"Miaka kadhaa iliyopita Vijana mtaani kwetu waligundua kuwa Kuna mama huwa anaacha wazi madirisha ya nyumba yake pindi akiwa anabadilisha nguo. Ni mama mgeni ambae alikua kahamia miezi michache tu iliyopita.
Alikua akifanya hivyo kila siku mida ya saa moja na nusu usiku akitoka kuoga.
Yule mama MashaAllah alijaliwa shape. Yani alikua na shape moja ya ukorofi sana. Alienda hewani.. huko nyuma ni kama pembe la ng'ombe tuu.. halifichiki.. hatari sana.
Basi Vijana ndo ukawa mchezo wao.. Taarifa ziliponifikia nikawa natamani nikamwambie yule mama kuna raia wanamla chabo maana alikua ni jirani yangu na ananifahamu vizuri tunaheshimiana halafu alikua mwalimu wa shule ya msingi.
Kila nikitaka kumfuata najishtukia.. zile habari sasa zikawa zinadai yule mama alikua akifanya maksudi maana vijana hata wakipiga makelele hata hashtuki.
Wanadai eti alikuwa na shanga nyingi sana.
Ni maneno hayo ndio yalianza nipa tamaa ya kuona.
Nikahama kutoka kwenda kumtonya hadi kwenda kumla chabo. Nilivumilia sana sana ila.. Kwa umri ule wa miaka 21 nisingeweza jizuia.
Siku moja natoka zangu maeneo nakuta vijana dirishani pale wanakula chabo.. Mara wakaondoka.
Nikasema "enhee pale hamna watu ngoja Leo zamu yangu leo".. nikasogea.
Nikakuta taa ya chumbani inawaka ila hakuna mtu ndani.. Nikazidi kodoa mijicho..
Ghafla nikasikia "Aaah Adam hata weweee" sauti ikitoka dirisha la sebuleni kulikokuwa na kiza ikizungumza na mimi niliekua kwenye mwanga wa taa ya chumbani.
Aisee nilikimbia.. nilikimbia mbio ambazo hazipo.. Kilichonifanya nikimbie Ni Ile aibu..
Nitamuangalia vipi yule mama, jirani yangu, rafiki wa mama yangu?
Kuna mzee mmoja tulikua tunakaa nae pale mtaani alikua anaheshimika sana. Kipindi l hicho niko katika process za mwisho kujiunga na jeshi la polisi na huyo mzee ndio alikua ananipigania nafasi.
Yule mama alienda muhadithia Yule mzee.. Daaah.. yule mzee hakuzungumza tena na mimi kuanzia 2011 mpaka Leo hii". Adam, Dar. #WatuNiStory
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
"Kuna demu mmoja nina urafiki nae kiasi kwamba binafsi nikiwa na shida yoyote ananisaidia. Mara nyingi huwa anakuja home hata nguo zangu huwa anafua na usafi anafanya. Chochote nitakachomwambia anafanya.
Alishaniweka wazi kuwa ana ngoma na mambo yake yote huwa hanifichi hata awe na mahusiano basi ataniweka wazi kwa kila kitu hata akalale na huyo mwanaume.
Tatizo linakuja sehemu moja, hatujawahi kuongelea swala la kuwa na mahusiano. Mimi na yeye huwa ni stori za kawaida tu.
Mimi nina mahusiano na demu mwingine na anamfahamu hata nikikosana na demu wangu anakuwa wa kwanza kutusuluhisha. Alishawahi kuolewa wakaachana na mume wake kisa huyo mwanaume alimwambia aache mazoea na mimi akakataa.
"Tangu naanza Shule Ya Msingi, O level na A level Mungu alinijalia Uwezo Mkubwa Darasani. Nikafanikiwa kumaliza kidato cha Sita Vizuri na kuweza kuchaguliwa kujiunga na Chuo kikuu Cha Afya Muhimbili.
Ndipo nilipo anza kuonja joto la kufeli masomo semester ya kwanza nikakamatwa kwenye moja ya somo gumu (Anatomy), second semester Nikapita vizuri, nikarudi October kuja kusapua.
Kutoka na maandalizi duni nikafeli tena nika carry.
Nikaingia mwaka wa pili semester ya Kwanza nikanasa tena kwenye somo moja konk (Micro 1 and 2).
Presha ikanianza kwamba semester inayofuata nikishikwa tena ndo disco.
Semester ya pili nikanasa tena kwenye somo konk (Pharmacology 1 and 2) Ila siku Disco.
"Kuna story ambayo baba yangu Mzazi (Mzee Eugeni) alinisimulia kuwa kipindi cha nyuma akiwa kijana alikuwa anaishi mwanza kufanya kazi ndogo ndogo katika harakati zake alioa Mwanamke ambaye anaitwa Maria na alipata naye watoto wawili.
Mtoto wa kwanza wa kike alikuwa anaitwa Agnes (Eugeni)alizaliwa 1979 na mtoto wa Pili alikuwa anaitwa Ana(Eugeni) alizaliwa 1983.
Mwaka 1984 baba alisafiri kusalimia Nyumbani kwake alipozaliwa ambapo ni Kilimanjaro.
Kutokana na maisha ya kipindi kile alishindwa kurudi Mwanza ilimlazimu yeye kubaki Kilimanjaro ambapo alioa mwanamke mwingine ambaye ni mama yangu mzazi.
"Nimetokea kwenye familia maskini sana na kibaya zaidi ilidharaulika sana, tena kwa pande zote mbili yaani upande wa baba na mama.
Nimekuwa huku kauli za kejeri zinasikika na kuishi masikioni mwangu.
Hilo kwangu ndio lilikuwa tatizo kubwa. Niliwachukia sana jamaa zangu mpaka nimekua mkubwa sikuwahi kuomba msaada wa aina yoyote kwao.
Hadi wazazi wangu niliwahi kuwakataza, niliwaambia shida zote na huduma wanibebeshe mimi.
Kuwaeleza shida zetu, ilikuwa kama kuwalilia njaa kwao.
Leo Mungu amesaidia tunakula kwa muda sahihi na tunalala pazuri. Kiukweli sitamani hata kuwapigia simu. Sasa hivi wamenibadilisha jina wanasema mimi ni jeuri.
"Mwaka 2005 nilihitimu chuo cha ualimu Kabanga kilichopo mkoani Kigoma. Sikukaa muda mrefu mtaani, mwaka 2006 nilifanikiwa kupata ajira wilayani Moshi.
Nilifundisha pale miaka mitatu nikakutana na jamaa mmoja tukawa marafiki. Kumbe alikuwa mganga wa kienyeji.
Katika harakati zake, akanishawishi nikawa chawa wake. Siku zilivyoenda nikajikuta na mimi nimetamani kuwa mganga.
Sikuwa na majini ila kutokana na ukaribu wetu na nilivokua naona watu wengi wenye shida wanakuja kwake wanamuachia hela nyingi kiasi kwamba hela ambayo alikuwa anaipata ilikua inazidi mshahara wangu kama mwalimu.
Nikashawishika kuacha kazi ya ualimu na nikawa mganga.