My Authors
Read all threads
FAHAMU MAMBO MUHIMU YA KUFANYA ENDAPO KUTATOKEA TETEMEKO LA ARDHI
-THREAD HOW TO BEHAVE DURING EARTHQUAKE-
Nimechambua machache na kuyaleta humu baada ya juzi kuona taharuki watu tukiwa hatujui nini cha kufanya endapo kutatokea earthquake.
🔁 Retweet ifike mbali
#ElimikaWeekend
Je unaufahamu juu ya tahadhari za kuchukua endapo kukitokea tetemeko la ardhi (Earthquake)
Tetemeko la ardhi linatokea hasa katika maeneo ya mlipuko wa volkano (Volcanic eruption zones). Eneo (point) ambapo matetemeko ya ardhi huanzia yanajulikana kama focus..Ukubwa wa matetemeko ya ardhi hupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa seismograph
Kwa kawaida Tetemeko La ardhi linatokea Kutokana msukumo wa nguvu za asili zinazosababishwa na mgandamizo  kupelekea miamba kukatika sasa hapo ndio Ardhi imepelekea kutikisika ndipo tunasema ndio Tetemeko la ardhi na mara nyingi huwa inatokea katika kina kirefu cha Ardhi
Tetemeko la ardhi linaleta madhara makubwa sanaa kulingana na ukubwa wake na pia hali ya maandalizi dhidi ya tetemeko yaan State of preparation....Piah umbali kutoka epicenter ,Mda wa tukio yaan usiku linaathiri sanaa, Majira ya mwaka , Na aina ya udongo husika
Mambo Muhimu ya Kuzingatia Kuepuka Madhara Yanayoweza Kusababishwa na Tetemeko la Ardhi.
Hapa nimejitahidi kuweka katika makundi 3 yaan kabla ya tukio,Wakati wa earthquake na baada ya earthquake kutokea
i. Kabla ya tukio:

⏩ 1: Elimu ya tahadhari inapaswa itolewe ili kila mmoja aelewe nini cha kufanya linapotokea tetemeko la ardhi kama mm ninavyokuletea huu uzi ...Na mamlaka husika na mashirika yasiyo ya kiserikali
Hii ni pamoja kupata mafunzo kutoka mamlaka husika na kwa watu wa msalaba mwekundu kuhusu namna ya kuhudumia majeruhi ama wahanga na pia jeshi la zima moto ili kupata elimu kuhusu namna ya kutumia kizimamoto.
Elimu na mafunzo hayo yatasaidia kuwaweka watu katika hali ya tahadhari na hii itasaidia kupunguza taharuki wakati wa tukio kwa vile watakuwa sasa wanajua namna ya kuchukua tahadhari
⏩ 2: Kufanya mazoezi ya kuchukua tahadhari hizo mara kwa mara ili kujizoesha kwani mara nyingi wakati wa matukio ya majanga kama hayo watu huchelewa kuchukua uamuzi wa haraka kujinusuru kwani huwa bado wanajiuliza kwamba wafanye nini.
⏩ 3: Wananchi pia wanashauriwa kujenga nyumba bora na imara kwa kuzingatia viwango halisi vya ujenzi, kuweka misingi imara wakati wa ujenzi, kupata ushauri wa kitaalamu wa aina ya majengo yanayofaa kujengwa katika eneo husika kulingana na ardhi ya mahali hapo
Kuepuka ujenzi wa nyumba katika miinuko mikali yenye kuambatana na mawe/ miamba (suspended boulders) na kuepuka ujenzi wa makazi katika maeneo tete yenye mipasuko ya miamba (faults) na uwezekano mkubwa wa kutokea matetemeko
Mambo ya kufanya Wakati wa tetemeko la ardhi

