Unahitaji Kujifunza COPYWRITING?... Basi Anzia Hapa....
.
Kama Umekuwa ukitafuta njia rahisi ya kujifunza Ujuzi # 1 Mtandaoni kwa sasa yaani Copywriting Skills, basi Shuka na Uzi huu mpaka mwisho....
.
[UZI MFUPI TU, Tenga dkk Zako 5 Tu]...👇🏽
Vitu ni vingi ila hapa nitakupa vile ambavyo utaenda kuvitumia kwenye Matangazo yako moja kwa moja..
.
Copywriting maana yake ni uwezo wa kuuza chochote kwenye maandishi au kutumia maneno kuwasiliana na wateja wako ili wafanye kile unachotaka 👇🏽
Au wanasema “Closing in Print/ Salesmanship in Print”
.
Uwezo wa kugeuza maneno Kuwa Pesa nk
.
Natumia umepata picha nzima juu ya ujuzi huu...
.
Unapotaka Kuuza chochote kwenye maandishi hakikisha unazingatia Vitu Hivi ili uone matokeo mazuri...👇🏽👇🏽
✅. Usitangaze Bidhaa/huduma yako, Tangazo kile kinachofanywa na bidhaa kwa wateja wako
.
Tangaza kile kinachotatuliwa na bidhaa yako kwa wateja yaani Utatuzi wa tatizo, watu hununua Solution ya matatizo yao sio bidhaa/huduma kama Jinsi ilivyo...👇🏽
Hawanunui gari kwasababu ya vyuma, hununua kile kinachofanywa na Gari kwao etc
.
✅. Wateja hawanunui bila kuwapa sababu...
.
Hata kama wanahitaji bidhaa yako usipowapa sababu ya Kununua Muda huo, hawanunui Ndio maana ni muhimu kutumia “Urgency & Scarcity”👇🏽
✅. Hakuna mtu anaejali kuhusu wewe kwenye Tangazo lako...
.
Kwahiyo usitumie Nguvu nyingi kuwaambia jinsi bidhaa yako ilivyo nzuri bali tumia Nguvu nyingi kuwaambia ni Jinsi gani bidhaa yako itawafanya wao Kuwa vizuri
.
Waambie kuna nini kwenye bidhaa👇🏽
Bidhaa yako kwa ajili yao? (WII-FM)
.
✅. Tumia zaidi Stories kwenye Matangazo yako... kwanini?...
.
Kwasababu watu maamuzi ya hununua chochote kwa kutumia hisia kisha uhalalisha maamuzi yao kwa kutumia Logic
.
Story zinagusa hisia za mteja moja kwa moja...👇🏽
✅. Hakikisha Tangazo lako halionekani kama ni Tangazo bali ni post ya kawaida tu ...kwanini?
.
Kwasababu watu huwa hawapendi kuuziwa ila wanapenda kununua, mtu yeyote akiona Tangazo lazima ataliepuka kwa Hali na Mali...
.
(Your Ad must Never look like an Ad)
✅. Tumia Zaidi shuhuda za wateja wako walioridhika na Kile unachokiuza
.
Shuhuda humaliza vipingamizi vyote vya wateja kichwani
.
Kama bado hauna toa bidhaa yako BURE kwa watu unaowaamini kabla ya kuipeleka Sokoni ili wakupe feedbacks
.
Mfano...👇🏽
Mimi kabla ya kukitoa kitabu changu nilimtumia kwanza my brother @GillsaInt akakisoma then akanipa feedbacks kisha nikakiingiza sokoni
.
✅. Tumia 90% ya Muda wako Kuandika “HEADLINE” ya Tangazo lako... kwanini?...
.
Kwasababu 60% ya wateja husoma headline👇🏽
Tu kutoka kwenye Tangazo lako
.
Wateja husoma headline mara 5 zaidi ya wanavyosoma Tangazo zima
.
Pesa mpya online kwasasa inaitwa “ATTENTION” na hiyo Ndio kazi pekee ya headline kupata attention ya walengwa wako, bila kupata attention yao huwezi kuuza chchte
✅. 80% ya Copy nzima ni research ya bidhaa na 20% Tu Ndio copy yenyewe
.
Copy haiandikwi, inapangwa (Copy is not written it’s Assembled)
.
I hope umejifunza kitu kipya...
.
Kama una swali lolote DM me..
.
P. S. Usifanye KOSA hili👇🏽...
.
Kuacha KURETWEET!
