"Kuna story ambayo baba yangu Mzazi (Mzee Eugeni) alinisimulia kuwa kipindi cha nyuma akiwa kijana alikuwa anaishi mwanza kufanya kazi ndogo ndogo katika harakati zake alioa Mwanamke ambaye anaitwa Maria na alipata naye watoto wawili.
Mtoto wa kwanza wa kike alikuwa anaitwa Agnes (Eugeni)alizaliwa 1979 na mtoto wa Pili alikuwa anaitwa Ana(Eugeni) alizaliwa 1983.
Mwaka 1984 baba alisafiri kusalimia Nyumbani kwake alipozaliwa ambapo ni Kilimanjaro.
Kutokana na maisha ya kipindi kile alishindwa kurudi Mwanza ilimlazimu yeye kubaki Kilimanjaro ambapo alioa mwanamke mwingine ambaye ni mama yangu mzazi.
Mzee alipoteza mawasiliano kabisa na familia aliyoiacha Mwanza, mwenyewe anasema ilikuwa maeneo ya Nyegezi karibia na Chuo cha uvuvi. Amewatafuta bila mafanikio ila kama kuna mtu yoyote anayeelewa familia hiyo anaweza msaidia baba kupata watoto wake.
Imebidi kama mtoto wake nimsaidie kutafuta ndugu zangu. Natumaini siku moja nitawakutanisha na mzee na nitaona tabasamu lake tena akiwa na wanawe hili likitimia.
Kama kuna mtu yoyote ana fahamu chochote kuhusu hii familia, naomba anisaidie kulikamilisha hili". Anonymous, Moshi, Kilimanjaro. #WatuNiStory
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
"Tangu naanza Shule Ya Msingi, O level na A level Mungu alinijalia Uwezo Mkubwa Darasani. Nikafanikiwa kumaliza kidato cha Sita Vizuri na kuweza kuchaguliwa kujiunga na Chuo kikuu Cha Afya Muhimbili.
Ndipo nilipo anza kuonja joto la kufeli masomo semester ya kwanza nikakamatwa kwenye moja ya somo gumu (Anatomy), second semester Nikapita vizuri, nikarudi October kuja kusapua.
Kutoka na maandalizi duni nikafeli tena nika carry.
Nikaingia mwaka wa pili semester ya Kwanza nikanasa tena kwenye somo moja konk (Micro 1 and 2).
Presha ikanianza kwamba semester inayofuata nikishikwa tena ndo disco.
Semester ya pili nikanasa tena kwenye somo konk (Pharmacology 1 and 2) Ila siku Disco.
"Nimetokea kwenye familia maskini sana na kibaya zaidi ilidharaulika sana, tena kwa pande zote mbili yaani upande wa baba na mama.
Nimekuwa huku kauli za kejeri zinasikika na kuishi masikioni mwangu.
Hilo kwangu ndio lilikuwa tatizo kubwa. Niliwachukia sana jamaa zangu mpaka nimekua mkubwa sikuwahi kuomba msaada wa aina yoyote kwao.
Hadi wazazi wangu niliwahi kuwakataza, niliwaambia shida zote na huduma wanibebeshe mimi.
Kuwaeleza shida zetu, ilikuwa kama kuwalilia njaa kwao.
Leo Mungu amesaidia tunakula kwa muda sahihi na tunalala pazuri. Kiukweli sitamani hata kuwapigia simu. Sasa hivi wamenibadilisha jina wanasema mimi ni jeuri.
"Mwaka 2005 nilihitimu chuo cha ualimu Kabanga kilichopo mkoani Kigoma. Sikukaa muda mrefu mtaani, mwaka 2006 nilifanikiwa kupata ajira wilayani Moshi.
Nilifundisha pale miaka mitatu nikakutana na jamaa mmoja tukawa marafiki. Kumbe alikuwa mganga wa kienyeji.
Katika harakati zake, akanishawishi nikawa chawa wake. Siku zilivyoenda nikajikuta na mimi nimetamani kuwa mganga.
Sikuwa na majini ila kutokana na ukaribu wetu na nilivokua naona watu wengi wenye shida wanakuja kwake wanamuachia hela nyingi kiasi kwamba hela ambayo alikuwa anaipata ilikua inazidi mshahara wangu kama mwalimu.
Nikashawishika kuacha kazi ya ualimu na nikawa mganga.
"Mwaka 2016 nilipoteza kazi niliyokuwa nimeajiriwa kwa makosa ambayo sikuhusika, lakini upepelezi ulipokuja kufanyika nilionekana ni kama na mimi nilihusika kwenye huo wizi ingawa ukweli sikuhusika.
Sikujua chochote na wala sikula hata sh 100.
Wanasema siku ya kusurubiwa kwako manabii wa uongo watakuja ili kukutolea ushahidi wa uongo lengo uangamie, ndio kilichonitokea mimi.
Baadae ya kupoteza kazi Mungu alinipa ujasiri sana maana sikuwahi kujutia kupoteza kazi bali nilianza kuwaza naishije kwa sasa na nafanya nini ili maisha yaende?.