UZI
πŸ‘‡πŸ‘‡

Tujadili kidogo Executive Protection.
Hapa chini nimeweka picha za inner cycle za ulinzi wa Rais JPM, Samia, Ndayishimiye (Burundi) na Mnangagwa (Zim).

Kwa kila Rais utaona 'First Ring' zao (hao walinzi wanaomzunguka Rais muda wote) lazima kuna afisa mmoja au wawili..
amebeba begi la mkononi

Umewahi kujiuliza hilo begi lina dhumuni gani.?

Hiyo picha hapo juu, JPM alikuwa chato na hapo alikuwa anakwenda kwenye kibanda cha simu kusajili line yake kwa alama ya vidole
Kwa hiyo hakuwa kwenye ziara au anakwenda kikaoni.. sasa hilo begi ni la nini?
Na si yeye tu.. siku ukibahatika kuwa mahala ambako Rais SSH yupo, tazama kwa makini wale walinzi wake, hasa ile 'first ring', wale walinzi wenye suti wanaomzunguka.. utaona vivyo hivyo pia, kuna maafisa wawili au watatu wana mabegi ya dizaini hii wamebeba mkononi.
Pia kama ulifuatilia juzi Rais SSH alipokwenda ziarani nchini Burundi.. kwenye 'inner cycle' ya walinzi Idara ya Ujasusi ya Burundi ambao waliokuwa wanawalinda yeye na Rais Ndayishimiye kwenye hasa ile 'first ring' kulikuwa na walinzi kadhaa ambao nao wana mabegi ya dizaini hii.
Na mfano mwingine ni Rais Emmerson Mnangagwa. Mara zote akionekana maeneo ya umma lazima baadhi ya walinzi wake pia wana mabegi ya dizaini hii.
Kwa mfano tazama hapa chini gari yake ikiwa imezingirwa na walinzi. Kuna maafisa kadhaa wana mabegi na dizaini hiyo pia...
Naweza nikakupa mifano mingine mingi tu wa walinzi wa marais kama vile Paul Kagame, Edgar Lungu, Filipe Nyusi, Cyril Ramaphosa n.k. ambao wote pia walinzi wao kwenye 'first ring' lazima kuna maafisa ambao wanabeba begi la namna hii.

Kwa hiyo narejea swali, hili begi lina nini.?
Wakati fulani niliwahi kuona watu mtandaoni wakijadili kuuliza kuhusu haya mabegi enzi za JPM.
Na katika mijadala ile kulikuwa na majibu matatu ambayo watu ndio walikuwa wakijadili sana na majibu haya matatu hayakuwa sahihi

Kuna watu walisema mabegi yale ni mabegi ya kawaida tu
walinzi wanambebea mzee document zake na personal effects za Rais kama vile saa, notebooks n.k.

Jawabu la pili, kuna watu walikuwa wanasema kwamba begi hili ndani yake lina vifaa vya huduma ya kwanza. Yaani kwamba, lina vifaa vya kidaktari ambavyo vyaweza kutumika kutoa huduma..
ya kwanza kwa dhahrura kama ikitokea Rais amejeruhiwa.

Jawabu la tatu, kuna watu wanasema kwamba begi hili lina silaha ndani yake.

Majibu yote haya matatu hayako sahihi. Hizi sio dhima za begi hizi unazoziona kwa maafisa wa ulinzi wa Rais hasa ile 'first ring' inayomzunguka..
Kabla sijajadili begi hizi zina kazi gani, kwanza tuangalie kwa nini majibu haya matatu sio sahihi.

Tuanze na jibu la kwanza kwamba begi lina personal effect za Rais.
Si sahihi kwa sababu kiprotokali personal effect za Rais zinabebwa na Mpambe wake (ADC). Ndio maana ukitazama..
Utaona kwamba Mpambe wa Rais ana begi la mkononi na baadhi ya maafisa wa ulinzi nao wana mabegi ya mkononi.
Hili begi linalobebwa na ADC ndilo lenye vitu binafsi vya Rais wakati mabegi yale mengine ya maafisa wa ulinzi yana shughuli nyingine kabisa.
Jawabu la pili kwamba mabegi haya ya maafisa wa ulinzi wa Rais yana vifaa ya huduma kwanza nalo si sahihi kwa sababu, mahala popote Rais anapokwenda lazima ana daktari wake pamoja na ambulance. Hii ambulance inakuwa equipped na vifaa vyote muhimu kwa ajili ya matibabu ya dharura
mpaka akiba ya damu ya blood group la Rais. Ambulance hii inakuwa equipped kwa capabilities za daktari wake kuweza hata kumfanyia upasuaji mdogo wa dharura ikihitajika kufanyika hivyo.
Kwa hiyo, vifaa tiba vinabebwa kwenye ambulance na sio zile begi.

