On This Day
TWA FLIGHT 800 😭
#RIP !!
#The aviation disaster, a Europe-bound Boeing 747, Exploded and Crashed off Long Island,NY
#Thread|StoryTime
#AllpeopleDied
📜Gaddafi, SADDAM HUSEIN wahusishwa | kwa upande wa USA ulikuwa usiku usiosahaulika.
RT @omari_manyama let's go👇
#Ikiwa ni dakika 12 tu baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy (JFKIA) uliopo mjini New York, ndege [TWA FLIGHT 800] iliyokuwa ikielekea Italia kupitia Paris ililipuka ghafla juu ya Bahari ya Atlantiki na kuua watu wote 230 waliokuwemo ndani ya ndege
Tukio hili lilitokea Trh km ya Leo majira ya saa 02:31 usiku Jumatano mnamo Julai 17, 1966, ambapo ndege hiyo kubwa ya masafa marefu aina ya BOEING 747 alimaarufu TWA FLIGHT 800 ya kampuni ya Trans World Airlines [TWA] ililiripuka karibu na pwani ya Long Island na kuua watu wote.
Ndege hii [TWA FLIGHT 800] ilitengenezwa na kampuni ya @Boeing mnamo Julai 1971 nchini Marekani na kupewa usajili wa nambari N93119 Boeing 747-131. Baada ya kutengenezwa ilipewa kibali cha kuruka anga za mashariki, Lkn waliokuwa wametoa oda ya kuinunua waliahirisha ikaizwa TWA
Unaweza kuifiatilia story Hii
ktk MOVIE iitwayo #TWAFlight800 imechezwa mwaka 2013 baada ya kuandikwa na kuongozwa Kristina Borjesso ikielezea tukio zima kutokana na uchunguzi uliofanywa na CIA na FBI
Stori ya #Thread hii unaweza kuifuailia ktk
🎬MOVIE moja inaitwa #TWAFlight800 iliyotengenezwa na Kristina Borjesso mnamo mwaka 2013.
Tuendelee..
Thead hii unaweza kuifuailia ktk
🎬MOVIE inayoitwa #TWAFlight800 iliyotengenezwa na Kristina Borjesso mnamo mwaka 2013.
Tuendelee 👇👇
#KwaUfupi: Kabla ya ndege FLIGHT 800 kulipuka ilikuwa imekamilisha safari takribani 16,869 na kukaa masaa 93,303 ktk anga ikifanya kazi na ilikuwa inatumia na Engine nne aina ya Pratt & Whitney JT9D-7AH turbofan.
Tuendelee na 👇👇
Kabla ya ajali ndege nyingine [FLIGHT 881] ya kampuni hiyo hiyo ilikiwa imetua ktk Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ellinikon huko Athens Ugiriki muda mchache ndipo Flight 800 ikaanza kujiandaa na safari ktk uwanja wa ndege wa kimataifa wa JFKIA majira ya jioni saa 10:38 jioni.
FLIGHT 800 ilipangwa kuondoka JFK kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles DeGaulle saa 1:00 jioni, lkn ilicheleweshwa hadi saa 8:02 za jioni kutokana na dharula. Kuna mzigo ulikuwa ndani ktk ndege hiyo ulionekana hauna mmiliki ikabidi watangaze mpk mhusika alipojitokeza.
Abiria wote wakatangaziwa kufunga mikanda tyr kwa kuanza safari ikarudi nyuma kutokea lango Na.27 na mida ya saa 02:04 usiku. Lkn kulikuwa na marekebisho ktk engine #3, hivyo engine #1, #2, na #4 ndio ziliwashwa na saa 8:14 jioni chombo ikaanza kuachia ardhi kupaa kuelekea Paris
Ndani ya chombo kulikuwa na marubani: Kapteni Ralph G. Kevorkian (58), Steven E. Snyder (57) na mhandisi mzoefu wa ndege Richard G. Campbell (63) [wote walikuwa maveterani wakuirusha TWA Flight 800] pamoja na Oliver Krick (25) mwanafunzi aliyekuwa mafunzo ya uendeshaji ndege.
