AKIWA Kijana, alifanya tukio. Hakujuta. Na akasahau. Akaishi miaka 44 mingine. Ndipo akatokea mtu akamkumbusha kile alichokifanya. Akaumia. Akatamani asahihishe makosa yake. Hakupata fursa hiyo. Miaka mi3 baadaye akafariki dunia akiwa mwenye huzuni kubwa
Zingatia, ujana ni tapeli mkubwa wa maisha. Ujana utakulaghai na kukufanya uone maisha ni hayohayo uliyonayo katika wakati uliopo. Ujana unaweza kukughilibu na kukusahaulisha ujio wa kesho. Ujana hufumba macho na huziba masikio. Si walisema ujana maji ya moto?
Ted Jorgensen, alipokuwa na umri wa miaka 17, alikutana na binti mrembo, Jacklyn Gise, aliyekuwa na umri wa miaka 16. Wakapendana. Wakaanza safari ya mapenzi. Jacklyn akanasa ujauzito.
Wakati Jacklyn anashika mimba, alikuwa mwanafunzi wa high school.
Ted alikuwa mcheza sarakasi aliyekuwa na ndoto za kufanikiwa kwenye mchezo huo.
Januari 12, 1964, mtoto akazaliwa. Jeffrey ndilo jina walilompa. Jeffrey alipozaliwa, Ted alikuwa ameshatimiza umri wa miaka 18, Jacklyn miaka 17.
Na sababu ya mtoto na malezi, ndoto za masomo zikayeyuka. Ted na Jacklyn wakafunga ndoa. Maisha ya ndoa yakawa magumu. Ted alkuwa mlevi kupndukia. Mara arudi nyumbani alfajiri au asirudi kabisa. Ted alkuwa na kipato kidogo lkn hakukitumia kulea familia, bali starehe zake binafsi
Baada ya miezi 17 ya ndoa, Jacklyn akaomba talaka. Ted akakubali. Wakaachana. Jacklyn akarudi kwa wazazi wake.
Miaka miwili baadaye, Jacklyn akapata mwanaume mwingine, Miguel Bezos. Wakafunga ndoa. Bezos akaomba kumuasili Jeffrey awe mwanaye kisheria.
Ted akasaini nyaraka zote kuhalalisha mtoto wake atwaliwe na Bezos.
Mwaka 2012, mwandishi Brad Stone alipokuwa anakusanya taarifa ili aandike kitabu “The Everything Store” kilichohusu maisha ya bilionea mmiliki wa kampuni ya Amazon, Jeff Bezos, alimfikia Ted.
Akamuuliza kama alikuwa na habari kuhusu mwanaye aliyezaa na Jacklyn mwaka 1964.
Ted akavuta kumbukumbu, kisha akajibu: “Nimekumbuka. Hivi yule mtoto bado yupo hai kweli?” Brad akamjibu: “Yupo hai. Ndio huyu bilionea mmiliki wa Amazon.”
Ted akasikitika, lakini akakiri hakuwa baba bora kwa Jeffrey wala mume mzuri kwa Jacklyn.
Kuanzia hapo, Ted alianza kutafuta nafasi ya kuonana na mwanaye Jeffrey, angalau wazungumze, japo amtambue. Nafasi hiyo angeipata wapi?
2014, Ted aliumwa sana. Akaandika barua nyingi kwa Jeff, kumjulisha hali yake na kiu yake ya kumuona kabla hajaaga dunia. Hakupata majibu.
Hakuna ajuaye kama Jeff aliziona hizo barua na kumkaushia au hakuziona kabisa. Ila ni uhakika kuwa alitambua kuwa baba yake mzazi alikuwepo
Mwaka 2015, Ted alifariki dunia bila kuonana na mwanaye wa damu, Jeffrey. Aliishia kumsoma na kumuona kwenye vyombo vya habari kama watu wengine.
Kuhusu maisha ya Ted; baada ya kuachana na Jacklyn, aliendelea na mitikasi yake ya kucheza sarakasi na ulevi.
Miaka 10 baadaye, akagundua maisha aliyokuwa akiishi hayakuwa na kesho nzuri. Akaacha ulevi. Akafungua duka la kuuza baiskeli. Hiyo ndio ikawa kazi yake mpaka alipofariki dunia.
Ted baada ya kuachana na maisha ya ulevi, alimuoa mwanamke mwingine, jina lake Linda.
Hakupata mtoto mwingine. Mkewe, Linda, alikuwa na watoto wanne.
Miaka miwili baada ya kifo cha Ted, taasisi ya utafiti wa mali na utajiri duniani ya Forbes, ilimtangaza Jeffrey kuwa tajiri namba moja duniani. Akimpita tajiri namba moja wa muda mrefu duniani, Bill Gates.
Kwa sasa, Jeffrey ana utajiri wa dola 183.6 billioni, ambazo ni sawa na Sh242.4 trillioni.
Jeffrey anatambua kuwa Ted ni baba yake, kwani cheti chake cha kuzaliwa na kumbukumbu zote za hospitali zinamtaja Ted ndiye baba yake.
Hiyo ni stori kuhusu tajiri namba moja duniani, Jeff Bezos na baba yake mzazi, Ted Jorgensen. Story kuhusu ujana na utapeli wake.
Ted angejua? Maskini hakujua. Alikufa akijuta. Angejua Jeff ndiye mwanaye wa pekee, angekubali kumwacha kwenye mikono ya baba mwingine?
