"SIRI YANGU🤫"

Napiga pafu moja kutoka kwenye glass...mkono unanipiga begani,tuji bia tunanimwagikia kidogo kwa tshirt,,naangalia nyuma kuangalia ni nani huyu fa**..
Nakutana na cheko moja la kihuni..kumbe Jose,
"Mjinga umemwaga bia yangu"
Ananicheki kwa dharau..anaita muhudumu ananiongezea mbili...
Inabidi nimuulize "hii jeuri imeanza lini kapuku wewe..😅

Anantizama af sura inabadilika.."kuna hela nilikua nadunduliza nimtoe mtoto wa mtu ila acha tuinywee tu bia..atleast siku niseme na mimi nshawahi kukutoa"
Nakaa nae kwa masaa kadhaa..kwakua mwana anafanya kazi ya boda naona kabisa narudi gheto vizuri kabisa...
Muda unayoyoma...nakuja cheki saa saba na nusu..nanyanyuka huku nikiwaambia wana wengine "kesho nayo siku"
Napigwa vijembe kadhaa pale..sijali namshtua mwana anisogeze ghetto
Nafika getini tunaagana..nafungua kwa umakini ili nisizingue wapangaji wenzangu,umeme umekatwa ...kimyaaaaa
Kigiza kinanikaribisha ila najongea kwa mazoea...
Mara nasikia vinyweleo vimesimama..vijipelepele vinachomoka..kichwa kama kinashika ganzi..nawaza ni pombe tu..sijali
Natafuta funguo sehem niliyoiacha..siioni..mbona kama nakumbuka nilifunga mlango..nawaza "mi huwaga fara saa nyingine nilikua nawahi wap sasa..nasukuma kitasa..kinaitika..
Napita sitting room huku nachojoa tshirt..nnachowaza ni kujirusha kitandani..
Nafungua mlango wa chumbani..nalegeza mkanda..nakaa kitandani..navuta pumzi ndefu..

Akili inahisi kama imesikia mtu akijigeuza..pombeeee hizi.

Huku nikiwa nahangaika kutoa raba mguuni.. nasikia mpalazo wa shuka,akili inanikaa sawa..pombe inajiengua kwa muda.
Nguvu kama zinaniishia flani,,bumbuwazi...akili haiwazi..giza nene sioni kitu..nachoropoka kitandani siangalii hata nyuma..uzuri sikufunga mlango wa chumbani..moja kwa moja sebuleni huku naona kama kuna kitu nacho kinanifata nyuma..purukushani la kufungua mlango wa kutokea nje..
Kelele za milango zinawaamsha wapangaji...
Juma anafungua mlango anachungulia...Lucy nae namwona dirishani kipazia kakisogeza pembeni..juma anauliza vipi...
Mwanaume nahema hoi kama nimetoka marathon za @Tigo_TZ ,najaribu kuzungumza ila nashindwa..
Lucy kidomodomo hatupendani..umbea mwingi kama kwenye kipindi cha "Uhondooo" redioni, anatoka na yeye "heh..kulikoni"...
Ghafla mlango wa mama mwenye nyumba kwa mbali kidgo unafunguliwa nao..ni giza ila mwili wake mkubwa unaonekana kajitanda khanga..."kuna nini huko mbona kelele"
Nimeinama najaribu kuvuta hewa..
Juma ananifuata huku lucy nae anasogea akifunga khanga vizuri..
Juma ananishika mgongoni.."Oya vipi..??"

"Humo ndani k**k sijui kuna mchawi sijui jini"..hapo nashindwa kuelewa ni nini kimetokea asee
Juma anachukua simu yake anawasha tochi kumulika ndani kwangu..lucy alisharud nyuma kidogo ila anasogea na yeye kwa uoga...naona na mimi nijitutumue nasogea na juma...tunasogeza mlango wa sitting room kumulika hamna kitu..nanyooshea mkono chumbani...tunasogea taratibu
Kama tunachungulia vile...juma anasukuma mlango ili tupate kuona chumba kizima...anamulika..
Kabatini..kupo sawa..
Kitandani shuka kidgo halijakaa sawa..nadhani ni ile purukushani..hapo tunapata nguvu ya kuingia chumbani huku tunaangaza..lucy yupo mlangoni nae..
Mama mwenye nyumba namwona kwa nje..hataki hata kuingia..
Juma anaanza kucheka "mjinga una wenge.."
Namwambia nilivyokua nahisi...anasema inatokeaga usiku kukiwa giza huwa tunahisi kuna vitu ila ni imagination tu..
Nachukua simu yangu niliiacha kitandani..sina amani kabisa
Nawaza haiwezekani yaliyonitokea UDSM yanataka jirudia..
Lucy anaanza kuondoka huku anacheka..mama mwenye nyumba anamuuliza vipi..."kev muoga tu kalale mama,mwanaume mzima unaogopa kivuli,mxieeww".
Juma nae anaanza kutoka huku akisema.."mwanangu kalale,hamna kitu"
Najiona mjinga.
Nafunga mlango huku nimewasha tochi..naingia chumbani namulika tena kujihakikishia..
Nasukuma mlango ili niufunge..NAGANDA😨..
Nyuma ya mlango kasimama kajibanza ukutani..mwili uliojaa vizuri..umezungukwa na khanga iliyomchora vizuri..wote tumetumbuliana macho.. "MATILDA"
Anajishika ghafla mdomoni ili ajizuie kucheka,nakosa cha kuongea.
Huku akitaka kunishika mikono yang "Nisamehe,sikujua kama ingekua hivi..nilidhani utajua nipo ndani ukikuta mlango haujafungwa"
Huku akiweka kichwa kifuani
"Wangeniona sijui ingekuaje.lucy,juma,mungu mama angeniua"
Ghafla anashtuka ananitazama usoni,macho yamemtoka.
Nami namwangalia kwa uoga,sio kwa macho alivyoyatoa..
"Matty,nini?"
Huku midomo inamtetemeka
"Kev,mama atafunga mlango niliuacha sijafunga ili niweze kurudi baadae,sa ntarudije mungu wangu"

