📡Lakini wengine ni wale wenye hofu ya kupoteza kazi zao, hasa madereva.
Hakuna wa kumlaumu mtu anayeiogopa AI kwa sababu ni kitu ambacho hata baadhi ya watu wa teknolojia wanashindwa kuelewa vizuri.
📡Miaka 2 iliyopita ungeniuliza iwapo kuna siku AI itaiteka dunia, ningejibu hiv, “Inawezekana iwapo tu tutafikia uwezo wa watu kama Tony Stark wa Iron Man.
Leo baada ya kuelewa AI kidogo nitajibu hivi, “Chochote kinawezekana na haina maana tuache kuboresha kwa sababu ya uoga.”
📡Tungeogopa miaka yote huenda leo hii Afrika bado tungekuwa ni watumwa wa mataifa ya magharibi.
Akili ya binadamu imeubwa kutaka zaidi na zaidi ya kile alichonacho, tunapofikia uwezo Fulani wa maisha tutataka zaidi ya pale.
📡Hivyo AI bado ina nafasi kubwa ya kukua zaidi na kuja kuweza kufanya maamuzi yake kama ilivyo kwa binadamu.
Adui mkubwa wa binadamu sio AI ni binadamu mwenyewe, na ndiyo sababu tuna watu wanaofanya maovu makubwa duniani.
📡AI yoyote iliyotengenezwa kuweza fanya maamuzi yenyewe inajifunza kulingana na mazingira inayofundishwa.
Chukua watoto wachanga 2, kwa muda wa miaka 10 mmoja uwe unamuonesha filamu za kivita tu, na mwingine filamu zinazofundisha upendo.
📡Matokeo utayaona yatakavyo kuwa tofauti kwenye tabia zao na namna wanafanya maamuzi. Basi hivyo ndivyo ilivyo AI.
Program ya AI inajifunza kutoka kwetu sisi binadamu, hivyo inapokuja kuteka dunia ni kwa sababu sisi wenyewe tunakuwa tumeifundisha.
📡Kwa miaka mingi sasa watengenezaji wa AI wamejaribu kuna na AI itakayoweza tatua matatizo bila kuhitaji uwepo wa binadamu.
Yaani AI ambayo inafanya maamuzi yenyewe na kufikiria yenyewe kama ilivyo akili ya binadamu.
📡Clune (mtafiti wa AI) alisema, “Tunaweza kuanza kwa kutengeneza algorithm ambayo isiyo na akili kubwa, na baadae tukaifikisha kuwa AGI.”
AGI (Artificial General Intelligence), ni AI ambayo inafundishwa kutatua tatizo zaidi ya moja, tofauti na AI ya kawaida yenye uwezo mdogo.
📡Ukweli ni kwamba AGI mpaka sasa bado ni ndoto, kwa sababu hakuna aliyeweza/anayeweza kutengeneza.
Tumeshafikia uwezo wa Technological singularity, huu ni uwezo ambao teknolojia inakua kwa kiasi tusichoweza kukidhibiti na kupelekea mabadiliko tusiyo tarajia.
📡June 2021 github walikuja na system iitwayo “Co-Pilot”. Co-pilot ni mfumo ambao uliwasadia developers kuchapa code.
Hiyo ni sawa na kusema AI iliyoweza kuchapa code za program yenyewe. Japo ilikuwa na makosa mengi lakini ni mafanikio makubwa sana kwa AI kuweza fanya hivyo.
📡Rui Wang (mtafiti wa AI pale Uber) alisaidia kutengeneza software iliyoitwa POET (Paired Open-Ended Trailblazer).
Hii ni software inayofundisha virtual robots. POET ina kazi ya kutengeneza vizuizi ambavyo hizi virtual robots zilitakiwa kuvuka na baada ya hapo kuzipa maksi.
📡Yote haya yafanyike bila binadamu kuhusika. Na mafanikio yalionekana kwasababu roboti hao walionekana kujifunza kulingana na makosa.
Rui Wang alisema, “Kila siku nafika ofisini nafungua kompyuta yangu na sijui nitegemee nini.”
📡Wang huwa anaacha POET inafanya kazi anapotoka ofisini kwenda nyumbani. Kila siku anakuta POET imeweka challenge mpya kulingana na virtual robots zilivyojifunza.
Kufikia hapo kuna uwezekano tuna chini ya miaka 10 kuwa na AI ambayo inaweza kujitambua kabisa na kujifunza yenyewe
📡Kumbuka binadamu tuna uraibu wa kutaka kutengeneza kitu ambacho ni sisi wenyewe, mfano roboti 2 maarufu Sofia na Grace.
Hii ni kwa sababu tunajua hatuwezi kuishi milele, Lakini vipi kama miili yetu itakufa na kuoza na akili zetu zikabaki kuishi zikijitambua?
