#Tanzania: Mvutano mkali unaendelea kutamalaki miongoni mwa watu binafsi, wanaharakati, wanasiasa, vyama vya siasa na viongozi wa chama tawala na vyama vya upinzani na serikali kuhusu uwezekano wa kupatikana Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya kabla ya UCHAGUZI MKUU 2025.
Madai ya Tume Huru yanasukumwa na hoja kwamba uwanja wa shughuli za siasa hauna usawa, bali unaweka mazingira ya kukipa faida zaidi chama tawala, huku kukiwa na madai ya mara kwa mara ya ukiukwaji wa sheria, ukosefu wa uhuru na kuwepo kwa mamlaka makubwa ya Rais juu ya Tume hiyo.
Madai ya Katiba mpya yanasukumwa na dhana kwamba Katiba Mpya ndilo jawabu la mambo mengi yanayolalamikiwa yakiwemo: mfumo wa uendeshaji nchi, madaraka ya Rais, Haki, Usawa, demokrasia, Uhuru wa kufanya siasa, Uhuru wa Mihimili katika kutekeleza majukumu yao na hata Tume Huru.
Uhuru wa Tume na viongozi wake ni miongoni mwa mambo yanayochukua mkondo na kukoleza ajenda ya madai ya Katiba mpya, licha ya Rais Samia Suluhu Hassan mnamo Juni mwaka 2021 kubainisha kuwa mpango wake ni kujikita katika masuala ya uchumi na kuweka kando Katiba Mpya kwa sasa.
Kumekuwa na malalamiko kutoka vyama vya siasa na wadau wengine wa siasa kuhusu michakato ya uchaguzi mkuu, ikiwemo ukosefu wa uhuru wa Tume ya Uchaguzi, jambo ambalo linaungwa mkono na hata viongozi wastaafu walioshiriki Kongamano la viongozi na wadau wa siasa.
Wadau wa siasa na wanazuoni wanashauri kuanza na Katiba Mpya kabla ya Tume Huru ya Uchaguzi huku wadau wengine wakishauri kwamba ianze Tume Huru kabla ya mchakato wa Katiba Mpya uundwaji wake unapingwa na kuaminika kuwa si suluhisho la kudumu katika uwanja wa demokrasia nchini.
kitendawili kigumu kinapatikana kwenye muundo wa Tume Huru; itaundwaje, viongozi watapatikanaje, kwa Katiba hii au ije Katiba Mpya, mamlaka ya uteuzi yatakuwa kwa nani,uendeshaji na vigezo vinavyohitajika kwa wajumbe vitakuja vipya au kubaki vilevie? Maswali ni mengi sana.
Kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 74(1) pamoja na vipengele vyake inafafanua vigezo vya watu wanaotakiwa kuwa viongozi wa Tume ya uchaguzi kuwataja kuwa.
Mwenyekiti anatakiwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani au mtu mwenye sifa ya kuwa wakili kwa kwa zaidi ya 15 years.
> Makamu Mwenyekiti anatakiwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Mahakama ya Rufani au ni mtu mwenye sifa ya kuwa wakili kwa muda usiopungua miaka 15.

> Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ambao hudumu kwa miaka 5.

> Mkurugenzi wa Uchaguzi ndiye Mtendaji mkuu wa shughuli za Tume ya Uchaguzi.
Viongozi wote hao wa TUME YA UCHAGUZI wanateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Swali pekee lililosalia ni je ikiwa kutakuwa na mabadiliko, ni nani atabeba majukumu ya kuwateua au watapatikana vipi katika mazingira ya sasa?
Sote tunaelewa kwamba Tume ya Uchaguzi ni kioo cha mwenendo wa demokrasia ndani ya Taifa letu. Ni mwakilishi wa uhuru wa taasisi ndani ya taifa. Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania 1977 Ibara ya 74 (6), Tume ya Uchaguzi ina majukumu yafuatayo;

👇🏻
> Kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapigakura katika uchaguzi wa Rais na Wabunge.

> Kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapigakura na uendeshaji wa uchaguzi wa madiwani.

> Kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uchaguzi wa wabunge.
> Kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

> Kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais na Wabunge.

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Goodluck 全能神的僕人

Goodluck 全能神的僕人 Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @RealHauleGluck

Mar 26
#TunduLissu asema waliompiga risasi ni Kikosi Kazi (TASK FORCE) cha Ofisi ya Rais (Dr. Magufuli) chini ya aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa DGI-TISS kwa sass Balozi Dr. Kipilimba.
@TunduALissu anasema alitarajia Rais @SuluhuSamia ataondokana na kivuli cha Rais JPM.
Comrade @TunduALissu awataja waliohusika kumshambulia.

