My Authors
Read all threads
BERMUDA TRIANGLE
Ijue Bermuda triangle na matukio mengi ya kusaajabisha juu ya Bermuda 🇧🇲 triangle

Chukua popcorn 🍿 kabisa shuka na huu uzii mpaka mwisho
-THREAD-
🔁Retweet iwafikie wengii
#FunFact

#FunFactFriday #wapwatuinuane
Bermuda Triangle ni eneo la Bahari ya Atlantiki pande zote mbili za ikweta mbele ya pwani ya Amerika Kaskazini, baina ya Florida, Puerto Rico na visiwa vya Bermuda.
Tangu mwaka 1964 jina la "pembetatu ya Bermuda" lilibuniwa na kusambazwa na waandishi wa habari wakijaribu kueleza kupotea kwa boti, meli na ndege katika eneo hili
Bermuda Triangle,ambayo pia inajulikana kama Devil's Triangle,ni eneo la magharibi wa bahari ya Atlantiki ya kaskazini ambapo idadi kubwa ya ndege na vyombo vya baharini vinanadaiwa kutoweka katika hali isiyojulikana ambayo haiwezi kuelezewa kama,hitilafu ya vifaa, maafa ya asili
Tamaduni maalufu zinahusisha kutoweka huku na jambo lisilo la kawaida ambalo haliwezi kuelezewa kwa njia za kisayansi, kutanguliwa kwa sheria za fizikia, au shughuli za viumbe visivyo vya kawaida.Jisomee hapa chini baadhi ya maajabu ya eneo hili
👇👇
1. Bermuda triangle ni eneo katika uso wa Dunia ambalo linahusishwa na masuala mbalimbali ya nguvu za maajabu, ni eneo ambalo maelfu ya watu wamepoteza maisha, ndege na meli nyingi sana zimezama katika eneo hilo pasipo kujulikana zinaelekea wapi.
Wanasayansi wengi wamepoteza pesa zao pasipo kutoa majibu kuhusu maajabu ya eneo hilo na kila aliyeenda hajafanikiwa kutoka na inasemekana Zaidi ya ndege na meli 1000 zimepotea kwa mud wa miaka 500.
2. Bermuda Triangle inapatikana pwani ya kusini mashariki ya marekani na iko katika bahari ya Atlantic. Kona zake huunda pembe tatu ambazo ni Miami huko marekani, San Juan Nchini Puerto Rico na Buermuda katika kisiwa kaskazini mwa kisiwa cha Atlantic.
3. Ajali/mgongano kati ya kimondo na dunia
Inasemekana kuwa Bermuda triangle ilitokea baada ya Dunia kugongana na kimondo huko angani miaka 11,000 iliyopita. Mgongano huo ulitokea katika eneo la bahari la Dunia na kusababisha bahari kuzama kwa futi 10,000 chini ya usawa wa bahari
Kimondo hicho kiliacha mionzi ambayo ambayo husababisha ndege kupoteza uelekeo inapofika katika eneo hilo na kuzamsha meli, ndege pamoja na binadamu.
4. Viumbe vigeni viishivyo sayari nyingine (aliens).
Inasemekana kuwa viumbe viishivyo angani, huwa vinakaa aktika eneo hilo la Bermuda triangle na hilo ni kama Mecca yao. Viumbe hao wana teknolojia ambayo hukinzana na teknolojia yetu ya Duniani,
kwahiyo basi ndege, meli pamoja na binadamu wanapopita pale huvutwa na kani ya uvutano ambayo ni kubwa sana toka kwa wale viumbe waishio katika ilo eneo hilo la bermuda.
5. Kituo cha majaribio ya silaha.
Inasemekana serikali huwa zinajaribia silaha ambazo zinakuwa zimetengenezwa na uangalizi wa silaha hizo, pia inasemekana kwamba serikali ikishirikiana na viumbe watokao sayari (Aliens) zingine huhusika katika majaribio hayo.
Na hiyo teknolojia ni kubwa kiasi cha kukinzana na teknolojia ya duniani na hatimaye kusababisha madhara kwa meli na ndege pia.
6. Mji uliopotea
Inasemekana katika eneo hilo kulikuwa na mjia wa kale chini ya maji katika bahari ya Atlantic, ulioitwa Atlantis, mji huo ulikuwa umejengeka kwa barafu ambazo zilikuwa kama kioo ambazo pia zilikuwa ni chanzo cha nishati.
Na huo mji ulisahaulika milele kwahiyo basi Bermuda iko kwenye huo mji uliozikwa kitambo ambapo kuna kani kubwa ambayo huharibu meli na ndege
7. Kituo cha Maharamia
Inasemekana Bermuda ni eneo kwa ajili ya maharamia kufanya kazi zao, maharamia hao ni wale wanaojulikana kwa bend-era nyeusi zenye picha ya fuvu. Lakini dhana hii imeshindwa kuelezea ni kwanini ndege na meli huwa zunapotea katika eneo hilo kwani
wachunguzi wa mambo wamehusisha na utekaji nyara wa meli baharini ambao hufanywa na maharamia hao.
8. Volkano.
Inasemekana Volkano pamoja na gesi ya methane katika eneo la Bermuda hupunguza mgandamizo wa maji katika eneo hilo na kufanya meli kupoteza uwezo wa kuelea na hatimaye kuzama. Eneo hilo mlimekuwa likitoa gesi hiyo ya Methane tangu miaka 15,000 iliyopita.
9. Ukungu wenye hali ya ki-electronic na sumaku
Ukungu wenye nguvu ya kuzalisha umeme ambapo husababisha dira hupoteza uelekeo na kuwachanganya marubani pamoja na manahodha. Na hatimaye ndege pamoja na Meli hizo hupotelea katika ilo eneo la Bermuda.
10. Mawimbi na hali ya hewa kubadilika kwa kasi.
Eneo la bahari ya Atlantic hasa upande wa Caribbean hukumbwa na kimbunga kikali pamoja na mawingu mazito, Bermuda ni eneo ambalo limepakana sana na Caribbean na hukabiliwa na upepo na wingu zito
ambavyo husababisha mushkeli kwa ndege, meli pamoja na binadamu.Upepo huu husababisha meli na ndege kushindwa kufanya safari zake vizuri na kupotea kusiki julikana
Matukio ya kupotea kwa meli na ndege yaliyohusishwa na bermuda Triangle
➡️ 1. Star Tiger and Star Ariel
Tiger ya G-AHNP Star ilipotea mnamo Januari 30, 1948, kwa ndege kutoka Azores kwenda Bermuda;
G-AGRE Star Ariel ilipotea mnamo Januari 17, 1949, kwa safari ya ndege kutoka Bermuda kwenda Kingston, Jamaica.
Zote mbili zilikuwa ndege za abiria za Avro Tudor IV zinazoendeshwa na Airways ya Amerika Kusini.Ndege zote mbili zilikuwa zikifanya kazi kwa mipaka ya anuwai na kosa au kosa kidogo katika vifaa vinaweza kuwazuia kufikia kisiwa kidogo.
@mpambazi_ @kellenMbwambo @itsjaqie @Happie_Thom @RehemaTanzania please naomba retweet zenu iwafikie wengi
@abdulazackabdul retweet yako muhimu uzi huu uwafikie wapwa wote jamuhuri ya wapa
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Mbwambo

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!