There is an exception though
kuna mara chache sana (nasisitiza mara chache sana) kwenye first ring ya ulinzi wa Rais afisa mmojawapo anatakiwa kubeba first aid kit.

Kwa mfano, kwa mujibu wa taarifa ambayo serikali ilitoa, walisema kwamba mpendwa wetu JPM alikuwa akiugua maradhi ya moyo kwa muda mrefu sana..
Sasa, kuna kitu sijui wangapi wali-notice. Katika miezi sita ya mwisho ya maisha ya JPM (kuanzia Aug 2020 mpaka Feb 2021) kwenye first ring ya ulinzi wake kulikuwa lazima kuwe na afisa amebeba ki-briefcase kidogo kama kibox hivi au cooler (tazama picha)

Yaani kulikuwa na maafisa
ambao walikuwa wanabeba yale mabegi meusi kama kawaida. Lakini pia kulikuwa na afisa mmoja ambaye muda woye yuko kando ya Rais akiwa na hiki kijibriefcase

Hii fasiri yake ni kwamba kwenye kipindi hiki hali ya maradhi ya mpendwa wetu ilikuwa mbaya na hivyo daktari wake akaelekeza
lazima muda wote kuwe na vifaa vya dharira vya tiba pembeni yake kama ikitokea hali yake imebadilika ghafla.
Kwa hiyo kijibriefcase hiki, kina vifaa mahususi kabisa kwa ajili ya matibabu ya dharura ya maradhi ambayo yalikuwa yanamsibu mpendwa wetu kipindi kile.

Hii ni exception
ndio maana sasa hivi hauoni mlinzi yeyote wa Mama SSH akiwa na kijibriefcase cha namna ile lakini bado wangali na walinzi wenye yale mabegi meusi kama kawaida

Jawabu la tatu kwamba begi hizi zina silaha si sahihi kwa sababu kadhaa.
Mosi, hao walinzi wote unaowaona wamevaa kaunda
suti. Wote wana side-arm kiunoni na wengine kiunoni na mguuni.

Pili, pengine wengi hawajui hili, kwamba kwa mfano likitokea shambulio la ghafla kwa Rais. Hii first ring ya ulinzi wa Rais kwa protokali za "Executive Protection" wao hawatakiwa kujibu mapigo, bali kazi yao ni...
kumuondoa Principal (Rais) kwenye eneo la hatari na kumpeleka eneo salama
Hawa uniformed officers tunaowaitaga 'makirikiri', hawa wao ndio wanatumika kama CAT (Counter Assault Team).
Hawa ndio wanajibu mashambulizi mpaka eidha wa-neutralize hiyo threat au mpaka Principal afike...
Mahala salama.
Lakini pia kwenye msafara kuna gari ambalo latumika kama hifadhi ya akiba ya ammunition, mabomu ya kurusha, ballistic shields, gas mask n.k.

Kwa hiyo zile begi nyeusi zinazobebwa na walinzi wa Rais sio kwa ajili ya kuhifadhi silaha.

Kwa hiyo, begi hizi zina nini?
Begi hizi zinazobebwa na walinzi wa Rais zinaitwa "Portable Bulletproof Shield" na zatumika kuzuia risasi.
Kama likitokea shambulio, begi hizi zinakunjuliwa (zinafikia urefu mpaka mita 2) kisha wanamzunguka Rais.

Hizi begi zimeundwa kwa aina maalumu ya fiber zinazoitwa Spectra
au kwa jina lingine UHMWPE (Ultra-high-molecular-weight Polyethylene)
Aina hii ya fiber ina impact streght ya juu kabisa na ndio sababu kwa nini ina uwezo wa kuzuia risasi.

