π—‘π—”π—‘π—œ π—”π—Ÿπ—œπ— π—§π—˜π—žπ—” 𝗠𝗧𝗒𝗧𝗒 π—ͺ𝗔 π—₯π—”π—œπ—¦, π— π—”π—­π—œπ— π—•π—¨, 𝗠𝗒π—₯π—’π—šπ—’π—₯𝗒.?

Kuna masuala huwa yanakuwa salama yakiachwa bila kuzungumzwa. Sababu ukianza kuhoji kuhusu ukweli na undani wake, unajikuta unafungua mlango wa hatari ambazo pengine hauko tayari kuzikabili...
Mojawapo ya masuala haya ni madhira ambayo yanafanywa na watu tuliowapa madaraka. Nyendo zao, na siri zao ni kana kwamba haupaswi kutamani kuzifahamu.

Lakini binadamu tumeumbwa na kiu ya kutaka kujua, na kiu hii ni kama upele, hauachi kuwasha mpaka uukune
Na pia historia ya nchi
zetu haiweze kukamilika kwa vizazi vinavyo kunufaika, kama kuna mawe tutayaacha yakiwa yamefunikwa.

Sasa,

Mojawapo ya skandali mbaya sana kwenye bara hili la Afrika, ni tukio la mtoto wa Rais ambaye alidhaniwa amefia mjini Lusaka, Zambia lakini baadae ikaja kuthibitika kwamba..
alikuwa akiishi hapa nchini kwetu Mkoani Morogoro tena akilindwa na vyombo vyetu.

Namna gani.?

Wajua,ni nadra sana kuwa na Rais ambaye hana familia. Si jambo la kawaida. Ndio maana enzi za utawala wake, Rais Thabo Mbeki alikuwa anashangaza sana kwa kutokuwa na familia. Nasema..
hakuwa na familia sababu, huyu muheshimiwa yeye na mkewe Zanele Mbeki hawakujaliwa kupata mtoto. Na si hivyo tu, bali pia kwa miaka mingi sana, japokuwa hawajatalikiana lakini wawili huwa hawaishi nyumba moja.
Kwa hiyo Mbeki alikuwa ni kama Rais asiye na familia.

Lakini japokuwa
Mbeki na mkewe hawana mtoto, lakini Thabo Mbeki yeye binafsi amewahi kupata mtoto. Na mtoto wake huyu ndiye ambaye amezua kizaa zaa cha aina yake na kuleta moja ya skandali mbaya zaidi hapa Afrika.

Kipindi Mbeki ni bwana mdogo kabisa anasoma shule ya upili, alikuwa na mpenzi wa
kike anayeitwa Olive Mpahlwa.
Kutoka na mahusiano yao haya ya kimapenzi, Olive akashika mimba.
Hapo wote walikuwa na miaka 16 tu.
Sasa, sio tu kisheria bali pia hata kwenye tamaduni za jamii ya watu wa kabila Xhosa ambalo Mbeki anatokea ni kosa kumpa mimba msichana mwenye umri...
mdogo.

Kwa hiyo wazee wa Mbeki na Binti Olive wakakutana kwa mujibu wa Tamaduni, na familia ya Mbeki ikapigwa faini ya ng'ombe watano kwa kijana wao kumtia mimba mtoto mdogo.

Baada ya hapo binti akalea mimba na kuzaa mtoto wa kiume ambaye walimuita jina Monwabisi Kwanda...
Kipindi huyu mtoto anazaliwa Thabo Mbeki alikuwa yuko Johannesburg akichukua masomo ya A-Level kwa hiyo hakuwahi kumuona mtoto wake akiwa mchanga.
Wakati pekee ambao Mbeki alimuona mtoto wake kwanda(ambayo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho) ni kipindi mtoto wake ana miaka
miwili aliporejea nyumbani kwao kujificha baada ya kuwa anatafutwa na vyombo vya ulinzi vya serikali ya Kibaguzi ya Afrika Kusini baada ya kuhamasisha migomo ya kuipinga serikali akiwa kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi.

Baadae yeye na wenzake wakivalia jezi kama timu ya...
mpira wa miguu wakakodi basi na kuvuka mpaka kwenda Botwasa na hatimaye Thabo Mbeki akakimbilia hapa Tanzania amapo kwa maelezo ya Oliver Tambo ambaye alikuwa kiongozi wa ANC, alimuomba Mzee Kenneth Kaunda asafiri na Mbeki kwenda London. Hii tutaongea zaidi siku nyingine.
Kule nyumbani SA, mtoto wake alipofikisha miaka 10 akapelekwa akaishi na mama yake Mbeki, ambapo aliishi naye kwa muda wa karibia miaka sita.

Mtoto huyu inaelezwa kwamba alikuwa na kiu kubwa sana ya kutaka kuonana tena na baba yake lakini kwa kipindi hicho watu 'high ranking' wa
ANC mahala ambako walikuwa wanaishi ilikuwa ni siri kubwa.

