TUMEWAHI KUWA NA CHANJO KWA MALENGO YA KISHUSHUSHU

Thread..

Kadiri ulimwengu unavyobadilika, stadi ya Ujasusi inazidi kuwa complex kwa kuhusisha mbinu ambazo nyingine ukizisikia unaweza kudhani labda watazama sinema au waota, lakini ndio uhalisia wa ulimwengu ulipo sasa katika
katika juhudi za mataifa na makampuni makubwa kupanua ushawishi wao juu ya dunia yote na kulinda maslahi.

Kuna kisa cha tofauti sana ningependa nikijadili leo hii. Kisa cha tofauti kabisa..

Wengi tutakuwa tumewahi kusikia shirika linaloitwa “Save the Children”. Ni moja ya…
Shirila kubwa zaidi la misaada ya kibinadamu ulimwenguni ambalo limejikita hasa kwenye kutoa misaada inayolenga kuboresha hali za maisha ya watoto wadogo.

Mwaka 2011 shirika hili lilikuwa kwenye shughuli zake mahala paitwa Khyber nchini Pakistan.
Save the Children walikuwa na…
wanaendesha mradi wa kupambana na utapiamlo kwa watoto.
Mradi huu walikuwa wanautekeleza kwa kushirikiana na wataalamu wa afya wa eneo hili. Na moja ya wataalamu hawa alikuwa ni Daktari bingwa anayeitwa Shakir Afridi.
Huyu somo alikuwa ni daktari wa kutegemewa wa eneo hili.
Lakini licha ya ubingwa wake wa masuala ya afya, huyu somo alikuwa kwenye matatizo makubwa dhidi ya kikundi cha wapiganaji wanaojiita “Lashkar-e-Islam”

Hawa walikuwa ni wapiganaji ambao walikuwa na ushawishi mkubwa sana kwenye eneo hili
Wajua nchi ya Pakistan namna inavyoongozwa
Ni tofauti mno na sehemu nyingi duniani. Pale Pakistan sio serikali pekee yenye nguvu bali pia makabila pamoja na vikundi vya wapiganaji hasa maeneo ya pembezoni mwa nchi

Sasa, wapiganaji wa kikundi hiki walikuwa wanamlazisha Dr. Afridi awalipe kiasi cha $80,000
Sababu ya kutaka
Walipwe hela hii, walikuwa wanadai kwamba ili ni faini kutokana na ‘kosa’ la Dr. Afridi kuwachaji wananchi hela nyingi mno anapowapatia huduma za kiafya.
Yaani kwamba, walidai wananchi wanalalamika kuwa Dr. Afridi huwapa bili kubwa mno akishawapatia matibabu kuzidi uhalisia.
Kwa hiyo wapiganaji wa kikundi hicho ambao walikuwa wameweka mkononi eneo hili, wakampa “onyo” la $80,000

Hiki kilikuwa ni kiwango kikubwa mno kwa Dr. Afridi ukizingatia kwamba wiki chache zilizopita watu hawa hawa alikuwa amewalipa $21,000 kwa faini ya kosa jingine

Sasa, mmoja
wa wafanyakazi wa Save the Children akafahamu changamoto hii inayomkabili Dr. Afridi.
Akamweleza Afridi kwamba kuna mtu anataka kumtambulisha kwake ambaye anaamini kwamba anaweza kumsaidia.

Siku mbili baadae mfanyakazi huyo akamtambulisha Afridi kwa mwanamama ambaye alikuja…
kumfahamu kwa jina moja tu la “Sally”.
Dr. Afridi na Sally walionana kama mara tatu hivi na kila walipoongea waliongea masuala kadhaa wa kadhaa ambayo Sally alikuwa akimuuliza maswali kama kumdadisi
Hatimaye Sally akamkabidi kiasi cha $100,000 na kumweleza kwamba ana kazi maalumu
Wiki kadhaa baadae Dr. Afridi alikuja kufahamu kwamba “Sally” alikuwa ni Afisa wa Shirika la Ujasusi la CIA.
Na kwa muda wa miezi kadhaa CIA wamekuwa wakimfutilia nyendo zake kumtathimini.

