My Authors
Read all threads
#UZI
💨 KISANGA CHA TIK TOK

✴️ Hii ni app iliotengenezwa na Zhang Yiming huko Beijing, China.

✴️ Imetengenezewa China lakini China imewazuia raia wake kuitumia.

✴️ Marekani, India ni baadhi ya nchi zilizoikataa.
#FLowMaTaTa tiririka nazo 👇👇 ImageImage
✴️ Huu ni mtandao wa kijamii wenye uwezo wa kutengeneza kusambaza video.

✴️ Unatumika kutengeneza video za kuchekesha, kucheza na za kuonyesha vipaji.

✴️ Hii app ya TikTok inamilikiwa na kampuni ya ByteDance iliyoanzishwa 2012 na Bw. Zhang Yiming.

✴️ 2017 ikatuletea hii Image
App ya TikTok katika simu za iOS na Android, soko lao kubwa likawa ni nje ya China.

✴️ Wana ofisi zao Los Angeles, New York, London, Paris, Dubai, Mumbai, Tokyo na miji mingine maarufu.

✴️ 2018 TikTok iliongoza kupakuliwa nchini Marekani, ikawa ni app ya kwanza kutoka Image
China kupata alama nyingi ugenini.

✴️ Mwaka huo huo ikawa inauwezo wa kuchakata lugha 75.

✴️ Feb 2019 ikawa ishapakuliwa na watu zaidi ya bilioni 1 duniani kote, isipokuwa raia wa China. Image
✴️ Takwimu zikaonyesha TikTok imekamata nafasi ya 7 kwa app zilizopakuliwa kati ya 2010-2019.

✴️ Kwa Marekani pekee imepakuliwa zaidi ya mara milioni 80, na duniani kwa ujumla ni zaidi mara bilioni 2. Image
✴️ Watu maarufu kama Jennifer Lopez, Will Smith, Justin Bieber, Jimmy Fallon na wengine wengi wakajiunga na TikTok.

✴️ Marekani, 52% ya watumiaji wa TikTok wanatumia iPhone.

✴️ Pia kwenye jinsia 44% ni wanawake huku 56% ni wanaume. Image
KWANINI HII APP INATILIWA MASHAKA?
✴️ Makao makuu ya hii app yapo Beijing, China. Lakini cha kushangaza serikali ya China imeifungia hii app.

✴️ Hairuhusiwi kutumia hii app ukiwa China, ila baadhi ya watu wanatumia VPN kuipumbaza mifumo ya mawasiliano China. Image
✴️ Ukiuliza ni kwanini China wameamua kufanya hivi, utaambiwa ni sababu za kiusalama.

✴️ 2019 Raisi wa Marekani Donald Trump naye akawakataza wanajeshi wa Marekani kutumia TikTok.

✴️ Kwamba inatumiwa na serikali ya China kudukua taarifa za watu. Image
✴️ China ni taifa lenye wapinzani wengi sana kibiashara.

✴️ Huko Australia, Scrutiny waliamua kuiweka TikTok chini ya himaya yao.

✴️ Kujua Kama ni kweli wanaiba taarifa za watu. Kitengo kikubwa cha ulinzi wa mtandao huko Australia kilianza kuchunguza mamilioni ya Image
Akaunti zinavyo-angaliwa na Beijing.

✴️ Fergus Ryan, huyu ni mchambuzi katika Australian Strategic Policy Institute (ASPI),

✴️ Alisema hii TikTok ni kama Facebook na Instagram.

✴️ "Taarifa zote zinazokusanywa kwenye hizi apps zinatuhusu sana". Image
✴️ Apps nyingi za mitandao ya kijamii zinakusanya taarifa za watu binafsi.

✴️ Kama camera ya simu, microphone, namba zote za watu zilizo kwenye simu yako na Sehemu ulipo. Image
✴️ Andrew Hastie huyu ni Federal MP huko Australia aliwaambia ABC New 👇

✴️ "Sheria ya Usalama wa Taifa la China ya 2017 inasema Serikali ya China ina haki ya kupata taarifa kwenye biashara yako" Image
✴️ "Kwaiyo, Nina shaka kama taarifa zetu zinatuzwa na kampuni iliyopo China"

✴️ "Watumiaji wakubwa wa TikTok ni vijana wadogo lakini ndio viongozi wa kesho". Image
✴️ "Viongozi wetu wa baadae wa kisiasa, kiuchumi na kijeshi tunahitaji kulinda taarifa zao kwa muda mrefu"

✴️ Ikabidi watu wa vyombo vya ulinzi vya Australia wazuiwe kutumia hii app. Image
✴️ Jun, 2020 India kama nchi wakafanya mdahalo (debate) kuhusu tabia na mienendo ya China.

✴️ India ikakubaliana kuzifungia apps 58 za China pamoja na TikTok.

✴️ Pigo kubwa limekua kwa TikTok Maana wamepata harasa ya dola bilioni 6. Kwa mujibu wa Forbes. Image
✴️ CEO wa TikTok Kelvin Mayer akaiambia India "Nitathibitisha kuwa serikali ya China haiwezi beba taarifa za watu wa India".

✴️ Kwa mujibu wa vyombo vya habari huko China inaonyesha ByteDance imewekeza zaidi ya dola bilioni 1 kutengeneza user base ya watu wa India. Image
✴️ Unaambiwa India imeifungia TikTok baada ya Secretary wa Marekani MIKE POMPEO kwenda kuwashawishi "clean app". Image
✴️ June, 2020 pia taarifa nyingine zitatolewa kwamba TikTok inaiba taarifa za watu wanaotumia iPhone.

✴️ Kampuni kubwa zilizopo China zinapitia kipindi kigumu sana kutokana na hii sheria ya China 2017. Image
✴️ Kwa simu kali, laptop n.k Wacheki @BongosmartTz

✴️ Hawa jamaa wapo njema sana, wapo Kinondoni Morocco & Kko City Centre pia wanatuma hadi mikoani kwa umakini sana. ImageImage
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Njiwa FLow 🇹🇿

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!