My Authors
Read all threads
Pata Elimu ya kutosha kuhusu "Hisa" na Namna ya Kumiliki hisa katika Kampuni.

Watu wengi wamekuwa wakitamani kufanya biashara au shughuli yoyote ambayo itakuza kipato chao, lakini wengi wao hukatishwa tamaa jinsi gani ataweza kusimamia biashara hiyo.

🔁RT
#Elimikaweekend
Changamoto ya usimamizi wa biashara ni kubwa sana kwa watu wengi hasa wale ambao ni wafanyakazi serikalini na kampuni binafsi.
Na wengi ambao wamejaribu kufanya biashara wameshindwa kutokana na usimamizi mbovu wa biashara zao. Wengi wanatamani kukuza vipato kwa njia nyingine.
Uwekezaji katika hisa ni suluhisho kwa wale wote ambao wanakutana na changamoto ya muda wa usimamizi wa biashara zao. Uwekezaji katika hisa ni rahisi, unahitaji muda mdogo wa usimamizi, unakua na kuongeza kipato kwa mwekezaji.
Yawezekana wengi hawafahamu kuhusu Hisa, Umuhimu wake na vitu vya kuzingatia kabla ya kununua hisa, mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa makala zetu katika Blog yetu ya Fumbuka karibu katika makala hii tuweze kujifunza hayo.
Nini Maana ya Hisa?

Wengi miongoni mwetu wamekuwa wakitaka kujua HISA ni nini, shauku hii imenifanya nidodose kidogo juu ya hisa kwa faida ya wengi. Kwa tafsiri lahisi HISA NI UMILIKI.
Kwa kifupi kuwa na hisa ni kumiliki sehemu ya kampuni au kuwa mmiliki wa kampuni hiyo kwa maana hiyo unakuwa na nafasi ya kushiriki kufanya maamuzi, kupata faida au hasara katika kampuni hiyo.
Mtu akisema nina hisa NMB anamaanisha ana miliki NMB. Umiliki huu unajionyesha wazi na bayana wakati wa kufanya maamuzi na kugawana gawio (faida). Mwenye hisa nyingi huwa na sauti au ushawishi mkubwa katika kufanya maamuzi na hupewa gawio kubwa kwa uwiano wa hisa zake.
Mfano-
Kampuni yaweza kuwa na hisa 1000, ikaamua kuuza hisa 500 na hisa 500 zikabaki akiba. Wale watakaonunua hizo hisa 500, wanakuwa wametoa mtaji kwa kampuni na kwa maana hiyo ndio wamiliki.
Mwenye kuweza kununua hisa 251 atakuwa amenunua hisa nyingi zaidi kuliko yeyote na anakuwa na nguvu ya maamuzi katika vikao na gawio atapata kubwa kwa sababu ndie aliechangia mtaji mkubwa.
Nawezaje Kununua Hisa Katika Soko la Hisa?

Unaweza kununua hisa katika soko la Hisa la Dar es salaam kupitia mawakala wake (Brockers) au kupitia Benki ya CRDB ukiwa mkoa wowote ule hapa Tanzania.
Unaweza pata taarifa zaidi kupitia website ya soko la hisa la Dar es salaam dse.co.tz
Wasiliana wakala utapata utaratibu wowote jinsi ya kununua hisa. Unachotakiwa kuwa nacho ni pesa yako kwa ajili ya kununua hisa, akaunti yako ya benki na mawasiliano ya Mawakala
Mambo gani ya kuzingatia kabla ya Kununua Hisa?

Kabla ya kununua hisa ni vyema ukaangalia mambo yafuatayo;
1. Performance ya kampuni.

