📡iOS ni Bora kuzidi Android mbali sana 👀

Hii vita tungewapa silaha nani atashinda? Tuachana na hayo tusifike huko.

Hii mada kila ikiwekwa mezani mashabaki wa hizo OS huongelea sana kwamba wanayotumia wao ni bora.

Je, Ni kweli?

#HabariTech
📡Najua kwamba kuna mtu tayari anajizuia sana mpaka amalize kusoma ndipo ajibu.

Kuwa mpole bro/sis maisha sio vita 😁.

Binafsi mimi ni shabiki mkubwa wa Android na huwezi nibadilisha kwa lolote, ila pale ambapo utaalamu utatumika ukweli lazima usemwe.
📡Kwa sababu hiyo kwa kujiamini kabisa naweza kusema kwamba iOS ni bora kuzidi Android kwa mtumiaji wa kawaida wa simu.

Swali tukiacha liwe na mjadala kwamba ipi bora kuna vitu lazima utasikia kutoka pande zote mbili.
📡Vitu utasikia

.Uhuru wa kufanya customization
.Urahisi wa file Sharing
.Side loading APK
.Privacy & Security
.Gharama za in app purchases

Mambo kama yote utayasikia. Unachotetea hapa ni nini?
📡Kikubwa utasikia kwa wengi ni kuhusu iOS kuwa salama zaidi na kujali privacy lakini ina vizuizi vingi🤦‍♂️.

Android ina uhuru mkubwa wa kufanya customization na kuna machaguo mengi ya simu za Android. 😢
📡Miaka 5 iliyopita ungeniambia hizo point ningekuunga mkono bila kuwaza.

Apple wamejitahidi kuondoa vizuizi vingi vilivyokuwepo, haimaanishi kwamba imekuwa customizable kuzidi Android, Hapana.

Upande wa customization Android bado iko juu.
📡Sasa hizi customization zote mtumiaji wa kawaida anazihitaji kweli? 🤷‍♂️

Achana na hawa wataalamu wa teknolojia ambao wanapata raha kuona simu zipo vile wanataka ziwe.

Wewe mtumiaji wa kawaida unahitaji kubadili muonekano wa simu yako?
📡Customization ndiyo ilikuwa moja ya sababu kubwa watu kufanya Jailbreaking na Rooting.

Kwa sasa ni wachache sana ambao bado wanafanya hivyo.
📡Kusema kwamba iOS bado iko limited imepitwa na wakati. Ukizingatia kwamba watu wengi saizi hawahangaiki kubadili launcher, wallpapers au ringingtones.

Sioni mtumiaji wa kawaida akihangaika na hivi vitu.
📡Kwanini UI ya Android inabadilika muonekano kila inapotoka version mpya?

User Experience inaomba kwamba consistency izingatiwe. Hiyo ndo sababu unaona icons za iOS huwa ziko vile vile kwa kila toleo.
📡Navigation ya iPhone imebaki vile vile kwa miaka yote, imebadilika kidogo tu tofauti na Android hehehe 😁.

Mtumiaji wa kawaida aliyekuwa anatumia Android Jelly Bean au Kit Kat muda Mrefu ukimpa hii Snow Cone (Android 12) atakesha hapo.
📡Sitaki kukubali kwamba mtumiaji anahitaji kujifunza na upya kila mara anaponunua simu mpya au kufanya upgrade kwenda OS mpya.

Smartphones inatakiwa zifanye iwe rahisi maisha yetu tusitumie akili nyingi.

Google anafanya nini na Android?
📡Stability ya OS na performance

Wataalamu mara ngapi umelazimika kudowngrade android version kwa sababu update imekuja na makosa mengi?

Vipi upande wa iOS?

Nikisema naweza mshawishi mtumiaji wa iOS kufanya upgrade siku ambayo update imetoka na asipate shida utakubali?
📡ila siwezi mwambia hivyo mtumiaji wa Android.

Wataalamu twende na fact kwa kuzingatia kiasi cha bugs huwa zinakuwepo kwenye Android update.

