My Authors
Read all threads
💨 YAHOO BOYS
💨 VIJANA HATARI WA NIGERIA

▫️Ni wanachuo na vijana wengine wanaofanya Utapeli mtandaoni.

▫️Mtaji wao ni Komputa na hirizi. Unamkumbuka HushPuppi vizuri?

▫️ Tatizo lao wanakamatwa kama kuku na hawaishi huko mtaani.
#FLowMaTaTa tiririka nazo 👇👇
▫️Yahoo Boys ni wanafunzi wa vyuo vya Nigeria walioamua kujitafutia kipato mtandani kwa njia za udanganyifu.

▫️Wengi wakianza shule huishia katikati na hata kumaliza.
▫️Hawa vijana huwa wana kasumba ya Kuinuana mmoja akipata sehemu yenye dili anaenda kuwachukua masela zake wote kitaa na kuwapa mchongo.

▫️Wanatumia mbinu kama 419 Nigeria kuwaibia watu huku mtandaoni.
▫️Wapo katika vikundi mbalimbali; Kuna wanaoanza, Kuna walio daraja la kati alafu kuna hawa Yahoo boys waliotoboa.

▫️Hawa jamaa wana hela namaanisha hela sio za kitoto.

▫️Ogopa mtu anaanza kazi akiwa na komputa na mahirizi pembeni ili atapeli vizuri na asikamatwe 😁😁
▫️Huko Nigeria huwaga wana mtindo wa kuwapambanisha kwamba nani mwenye mpunga mrefu zaidi ya mwenzake.

▫️Mfano Davido aliyechangamka na Yahoo boy mmoja aliyechangamka.

▫️Matajiri wakubwa ni Hush Puppi, Naira Marley, Shy Boss, Mompha, Opa6ix, B Naira na Deskid Wayne.
▫️Utapeli wanaoufanya huangalia ni sehemu gani wataweka kambi. Hujifunza namna ya usalama wa kimtandao.

▫️ Mfano kwenye online transaction hapa ndio "Yahoo boys" hutumia mbinu tofauti tofauti.
▫️Hutuma ujumbe wa udanganyifu kwenye websites za watu na Social media.

▫️Hawa vijana hutumia mbinu nyingi kuweza kupata username, password na kadi za benki.
▫️ Mifumo isiyo rasmi ya kupokea pesa imekua furaha kwa hawa vijana. Pesa zao nyingi hupitia kwenye Western Union.

▫️ Wafanyakazi zaidi ya 2,000 wamepoteza ajira zao kwenye mabenki kutokana na mfumo mbovu wa fedha na kuporomosha uchumi.
▫️Mara nyingi Yahoo Boys hufanya scam zao kwenye internet cafe ili wasijulikane.

▫️Cafe nyingi zimepata tabu sana dhidi ya polisi. Tatizo la Yahoo Boys wanakamatwa sana kizembe👇👇
Twende Chap Chap
▫️ April. 2012, Kuna Mwamba mwanafunzi wa chuo cha Olabisi Onabanjo huko Nigeria alitungwa kifungo cha miaka 5 kwa Uhalifu wa kimtandao.

▫️June, 2012, Mahakama ya Kaduna ikamfunga Imonina Kingsley wa Chuo Cha Ilorin, kifungo cha miaka 20.
▫️Huyu Mwamba alimdaganya raia wa Australia kwamba yeye ni shoga kutoka Benin.

▫️Akampiga Muustralia dola 1,000, akahukumiwa kwa kosa la kuiga, kumiliki nyaraka za udanganyifu na kujaribu kupata pesa kwa udanganyifu na uongo.
▫️Hizi kesi ndizo zinaendelea kwenye vyuo vikuu vya Nigeria mpaka leo.

▫️Hasa Chuo Cha Ibadan yaani mzazi akisikia mtoto wake anasoma huko anaona tayari maisha yashakaa kwenye mstari.
▫️Jan. 2019, Ofisa wa Ibadan wakafanikiwa kumkamata mtu mzima Stanley Awam(38) kiongozi wa kikundi.

▫️Pamoja na wanzake 10 wa "Yahoo Boys" katika sehemu tofauti tofauti. (Via The News Nigeria).
▫️Feb. 2019, huko huko Ibadan Wakakamatwa wengine tena 14 wakapewa kesi ya Cyber crimes.

▫️Walikutwa na gari 2, line 100 za mitandao tofauti, laptops, simu, international passport na documents nyingi za uongo. (Via Lailas News).
▫️April. 2019, Yahoo Boys wengine 11 wakakamwata na polisi.

▫️ Point ni zile zile Uhalifu kwa kimtandao ushahidi ni laptops 😁😁

▫️Hawa jamaa walikutwa na simu na documents nyingi sana huko Ibadan. (Via Pm News Nigeria).
▫️June. 2019, Wakakamatwa tena wengine 2. Hawa jamaa Johnson Okuselu, 23 na Saheed Olanrewaju, 25.

▫️ Walikua kwenye uwanja wa ndege wa Ilorin, huyu Okuselu ashawai jifanya parody wa kike wa Kiamerika.

▫️Walihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja. (Via Elendu Report).
▫️Oct. 2019, Wakakamwata wengine 18 tena huko Lagos katika mitaa tofauti.

▫️Kuna 5 waliojaribu kutoroka kwa kukimbilia kwenye dari, ila haikusaidia Wakakamatwa. (Via Pm News).
▫️Nov. 2019, Mother of Yahoo Boys akakamatwa na polisi na kupelekwa gerezani.

▫️ Walikamatwa pia vijana wengine wengi waliokua pamoja kwenye huo msala.

▫️Huyu Mwanamama ndio alikua Association wao, alisema Yetunde Longe, DC Police.
▫️March. 2020, Kuna Mwamba alikamatwa akiwa na kigeneza kidogo kilichokua kimebebea vitendea kazi.

▫️Alikua na wenzake watano hawa mijamaa kazi yao ilikua ni kujichote fedha mitandaoni.
▫️Ndani ya wiki hiyo alikamatwa pia Mwanadada Toyinsola.

▫️Vitu walivyokutwa navyo ni magari 4, simu na ATM card. (Via Kanyi Daily).
▫️June. 2020, Wakakamatwa tena wengine 24 huko Ibadan.

▫️Nikiweka idadi ya waliokamatwa hatutamaliza leo. Hii ndio Nigeria Dunia nzima inaelewa.

▫️ Marekani kama Kiranja huwa anakusanya sana anadili na Mabroo, mtu kama HushPuppi aliyekamatiwa Dubai. Uzi wake huu 👇👇
▫️Huwa wanawawinda kwenye social media maana Hawa Yahoo Boys wanafanya sana matanuzi.

MWISHO

Sio kila Picha inaendana na tukio.

Written by @njiwaflow
Naombeni msisahau ku-Retweet 🙏
💨 Uzi wa HUSH PUPPI HUU HAPA 👇👇

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Njiwa FLow 🇹🇿

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!