📡Hapo ndipo inakuja kitu inaitwa “Clone”. Binadamu wengi wanatamani kuwa na clone ambayo inaakili kama yake yote na kumbuka zote.
Clone hii sasa ndiyo AI ambayo itaweza kuishi muda mrefu zaidi ya binadamu wa kawaida.
📡Tunajua kwamba kama dunia itakuwepo bado 2300 sisi wote hatutakuwepo ila kuna uwezekano akili zetu zikawepo na kutambua kila kinachoendelea.
Hivyo kwanini basi tusiendelee kukuza AI na kuzifundisha ili tuweze kuisha mda mrefu zaidi japo kiakili?
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
📡Kwa vizazi vya sasa Mass Surveillance haikuonekana mpaka miaka ya mwisho ya 1940s baada ya UK na USA walikubaliana kubadilishana taarifa za intelejensia.
Baadae katika makubaliano haya ziliongezeka Canada, Australia na New Zealand na kufanya muunganiko huu kuitwa “Five Eyes”.
📡Muungano huu baadae mwaka 1971 ulileta kitu kilichoitwa “Global Surveillance Network” ambayo ilipewa jina la “ECHELON”.
ECHELON ni mtandao maalum wa uliofuatilia mawasiliano ya kijeshi na kidiplomati ya Soviet Union na washirika wake wa Mashariki kipindi cha Vita Baridi.
📡Hakuna Tesla iliyotengenezwa China kuingia nchini India.
Hivi karibuni waziri wa usafiri wa barabara nchini India amesem, aliongea na Elon Musk na kumuomba kwamba Tesla kwa za india zitengenezwe nchini India.
Maalumu kabisa hakutaka Tesla za China kuwepo India.
📡Akongea katika "India Today Conclave 2021", waziri huyo alisema kwamba, Gari za umeme zilizoundwa na Tata Mottors zina ubora unaokaribiana na zile za Tesla.
Hivyo Tesla za kuuzwa India inabidi zitengenezwa ndani ya India na sio China na kuuzwa kutoka India kwenda nchi jirani.
📡Sambamba na hilo alisisitiza kuwa, Tesla watapata sapoti yoyote wanayohitaji kutoka serikali ya India.
Tesla waliomba kupata punguzo la ushuru wa kuingiza gari za umeme India. Mpaka sasa hawajafikia muafaka na serikali ya India kuhusiana na maombi haya yote.
📡Kati ya watumiaji hawa kuna wengi wasiofahamu baadhi ya settings ambazo zinakusanya taarufa zao, zinawafanya waone matangazo mengi au kufanya PC zao ziwe pole pole.
Ukiacha madhaifu ubora wa Win10 ukilinganisha na zile za nyuma, bado ina madhaifu mengi unakutana nayo kila siku
📡Kati ya hayo ni pamoja na kutokuwa na uhuru wa usiri (Privacy) wako, spidi ya OS na urahisi wa kutumia.
Leo tuchambue baadhi ya settings ambazo ni vyema ukaziweka off ili uendelee kutumia Win10 yako kwa raha.
📡Watazamaji wa Sci-Fi movies mtakuwa mmewahi kutana na zile simu ambazo ni kioo tu lakini zinafanya kila kitu.
Huenda huko ni mbali sana kufika labda 2050 huko. Twende mpaka 2030 ambapo nadhani huenda tutakuwa na simu zisizo na button yoyote, headphone jack wala tundu la chaji.
📡Unakumbuka iPhone X ilikuja na notch 2017? ikawa mwanzo wa kubadili muundo wa display za simu. Hapo tayari iPhone hazikuwa na port ya earphone
Oppo F9 ikawa simu ya kwanza kuja na teardrop screen na kumpa mtumiaji nafasi ya kutumia screen nzima.
Whatsapp ni mtandao wenye watumiaji takribani 2 billion dunia nzima. Mtandao huu umekuwa maarufu kwa sababu umerahisisha sana mawasiliano kwa njia ya Internet.
Hivi karibuni huenda Whatsapp web ikabaki kujitemea bila uhitaji wa Mobile version.
Whatsapp Web ni version ya Whatsapp ambayo hutumika kwenye browser za computer au kwenye app ya Whatsapp ya Windows au MacOS.
Whatsapp web inabeba text, zile zile ambazo unazion kwenye simu yako. Kwa maana hiyo inatumia akaunti yako ile ile.
Ili utumie Whatsapp Web ilikuwa ni lazima ile ya kwenye simu iwepo online na ya PC pia iwepo online.
Hili litabadilika hivi karibuni baada ya Whatsapp kuanza fanyia kazi version ambayo haitahitaji zote mbili kuweo online.