WATU wote waliokuwa kwenye ndege hiyo ni 230 raia kutoka nchi 13 tofauti, ambapo 40 walikuwa raia wa Ufaransa, 169 raia wa Marekani, wengine ni 8 raia wa Italy, 5 wa Portugal pamoja na wengine kutoka nchi za Ivory coast, Germany, Israel, Spain, Sweden na wawili raia wa Norway.
Haijawahi kutokea Marekani ilijikuta ktk wakati mgumu kutafuta chanzo cha mlipuko wa ndege.
Marekan ilitumia zaidi ya 40M Dollars kufanya uchunguzi wa tukio lile. Baadae FBI ilitoa ripoti ya uchunguzi na kusema mlipuko ulisababishwa na hitilafu ya kiufundi kwenye ndege hiyo.
Uvumi mkubwa ulienea nchini humo na kuchochea nadharia kwamba lilikuwa tukio la kigaidi na huwezi kuamini aliyekuwa Rais wa Libya kipindi hicho MUAMMAR Gadhafi pamoja na Rais wa Iraq SADDAM HUSSEIN ndio walikuwa washukiwa wa kwanza ktk tukio hili.
RT @Vet_doctor87 @balozi_twita
Wasiwasi juu yao ulisababishwa na tukio la Dec 21, 1988. Niliwahi kuwaletea #Uzi wa kikundi cha #Black_September, ambapo Pan Am 103 Flight ililipuliwa huko Lockerbie, Scotland na kuua watu wote 270 baadae Abdel Baset Ali Mohmed al Megrah (mlibya) akakutwa na hatia ya mauaji.
Mashahidi waliokuwa eneo tukio wapatao 755 walihojiwa na kutoa shuhuda zao jinsi mlipuko ulivyotokea angani usiku ule. Wachache walisema waliona kitu km kombora (roketi) kikielekea kwenye ndege kabla ya kulipuka na kuongeza dhana kwamba ndege hiyo ililipuliwa shambulio la kigaidi
Ilikuwa ni ngumu Mmarekani kuamini kwamba ndege ile ililipuka yenyewe kutokana na matukio mfuatano ya kigaidi.
MFANO ni mlipuko wa ndege Lockerbie Scotland mnamo 1992, karakana ya kituo cha biashara (1993),uwanja wa Olimpiki wa Atlanta Centennial (1996)
Msiba huo mkubwa ulitokea siku mbili tu kabla ya kufunguliwa kwa mashindano ya michezo ya Olimpiki ya msimu wa XXVI huko Atlanta, Georgia, na watu wengi walishuku ugaidi.
.
Uchunguzi uliendeshwa kitaalam ambapo karibu vipande vyote vya ndege hiyo iliyokuwa na uzito tani 170 vilipatikana pwani ya baharini na kujengwa upya kama sehemu ya uchunguzi
Ijapokuwa chanzo hasa ambacho kilichosababisha mlipuko huo hakikugunduliwa kamwe, ripoti ya uchunguzi ilihitimisha mwaka 1998 kuwa sababu ya ajali hiyo haikuwa shambulio la kigaidi, bali hitilafu ya umeme ndio iliwasha tanki la mafuta lililokuwa karibu ktk ndege hiyo.
Tukio hilo linabaki kuwa moja ya ajali mbaya zaidi za ndege kuwahi kutokea ktk historia ya Marekani.
Majina ya watu wote waliofariki yamewekwa kwenye kumbukumbu ya TWA Flight 800 International mnara wa Smith Point County Park huko Long Island, New York.
Na iliwekwa wakfu Julai 14, 2004, na kujumuisha bendera kutoka nchi 13 waathiariwa.
Shirika la Usafiri wa anga (NTSB) Julai 7, 2021 miaka 25 baada ya ajali hiyo ilitangaza kuondoa mabaki ya ndege hiyo na mwaka 2022 itajenga kituo cha Skena 3-D kwa ajili kumbukumbu ya kihistoria.
**Typing Error
Mnamo Julai 17, 1996
Share this Scrolly Tale with your friends.
A Scrolly Tale is a new way to read Twitter threads with a more visually immersive experience.
Discover more beautiful Scrolly Tales like this.