Angefunuliwa kuwa Jeff angekuwa tajiri namba 1 duniani, unadhani angemtelekeza?
Hata hivyo usimlaumu sana Ted. Alitapeliwa na ujana. Siku zote elewa hili, ujana ni tapeli mkubwa mno kwenye safari ya maisha.
KWANINI SIKU HIZI VIJANA WADOGO WANA KIWANGO KIKUBWA CHA STRESS NA DEPRESSION?
Wadau wa Twitter.
Leo ningependa tujadili kidogo hali ya afya ya akili inayoendelea kuwatafuna vijana wenzetu mitaani bila jamii kuangazia.
Leo ni hali ya kawaida kukuta kijana teenager anayesoma sekondari au chuo kikuu akilalamika kuwa na msongo mkubwa wa mawazo au kitaalamu inaitwa Sonona (depression).
Hali hiyo imepelekea baadhi yao kujizuru hadi kufikia hatua ya kujaribu kujiua.
SWALI LA KUJIULIZA:
Nini kimepelekea ongezeko kubwa la vijana wadogo kuwa na depression?:
✔Je, ni kukosa malezi mazuri?,
✔kushindwa kufikia ndoto na malengo yao?
✔ Je, mitandao ya kijamii imesababisha wao kutamani maisha ya kifahari wanayoyaona kwenye 'status' za wenzao?
MUDA WA MWANAMKE KUFIKA KILELENI, AFRIKA YAWA GUMZO
Muda muafaka unaotakiwa kwa mwanamke kufika kileleni ni miongoni mwa mambo yanayoumiza vichwa vya wanaume. Wengi wao wanajiuliza kuhusu muda wa kawaida ambao wanatakiwa kuutumia ili kuwafanya wake zao wafike kileleni.
Licha ya maendeleo ya kisayansi na uwepo wa tafiti nyingi za kitaalamu kuhusu suala hili lenye kuwatia wasiwasi wanaume, imebainika kuwa kila bara duniani linatofautiana na bara nyingine kuhusu muda muafaka ambao wanawake wanahitaji ili kufika kileleni wakati wanapofanya tendo la
ndoa na waume zao.
Katika ripoti ifuatayo, utaweza kufahamu wastani wa muda ambao ulioneshwa na matokeo ya wataalamu waliofanya utafiti wa jambo hilo katika mabara mbalimbali ulimwenguni.
JINSI WATOTO WANAVYO SABABISHA BABA ZAO KUFA MAPEMA!!
Baba anapokuwa bado ana nguvu, yuko kazini, ni mkulima, au anafanya biashara; huwa anakua na nguvu na ushawishi mkubwa sana kwenye familia yake: Familia humsikiliza, humjali humpenda, na huzingatia na kutambua uwepo wake.!
Tatizo huanza pale baba anapozeeka, nguvu za uzalishaji mali zimekwisha, au amestaafu.! Na pale watoto wanapokua wamekua watu wazima wameanza maisha yao.! Hapo ndipo mambo kwa baba huanza kuharibika na kupewa kisogo na wanae.!!
Mkewe huanza kumchukulia poa! Ile heshima aliyokuwa akipewa huanza kupungua taratiibu.. Baba hasikilizwi tena Kama zamani, isitoshe anakua hahusishwi sana tena kwenye mambo ya mkewe sababu hata akiambiwa atasaidia nini na pesa hana?
Watu wengi wanapolala huwa wanakoroma na tatizo hilo huwakera wengi wasiokoroma ambao labda hulala chumba kimoja na mtu mwenye hali hiyo. Lakini ni kwa nini watu hukoroma?
✔Mirija ya hewa iliyoziba kwa kitaalamu obstructive sleep apnea (blocked airways)
✔Unene kupita kiasi.
✔Tatizo la mfumo wa mdomo wako, pua, ama koo
✔kukosa kulala kimakusudi (sleep deprivation).
✔ kulala chali
✔ kunywa pombe muda mfupi kabla ya kwenda kulala.
NJIA ZA KUZUIA KUKOROMA
1. Punguza unene na kuzingatia mlo bora.
Kuwa na uzito mkubwa (unene) kunaweza kusababisha mtu kukoroma. Mafuta yaliyozunguka shingo hubana mirija ya hewa na kuzuia hewa kupita kiurahisi kutoka nje au kuingia ndani
JE, NI KIPI HUMFANYA MWANAUME KUINGIA RASMI KWENYE NDOA?
👇👇
Wanaume huwafuata Wanawake kwa mambo mawili, ambayo ni MAPENZI na SEX. Lakini inapofika hatua ya Kuoa, Wanaume hawaoi kwa sababu ya SEX au MAPENZI, wanaoa kwa sababu ya kutafuta AMANI NA UTULIVU WA NAFSI (STABILITY).
Mwanaume anaweza kukupenda na asikuoe,
Mwanaume anaweza kuwa anafanya mapenzi na wewe tena mkadumu kwa muda mrefu lakini asikuoe.
Lakini akampata mtu mwingine akamuoa hata kama mahusiano yake na mtu huyo yalikuwa ya miezi miwili.
Wanaume wengi hutizama mbali zaidi pale wanapotaka KUOA. Huwa hawafikirii habari za suti kali za harusi na sherehe ya gharama, vitu ambavyo hufikiriwa zaidi na wanawake kila wanapoiwaza ndoa.