Naam, niwamalizie sasa hiki kisa. Kama haujasoma sehemu ya kwanza, angalia kwenye profile yangu juu kabisa pinned tweet.
Sasa,
Wale wakimbizi waliorejea SA, tokea hapa Morogoro...
wakaeleza namna ambavyo waliishi kambini Mazimbu na kijana anayeitwa Louis Mathakoe ambaye sasa hivi wanaonyeshwa picha kwamba identity halisi kijana huyo ni mtoto wa Rais Mbeki.
Wajumbe wa Tume ya TRC walivyo endelea kuhoji kuhusu nyendo za kijana Kwanda akiwa hapo Mazimbu..
Ndipo wakaelezwa nini kilimpata kijana Kwanda pale Mazimbu.
Wakimbizi hawa walieleza kwamba kijana huyo aliishi kambini Mazimbu kuanzia mwaka 1983 mpaka mwaka 1989.
Wakaeleza kwamba kuna siku kambini hapo walifika watu ambao waliwahisi kuwa ni maafisa wa vyombo vya ulinzi vya...
Tanzania (sababu walikuwa wakizungumza kingereza chenye lafudhi ya kiswahili) walifika kambini hapo na kuomba kuonana na kijana Louis Mathakoe.
Wakimbizi hawa wakaeleza kwamba watu hao waliongea na Louis kwenye ofisi za viongozi wa kambi kwa takribani saa nzima na kisha baada...
maongezi hayo wakampandisha kwenye gari yenye namba za serikali na kisha kuondoka naye
Na hii ndio ilikuwa mara ya mwisho kwa kijana Louis (Kwanda) kuonekana mahala popote pale duniani
Yaani tangu siku hii haijawahi kupatikana taarifa yoyote ya kuonekana tena kwa Kwanda kwa muda
wa miaka 32 iliyopita.
Wale waswahili waliomchukua Louis walikuwa ni akina nani.? Walimpelenea wapi.? Kwa sababu gani.?
Haya ni maswali ambayo tume ya TRC walijiuliza na kuyachunguza kwa undani sana lakini hawakuambulia kufikia popote kupata jawabu.
Kwa hiyo maswali yakawa...
lukuki...
Kwanza; nini kilimpata kijana Kwanda alipokwenda nchini Swaziland.?
Kwa nini serikali ya SA ilijaribu kumuua.?
Pia; sasa hivi maswali mengine yakaongezeka.. wale waswahili waliomchukua pale ni akina nani? Walimpelea wapi.? Kwa sababu gani?
Haya ni maswali magumu sana
Na pengine kuna watu wachache sana wenye majibu ya maswali haya na kamwe kuna uwezekano hawatakuja kuongea ukweli huo.?
Kuna watu watatu tu ambao labda wanaujua ukweli (nasisitiza 'labda') kuhusu lilichompata Kwanda.
Watu hawa ni Thabo Mbeki, kaka yake Jama Mbeki na rafiki yake..
Phindile Mfeti.
Pale Afrika Kusini kwenye chama cha ANC kutokana na mkasa huu wa Kwanda, kumeibuka minong'ono mingi kuhusu ukweli wake
Maneno yanayosemwa sana kuhusu kilichompata Kwanda ni hiki;
Kwamba, kijana Kwanda alipokwenda nchini Swaziland kumtafuta baba yake alipokelewa
na viongozi fulani ambao walikuwa wamejificha huko.
Minong'ono hii inadai kwamba kwa muda wa miezi mitatu ambayo alikaa hapo Swaziland kijana huyu eidha ni kwa bahati mbaya au makusudi, kuna kitu cha hatari kijana huyu alikiona (nyaraka fulani au kikao fulani).
Kitu hili ambacho
alikuwa amekiona kilikuwa kinathibitisha juu ya uwepo wa maajenti mapandikizi wa serikali ya kibaguzi ndani ya chama cha ANC.