Baada ya vikao vingine kadhaa kati ya Sally na Afridi hatimaye dokta akatambulishwa kwa..
mtu mwingine tena anaitwa Amir Aziz.
Huyu Amir alikuwa naye ni daktari bingwa hapo Pakistan. Amir Aziz alikuwa anafahamika kwa msimamo wake mkali wa kuunga mkono vikundi vya wapiganaji wa kidini.
Jambo ambalo kipindi hicho alikufahamika ni namna ambavyo Amir alikuwa anatumia hii
cover kuwa karibu na wapiganaji wa vikundi hivyo ili kufanyakazi anayotumwa na CIA
Kutokana na msimamo wake mkali, Amir mara nyingi alikuwa anasafirishwa kwenda kutibia viongozi wa vikundi kama vile Taliban. Kwa zaidi ya miaka mitano CIA walikuwa wakimtumia kupata medical records
za viongozi hao wa vikundi vya wapiganaji pamoja na sampuli zao za damu ambazo ziliingizwa kwenye database ya CIA.

Kwa hiyo Dr. Afridi akakutanishwa na somo huyu Amir Aziz na wakaanza kufanyakazi pamoja kwa niaba ya CIA.

Mwezi February mwaka 2011 Sally alimfuata Dr. Afridi na..
kumweleza kwamba alikuwa anakazi maalumu ambayo alikuwa anahitaji aifanye. Kazi muhimu zaidi kuliko kazi yoyote ambayo amewahi kumtuma.

Akamweleza kwamba, kuna nyumba iko maeneo ya Abbottabad. Nyumba hiyo ya kifahari wakazi wa hapo Abbottabad wameibatiza jina “Waziristan Haveli”
ikimaanisha “Kasri la Waziristan”.

Sally akamweleza Dr. Afridi kwamba wanahitaji kupata sampuli za damu za watoto wote wanaoishi kwenye kasri hilo. Sio watu wazima, hapana.. sampuli za damu za watoto

Akamweleza kwamba CIA wamebuni mkakati wa namna gani sampuli hizo zitapatikana
Dr. Afridi ataaandika ‘proposal’ kuomba fedha toka shirika la misaada la USAID. Proposal yake hii itahusu mpango wa yeye kutoa chanjo kwa watoto dhidi ya Homa ya Ini - HBV (Hepatitis B Virus).

Chanjo hii itatolewa mahususi kwenye eneo hilo la Abbottabad.

Sally akamweleza Afridi
kwamba chanjo hiyo ataitoa kwa watoto wote wa eneo la Abbottabad lakini ikifika zamu ya kuwapa chanjo watoto waliomo kwenye hilo jumba wanalolilenga, atapaswa atumie ujuzi wake wote kubakisha damu kwenye mabomba ya sindano atakayowachomea chanjo na kisha mabomba hayo ya sindano..
ayatenge pembeni na kuyahifadhi kwenye ‘cooler box’ na kisha aje kumkabidhi Sally.

Kwa hiyo mwezi huo February Dr. Shakil Afridi akaandika proposal kwenda USAID kuomba “msaada” wa $140,000 ili aweze kufanikisha wiki mbili za utoaji chanjo kwa watoto wa Abbottabad.

Mwezi March…
USAID wakampatia Dr. Afridi hiyo grant.

Dr. Afridi akaandaa timu ya manesi wake wapatao 12 kwa ajili ya kumsaidia kwenye zoezi hili.

Nidokeze jambo hapo. Dr. Afridi hakuwa anajua kwa nini CIA walikuwa wanataka sampuli za damu za watoto waliopo kwenye hilo jumba hapo Abbottabad.
Kwa nini CIA walikuwa wanasaka hizo sampuli za damu?

Kwa zaidi ya miaka 11 toka kutokea kwa shambulizi la 9/11 vyombo vya ulinzi vya Marekani wakiongozwa na CIA walikuwa wanahaha kumsaka mastermind wa ugaidi duniani bwana Usama Bin Laden.
Walikuwa wametumia kila aina ya mbinu na
Kila rasilimali bila mafanikio. Lakini juhudi zao hizo baadae zikaanza kuzaa matunda baada ya miaka 11.

