📡Huenda tabia zetu na namna tunatumia hivi vifaa ikawa ni sababu ya hizi mashine kuharibika haraka
📡Hakuna kitu kinachodumu milele na hasa vifaa vya elektroniki. Watengenezaji wa vifaa hutengeneza vifaa wakiwa na malengo kwamba kwa matumizi sahihi hicho kifaa kitadumu kwa miaka kadhaa.
Muda huo huwa sahihi ukitumia ipasavyo kwa usahihi.
Nini kinaua PC yako mapema?
📡1. Kutojali kiasi cha joto kinachokuwepo kwenye PC.
Adui mmoja mkubwa wa PC ni joto. Kama PC yako itapata joto la kuzidi, PC yako itafanya kazi polepole ili kupunguza mzigo joto lipungue.
Wakati mwingine inaweza amua hata kujizima ili ibaki salama.
📡Kutumia PC katika hali ya joto la kuzidi kwa muda mrefu kunaweza punguza maisha ya processor, feni n ahata betri ya PC, bila kusahau vile ambavyo PC itapiga kelele nyingi.
📡Kwa Desktop PC ni rahisi, hakikisha case yako inapata mzunguko wa hewa ya kutosha, ili vifaa vya ndani visizidi joto.
Kwa Laptop kuna ugumu kidogo, zinahitaji uangalizi makini zaidi. Kwa kuwa zinakuruhusu kutumia popote unapotaka kutumia.
📡Wengine huzitumia sehemu kama kitandani kwenye mashuka. Hii inazuia mzunguko wa hewa kuwa mzuri kulingana na namna mashuka yanavyo funika sehemu za hewa.
📡Kila inapowezekana tumia laptop yako juu ya meza au laptop stand. Zaidi ya hapo usitumie PC yako kwa muda mrefu kwenye mazingira ya joto kali.
📡2 Kuacha Vumbi na maji maji kuingia ndani ya PC.
PC zote hubeba vumbi kadri muda unavyokwenda na kupelekea joto kuwa kubwa ndani ya PC. Kuisafisha PC yako kila baada ya muda fulani kutasaidi kuitunza idumu muda mrefu.
📡Lakini Pia ni muhimu kuzuia vitu vingine visiingie ndani ya PC.
Vitu kama manyoya ya wanyama. Maji, soda na kutumia PC kwenye sakafu itafanya uchafu wa hivi kuingia kwa wingi ndani ya PC.
📡Na usijaribu kusema una carpet litazuia haya yote. Carpet ni mbaya zaidi hasa zile za vitambaa zinatunza vumbi nyingi na kuzuia mzunguko wa hewa.
📡Usipende kula karibu na PC, vimiminika visivyo salama vikiingia ndani ya PC utafunga safari kwenda kununua PC mpya au kifaa kipya kubadirisha kilicho haribika.
Tunajua unapenda kuona Screen ya PC yako safi muda wote, basi kuwa makini unapoisafisha.
📡Aidha usitumie kimiminika chochote au tumia kiasi kidogo sana.
Maji yakiingia yapotakiwa utajutia. Unaposafisha screen lowesha kitambaa kwa kaisi kidogo ndipo usafishe usinyunyuzie maji kwenye screen moja kwa moja.
📡3 Zingatia namna unaibeba PC yako
Desktops huwa zinakaa mahala pamoja. Laptop zinakutana na shuruba ya kuhamishwa hamishwa sana. Unapohamisha PC kutoka sehemu moja kwenda nyingine jitahidi kuibeba kwa usahihi.
📡Nimeona watu wakibeba Laptop zao kwa kushika display yake tu. Kuna vitu vinaitwa hinges vinashikilia ile display.
Hinges zikiachia diplay itatenganishwa na PC na unaweza hata haribu ile housing ya PC. Kuwa makini sana na hili.
📡Kwa sababu unaenda kuitumia kitandani basi unaitupa tu juu ya kitandani kwa sababu pako soft. Sawa pako salama, siku utakuja rusha vibaya utaharibu hiyo PC.
📡PC ni gharama sana huko sokoni jitahidi kuijali. Binafsi huwa nasema, “PC yangu ni mpenzi wangu.” Kwa sababu hii naijali kwa kila namna.
📡4 Kutojali betri ya Laptop
Laptop yenye betri mpya inaweza kaa na chaji zaidi ya saa 5, lakini muda unapozidi kwenda na unatumia laptop yako, kiwango hiki hupungua.
