My Authors
Read all threads
MPANGO WA BIASHARA (BUSINESS PLANNING)

Mpango wa Biashara (Business Plan), ni nyenzo muhimu katika mafanikio ya biashara. Mpango wa Biashara humsaidia mjasiriamali ku-shape wazo lake la biashara na kulifanya kuwa fursa (Opportunity).
FAIDA ZA KUWA NA MPANGO WA BIASHARA
Hutoa taarifa za msingi juu ya biashara; zinazomuwezesha mjasiriamali kutafuta vyanzo vya fedha kwa ajili ya kuendeshea biashara.
Huweza kutumika kwa ajili ya kuvuta rasilimali watu.
Humsaidia mjasiriamali katika kutafuta na kupata mshirika/washirika katika biashara (Strategic Partiner)
Mpango wa Biashara hupaswa kujikita katika maeneo ya msingiya mfumo wako wa biashara (business model) na kutoka hapa ndipo tunapata mtindo au "format" ya Mpango wa Biashara.
Busara (wisdom) ni kuamini kwamba Mpango wa Biashara ni nyaraka iishiyo "living document" maana ya dhana hii ni kwamba; kadiri siku zitakapokuwa zinakwenda, Mpango utakuwa unahuishwa kutokana na mabadiliko ya kimazingira katika biashara.
MTIRIRIKO/MUUNDO WA MPANGO WA BIASHARA/BUSINESS PLAN FORMAT

(A) THE COVER
Sehemu hii; inapaswa kujumuisha JINA LA KAMPUNI, MTU WA KUWASILIANA NAE (CONTACT PERSON), ANUANI, n.k

Kumbuka kwamba, vipengele hivii vinapaswa kuelezewa kiundani zaidi katika sehemu za mbele.
➡️Ufafanuzi juu ya fursa(Description of Opportunity)
➡️Dhana ya biashara(Business Concept)
➡️Hali ya biashara(Industry Overview)
Soko lengwa(Target Market)
➡️Faida ya kiushindan(Competitive Advantage)
➡️Mtindo wa biashara
Team
➡️Muhtasari wa masuala ya fedha (Financial Snapshot)
(C) TABLE OF CONTENTS
Hii ni sehemu muhimu pia katika Mpango wa Biashara, na ni ramani "road-map"; kwa maana ya kwamba inaonyesha "major sections/sub-sections" za Mpango wa Biashara
(D) INDUSTRY, CUSTOMER AND COMPETITOR

Industry: Lengo la sehemu hii, ni kuelezea fursa na namna utakavyo ikumbatia (capturing). Pia unapaswa kuelezea aina na ukubwa wa soko kwa wakati husika na namna unavyotaraji ukuaji wa soko hilo. Historia inatuonyesha kwamba;
fursa (best opportunities) hupatikana zaidi katika masoko yanayochipukia (emerging markets). Kwa mfano; miaka ya 1980 soko la kompyuta (Personal Computers) lilianza kuchipuka, hivyo likapelekea uwepo wa makampuni kama Apple, Microsoft, Intel n.k.
Pia katika miaka ya 1990 soko la mtandao (Internet) lilianza kuchipuka, hivyo likapelekea uwepo wa makapuni kama Google, Facebook, eBay n.k

Customer: Baada ya kuwa umeainisha sehemu yako ya soko (market space) unayotaraji kuiingia, ni wakati sasa wa kufanya
uchambuzi wa kina juu wateja wako (examining your customers' details). Uchambuzi wa wateja unapaswa kuzingatia kipengele cha saikolojia na makundi ya watu (psychological and demographic factors).
Fahamu kwamba kadiri unavyozidi kuwachambua wateja wako, ndivyo uwezekano wa kuwapelekea bidhaa wazitakazo unakuwa mkubwa,.epuka kuwa na dhana ile isemayo KILA MTU MWENYE NJAA BASI ATAKUWA MTEJA KATIKA MGAHAWA WAKO.
Competition: Tayari umeshatambua soko lako (market segment) , umekusanya taarifa za kina za wateja wako (customers' profile) pia umejua ni nini hasa wateja wako wanahitaji. Kinachofuata nikuangalia kwa namna gani mshindani wako, anatimiza mahitaji ya wateja husika.
Hapa utakuja kujua udhaifu wake (weaknesses) na umadhubuti wake (strengths)
COMPANY AND PRODUCT DESCRIPTION
Katika sehemu hii, utapaswa kutoa maelezo juu ya kampuni yako ikijumuisha jina la kampuni, mahala ambapo kampuni imesajiliwa, lakini pia na sheria iliyotumika kusajili kampuni hiyo, pia utapaswa kuelezea dira na malengo ya kampuni yako..
Mbali na uelezaji wa taarifa za kampuni; sehemu hii pia hutoa maelezo juu ya bidhaa/huduma zako, katika bidhaa/huduma, utapaswa kuelezea sifa za bidhaa/huduma yako (features) pia utofauti uliopo kati ya bidhaa/huduma yako dhidi ya za wengine.
MARKETING PLAN
Katika sehemu hii, unapaswa kuonyesha ni kwa namna gani utaingia katika soko, lakini pia mbinu gani utazitumia katika kukuza biashara yako na hatimaye kufikia malengo uliyojiwekea. Sehemu hii; kimsingi inapswa kujumuisha mbinu zifuatazo;
Mbinu juu ya soko lengwa (Target Market Strategy)
Mbinu juu ya bidhaa/huduma (Product/Service Strategy)
Mbinu juu ya bei (Pricing Strategy)
Mbinu katika usambazaji wa bidhaa/huduma (Distribution Strategy)
Mbinu za mawasiliano kimasoko
Mbinu katika mauzo (Sales Strategy)
OPERATIONS PLAN
Sehemu hii inapaswa kuonyesha namna shughuli za biashara zitakavyoongeza thamani kwa wateja wako. Mbali na hivyo; sehemu hii pia inapaswa kuonyesha muda ambao kampuni itatumia katika uzalishaji wa bidhaa/huduma.
DEVELOPMENT PLAN
Katika sehemu hii,utapaswa kuonyesha mbinu katika uendelezaji na ukuaj wa biasharai yako.Katika sehemu hi utapaswa kuja na "Development Strategy" ambayo itazingatia "risks" ambazo biashara inakutana nazo,vitu vinavyopaswa kuwepo ili kutokee maendeleo ya biashara
TEAM
Hapa unapaswa kuonyesha timu ya rasilimali watu ambayo inahitajika katika kuhakikisha malengo ya biashara yako yanatimia. Ni vyema ukachagua watu wenye sifa stahiki na wenye ubunifu. Katika kampuni nyingi, muanzilishi mara nyingi hujipa cheo cha CEO.,
ikiwa wewe kama muanzilishi huna uzoefu wa kutosha au labda unamajukumu mengine, basi ni vyema ukamtafuta mtu mwenye uzoefu akakalia nafasi ya u-CEO.
CRITICAL RISKS
Biashara yoyote hukabiliwa na vikwazo au hatari, ili biashara yako iweze kusonga mbele, ni vyema hatari katika ukuaji wa biashara yako (risks) zika-ainishwa na kisha ukatengenezwa mpango wa kukabiliana nazo "Risk Mitigation Measures".
FINANCIAL PLAN
Hapa ndipo kulipo na uti wa mgongo au sehemu ya msingi zaidi katika Mpango wa Biashara, hususani Mpango huo unapotarajiwa kutumika kwa ajili ya kutafuta mtaji. Sehemu hii huonyesha makisio ya mapato na matumizi ya biashara yako.
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Mbwambo

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!