Kwenye upelelezi wao wa miaka 11 waligundua jambo la ajabu sana. Kwamba kila kamanda wa Al-Qaida waliyekuwa wanamkamata na kumtesa kwenye black-sites zao, wote baada ya mateso
walikuwa wanaeleza kwamba wana miaka kadhaa hawajawahi kuonana na Bin Laden. Ilikuwa ajabu mpaka mtu kama KSM ambaye alikuwa ni kiongozi wa juu kabisa naye hakuwa ameonana na Osama kwa miaka kadhaa.

Wote walikuwa wanaeleza kwamba maagizo toka kwa Osama yalikuwa yanafikishwa kwao
kwa mdomo au barua na mtu anayeitwa “Abu Ahmed al-Kuwait”
Kwamba huyo somo ndiye mtu pekee chini ya jua mwenye ‘access’ ya kuonana na Bin Laden.

Hii ilikuwa ajabu sababu CIA walikuwa wanajua viongozi wote wa Al-Qaida lakini hawakuwahi kumsikia huyu mtu

Ikabidi CIA ibadili mbinu
Baadae kidogo naweka mwendelezo wa huu uzi.

Pia nimetengeneza Group la Whatsapp ambalo nachambua kwa wingi zaidi makala zihusuzo masuala ya Ujasusi na mikasa ya kweli inayotikisa ulimwengu.
Tunalipia kiasi cha shilingi elfu tano kwa mwezi kuwa member.
Nitumie ujumbe 0759 181 457
SEHEMU YA 2

Kwa hiyo baada ya CIA kuambiwa na makamanda kadhaa wa Al-Qaida waliowakamata kwamba maagizo toka kwa Bin Laden wanayapata kupitia kwa mtu anayeitwa Abuu Ahmed al-Kuwait na kwamba wana miaka mingi hawajawahi kuonana na Osama.

CIA wakaamua kubadili mbinu kimkakati..
Badala ya kutumia rasilimali nyingi na muda kumtafuta Bin Laden, CIA wakaamua kwamba wabadili lengo. Badala ya kumtafuta Bin Laden, waweleze nguvu zao kumtafuta “Abuu Ahmed al-Kuwait”.

Walihisi kwamba, kama al-Kuwait alikuwa ndiye mtu pekee ambaye anasemekana kuwa na ‘access’…
kuonana na Bin Laden, maana yake ni kwamba kama wakiweka kumpata al-Kuwait, wanaweza kumtumia yeye kuwaongoza mpaka kumpata Bin Laden.

Sasa, nimewahi kuandika makala maarufu inayoitwa “Geranimo E.K.I.A” (Operation Neptune Spear) ambayo ndani yake nimeeleza hatua kwa hatua namna
ambavyo CIA waliweza kuendesha oparesheni kadhaa za kishushushu mpaka hatimaye kufanikiwa kumtambua “Abuu Ahmed al-Kuwait” ni nani na wapi anaishi.

Tafadhali itafute makala hii na kuisoma.

Sasa, kwa kifupi tu, CIA walikuja kufahamu kwamba Abuu Ahmed al-Kuwait jina lake halisi..
Anaitwa Ibrahim Saeed Ahmed. Wakafahamu kwamba alikuwa akiishi nchini Pakistan eneo laitwa Abbottabad kwa jina lingine la bandia la Arshad Khan.

CIA walipofanya uchunguzi zaidi kwenye eneo hilo la Abbottabad, wakagundua kwamba al-Kuwait alikuwa akiishi na familia yake pamoja na
Kaka yake pamoja naye na familia yake kwenye jumba kubwa mtaani hapo.

Kwa namna ambavyo jumba hili lilikuwa limejengwa lilikuwa linatia mashaka.
Kwa kutumia Idara ya Ujasusi wa Anga na Ramani ya Marekani (National Geo-Spatial Intelligence Agency) CIA walifanikiwa kupata ramani
ya nyumba hiyo na mjengeko wake.

Namna ambavyo jumba hili lilikuwa limejengwa ilikuwa inatia mashaka sana.
Nyumba ilikuwa na layer mbili za ukuta wa Ulinzi. Yaani ukipita ukuta wa kwanza kwa ndani unakutana na eneo kubwa la wazi kisha kuna ukuta mwingine na geti lingine. Pia…
ukuta wenyewe ulikuwa mrefu mno kupita urefu wa kawaida unaotakiwa kwenye nyumba ya makazi ya kiraia.