Mfano mdogo tu hii Android 12. Tuishi hapo kidogo.
📡Tunajua kwamba kuna brand nyingi sana za Android na Google hawawezi tengeneza OS ambayo itafanya kazi bila shida kwa hizi simu zote.

Hongera kwa Apple iOS ni kwa iPhones tu zinazotengenezwa na Apple wenyewe. Inafanya iPhones kufanya kazi vizuri sana.
📡Hapo hatujaongelea RAM.

Ukimpa uwanja @AbilMdone hapa tutakesha. Kwa ufupi ni hivi mfumo wa RAM management wa Android ndiyo unafanya Android ziwe na RAM kubwa vile.

Lakini bado iOS ina RAM management nzuri na zile RAM zake ndogo bado zinafanya vizuri kuzidi za Android.
📡Android huenda zitaanza pokea updates kwa zaidi ya miaka miwili kuanzia mwakani.

iPhone 6S ilitoka 2015 lakini bado inapokea OS updates mpaka leo. Updates ni muhimu hasa kwa usalama wa kifaa chako.
📡Google wanazipa Google pixel kipaumbele zaidi. Zinapokea updates kwa miaka 3 baada ya kutolea. Na updates za security kwa miaka 5.
📡iPhone users mnaweza tuambie mara ngapi umetamani kuinstall app bila kutumia App Store?

Yani kufanya sideloading.

Basi sawa, na wewe wa Android je? Kuna apps zaidi ya 1.85 million Play Store kuna ipi ambayo mtumiaji wa kawaida atahitaji aikose katika hizo?
📡Kulingana na takwimu Android ina usalama mdogo kuzidi iOS. Apple namna wameweka usalama wa iOS inamzuia mtu kuwa huru na mambo mengi ila ndicho kinaweka usalama zaidi.

Google wanatengeneza pesa nyingi kupitia matangazo kwa hiyo wanahitaji kukusanya data za mtumiaji wa Android.
📡Hii inawasaidia kuweza mpa mtumiaji matangazo yanayoendana na namna mtumiaji anatumia Android OS.

Apple na Google wanaigana sana kwenye features lakini mmoja anaboresha kuliko mwingine. Kuboresha huko ndiko kunamfanya Apple aseme "It just works" 😁
📡Kwa ufupi wa huu uzi, OS ipi inamfaa mtumiaji wa kawaida asiye hitaji mambo mengi?

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with HabariTech

HabariTech Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @HabariTech

18 Nov
Sio expert sana upande wa engineering ila naweza jibu hivi.

Sidhani kama quantum computing itakuja kuuzwa kwa watumiaji wa kawaida kama mimi na wewe.

Labda sio kwa miaka 100 ijayo 😁 watumiaji wa kawaida kama mimi na wewe tunahitaji quantum computing ability kwa ajili ya nini?
Anyway tuseme itakuwa available kwa consumers nani yuko tayari kulipia gharama za kumiliki na kumaintain running costs za quantum computer?

Kila mtu anatamani kuwa na kifaa chenye super conducting ability, ila nikiwaza huo umeme wake 😂.
Alafu kuna ishu ya cooling. Kifaa cha quantum kinahitaji kuwa na cooling system iliyopo efficient sana na inaweza kuwa kubwa sio kawaida.

Kitu ambacho kufit kwenye PC ni meh! 🤔

Quantum computers zina advantage kunwa zikitumika kwenye sehemu kama data centers.
Read 5 tweets
8 Nov
📡Tabia zinazo haribu PC yako kwa haraka.

Sisi sote tunapenda kuona vifaa vyetu kama PC zikidumu kwa muda mrefu, lakini mara nyingi huwa zinaharibika mapema tofauti na mategemeo yetu.

#HabariTech Image
📡Huenda tabia zetu na namna tunatumia hivi vifaa ikawa ni sababu ya hizi mashine kuharibika haraka Image
📡Hakuna kitu kinachodumu milele na hasa vifaa vya elektroniki. Watengenezaji wa vifaa hutengeneza vifaa wakiwa na malengo kwamba kwa matumizi sahihi hicho kifaa kitadumu kwa miaka kadhaa.

Muda huo huwa sahihi ukitumia ipasavyo kwa usahihi.