Nitoe mfano halisi,

Wiki mbili zilizopita, helikopta iliyombeba Rais wa Colombia Ivan Duque ilishambuliwa
kwa risasi ikiwa hewani na kulazimu kutua kwa dharura

Helikopta ilipotua, kama uli-notice utaona walinzi wake waliobeba mabegi mikononi, wakiyakunjua yale mabegi na kisha kuyavaa mgongoni (Tazama picha)

Huu ni moja ya mifano adhimu ya Portable Bulletproof Shield ikiwa inatumika
Kwa hiyo ukimuona Rais yuko eneo la umma na walinzi waliomzunguka baadhi yao wana mabegi mkononi, basi ujue sio document zile walizobeba.
Ile ni sehemu ya mkakati wa dharura wa 'extraction' kama ikitokea Rais anashambuliwa.

Kindly Retweet

Habibu B. Anga
To Infinity and Beyond

β€’ β€’ β€’

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
γ€€

Keep Current with Habibu B. Anga

Habibu B. Anga Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @habibu_anga

17 Jul
π—‘π—”π—‘π—œ π—”π—Ÿπ—œπ— π—§π—˜π—žπ—” 𝗠𝗧𝗒𝗧𝗒 π—ͺ𝗔 π—₯π—”π—œπ—¦, π— π—”π—­π—œπ— π—•π—¨, 𝗠𝗒π—₯π—’π—šπ—’π—₯𝗒.?

FINALE

Naam, niwamalizie sasa hiki kisa. Kama haujasoma sehemu ya kwanza, angalia kwenye profile yangu juu kabisa pinned tweet.

Sasa,

Wale wakimbizi waliorejea SA, tokea hapa Morogoro...
wakaeleza namna ambavyo waliishi kambini Mazimbu na kijana anayeitwa Louis Mathakoe ambaye sasa hivi wanaonyeshwa picha kwamba identity halisi kijana huyo ni mtoto wa Rais Mbeki.

Wajumbe wa Tume ya TRC walivyo endelea kuhoji kuhusu nyendo za kijana Kwanda akiwa hapo Mazimbu..
Ndipo wakaelezwa nini kilimpata kijana Kwanda pale Mazimbu.

Wakimbizi hawa walieleza kwamba kijana huyo aliishi kambini Mazimbu kuanzia mwaka 1983 mpaka mwaka 1989.
Wakaeleza kwamba kuna siku kambini hapo walifika watu ambao waliwahisi kuwa ni maafisa wa vyombo vya ulinzi vya...
Read 25 tweets
16 Jul
π—‘π—”π—‘π—œ π—”π—Ÿπ—œπ— π—§π—˜π—žπ—” 𝗠𝗧𝗒𝗧𝗒 π—ͺ𝗔 π—₯π—”π—œπ—¦, π— π—”π—­π—œπ— π—•π—¨, 𝗠𝗒π—₯π—’π—šπ—’π—₯𝗒.?

Kuna masuala huwa yanakuwa salama yakiachwa bila kuzungumzwa. Sababu ukianza kuhoji kuhusu ukweli na undani wake, unajikuta unafungua mlango wa hatari ambazo pengine hauko tayari kuzikabili...
Mojawapo ya masuala haya ni madhira ambayo yanafanywa na watu tuliowapa madaraka. Nyendo zao, na siri zao ni kana kwamba haupaswi kutamani kuzifahamu.

Lakini binadamu tumeumbwa na kiu ya kutaka kujua, na kiu hii ni kama upele, hauachi kuwasha mpaka uukune
Na pia historia ya nchi
zetu haiweze kukamilika kwa vizazi vinavyo kunufaika, kama kuna mawe tutayaacha yakiwa yamefunikwa.

Sasa,

Mojawapo ya skandali mbaya sana kwenye bara hili la Afrika, ni tukio la mtoto wa Rais ambaye alidhaniwa amefia mjini Lusaka, Zambia lakini baadae ikaja kuthibitika kwamba..
Read 25 tweets
15 Jul
π— π—§π—”π—‘π—­π—”π—‘π—œπ—” #1: π—π—”π—¦π—¨π—¦π—œ π—ͺ𝗔 π—žπ—¨π—žπ—’π——π—œ, π—¨π—π—”π—¦π—¨π—¦π—œ π—ͺ𝗔 π—•π—œπ—”π—¦π—›π—”π—₯𝗔

#7

Majukumu wakuu, mniwie radhi.