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
SIRI Ndogo Iliyomsaidia Muddy Wa Dodoma Kuuza Iphone 📱 10 Kila Siku Mtandaoni....
.
Hey, “Amosi Nyanda” Hapa Nimeandika Kitabu Kinachoelekeza Jinsi ya Kuuza Bidhaa zako kwa njia ya maandishi Mtandaoni...
.
...Na Hii Ndio Siri Iliyomsaidia Muddy...
.
[UZI]👇🏽
Nakumbuka ilikuwa ni mwezi wa kwanza mwishoni hivi kwenye tar 20...
.
Muddy alinicheki DM baada ya kusoma baadhi ya Uzi wangu
.
Na hiki ndicho kilichokuwa kinamyima usingizi Katika biashara yake...
.
“Kila alipokuwa anapost Matangazo ya Simu zake Online 👇🏽
Hasa hasa Instagram na Twitter alikuwa haambulii chochote zaidi ya Comments, Likes, na Retweet lakini hakuna Oda kabisa
.
Yaani kwa kifupi likes kibao ila hela hakuna...
.
Hali ile ilikuwa inampasua kichwa mno kwasababu ilifika Muda Mpaka akawa anakosa 👇🏽
Jinsi Kijana Alieishia La Saba Anavyouza Sabuni Zake Mtaani Kama Njugu...
.
Kama Umekuwa ukitafuta Siri Mpya ya kuuza Moja kwa moja (Direct selling) bidhaa zako mtaani, basi Uzi huu ni zaidi ya zawadi kwako..
.
[UZI WA Dkk 4 TU]..👇🏽
Siku ya Jumamosi mida ya jioni hivi tulikuwa tumekaa kwenye kijiwe fulani Hivi na washkaji tunapiga story huku tunakunywa Kahawa Maeneo ya moshono Arusha..
.
Wakati tunaendelea kupiga story akaja jamaa mmoja na kibegi mgongoni huku ameshika sabuni 2 mkononi👇🏽
Kama samples...
.
Baada ya kutupa Hi 👋 akaanza kuprisent sabuni zake, yaani sabuni inafanya kazi gani na ina faida gani kwetu...
.
Wakati anaongea kuhusu sabuni zake nikiwaangalia washkaji pembeni yangu wote wanachezea siku zao..💪🏻
🚫TAHADHARI : Kama Una Mpango Wa Kuuza Courses Au Ebooks Mtandaoni Usifanye Kosa Hili...
.
[UZI 👇🏽]
.
Kama Una Mpango wa Kuuza Knowledge, skills au Taarifa zozote Mtandaoni usipuuze uzi huu kwasababu nakwambia ukweli uliopo sokoni
.
Binafsi naamini kama 👇🏽
Kitu haukiishi basi haukijui (If you don’t live it, you don’t know it)
.
Kabla sijakwambia ni Kitu gani nataka nikupe story fupi kuhusu my own experience kwenye Hii Topic
.
Mwaka 2018 niliacha kazi na kuamua kufanya online business kama full time job 👇🏽
Kwasababu tayari nilishajenga ujuzi wa Copywriting na Closing skills
.
Kwahiyo nilikuwa na uwezo wa kuuza bidhaa/huduma yoyote online aidha ni ya kwangu binafsi au ya watu wengine (Affiliate & dropshipping) na nikatengeneza pesa on my own time
.
👇🏽
Je Una Kampuni ya Utalii Chukua Hii...👇🏽
.
(UZI MFUPI 👇🏽)
.
Kabla ya Janga la Corona nakumbuka ilikuwa ni Mwezi wa 2 hivi kuna Jamaa anaitwa SAI, alinipigia simu akasema anahitaji kupata wageni kutoka nje lakini bado Hana ujuzi wa kutumia Mtandao
.
👇🏽👇🏽
Nikaweka appointment nae kisha nikakutana nae baada ya kumuuliza maswali kadhaa hasa hasa kuhusu soko lake akasema soko lake kubwa lipo “Canada, China, South Africa (SA), Australia na USA
.
Vile vile nikamuuliza mara nyingi huwa anatumia mbinu gani kupata👇🏽
Clients online? , akasema huwa anarun tu matangazo ya kawaida kwenye page zake kisha anaboost (na wengi wanafanya hivi)
.
Nikamuuliza huwa anaandika matangazo gani?, akasema Mara nyingi yenye picha za wanyama
.
Uzi ndo unaanza Hapa kwasababu wengi..👇🏽