-THREAD AQUACULTURE-
Leo tushare ideas juu ya ufugaji wa samaki moja ya biashara inayowaingizia pesa sanaaa Bara la Asia huku 🇹🇿 ikisahaulika japo tukijitahidi
#NipeDili
#KilimoFursa
🔁Retweet ifike mbali
Tasnia ya ufugaji wa samaki inajumuisha ukuzaji wa viumbe vya kwenye maji (bahari na maji baridi) katika mazingira tofauti na yale ya asili. Lengo kuu ni kukuza kwa muda mfupi ili kujipatia lishe, kipato na kutunza mazingira ya bahari, mito, maziwa nk.
Zifuatazo ni aina/level za ufugaji ambazo mkulima anaweza kufanya kulingana na malengo na uwezo wake:
Idadi ya samaki wanaopandikizwa: samaki 2-3 kwa mita ya mraba
Samaki hutegemea chakula cha asili (mimea ya majini-phytoplankton, wadudu/viumbe vidogo vya majini-zooplankton)
Hauitaji ubadilishaji wa maji
Hauihitaji huduma ya ziada ya hewa
Idadi ya samaki, 4-7 kwa mita ya mraba
Chakula cha asil na chakula cha ziada huitajika
Maji hubadilishwa sentimenta 10-20 kila baada ya 3-4weeks kulingana na hali ya samaki na maji yako.Huduma ya hewa ya ziada sio ya ulazima
Idadi ya samaki kwa mita ya mraba ni 10-25
Chakula cha asili na cha ziada
Huduma ya hewa ya ziada lazima
Maji hubadilishwa kila siku au kila baada ya siku kadhaa (15-25 cm)
Idadi ya samaki ni zaidi ya 25 kwa mita ya mraba
100% chakula cha kutengenezwa
Maji ni kuingia na kutoka
Hewa ya ziada masaa yote
Eneo linalotumika ni dogo ukilinganisha na mifumo mingine
Samaki wanaweza kufugwa katika miundombinu mbalimbali kama ifuatayo:
Bwawa
Kina 0.8-1.5m
Ukubwa 100 mita za mraba- 1ha
Umbo-mstatili au mviringo nk
Kina 1-1.5m
Kipenyo kwa lile la mduara 3-10m
Ukubwa kwa la mstatili inategemea na uwezo lakini lisiwe kubwa ili kuhimili nguvu ya maji
Materials:Plastic,cement,chuma
NB: Simtank linafaa( Faida inapatikana kama utalitumia kwa intensive system)
Huwekwa katika maji ya asili kama vile ziwani, baharini au katika bwawa. Vipo vinavyoundwa kwa local materials kama mianzi na vipo vya aluminium.
Baadhi ya maeneo yanayofaa ni yale mashamba ya mpunga, na maeneo yaliyo karibu na vyanzo vya maji. Zifuatazo ni sifa za maeneo yanayofaa:
Eneo liwe na maji ya uhakika. Vyanzo vya maji ni kama vile mito, bahai, maziwa, chem chem., kisima, maji ya dawasco na mvua. Maji yasiwe na kemikali hatarishi kwa viumbe.
4. Eneo lisiwe na historia ya mafuriko ili kuzuia athari za mafuriko kwa miundombinu yako. Utatumia gharama nyingi katika kuimarisha miundombinu yako.Jamii/aina ya samaki
6. Miundombinu ya umeme ni sifa ya ziada hususan kwa mkulima wa kati na wajuu kwa ajili ya kutumika katika kuendesha visambaza hewa.
7. Ulinzi muhimu
Aina ya samaki unaoweza kufuga Tanzania kwa sasa
Maji baridi
Sato/perege, Kambale, Kambamiti wa maji baridi na Trout (maeneo ya baridi kama vile Iringa, Kilimanjaro Arusha na Mbeya)
Kambamiti wa maji bahari, mwatiko, chewa, kaa, chaza wa lulu
Upatikanaji wa Vifaranga vya samaki husika
Vyanzo vya vifaranga ni kutoka katika mito, bahari, maziwa na wale wa kuzalishwa katika vituo vya kuzalishia vifaranga.
Vituo vya serikali Utapata sato wa kike na kiume mixed sex). Kingolwira Morogoro, LuhiraSongea, Mbegani-Bagamoyo . Kifaranga huuzwa Tsh. 50-100 kwa kifaranga.
Trout
Mayai huagizwa toka Marekani, Israel
Kamba miti wa baharini Alphakrust Mafia.
Chakula cha asili
Hurutubishwa kwa mbolea ya wanyama kama vile kuku, ngombe, mbuzi nk. Kwa kiwango cha 1000kg/ha. Mbolea ya kuku ni kali hivyo unaweza punguza ikawa 250-500kg/ha.
Samaki huitaji protein ili akuwe na kila samaki ana mahitaji yake hivyo ni species specific.Formula zipo kwa wale wanaotaka kutengeneza.Tanzania hakuna kiwanda kinachotengeneza. Ingredients zake ni kama vile dagaa, pumba,soya,unga wa ngano,unga wa muhongo
Kwa kawaida ni miezi 4-6 amabapo unapata 250-400g kulingana na ulishaji wako. Kwa prawns ni miezi 3-6 wanafikia 30-50g ambayo ni ukubwa wa soko.
Perege/sato Mfano:
Ukubwa wa bwawa ni 20m by 30m= 600 mita za mraba
Idadi ya samaki (7 kwa mita ya mraba) kwa monosex tu= 600 x 7=4200 fish
Uzito hadi kuvuna (4-6months)- 250g= 4200 x 250g= 1050kg (Nimesha convert gram to kg) Bei kwa kilo ni 6000-8000 6m-8m.
Ujenzi wa bwawa
Kuchimba kwa vibarua ni 500,000-600,000
Kuchimba kwa machine ni 1,000,000-1,500,000 kulinganana mahali.Kama udongo ni kichanga itabidi ujengee (kujengea ni gharama na inaweza ikafika 3.5-4m kwa gharama zote kuanzia kuchimba hadi kujengea)
Gharama ya vibarua 150,000-250,000 kwa mwezi.
Utakuwa na gharama ya chokaa kwa ajili ya kuua vidudu (laki 100,000-200,000),
Jinsi ya kuhudumia bwawa, kuandaa chakula nitaandaa tips zingine.
@adamlutta @Mwacha5 @IALLAND0 @Michael______7 @njiwaflow @tanganyika_m @PaulJaffah @BaloziMtaa @babalao__ @nuhmnyalu @bentemba2019 @sonnino123 @SAM_wa28 @sophysadam @ChapArnold @sonnino123 @adamlutta @Obofficial3 @Kichomi11 @RaphaelMheta
@Brendaulomy @babalao__ @MudathirLibra @adamlutta @plexino @PKefand @rollymsouth