Hii haikimbiliki ni lazima tu betri itaanza kupungua uwezo na baada ya muda utalazimika kubadilisha.
📡Unaweza kuwa unafanya betri ipungue uwezo haraka zaidi kama unaacha siku zote iwe inafika mpaka 0% kabisa.
Kutunza betri ya laptop yako usiache iwe inashuka chini ya 15% mara kwa mara, pia usiitumie sio siku zote uitumie ikiwa kwenye chaji.
📡Ni vizuri mara moja moja ukaitumia bila kuwepo kwenye chaji.
MUHIMU kama unaona betri imevimba ni vyema ukaacha kutumia hiyo PC mpaka utakapo badili hiyo betri. Betri ikivimba kuzidi, ikabanwa sana na kupata joto kali huwa zinalipuka.
Jali maisha yako, tumia kifaa salama.
📡5 Jitahidi kuzijali ports na cable zinazotumika na kifaa chako.
Usilazimishe kuchomeka cable isiyofaa kwenye PC yako. Kama cable haiendani na PC yako kwa namna yoyote ile usilazimishe kuiweka.
📡Unaweza lazimisha USB isiyofaa kuingia kwenye PC yako ukaishia kuharibu USB yenyewe na port ya PC.
🚀Mpaka sasa Makala ya Teknolojia kwa Kiswahili ya HabariTech imepata wasomaji zaidi ya 250, unasubiri nini kuisoma pia?
📡Unapochagua kusajili sim card ya mtandao uupendao unakuwa umesajili akaunti ambayo utakuwa unailipia bando ili kuweza pata huduma zao.
Huwa tunasema SIM Card bila kujua maana yake ni nini.
📡SIM ni kifupi cha Subscriber Identity Module. Ni card ambayo inatunza IMSI (International Mobile Subscriber Identity) na funguo za kumtambulisha na kumthibitisha mtumiaji katika mfumo wa mawasiliano.
📡Lakini wengine ni wale wenye hofu ya kupoteza kazi zao, hasa madereva.
Hakuna wa kumlaumu mtu anayeiogopa AI kwa sababu ni kitu ambacho hata baadhi ya watu wa teknolojia wanashindwa kuelewa vizuri.
📡Miaka 2 iliyopita ungeniuliza iwapo kuna siku AI itaiteka dunia, ningejibu hiv, “Inawezekana iwapo tu tutafikia uwezo wa watu kama Tony Stark wa Iron Man.
Leo baada ya kuelewa AI kidogo nitajibu hivi, “Chochote kinawezekana na haina maana tuache kuboresha kwa sababu ya uoga.”
📡Kwa vizazi vya sasa Mass Surveillance haikuonekana mpaka miaka ya mwisho ya 1940s baada ya UK na USA walikubaliana kubadilishana taarifa za intelejensia.
Baadae katika makubaliano haya ziliongezeka Canada, Australia na New Zealand na kufanya muunganiko huu kuitwa “Five Eyes”.
📡Muungano huu baadae mwaka 1971 ulileta kitu kilichoitwa “Global Surveillance Network” ambayo ilipewa jina la “ECHELON”.
ECHELON ni mtandao maalum wa uliofuatilia mawasiliano ya kijeshi na kidiplomati ya Soviet Union na washirika wake wa Mashariki kipindi cha Vita Baridi.
📡Hakuna Tesla iliyotengenezwa China kuingia nchini India.
Hivi karibuni waziri wa usafiri wa barabara nchini India amesem, aliongea na Elon Musk na kumuomba kwamba Tesla kwa za india zitengenezwe nchini India.
Maalumu kabisa hakutaka Tesla za China kuwepo India.
📡Akongea katika "India Today Conclave 2021", waziri huyo alisema kwamba, Gari za umeme zilizoundwa na Tata Mottors zina ubora unaokaribiana na zile za Tesla.
Hivyo Tesla za kuuzwa India inabidi zitengenezwa ndani ya India na sio China na kuuzwa kutoka India kwenda nchi jirani.
📡Sambamba na hilo alisisitiza kuwa, Tesla watapata sapoti yoyote wanayohitaji kutoka serikali ya India.
Tesla waliomba kupata punguzo la ushuru wa kuingiza gari za umeme India. Mpaka sasa hawajafikia muafaka na serikali ya India kuhusiana na maombi haya yote.