Sikuwahi kuona uoga kama ule machoni
Usitake kujua asubuhi kilichojiri..hiyo ndo siri yangu nimeitoa leo.. ila jua

WATOTO WA KIKE WANAFANYAGA YASIYOWEZEKANA WAKIPENDA MTU"

#fanani✍️ hapa reporting on duty
Tulike na Turetweet

@chawanyu @troniofficial @Joki_Aaron
@tweetsrifle @Mshambaflan @Eric_Bernard94

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Urs truly✍️

Urs truly✍️ Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @urztrue

23 Oct
"NILILAMBA JOKERI🃏.."

Nipo kwenye gari nna hasira flani..nafungua whatsapp natafuta convo yetu mwanzoni kabsa..naandika "mnazingua"
Huyu ni rafiki angu wa kike,Ney, tumepanga kwenda premier ya movie flani ilikua inatoka af tuna ka dk 10 ianze,ameomba aje na rafiki zake wawili
Mi nipo na mchizi,ye ndo kamaindi mbaya. Kanimaindi mimi pamoja na huyo rafiki angu.."kubabeki,tunaenda kuanza movie nusu..si bora tukanywe bia tujue moja" 🤔nkawaza sio wazo baya ujue..
Mara nasikia milango inafunguliwa siangalii hata nyuma nawasha gari..
Nasikia sauti ya ney "kelvin,we are sorry" naongeza sauti ya mziki..
Mchzi anageuza shingo anawasalimu..naona kashalegea kuona vimwana,anaanza kuwapigisha stori pale
Njia nzima nipo kimya..hadi tunafika.
Wanashuka na mimi kma dereva nachek kma vitu vipo sawa kabla sijashuka
Read 17 tweets
15 Aug
"THUBUTUU...🤧"

Sijui ilikuwaje hadi nkasahau kuandika kuhusu hiki kisa..🤭
Nadhani kwasababu mchizi hakua mtu wangu wa karibu sana..ilikua ni kuonana kwenye vigenge vya stori na kitaa.

Ila siku tulijikuta wawili tu kwenye kota za tanesco anapokaa,chobingo moja yetu pendwa..
Mchizi aliitwa Saleh..
Tulisalimiana kiwana tukiulizana mishe zinaendaje na vijistori vya hapa na pale vya kupoteza muda.
Mchizi alitoa sigara mbili huku akiniuliza kama natumia..nilimjibu situmii hvyo aliiwasha yake akavuta pafu mbili kubwa..alitoa moshi nje af akabaki kaduwaa
Ilibidi nimuite mara mbili,aliposhtuka ilibidi ajicheke..nikamuuliza vipi asee mbona umeniacha peke yangu..
Nakumbuka alinambia
"aahh kmmk,nna kipengele kimoja hicho na sijui itakuaje" nkamwambia "nipange"
Alisita kidogo akaangalia sigara yake kidgo kisha akaanza kunipa stori
Read 26 tweets
27 Jun
"KARMA..🎭"

🌡Kama huna kifua basi usisome uzi huu haukufai maana mi natoa visa vya ukweli kama ifuatavyo...👇

Nipo na mwana ananionesha picha af ananiuliza "unaikumbuka hii"..naichek af nacheka ni picha ya kitambo kidgo,tukiwepo sisi na wasichana watatu..mmoja wao akiwa VERO
Vero mi nilimjua kipindi anatoka na mchizi wangu huyo..baada ya kukutana nae viwanja..tulikula sana bata za hapa na pale na huyu manzi,kipindi hicho anakaa mitaa ya sabasaba na wenzake.. walikua wamoto..kila weekend lazima niulizwe "shem leo wap!!nna rafki yangu nataka nikususie"
Kiukweli mchizi wangu alikua sio mtuliaji so wana tulikua tunajua saa yoyote kinaweza nuka..ila cha kushangaza haikua hvyo kwa muda mrefu..nadhani style za maisha ziliendana kiasi kwamba ilikua haiboi..
Basi hapo kati Vee kama nilivyokua namwita akapata mimba ya mchizi
Read 18 tweets
7 May
"LAANA...."🧞‍♂️

Wiki moja baada ya kuanza darasa la kwanza kutokana na umbo langu kua dogo kidgo kuliko wengne ilinipa ugumu maana nilishindiliwa uonevu wa kila namna..ila siku,mmoja wa wanafunzi alinikingia kifua..na si mwingine bali ni "MUDI" kama wengi tufupishavyo, jembe langu
Sikuwah kuonewa kuanzia siku hiyo na ndipo nilipojifunza ubabe..sikuwah kumwambiaga ila alikua kama kaka angu japo tulikua umri sawa ila kwa mwili wake na udogo wangu tofauti ilikua kubwa,alikua ndo rafiki wangu wa kwanza kishule shule. Alinifunza kujihami,kujilinda na ni yeye
alinifunza utukutu..asee shule nzma ilikua inamtambua. Kwa kila walimu walichomsema basi na mm nilihusika ila kwakua wengi hawakuamini mi kuhusika ivo mudi alichkua adhabu zote na hakuwah kunitaja. Ila nami nilihakikisha hafeli mitihani kwa njia yoyote na hakuwahi kuniangusha
Read 22 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!