📡Unapochagua kusajili sim card ya mtandao uupendao unakuwa umesajili akaunti ambayo utakuwa unailipia bando ili kuweza pata huduma zao.
Huwa tunasema SIM Card bila kujua maana yake ni nini.
📡SIM ni kifupi cha Subscriber Identity Module. Ni card ambayo inatunza IMSI (International Mobile Subscriber Identity) na funguo za kumtambulisha na kumthibitisha mtumiaji katika mfumo wa mawasiliano.
📡IMSI ni namba ambayo inamtumbulisha mtumiaji yeyote wa cellular networks katika mtandao wa mawasiliano.
IMSI ni kama namba za NIDA ambazo kila mtanzania anayo yakwake. Kwenye mawasiliano kila SIM Card ina IMSI yake.
📡Sim cards zinatunza taarifa kama PIN, PUK, IMSI, taarifa za usalama na taarifa kuhusu mtandao.
Pia Sim Cards zinatunza application data ambazo zinatumika kufanya mawasiliano kati ya simu yako na server za mtandao unaotumia.
📡Hapa naongelea kitu kama SMS service number, jina la mtoaji huduma wako, namba za mtoaji huduma na vitu vingine vingi.
Sim Card yako ndicho kiunganishi kati ya simu na akaunti yako kwa mtoa huduma wako. Kiufupi ni kwamba sim card ndiyo inakuunganisha na mitandao.
📡Ninapoongelea akaunti yako kwa mtoa huduma inajumuisha kiasi gani unatumia mtandao wao, mahali ulipo, kiasi cha SMS unazotuma, muda wa maongezi na ni aina gani ya vifurushi/huduma zao unatumia.
📡Hizi ni taarifa ambazo hazipo kwenye simu yako wala Sim Card. Zinatunzwa katika database ya mtoa huduma wako kwenye server zao.
📡Kwa kumaliza niseme kwamba Sim Card ndiyo mlango wa wewe kutumia mtandao kwa namna yoyote ile. Bila Sim Card antenna za simu yako zitadaka radio waves za cellular network na hazitajua zifanye nini na mawimbi hayo.
📡Ni sawa na kuwa mtu mweusi usiyekuwa na utaifa. Utazurula sana bila kukubalika kihalali katika Nchi yoyote ya Afrika.
Unapowasha simu yako Sim card yako inaanza kutafuta mtandao wa kutumia. Hapo ndipo inachambua katika zile radio waves ni mtandao upi unatumika kwako.
📡Bila sim cards Simu yako haiwezi elewa ni radio wave ipi itumike kwako, unapokuwa na sim card sasa ndipo zile taarifa zote ndani ya sim card zinatumika.
Taarifa za jina la mtandao, SMSC na taarifa nyingine za mtoa huduma zinatumika kukuunganisha wewe na mtandao wako.
📡Nilipoongelea base station nilisema kila mtandao unabase station (mnara) yake.
Tufanye unatumia Tigo. Utakapokuwa eneo ambalo hakuna mnara wa tigo unafikisha mawimbi eneo hilo sim card yako itashindwa kutambua ijiunge na mtandao upi.
📡Hapa huwa tunasema, “Sipati mtandao, bars zipo chini kabisa.”. Ndo inakuwa kwamba Sim card imeshindwa kupata mtandao wake husika.
Kulingana na taarifa ilizotunza hakuna mtandao unaendana nazo.
📡Mnara unapopokea ombi la sim card yako kutumia mtandao wake unatumia IMSI yako kuhakikisha kama upo kwenye mnara sahihi na Sim Card yako imethibitishwa kutumia mtandao huo kwa kutumia ule ufunguo wa uthibitisho.
📡Ili kuhakikisha mawasiliano yako yanakuwa salama kuna mfumo wa usalama hapa huwa unatumika.
Mnara utakapo ikuta IMSI yako kwenye rekodi za mtandao itakuthibisha kwa kukutumia funguo. Tuite hii funguo A. Hizi funguo ni copy ya maneno flani ambayo sio rahisi kuyaelewa kibinadam.
📡Baada ya kukuthibitisha kwa funguo A, itatengenezwa funguo nyingine kwa ajili ya mnara tuite Funguo B.
Funguo B itatumwa kuja kwenye simu yako pamoja na funguo A ya uthibitisho. Simu yako itahakikisha funguo A na kutengeneza funguo nyingie C.