Lakini pia nyumba ilikuwa na madirisha madogo sana ikionekana kama tahadhali ya watu wasione ndani hata kwa darubini.
Lakini pia nyumba ilikuwa na camera kadhaa za ulinzi.
Wakazi wa eneo hili walikuwa wameibatiza nyumba hii jina la “Waziristan Haveli” (Kasri la Waziristan)
Sababu Al-Kuwaita alipohamia hapo mtaani alikuwa amewaambia wenyeji wake kuwa yeye ni mzaliwa wa mkoa wa Waziristani.

Sasa, namna nyumba hii ilikuwa imejengwa kwa tahadari na…
na kiwango kikubwa cha usalama, ukijumlisha kwamba al-Kuwait ndio mtu pekee waliambiwa kuwa ana ‘access’ ya kuonana na Osama, iliwafanya CIA wahisi kwamba jumba hilo lina uwezekano mkubwa wa kuwa linamuhifadhi mtu muhimu zaidi wanayemtafuta kwa udi na uvumba kwa zaidi ya miaka 20
Lakini hawakuwa na namna nyingine ya kuthibitisha huu wasiwasi wao kwamba yawezekana Osama pia yuko anaishi ndani ya nyumba hiyo.

Sasa, ili kujiridhisha ndio wakaamua wafanya ule mpango wa chanjo feki kwa kumtumia Dr. Shakil Afridi kama ambavyo nilikuwa nimeanza kuwaeleza.
Kwa hivyo Dr. Afridi akapewa grant na shirika la USADI.
Akaunda timu yake ya manesi 12 kumsaidia.

Mwezi April akaingia kazini kutoa chanjo hiyo feki ya homa ya ini kwa watoto wa eneo la Abbottabad.

Wiki ya kwanza chanjo ilitolewa kwenye mitaa waishia watu wa hali ya chini kama
vile mitaa ya Nawa Sher.
Wiki iliyofuata Dr. Afridi na timu yake wakaamza kutoa chanjo kwenye mitaa ya watu wenye uwezo kama vile mtaa wa Tabil ambapo ndipo hasa jumba hilo linaloshukiwa na CIA lilipo.

Ilipofila zamu ya kutoa chanjo kwa watoto waliopo kwenye hilo.. wenyeji wao..
waliwakaribisha kwa bashasha mpaka ndani.
Manesi “wakatoa chanjo” na kama ambavyo walikuwa wameelekezwa, kwa ustadi mkubwa wakaacha damu kwenye mabomba ya sindano ambazo zilitumika kudunga chanjo watoto wa nyumba hii.

Mabomba haya ya sindano Dr. Afridi akaenda kumkabidhi “Sally”
ambaye naye akayasafirisha mpaka kambi ya kijeshi ya Marekani ya Bagram iliyoko nchini Afghanistan.

Marekani walikuwa na sampuli ya vinasaba vya dada yake Osama ambaye alifariki jijini Boston nchini Marekani mwaka 2010

Vinasaba vya damu hizi zilipolinganishwa zikakutwa zinaoana
ikimaanisha kwamba baadhi ya watoto wale kwenye lile jumba walikuwa ni watoto wa Usama bin Mohammed bin Awad bin Laden.

Taarifa ikatumwa makao makuu ya CIA nchini Marekani.
Kisha taarifa moja kwa moja ikapelekwa kwa Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Marekani Barack Obama kipindi hicho..
Baada ya kupatikana kwa hii confirmation iliyokuwa inahitajika.. ndipo ukafanyika uamuzi wa kufanywa oparesheni ya mahiri ya kijeshi kuvamia hilo jumba bila taifa la Pakistan wenyewe kujua.

Nimendika pia kwa undani kuhusu Oparesheni hii hatua kwa hatua.. kuanzia maandalizi yake,
utekelezwaji wake mpaka kuhitimishwa katika makala yangu ya “Geranimo EKIA”. Hakikisha unaipata makala hiyo na kuisoma.

Kwa andishi hili nitaishia hapa.
Huu ulimwengu wetu umejawa na siri nzito sana.