Na kwamba baadhi ya mapandikizi hao waliokuwa wanatumiwa na serikali ya kibaguzi ndani ya chama cha ANC wengine walikuwa na nyadhifa za juu ndani ya chama
Yaani kwamba ndani ya chama cha ANC kuna watu walikuwa wamepandikizwa kishushushu na serikali ya kibaguzi ili wawe wanawapa taarifa kuhusu mipango ya ANC na pia kusoma mienendo ya viongozi wa ANC ili wawakamate.
Nadharia hii inasema kwamba, kijana Kwanda Mbeki akiwa Swaziland...
kuna kitu aliona kuthibitisha watu hao (mapandikizi wanaovujisha taarifa za ANC) walikuwa ni akina nani hasa wenye nyadhifa kubwa ndani ya ANC.
Kuthibitisha hili, huwa unatolewa mfano wa moja ya 'memo' iliyovujishwa kipindi cha serikali ya kibaguzi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya
Ndani kwenda kwa Mkuu wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Kazi Maalumu ambapo kwenye memo hiyo anawasisitiza kuhakikisha wanamkamata mtu ambaye anatishia uendelevu wa serikali kupata taarifa za ndani za chama cha ANC.
Inaaminika kwamba mtu ambaye Waziri wa Mambo Ndani alikuwa...
akimuongelea kwenye memo hiyo alikuwa ni kijana Kwanda.
Hili suala la kuwepo kwa mapandikizi ndani ya chama cha ANC kipindi wanapigania ukombozi wa watu weusi pale SA ni suala ambalo liliitafuna sana ANC miaka hiyo.
Kwa mfano, mojawapo ya watu ambao wamekuwa wanashutumiwa sana
alipokwenda kwa Oliver Tambo kuomba ruhusa ya kumuoa Zanele.. Oliver Tambo alikataa au kwa usahihi zaidi alimkataa Zanele
Kwa miezi kadhaa Mbeki alikuwa anamsisitiza Tambo kiasi kwamba mpaka akafikia hatua ya kumwambia kama hatompa ruhusa ya kumuoa Zanele basi hatooa tena maisha
yake yote. Baada ya Mbeki kuweka presha kiasi hiki ndipo Tambo akamruhusu Mbeki kumuoa Zanele.
Baadae Thabo Mbeki alipelekwa Lusaka, Zambia kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi la ANC (ANC's Revolutionary Council).
Wakiwa hapo Lusaka, Zanele akapata kazi kwenye taasisi yaitwa
International University Education Fund.
Baadae taasisi hii ilifungwa, baada ya kugundulika kwamba, Mkurugenzi wa Taasisi hii aliyeitwa Craig Williamson alikuwa ni 'spy' wa serikali ya kibaguzi ya Afrika Kusini.
Hii ilikuwa ni mwaka 1981. Na kipindi hiki ambacho watu kama akina
Joe Gqabi walikuwa assasinated na jeshi la South Africa baada ya anuani ya makazi yake mjini Harare kuvujishwa kwa Jeshi la Afrika Kusini.
Kwa hiyo maswali mengi yakaibuka kwamba je, ni Craig Williamson bosi wa Zanelee pekee alikuwa ni 'spy' wa serikali ya Africa Kusini, au hata
Zanele na yeye alikuwa ni 'spy'.
Nadhani unanielewa sasa ninavyosema kwamba kulikuwa na watu mpaka kwenye nafasi nyeti ndani ya ANC walikuwa wanatumika kuvujisha taarifa.
Pia hii nadharia ya kwamba Kwanda aliona jambo akiwa kule Swaziland inaleta mashiko sababu, kipindi akiwa..
huko mwaka 1976 ni muda huo huo pia ambao Jacob Zuma (ambaye kipindi hicho alikuwa ni Boss wa Idara ya Ujasusi ya ANC) pamoja na Albert Dhlomo (mshauri wa masuala ya ulinzi wa ANC) walikamatwa wakiwa huko hapo Swaziland.