📡Funguo C itatumwa kurudi kwenye mtandao pamoja na ile funguo A. Mtandao utaziangalia funguo B & C, kisha kwa kutumia funguo A itahakikisha kwamba funguo B & C zinaendana.
Zikifanana hizo funguo simu yako itapata ruhusa ya kutumia mtandao ambao sim card yako iliomba kutumia.
📡Huu mfumo wa usalama ni ili kuhakikisha hakuna mtu mwingine atatumia namba yako kutumia mtandao, na hizi funguo huwa hazijirudii kwa mtu yeyote. Zikiwa tofauti utakuwa na Sim Card isiyoweza kupata mtandao.
Kwa maelekezo mepesi hivyo ndivyo Sim Card inafanya kazi.
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
📡Lakini wengine ni wale wenye hofu ya kupoteza kazi zao, hasa madereva.
Hakuna wa kumlaumu mtu anayeiogopa AI kwa sababu ni kitu ambacho hata baadhi ya watu wa teknolojia wanashindwa kuelewa vizuri.
📡Miaka 2 iliyopita ungeniuliza iwapo kuna siku AI itaiteka dunia, ningejibu hiv, “Inawezekana iwapo tu tutafikia uwezo wa watu kama Tony Stark wa Iron Man.
Leo baada ya kuelewa AI kidogo nitajibu hivi, “Chochote kinawezekana na haina maana tuache kuboresha kwa sababu ya uoga.”
📡Kwa vizazi vya sasa Mass Surveillance haikuonekana mpaka miaka ya mwisho ya 1940s baada ya UK na USA walikubaliana kubadilishana taarifa za intelejensia.
Baadae katika makubaliano haya ziliongezeka Canada, Australia na New Zealand na kufanya muunganiko huu kuitwa “Five Eyes”.
📡Muungano huu baadae mwaka 1971 ulileta kitu kilichoitwa “Global Surveillance Network” ambayo ilipewa jina la “ECHELON”.
ECHELON ni mtandao maalum wa uliofuatilia mawasiliano ya kijeshi na kidiplomati ya Soviet Union na washirika wake wa Mashariki kipindi cha Vita Baridi.
📡Hakuna Tesla iliyotengenezwa China kuingia nchini India.
Hivi karibuni waziri wa usafiri wa barabara nchini India amesem, aliongea na Elon Musk na kumuomba kwamba Tesla kwa za india zitengenezwe nchini India.
Maalumu kabisa hakutaka Tesla za China kuwepo India.
📡Akongea katika "India Today Conclave 2021", waziri huyo alisema kwamba, Gari za umeme zilizoundwa na Tata Mottors zina ubora unaokaribiana na zile za Tesla.
Hivyo Tesla za kuuzwa India inabidi zitengenezwa ndani ya India na sio China na kuuzwa kutoka India kwenda nchi jirani.
📡Sambamba na hilo alisisitiza kuwa, Tesla watapata sapoti yoyote wanayohitaji kutoka serikali ya India.
Tesla waliomba kupata punguzo la ushuru wa kuingiza gari za umeme India. Mpaka sasa hawajafikia muafaka na serikali ya India kuhusiana na maombi haya yote.
📡Kati ya watumiaji hawa kuna wengi wasiofahamu baadhi ya settings ambazo zinakusanya taarufa zao, zinawafanya waone matangazo mengi au kufanya PC zao ziwe pole pole.
Ukiacha madhaifu ubora wa Win10 ukilinganisha na zile za nyuma, bado ina madhaifu mengi unakutana nayo kila siku
📡Kati ya hayo ni pamoja na kutokuwa na uhuru wa usiri (Privacy) wako, spidi ya OS na urahisi wa kutumia.
Leo tuchambue baadhi ya settings ambazo ni vyema ukaziweka off ili uendelee kutumia Win10 yako kwa raha.
📡Watazamaji wa Sci-Fi movies mtakuwa mmewahi kutana na zile simu ambazo ni kioo tu lakini zinafanya kila kitu.
Huenda huko ni mbali sana kufika labda 2050 huko. Twende mpaka 2030 ambapo nadhani huenda tutakuwa na simu zisizo na button yoyote, headphone jack wala tundu la chaji.
📡Unakumbuka iPhone X ilikuja na notch 2017? ikawa mwanzo wa kubadili muundo wa display za simu. Hapo tayari iPhone hazikuwa na port ya earphone
Oppo F9 ikawa simu ya kwanza kuja na teardrop screen na kumpa mtumiaji nafasi ya kutumia screen nzima.