Kampuni kama inafanya kazi vizuri kwa weledi na inamategemeo ya ukuaji wa kampuni hiyo kama kutanua matawi, kuongeza product au kukua kwa biashara katika kampuni hiyo basi hiyo ni kampuni nzuri.
Mfano;- Ukisikia kampuni imetanua soko lake kama CRDB ilivyofungua matawi nchi za nje inamaana ya kuwa faida ya kampuni hiyo itaongezeka na hivyo gawio linaweza kuwa kubwa na wewe kupata faida na pia bei ya hisa itaweza kuongezeka hivyo utapata faida pia pindi ukiamua uza hisa
2. Bei ya hisa na uimara wake (stable share price)

Kuna kampuni ambazo bei zao za hisa wakati wote ni nzuri kwa maana hazishuki sana au mara kwa mara na pia zina tabia za kuongezeka mfano;- TBL, SWISS PORT, TCC.
3. Wakati wa kununua hisa

Ni muhimu pia kuangalia ni wakati gani unanunua hisa, mfano wakati ambao hisa ndio zinaingizwa au kuuzwa kwa mara ya kwanza kwenye soko la hisa bei huwa ni ndogo sana na baada ya hapo mara nyingi bei huongezeka ingawa kuna wakati hushuka pia.
Lakini bei ya hisa hupanda kushuka kutokana na nyakati katika mwaka mfano ifikapo mwishoni mwa mwaka na mwanzoni mwa mwaka bei hushuka na kuwa ndogo zaidi ila katikati ya mwaka bei huanza kupanda kwa kasi kubwa zaidi
4. Uwepo wa taarifa nzuri katika Kampuni.
Ie imekuwa ikisikika kuwa benki ya xX itakuwa inatumika kulipia mishahara ya baadhi ya wafanyakazi wa serikali basi siku ukisikia imeingia mkataba huo au imeanza kutumika kulipia mishahara hiyo basi nenda kanunue hisa hizo
5. Wingi wa makampuni katika soko la hisa.

Mfano kuna mabenki zaidi ya matano hii inamaana benki hizi zinagombea wateja hii ni kwa wateja wote wale wanaowahudumia na wale wa kwenye soko la hisa hivyo bidhaa zao zipo za kutosha na bei itakuwa ya kawaida mambo ya demand na supply
Faida za Hisa
1. Gawio
Ukiwa miliki wa hisa utapata gawio ikiwa Kampuni itapata faida katika kipindi hicho cha mwaka na wanahisa wakaridhia utoaji wa gawio. Gawio hutolewa mara mbili au moja kwa mwaka kutokana sera ya kampuni na maamuzi ya wanahisa
2. Ongezeko la thamani

Wanahisa pia huweza kupata faida itokanayo na ongezeko la thamani iwapo bei ya hisa itaongezeka kwenye soko la hisa. Ikiwa ulinunua hisa moja kwa Tsh 800 na baada ya mwaka hisa hizo sokoni zikauzwa kwa Tsh 1,400 basi unakuwa umepata ongezeko la
thamani ya shilingi 6,00 kwa kila hisa. Hii ni faida tofauti na gawio, ikiwa utawekeza katika kampuni nzuri utapata gawio na ongezeko la thamani ndani ya mwaka mmoja.

3. Dhamana
Hisa kwa mwekezaji anaweza kuzitumia kama dhamana anapohitaji kupata mkopo.
4. Huokoa muda wa usimamizi
Ni uwekezaji ambao humpatia mwekezaji uhuru wa kufanya shughuli nyingine na kwa wale ambao hawana muda wa usimamizi katika biashara huu ni uwekezaji mzuri kwao

5.Ni mali inayohamishika kwa urahisi

6. Akiba
Njia ya kujiwekea akiba
7. Ushiriki wa jamii katika Uchumi
Huongeza ushirik wa jamii katika shughuli za kifedha na kukuza uchum

Napata Hasara gani nikimiliki Hisa?