Tuendelee,

Mara ya mwisho nilisema, kuna Mtanzania ambaye mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu alidai kwamba alinyang'anywa passport na Idara ya Intelijensia Image
na kisha kupewa Hati ya Kusafiria ya nchi ya Afrika Kusini

Nikaeleza kwamba mtu huyu ambaye alikwenda Afrika Kusini kutafuta maisha mwanzoni mwa miaka ya tisini, mojawapo ya harakati zake kubwa za kwanza ni pale alipomshawishi Nelson Mandela na taasisi yake ya Mandela Foundation
kutuma ombi la kuandaa pambano la masumbwi la marudiano kati ya Evender Holyfield Vs Lennox Lewis yeye akiwa kama 'promota'.

Pia nikaeleza namna gani ambavyo kampuni ya Vodacom walimdondokea kumuomba awasaidie kuwatoa korokoroni wajumbe wao wa Bodi ya Wakurugenzi nchini Congo...
Read 19 tweets
11 Apr
MTANZANIA #1: JASUSI WA KUKODI, UJASUSI WA BIASHARA

Thread..

Si rahisi kuwa mahususi sana ni mwaka gani, lakini tunakadiria kwamba katikati ya miaka ya tisini hivi Mtanzania ambaye kwa sasa nimtaje kwa jina lake moja tu la Matiko aliondoka jiji Dar kwenda nchini Afrika Kusini
Kwa ajili ya kutafuta maisha. Lakini tofauti na Watanzania wengi wanaozamia SA ambako wakifika uanza kwa kufanya shughuli za hali ya chini, ilikuwa tofauti kabisa na bwana Matiko ambaye aliingia SA akiwa na mtaji wa kuridhisha kutokana na fedha ambazo alizipata toka kwenye mauzo
ya sehemu ya shamba lake la karibia Ekari 300 zilizoko kijiji cha Ghesaria Wilayani Serengeti.

Matiko akatumia mtaji huo akiwa hapo SA kuanzisha biashara ndogo ndogo
Moja ya biashara aliyoanzisha ambayo ilipanda mbegu ya kumbadilisha Matiko na kumfanya aingie kwenye ulimwengu wa
Read 25 tweets
5 Apr
Kuna uzi niliandika hapa Mwezi March kuhusu dhana nzima ya Ulinzi wa viongozi wa juu.
Nikasisitiza sana kwamba sula la ulinzi wao sio tu kulinda wasidhuriwe kimwili bali pia kulinda hadhi zao, heshima zao na siri zao.

Kitimbwi ambacho kimetokea leo cha Rais wa nchi

ThreadπŸ‘‡πŸ‘‡ Image
Kuteua na kufukuza Mkurugenzi wa TPDC ndani ya masaa machache kabisa... ni failure kubwa ya kitengo cha intelijensia ya nchi ambao wana jukumu la kulinda hadhi na heshima ya Rais.
Mtu yule aliyeteuliwa huku akionekana kwamba hana sifa kabisa ya kushika wadhifa ule, ina reflect..
ombwe la weledi ambalo linaikumba idara hii adhimu ya ujasusi.

Mhe. Rais @SuluhuSamia ambaye watu wametokea kuwa na imani naye sana, tukio la leo kwa kiwango fulani limetia doa hadhi yake na kuzua maswali mengi sana

Kwamba, kosa la dhahiri namna ile limetokeaje?
Intelijensia ya
Read 18 tweets
2 Apr
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

PART 5 (HITIMISHO)

Nikiwa nahitimisha ni vyema kusisitiza kwamba, kikosi hiki cha makomando wa Kenya ambacho kinaendeshwa kwa amri ya CIA na NIS (Idara ya Ujasusi Kenya) kwa sasa kimegawanywa kwenye vitengo viwili.. Image
Kitengo cha kwanza ndio ile Rendition Operations Team; hawa wanahusika sana kama target anatakiwa kukamatwa akiwa hai

Alafu siku hizi kuna RRT (Rapid Response Team) hawa wanatumika zaidi kama target anatakiwa kuwaneutralized (kuuwawa) au kuhusika kuokoa mateka kama watekaji wana
mafungamano na vikundi vya kigaidi na si lazima kuwakamata wakiwa hai.

Sasa nieleze baadhi ya Oparesheni ambazo makomando hawa wa Kenya na CIA wamewahi kuzifanya.

1. Kuuwawa kwa Sheikh Aboud Rogo

- Sheikh Aboud Rogo ni moja ya watu maarufu sana kwenye masuala ya dini kuwahi...
Read 25 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(