Umekua furaha yangu kila nikikuona ukipita mwenyewe au na wenzio, umekua my mood changer maana nawezakua naskiliza reggae lakini ukipita tuu nahisi nachosikiliza ni blues.
Unaniweza sana dear crush maana simu yangu imejaa screenshots nyingi za picha zako
Huwezi amini umetawala kichwa changu nakumbuka ile siku tumekutana ulivonambia nimependeza ilibidi nipite dukani kwa Mangi ninywe soda kwa kujipongeza 😁
My dear, msonyo wako kwangu naona kama busu
Nakionea wivu kioo chako ambacho kila siku wajitazamia, nadhani kila siku vinabishana na chanuo la nywele zako jinsi kioo kinafaidi kuliko wenzie
Angalia, nilidhani napenda cheko lako mpaka pale nilipoona mwendo wako, nilihisi unaigiza kumbe ndio tembea yako wewe si Animalia ,wewe si Plantae, wala si Fungi nadhani Biologist wakutafutie kundi lako ❤
Umekua Ummy Mwalimu wangu unaetoa Updates za new cases za hisia zangu kwako na number of deaths za zile sababu zinazoashiria mimi kutokukupata. You're amazing
Nadhani hizi hisia zangu ni za kweli kwako, kuna wakati nahisi ilibidi wewe utokee,ilibidi mimi nipitie haya ili mwisho wa yote nikupate
"Tafuta hela" ndio majibu ninayopata kwa washkaji kila nikiwaeleza jinsi umeuteka moyo wangu. Nawakatalia maana wewe ni roho unaestahili kupendwa na sio kitu kinachostahili
Sijiwezi kwako mpaka ukinipiga bluetick natamani nikwambie " thank you for this blue "
Cute,sitaki unipendee huruma nachotaka tumia mzani wa hisia upime kiasi na uzito wa mapenzi