Hasara ni pale unapokuwa na hisa chache kwani unakuwa kama unasindikiza wengine.Gawio unapata dogo na unakuwa huna ushawishi katika maamuz
Hasara nyingine ni pale kampuni inapofanya vibaya, thamani ya hisa hupungua, waweza nunua hisa 1 kwa tsh 1000 ukauza 500 au hela zako zikazama. Ni vyema kupata ushauri wa kitaalamu kabla ya kununua HISA.
AINA ZA HISA.
Hisa sio hisa kama wengi tunavyojua isipokuwa hisa zina aina zake.Sio kila mwenye hisa ana hisa isipokuwa ana hisa gani au za aina gani.Aina za hisa za mtu katika kampuni ndio humwezesha kujua ana haki na wajibu gani katika kampuni.
Kwa hiyo haki, wajibu(duty) na uwajibikaji(liability) katika kampuni hutofautiana kutoka mwanahisa mmoja hadi mwingine kutokana na aina za hisaanazomiliki. Wanahisa wote hawana haki sawa, na hawawajibika sawa pamoja na kuwa katika kampuni moja.
Hapa chini tutaona aina za hisa
a) HISA ZA WAMILIKI ( EQUITY SHARES).
Hizi ni aina za hisa ambazo huwa ndio nyingi katika kampuni.Wale wanaomiliki hisa nyingi katika kampuni hisa zao huitwa hisa za wamiliki.
Huitwa hisa za wamiliki kwakuwa hawa huhesabika kama ndio kampuni yenyewe na hivyo wenye hisa hizo ndio wamiliki wa kampuni.Nimesema hapo juu kuwa wanahisa hawana haki sawa,wajibu pamoja na uwajibikaji.
Wenye hisa hizi wana haki kubwa ya kimaamuzi katika shughuli zote za uendeshaji wa kampuni kwakuwa wao kila hisa moja huwa ni kura moja na kwahiyo kila kitu hupitishwa kwa kura zao.Pia wana haki ya kupata mgao mkubwa kuliko wengine.
Hata hivyo wanawajibika zaidi linapotokea tatizo kwa mfano inapotokea hasara wao ndio hupoteza zaidi.Kwa jina jingine hisa za hawa huitwa HISA ZA SIMBA( LIONS SHARE).Hii ni kwasababu huko mwituni simba hupata mgao mkubwa wa nyama kati ya wanyama wote.
( b) HISA ZA KAWAIDA.
Hizi ni zile hisa ambazo humilikiwa na watu wengine wa kawaida katika kampuni. Mara nyingi hawa ndio huwa wengi japo kila mtu huwa na hisa kidogo kidogo. Mgao wao wa faida hutokana na asilimia ya kile mtu anachomiliki
Maamuzi yao katika kampuni huwa ni madogo ukilinganisha na wenye zile hisa za umiliki( equity shares).Hata hivyo uwajibikaji wao nao ni mdogo pia kwani hupata hasara kidogo pale kampuni inapopata hasara.
(c) HISA ZA WAANZILISHI ( DEFERRED SHARES).
Hizi ni hisa ambazo hutolewa kama zawadi kwa waanzilishi wa kampuni. Mgao wa faida wa hisa hizi huwa sio wa moja kwa moja isipokuwa hutegemea na faida inayozidi
Kawaida mgao wa faida kwa wanahisa wengine hutoka katika faida ya kawaida lakini hawa hawapewi mgao kutoka faida ya kawaida isipokuwa hupata pale faida inapozidi au kuvuka kiwango ilichotegemewa.
( d ) HISA ZA KAMPUNI( CORPORATE
SHARES).

Zote nilizotaja juu ni hisa za kampuni lakini bado jina hili hupewa hisa hizi kutokana na kuwa ni hisa maalum ambazo hutolewa kwa waajiriwa/wafanyakazi katika kampuni husika.
Waajiriwa hutengewa hisa zao na mwenye uwezo huweza kuchukua hisa hizo kwa kiwango cha uwezo wake. Mwajiriwa huendelea kuwa na hisa hizo hata baada ya utumishi wake kukoma .Kwa ufupi sana niseme tu kuwa hisa sio hisa ila hisa ni una hisa za aina gani.
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Mbwambo

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!