Nini kinaua PC yako mapema?
Read 23 tweets
21 Oct
📡Part 2: Sim Cards zinaiwezesha vipi simu kufanya kazi?

Simu yako haina maana kama utashindwa kupiga/kupokea simu za kawaida au kutuma SMS.

Unapokuwa na simu utahitaji kuunganishwa na mtandao flani ili kupata huduma ya za simu.

#HabariTech
📡Unapochagua kusajili sim card ya mtandao uupendao unakuwa umesajili akaunti ambayo utakuwa unailipia bando ili kuweza pata huduma zao.

Huwa tunasema SIM Card bila kujua maana yake ni nini.
📡SIM ni kifupi cha Subscriber Identity Module. Ni card ambayo inatunza IMSI (International Mobile Subscriber Identity) na funguo za kumtambulisha na kumthibitisha mtumiaji katika mfumo wa mawasiliano.
Read 18 tweets
15 Oct
📡A.I inajifunza kujitengeneza Yenyewe

Hofu kubwa ya watu duniani ni kuona AI ikiiteka dunia na binadamu tukawa ni watumwa wa AI.

Wenye hofu wengi ni watazamaji wa filamu kama Terminator, iRobot, Transcendence na Matrix.

#HabariTech
📡Lakini wengine ni wale wenye hofu ya kupoteza kazi zao, hasa madereva.

Hakuna wa kumlaumu mtu anayeiogopa AI kwa sababu ni kitu ambacho hata baadhi ya watu wa teknolojia wanashindwa kuelewa vizuri.
📡Miaka 2 iliyopita ungeniuliza iwapo kuna siku AI itaiteka dunia, ningejibu hiv, “Inawezekana iwapo tu tutafikia uwezo wa watu kama Tony Stark wa Iron Man.

Leo baada ya kuelewa AI kidogo nitajibu hivi, “Chochote kinawezekana na haina maana tuache kuboresha kwa sababu ya uoga.”
Read 17 tweets
12 Oct
📡Mass Surveillance Afrika na Duniani kote.

Huu ni uchunguzi ambao unajikita kufatilia umati mkubwa wa watu na mara nyingi huwa kwa kigezo cha kupunguza uharifu na kuzuia ugaidi.

Mass surveillance inasemakana kuanza miaka ya 3800 kabla ya kristo huko Babylon.

#HabariTech Image
📡Kwa vizazi vya sasa Mass Surveillance haikuonekana mpaka miaka ya mwisho ya 1940s baada ya UK na USA walikubaliana kubadilishana taarifa za intelejensia.

Baadae katika makubaliano haya ziliongezeka Canada, Australia na New Zealand na kufanya muunganiko huu kuitwa “Five Eyes”. Image
📡Muungano huu baadae mwaka 1971 ulileta kitu kilichoitwa “Global Surveillance Network” ambayo ilipewa jina la “ECHELON”.

ECHELON ni mtandao maalum wa uliofuatilia mawasiliano ya kijeshi na kidiplomati ya Soviet Union na washirika wake wa Mashariki kipindi cha Vita Baridi. Image
Read 19 tweets
11 Oct
📡Hakuna Tesla iliyotengenezwa China kuingia nchini India.

Hivi karibuni waziri wa usafiri wa barabara nchini India amesem, aliongea na Elon Musk na kumuomba kwamba Tesla kwa za india zitengenezwe nchini India.

Maalumu kabisa hakutaka Tesla za China kuwepo India.

#HabariTech
📡Akongea katika "India Today Conclave 2021", waziri huyo alisema kwamba, Gari za umeme zilizoundwa na Tata Mottors zina ubora unaokaribiana na zile za Tesla.

Hivyo Tesla za kuuzwa India inabidi zitengenezwa ndani ya India na sio China na kuuzwa kutoka India kwenda nchi jirani.
📡Sambamba na hilo alisisitiza kuwa, Tesla watapata sapoti yoyote wanayohitaji kutoka serikali ya India.

Tesla waliomba kupata punguzo la ushuru wa kuingiza gari za umeme India. Mpaka sasa hawajafikia muafaka na serikali ya India kuhusiana na maombi haya yote.
Read 5 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(