Until next time…

Habibu B. Anga
To Infinity and Beyond
0759 181 457

• • •

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
 

Keep Current with Habibu B. Anga

Habibu B. Anga Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @habibu_anga

14 Oct
𝗕𝗜𝗡𝗧𝗜 𝗝𝗔𝗦𝗨𝗦𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗜𝗔𝗞𝗔 25 𝗔𝗡𝗔𝗬𝗘𝗜𝗧𝗜𝗞𝗜𝗦𝗔 𝗔𝗙𝗥𝗜𝗞𝗔 𝗠𝗔𝗦𝗛𝗔𝗥𝗜𝗞𝗜

Thread..

Siku ya 30 May 2019, maafisa Usalama Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JKIA, Nairobi walimuweka kizuizini abiria mmoja mwenye hati ya kusafiria ya kidiplomasia, mwanaume.. Image
wa asili ya kisomali. Japokuwa watu wenye diplomatic passport wapata exemptions kadhaa kwenye kaguzi za uwanja wa ndege, lakini ilikuwa ni lazima kwa maafisa hawa kumuhoji abiria huyu kutokana na utata wa mzigo ambao alikuwa nao.

Huyu somo alikuwa na briefcase ambalo ndani yake
alikuwa amebeba fedha cash dola za Kimarekani milioni moja na nusu.

Mtu huyu nyaraka zake zilikuwa zinaonyesha kwamba alikuwa safarini kuelekea nchini Ethiopia.

Maafisa hawa wa Usalama. Wakaanza kumuhoji abiria huyu sababu za kusafiri na kiwango kikubwa hivyo cha fedha na pia.. Image
Read 98 tweets
4 Sep
𝗞𝗔𝗕𝗟𝗔 𝗬𝗔 𝗜𝗞𝗨𝗟𝗨.. 𝗞𝗪𝗔𝗡𝗭𝗔 𝗔𝗗𝗛𝗔𝗕𝗨 𝗬𝗔 𝗞𝗜𝗙𝗢

Thread..

Ukiwa unatoka Lusaka kwenda Jimbo la Magharibi, kabla hujaingia mji wa Mongu kuna kipande cha barabara kinajulikana kama Limulunga Road.
Kipande hiki cha barabara mwaka juzi kimetupa tukio la kipekee
ambalo kwa kiwango kikubwa tukio hili limebadili mwelekeo wa siasa la bara zima la Afrika na hasa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.

Pengine pasipo tukio hili huyu Hichilema tunayemuona leo asingelikuwa Rais. Lilikuwa tukio la kipekee kabisa..

Kila mwaka pale Zambia huwa wana
sherehe maarufu zinaitwa "Kuomboka Ceremony".
Wenzetu mpaka leo hii bado wanatambua cheo cha asili cha "Litunga" ambaye ni Mfalme wa kabila la Walozi.
Kila mwaka mwishoni mwa msimu wa mvua mfalme huwa anahama kutoka makazi yake ya bondeni ya Lealui na kuhamia makazi yake yaliyo..
Read 41 tweets
10 Aug
𝗨𝗧𝗔𝗝𝗜𝗥𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗦𝗛𝗔𝗞𝗔 𝗪𝗔 𝗪𝗔𝗟𝗜𝗡𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗩𝗜𝗢𝗡𝗚𝗢𝗭𝗜

Thread..

Mwaka juzi kwenye hafla ya mapokezi ya ndege kwenye nchi fulani hivi hapa Afrika Mashariki kuna incident ndogo tu ilitokea lakini wengi ikatufikirisha sana.

Dakika chache baada ya Rais wa...
nchi hiyo kumaliza kuongoza hafla hiyo ya mapokezi ya ndege akashuka jukwaani na akianza kuandoka.
Lakini kabla hajakwenda kupanda gari, kama ambavyo ilikuwa ada kwa Rais yule akaelekea upande waliokaa wananchi wake na ili awasalimie.
Na kusalimia huku akaanza jukwaa ambalo...
walikuwa wamekaa wageni VIP.

Wageni wale mashuhuri wakasimama na Rais akawa anapita akiwapa mkono.

Mojawapo ya wageni wale mashuhuri alikuwa ni mfanyabiashara maarufu sana mwenye asili ya kihindi.
Rais alipopita mbele yake, mfabiashara huyu akanyoosha mkono ili asalimiane na...
Read 25 tweets
20 Jul
UZI
👇👇

Tujadili kidogo Executive Protection.
Hapa chini nimeweka picha za inner cycle za ulinzi wa Rais JPM, Samia, Ndayishimiye (Burundi) na Mnangagwa (Zim).