(a) Wakati wa tukio la tetemeko la ardhi unashauriwa kukaa mahali salama kama vile sehemu ya wazi isiyo na majengo marefu, miti mirefu na miinuko mikali ya ardhi. Watu wanashauriwa kukaa nje ya nyumba katika sehemu za uwazi.
(b) Endapo tetemeko litakukuta ukiwa ndani ya nyumba unashauriwa ukae chini ya uvungu wa meza imara, ama kusimama kwenye makutano ya kuta na pia ukae mbali na madirisha na makabati ya vitabu, vyombo au fenicha ili kuepuka kuangukiwa na vitu hivyo.
(c) Unashauriwa usitembee umbali mrefu kwa lengo la kutafuta mahali salama kwa sababu tetemeko la ardhi hutokea ghafla na huchukua muda mfupi. Takwimu zinaonesha kwamba watu wanaotaharuki na kukimbia ovyo wakati wa tukio la tetemeko ndio hupata madhara ama kuumia.
(d) Salimisha macho yako kwa kuinamisha kichwa chako wakati wa tukio.Hii itakusaidia kuyaweka macho yako salama

(e) Baki mahali salama hadi hapo mitetemo itakapo malizika na kisha ujikague kuona kama hujaumia na ndipo utoe msaada kwa wengine ambao watakuwa wameumia.
(f) Ondoka mahali ulipo kwa uangalifu kuepuka vitu ambavyo vitakuwa vimedondoka na kuvunjika kwani vinaweza kukudhuru.

(g) Jiandae kwa mitetemo itakayofuata baada ya mtetemo mkuu. Tetemeko kuu huwa mara nyingi linafuatiwa na mitetemo mingi midogo midogo.
(h) Kumbuka kuwa matukio ya matetemeko ya ardhi huweza kuambatana na moto hivyo jihadhari na matukio ya moto kwa vile tetemeko la ardhi linaweza kusababisha kupasuka kwa mabomba ya gesi au kukatika kwa nyaya au kuharibika kwa vifaa vinavyotumia umeme na kusababisha hitilafu
(i) Kama uko nje ya jengo wakati tetemeko linatokea unashauriwa kubaki nje,simama mahali pa wazi na uwe mbali na majengo, miti mikubwa, nguzo na nyaya za umeme na ujikinge kichwani kadri inavyowezekana kwani paa za nyumba, miti, nguzo na nyaya za umeme vinaweza kudondoka
(j) Endapo utakuwa unaendesha chombo cha moto wakati wa tukio la tetemeko la ardhi unashauriwa usimame kwa uangalifu sehemu salama na usubiri hadi mitetemo imalizike ndipo uendelee na safari yako kwani tetemeko linaweza kusababisha barabara au madaraja kukatika.
(k) Endapo utakuwa kwenye maeneo ya miinuko au milima uwe mwangalifu ili kuepuka kuporomokewa na mawe au kuangukiwa na miti,

(l) Baada ya mitetemo kumalizika endapo itakulazimu kuondoka mahali ulipo ukiwa katika jengo refu unashauriwa kutumia ngazi badala ya lifti au kipandishi.
iii Baada ya tukio:

(a) Wananchi tunashauriwa baada ya tukio kuzima umeme katika majengo ili kuepuka kutokea kwa hitilafu ya umeme kwani mitetemo huenda ikaendelea tena.
(b) Kukagua majengo kwa uangalifu ili kuhakikisha kama hayakupata madhara kama vile nyufa n.k,na kwamba yanaweza kuendelea kutumika na kama ikibidi basi unashauriwa kuwaita wataalamu wa majengo ili wayafanyie ukaguzi.
(c) Endapo utaangukiwa na vitu vizito usijaribu kutumia nguvu nyingi ili kujinasua kwani hujui vitu hivyo vina uzito kiasi gani, omba msaada kwa kuita kwa sauti lakini usifanye hivyo mara nyingi ili usipoteze nguvu nyingi mwilini maana hujui ni lini utaokolewa,
(d) Toa msaada unaowezekana kwa watu walioathirika na tetemeko na utoe taarifa kwa vyombo vinavyohusika na uokoaji

Hayo ndio machache niliyofanikiwa kuyaleta mbele zenu....kama kuna lolote waweza ongeza hapaa
👇👇👇👇
@gudume_ retweet yako mzee
@mpambazi_ maoni yako juu ya tetemeko na retweet yako muhimu
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Keep Current with Mbwambo

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!