Kuna uwezekano Kwanda ambaye alikuwa anaishi na viongozi..
wa ANC nchini Swaziland kwa namna fulani alishuhudia mtu wa ndani ya ANC aliyevujisha 'location' ya Zuma na Dhlomo.
Unanielewa.?
Ndio maana kaka yake Mbeki pamoja na rafika yake Mbeki Phindile Mfeti wakamtorosha Kwanda kwenda Zambia na kumtengenezea identity ya uongo ili sio tu
kumlinda dhidi ya serikali ya SA bali pia dhidi ya wasaliti ndani ya ANC.
Inaaminika kwamba kuna watu/mtu aliyekaribu na Mbeki alikuja kugundua kwamba, Kwanda alikuwa anaishi Morogoro, Tz kwa identity mpya.
Sasa swali linabakia, wale waswahili waliomchukua Kwanda pale Mazimbu..
Walikwenda kumficha au walimteka kwenda kumdhuru?
Hatujui,
Lakini uwezekano mkubwa ni kwamba walimchukua ili kumficha na kumlinda asidhuriwe.. na yawezekana mpaka leo hii, Monabwisi Kwanda Mbeki bado anaishi hapa Tanzania kwa identiy mpya.
MWISHO
Habib
To infinity and Beyond
β’ β’ β’
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
Kuna masuala huwa yanakuwa salama yakiachwa bila kuzungumzwa. Sababu ukianza kuhoji kuhusu ukweli na undani wake, unajikuta unafungua mlango wa hatari ambazo pengine hauko tayari kuzikabili...
Mojawapo ya masuala haya ni madhira ambayo yanafanywa na watu tuliowapa madaraka. Nyendo zao, na siri zao ni kana kwamba haupaswi kutamani kuzifahamu.
Lakini binadamu tumeumbwa na kiu ya kutaka kujua, na kiu hii ni kama upele, hauachi kuwasha mpaka uukune
Na pia historia ya nchi
zetu haiweze kukamilika kwa vizazi vinavyo kunufaika, kama kuna mawe tutayaacha yakiwa yamefunikwa.
Sasa,
Mojawapo ya skandali mbaya sana kwenye bara hili la Afrika, ni tukio la mtoto wa Rais ambaye alidhaniwa amefia mjini Lusaka, Zambia lakini baadae ikaja kuthibitika kwamba..
Mara ya mwisho nilisema, kuna Mtanzania ambaye mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu alidai kwamba alinyang'anywa passport na Idara ya Intelijensia
na kisha kupewa Hati ya Kusafiria ya nchi ya Afrika Kusini
Nikaeleza kwamba mtu huyu ambaye alikwenda Afrika Kusini kutafuta maisha mwanzoni mwa miaka ya tisini, mojawapo ya harakati zake kubwa za kwanza ni pale alipomshawishi Nelson Mandela na taasisi yake ya Mandela Foundation
kutuma ombi la kuandaa pambano la masumbwi la marudiano kati ya Evender Holyfield Vs Lennox Lewis yeye akiwa kama 'promota'.
Pia nikaeleza namna gani ambavyo kampuni ya Vodacom walimdondokea kumuomba awasaidie kuwatoa korokoroni wajumbe wao wa Bodi ya Wakurugenzi nchini Congo...
MTANZANIA #1: JASUSI WA KUKODI, UJASUSI WA BIASHARA
Thread..
Si rahisi kuwa mahususi sana ni mwaka gani, lakini tunakadiria kwamba katikati ya miaka ya tisini hivi Mtanzania ambaye kwa sasa nimtaje kwa jina lake moja tu la Matiko aliondoka jiji Dar kwenda nchini Afrika Kusini
Kwa ajili ya kutafuta maisha. Lakini tofauti na Watanzania wengi wanaozamia SA ambako wakifika uanza kwa kufanya shughuli za hali ya chini, ilikuwa tofauti kabisa na bwana Matiko ambaye aliingia SA akiwa na mtaji wa kuridhisha kutokana na fedha ambazo alizipata toka kwenye mauzo
ya sehemu ya shamba lake la karibia Ekari 300 zilizoko kijiji cha Ghesaria Wilayani Serengeti.