Bw. Lissu amesema Walionipiga risasi ni Kikosi kazi kilichopo chini ya Rais kikisimasimaiwa na Mkuu wa TISS Kipilimba. Kikosi kazi kimeua watanzania wengi sana.
Kimeua watu wengi sana, Kikosi kazi hicho kilijumuisha watu wa Usalama wa taifa, Watu wa Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi. Kinaitwa kikosi kazi cha kupambana na Ugaidi na madawa ya kulevya na uwindaji haramu (Poaching).
Read 5 tweets
Mar 26
Cries of victims in Ethiopia and Yemen go unheard as the West focuses on Ukraine.

For the past one month, the entire world has been justifiably horrified by the events in Ukraine. Ever since Russia started its invasion of Ukraine in February 2022… opindia.com/2022/03/victim…
For the past one month, the entire world has been justifiably horrified by the events in Ukraine. Ever since Russia started its invasion of Ukraine in February 2022, thousands have died, and millions have become refugees leaving their homes.
The Western world has acted as one and has imposed strict sanctions on Russia while providing Ukraine with Billions of dollars worth of aid and weapons. Meanwhile, there are other conflicts around the world, including in Ethiopia, Yemen and other places,
Read 4 tweets
Mar 21
Kwa kifupi, mabadiliko hayo yalianza mwaka 1979 yaliyopelekea kuunzishwa na kuingizwa kwenye Katiba Mahakama ya Rufani baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Mabadiliko ya pili yalikuja Mwaka 1980 ambayo yalilenga kupunguza kero mbalimbali za muungano.
Mwaka huo huo kulitokea mabadiliko ya tatu ambayo yalifafanua mfumo mzima wa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, serikali yake pamoja na Baraza la Wawakilishi. Mabadiliko ya nne yalitokea mwaka 1982 yakiwa na kusudio la kuboresha uteuzi wa wakuu wa Mikoa.
Mwaka 1984 yalitokea mabadiliko mengine ya tano na kuingiza tamko la Haki za Binadamu kwenye Katiba ya Mwaka 1977. Mwaka 1990 kulitokea mabadiliko mengine mawili katika nyakati tofauti ya sita na saba na kuanzisha tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC)
Read 11 tweets
Mar 1
Juma Duni Haji: Wapinzani tusipoungana CCM itaendelea kutawala miaka 100 ijayo. Alichoongea @zittokabwe Zitto ndicho @TunduALissu alichoongea na Rais @SuluhuSamia walipokutana nchini Belgium.
Mwenyekiti wa ACT - Wazalendo mzee Juma Duni Haji amesema endapo Wapinzani hawataamka kutoka usingizini na kuungana basi CCM itaendelea kutawala kwa zaidi ya miaka 100 ijayo.
Mzee Duni amesema alichokiongea Zitto Kabwe pale Dodoma mbele ya Rais Samia ndio hicho hicho alichokiongea Tundu Lisu na Rais Samia kule Ubelgiji hivyo tofauti ni sehemu tu ya kuongelea.
Read 5 tweets
Feb 28
How many nuclear weapons does Russia have?

According to the Federation of American Scientists, Russia has a total nuclear warhead inventory of 5,977 - this is the biggest in the world.

#Russia #Ukraine news.sky.com/story/ukraine-…
In comparison, the US has 5,428 while France has 290 and the UK has 225.

The Bulletin of the Atomic Scientists says the Russian arsenal includes 4,447 warheads of which 1,588 are deployed on ballistic missiles and at heavy bomber bases.
It says there are an "approximate additional 977 strategic warheads, along with 1,912 nonstrategic warheads" being held in reserve.
Read 4 tweets
Feb 28
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amejipa madaraka zaidi katika kura ya maoni iliyofanyika siku ya Jumapili.

Tume ya uchaguzi mjini Minsk ilisema asilimia 65 ya watu walipiga kura katika zoezi hilo, wakiridhia mabadiliko ya katiba huku asilimia 10 ikipinga hilo.
Mabadiliko ya katiba yananuiwa kumpa rais Lukashenko aliyeiongoza Belarus tangu mwaka 1994, muda zaidi madarakani na kumuhakikishia kinga ya maisha dhidi ya kufunguliwa mashitaka pindi atakapoondoka madarakani na kuachana na siasa.
Mabadiliko hayo ya katiba pia yataridhia wanajeshi wa Urusi na silaha za nyuklia kuwepo nchini Belarus katika siku za usoni.
Read 4 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Don't want to be a Premium member but still want to support us?

Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(