Maana nilikuwa mbabe sana na mtu mwenye matukio mengi sana mtaani.

Ilikuwa ni ngumu sana kwangu kupitisha wiki na sijafanya tukio lolote la kibabe au kuogopwa. Hayo ndio yalikuwa maisha yangu.
Kama unavojua hii kazi huwezi kwepa kufuatiliwa na jeshi la polisi, yaani kila muda wanakutamani.

Mimi nimekamatwa na kushtakiwa mara tatu kwa kuuza bangi.
Read 10 tweets
27 Oct
"Kuna story ambayo baba yangu Mzazi (Mzee Eugeni) alinisimulia kuwa kipindi cha nyuma akiwa kijana alikuwa anaishi mwanza kufanya kazi ndogo ndogo katika harakati zake alioa Mwanamke ambaye anaitwa Maria na alipata naye watoto wawili. Image
Mtoto wa kwanza wa kike alikuwa anaitwa Agnes (Eugeni)alizaliwa 1979 na mtoto wa Pili alikuwa anaitwa Ana(Eugeni) alizaliwa 1983.

Mwaka 1984 baba alisafiri kusalimia Nyumbani kwake alipozaliwa ambapo ni Kilimanjaro.
Kutokana na maisha ya kipindi kile alishindwa kurudi Mwanza ilimlazimu yeye kubaki Kilimanjaro ambapo alioa mwanamke mwingine ambaye ni mama yangu mzazi.
Read 6 tweets
24 Sep
"Nimetokea kwenye familia maskini sana na kibaya zaidi ilidharaulika sana, tena kwa pande zote mbili yaani upande wa baba na mama.

Nimekuwa huku kauli za kejeri zinasikika na kuishi masikioni mwangu.
Hilo kwangu ndio lilikuwa tatizo kubwa. Niliwachukia sana jamaa zangu mpaka nimekua mkubwa sikuwahi kuomba msaada wa aina yoyote kwao.

Hadi wazazi wangu niliwahi kuwakataza, niliwaambia shida zote na huduma wanibebeshe mimi.
Kuwaeleza shida zetu, ilikuwa kama kuwalilia njaa kwao.

Leo Mungu amesaidia tunakula kwa muda sahihi na tunalala pazuri. Kiukweli sitamani hata kuwapigia simu. Sasa hivi wamenibadilisha jina wanasema mimi ni jeuri.
Read 4 tweets
23 Sep
"Mwaka 2005 nilihitimu chuo cha ualimu Kabanga kilichopo mkoani Kigoma. Sikukaa muda mrefu mtaani, mwaka 2006 nilifanikiwa kupata ajira wilayani Moshi.

Nilifundisha pale miaka mitatu nikakutana na jamaa mmoja tukawa marafiki. Kumbe alikuwa mganga wa kienyeji.
Katika harakati zake, akanishawishi nikawa chawa wake. Siku zilivyoenda nikajikuta na mimi nimetamani kuwa mganga.
Sikuwa na majini ila kutokana na ukaribu wetu na nilivokua naona watu wengi wenye shida wanakuja kwake wanamuachia hela nyingi kiasi kwamba hela ambayo alikuwa anaipata ilikua inazidi mshahara wangu kama mwalimu.

Nikashawishika kuacha kazi ya ualimu na nikawa mganga.
Read 5 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(