Matiko akatumia mtaji huo akiwa hapo SA kuanzisha biashara ndogo ndogo
Moja ya biashara aliyoanzisha ambayo ilipanda mbegu ya kumbadilisha Matiko na kumfanya aingie kwenye ulimwengu wa
Kuna uzi niliandika hapa Mwezi March kuhusu dhana nzima ya Ulinzi wa viongozi wa juu.
Nikasisitiza sana kwamba sula la ulinzi wao sio tu kulinda wasidhuriwe kimwili bali pia kulinda hadhi zao, heshima zao na siri zao.
Kitimbwi ambacho kimetokea leo cha Rais wa nchi
Threadππ
Kuteua na kufukuza Mkurugenzi wa TPDC ndani ya masaa machache kabisa... ni failure kubwa ya kitengo cha intelijensia ya nchi ambao wana jukumu la kulinda hadhi na heshima ya Rais.
Mtu yule aliyeteuliwa huku akionekana kwamba hana sifa kabisa ya kushika wadhifa ule, ina reflect..
ombwe la weledi ambalo linaikumba idara hii adhimu ya ujasusi.
Mhe. Rais @SuluhuSamia ambaye watu wametokea kuwa na imani naye sana, tukio la leo kwa kiwango fulani limetia doa hadhi yake na kuzua maswali mengi sana
Kwamba, kosa la dhahiri namna ile limetokeaje?
Intelijensia ya
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI
PART 5 (HITIMISHO)
Nikiwa nahitimisha ni vyema kusisitiza kwamba, kikosi hiki cha makomando wa Kenya ambacho kinaendeshwa kwa amri ya CIA na NIS (Idara ya Ujasusi Kenya) kwa sasa kimegawanywa kwenye vitengo viwili..
Kitengo cha kwanza ndio ile Rendition Operations Team; hawa wanahusika sana kama target anatakiwa kukamatwa akiwa hai
Alafu siku hizi kuna RRT (Rapid Response Team) hawa wanatumika zaidi kama target anatakiwa kuwaneutralized (kuuwawa) au kuhusika kuokoa mateka kama watekaji wana
mafungamano na vikundi vya kigaidi na si lazima kuwakamata wakiwa hai.
Sasa nieleze baadhi ya Oparesheni ambazo makomando hawa wa Kenya na CIA wamewahi kuzifanya.
1. Kuuwawa kwa Sheikh Aboud Rogo
- Sheikh Aboud Rogo ni moja ya watu maarufu sana kwenye masuala ya dini kuwahi...
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI
PART 4
Ile taarifa ambayo Asad aliwapatia ilikuwa ya maana sana kwa CIA.
Mpaka muda huu ambapo Asad alikuwa anahojiwa (kumbuka hiyo ni mwaka Oct 2003) huyo "bwana somba" Odeh tayari alikuwa ameshakamatwa
na yuko gerezani Guatanamo Bay (alikamatwa tangu mwaka 1998).
Taarifa hii ya Asad iliwapa CIA kitu kimoja muhimu sana.. walithibitisha intelijensia yao kuhusu shirika la al-Haramain kutumiwa na al-Qaida kusambaza fedha ulimwenguni kwa watu wao.
Ushahidi huu ulitumiwa na Marekani
kushawishi Umoja wa Mataifa kulipiga marufuku shirika hilo na mpaka leo hii ninavyoandika shirika hilo ofisi zake zote ulimwenguni zimefungwa
Lakini hicho sicho ninachotaka kuandika
Ninachotaka kuandika ni namna ambavyo ile confirmation ya Asad iliwasaidia CIA kuanza kunusa kila