Kwa kila Rais utaona 'First Ring' zao (hao walinzi wanaomzunguka Rais muda wote) lazima kuna afisa mmoja au wawili..
amebeba begi la mkononi

Umewahi kujiuliza hilo begi lina dhumuni gani.?

Hiyo picha hapo juu, JPM alikuwa chato na hapo alikuwa anakwenda kwenye kibanda cha simu kusajili line yake kwa alama ya vidole
Kwa hiyo hakuwa kwenye ziara au anakwenda kikaoni.. sasa hilo begi ni la nini?
Na si yeye tu.. siku ukibahatika kuwa mahala ambako Rais SSH yupo, tazama kwa makini wale walinzi wake, hasa ile 'first ring', wale walinzi wenye suti wanaomzunguka.. utaona vivyo hivyo pia, kuna maafisa wawili au watatu wana mabegi ya dizaini hii wamebeba mkononi.
Read 25 tweets
17 Jul
𝗡𝗔𝗡𝗜 𝗔𝗟𝗜𝗠𝗧𝗘𝗞𝗔 𝗠𝗧𝗢𝗧𝗢 𝗪𝗔 𝗥𝗔𝗜𝗦, 𝗠𝗔𝗭𝗜𝗠𝗕𝗨, 𝗠𝗢𝗥𝗢𝗚𝗢𝗥𝗢.?

FINALE

Naam, niwamalizie sasa hiki kisa. Kama haujasoma sehemu ya kwanza, angalia kwenye profile yangu juu kabisa pinned tweet.

Sasa,

Wale wakimbizi waliorejea SA, tokea hapa Morogoro...
wakaeleza namna ambavyo waliishi kambini Mazimbu na kijana anayeitwa Louis Mathakoe ambaye sasa hivi wanaonyeshwa picha kwamba identity halisi kijana huyo ni mtoto wa Rais Mbeki.

Wajumbe wa Tume ya TRC walivyo endelea kuhoji kuhusu nyendo za kijana Kwanda akiwa hapo Mazimbu..
Ndipo wakaelezwa nini kilimpata kijana Kwanda pale Mazimbu.

Wakimbizi hawa walieleza kwamba kijana huyo aliishi kambini Mazimbu kuanzia mwaka 1983 mpaka mwaka 1989.
Wakaeleza kwamba kuna siku kambini hapo walifika watu ambao waliwahisi kuwa ni maafisa wa vyombo vya ulinzi vya...
Read 25 tweets
16 Jul
𝗡𝗔𝗡𝗜 𝗔𝗟𝗜𝗠𝗧𝗘𝗞𝗔 𝗠𝗧𝗢𝗧𝗢 𝗪𝗔 𝗥𝗔𝗜𝗦, 𝗠𝗔𝗭𝗜𝗠𝗕𝗨, 𝗠𝗢𝗥𝗢𝗚𝗢𝗥𝗢.?

Kuna masuala huwa yanakuwa salama yakiachwa bila kuzungumzwa. Sababu ukianza kuhoji kuhusu ukweli na undani wake, unajikuta unafungua mlango wa hatari ambazo pengine hauko tayari kuzikabili...
Mojawapo ya masuala haya ni madhira ambayo yanafanywa na watu tuliowapa madaraka. Nyendo zao, na siri zao ni kana kwamba haupaswi kutamani kuzifahamu.

Lakini binadamu tumeumbwa na kiu ya kutaka kujua, na kiu hii ni kama upele, hauachi kuwasha mpaka uukune
Na pia historia ya nchi
zetu haiweze kukamilika kwa vizazi vinavyo kunufaika, kama kuna mawe tutayaacha yakiwa yamefunikwa.

Sasa,

Mojawapo ya skandali mbaya sana kwenye bara hili la Afrika, ni tukio la mtoto wa Rais ambaye alidhaniwa amefia mjini Lusaka, Zambia lakini baadae ikaja kuthibitika kwamba..
Read 25 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal

Or Donate anonymously using crypto!

Ethereum

0xfe58350B80634f60Fa6Dc149a72b4DFbc17D341E copy

Bitcoin

3ATGMxNzCUFzxpMCHL5sWSt4DVtS8UqXpi copy

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(