Kwenye kumtafuta baba yake, kijana huyu Kwanda akakutanishwa na rafiki wa zamani wa Thabo Mbeki anayeitwa Phindile Mfeti.
Mfeti alimueleza Kwanda kwamba baba yake amejificha nchini Swaziland.
Wote wawili, Kwanda na Mfeti
Wakasafiri kwenda nchini Swaziland.

Lakini miezi mitatu baadae wakarejea bila mafanikio yoyote ya kumpata Mbeki.

Sasa, waliporejea ndipo vitu vya ajabu vikaanza kutokea ambapo mama yake Mbeki ambaye alikuwa akiishi na Kwanda kipindi hicho hakuweza kuelewa.

Kulitokea majaribio
matatu ya kutaka kumteka au kumuua kijana kwanda.
Majaribio haya yalitokea mara tu aliporejea toka Swaziland.

Kutokana na hatari hii, bibi yake akamtorasha kwake na kumpela kwa mjomba ake (kaka yake Thabo Mbeki) anayeitwa Jama Mbeki.

Jama hakutaka kufanya mchezo na maisha yao..
Kwa hiyo, yeye pamona na Kwanda wakafungasha virago na kuanza safari ya kukimbilia nchini Zambia.
Lengo lake lilikuwa ni kwenda kumkabidhi Kwanda kwenye kambi ya ANC iliyoko Lusaka ambako aliamini huko Kwanda atakuwa salama.
Wakavuka mpaka na Jama akamwelekeza Kwanda aelekee wapi
na kisha yeye akarejea Afrika kusini.
Na hii ndio ilikuwa mara ya mwisho mtu yeyote kumuona Kwanda.
Yaani alipoachana tu na mjomba wake, Kwanda hakuwahi kuonekana tena, au kuwasiliana tena na mtu yeyote.

Kwa miaka mingi sana familia ya Thabo Mbeki iliishi kwenye jinamizi...
wakijiuliza nini kilimpata kwanda.?
Ni nini kilitokea nchini Swaziland ambacho kilisababisha aliporejea Afrika Kusini, serikali ya Kibaguzi itake kumuua.?
Alipoingia Zambia nini kilimpata mpaka hakuwahi kuonekana tena.

Baada ya miaka kadhaa wakakata tamaa na kuamini kwamba...
Kwanda alikuwa ameuawa na maajenti wa serijali ya SA, mara tu baada ya kuingia Zambia.

Lakini swali bado lilikuwa linawatesa kwa miaka mingi.. kwa nini?

Haueni ilikuja kupatikana baada ya ANC kushika nchi mwaka 1994 ambapo Thabo Mbeki alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais kwenye...
serikali ya Nelson Mandela.

Lile kovu bado lilikuwa moyoni mwa Thabo Mbeki ukizingatia Kwanda ndiye alikuwa mtoto wake pekee.

Mbeki akasimamia kuundwa kwa tume iliyoitwa TRC (Truth and Reconciliantion Commission).
Mojawapo ya kazi ta Tume hii ilikuwa ni kuchunguza kesi za watu
ambao waliuwawa au kupotea kwenye mazingira ya kutatanisha kipindi cha serikali Baguzi.
Moja wapo ya kesi ambayo ilipewa uzito mkubwa ilikuwa ni kesi ya kupotea kwa Monwabisi Kwanda Mbeki.

Kwenye uchunguzi wa tume wakaja kuvumbua jambo la ajabu mno ambalo halikutegemewa kabisa..
Wakati wajumbe wa Tume wanafanya mahojiano na Wanachama wa ANC waliorejea South Africa kutokea uhamishoni hapa Tanzania, wengi wa watu hao walipoonyeshwa picha ya Kwanda walisema kwamba wanamfahamu na ameishi kwenye kambi ya Mazimbu, Morogoro kwa muda wa miaka mitatu. Na kwamba..
kipindi akiishi hapo Mzimbu, hakuwa hakitumia jina hilo la Kwanda Mbeki bali alikuwa anafahamika kama Louis Mathakoe.

Yani sio mtu mmoja au wawili, bali asilimia kubwa ya walowezi wa ANC kutoka Tanzania waliokuwa wamerejea SA walikiri kumfahamu Kwanda kwa jina la Louis Mathakoe
Watu hawa walidai kwamba, huyo kijana aliwasili kambini Morogoro mwaka 1983 na akaishi hapo kwa miaka sita mpaka mwaka 1989.

Kumbuka kwamba, Kwanda alikuwa amepotea toka 1978 na familia yake walikuwa wanaamini kwamba aliuwawa huko Zambia, lakini leo hii zaidi ya miaka 15 baadae
wanaambiwa kwamba, Kwanda alikuwa ameingia Tanzania na alikuwa akiishi kwa kutumia identity bandia akijulikana kama Louis Mathakoe.

- - -

Naimaliza hii usiku huu huu.. usiende mbali.

Retweet tumfikie kila mtu.

Habibu B. Anga
To Infinity and Beyond

β€’ β€’ β€’

Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh
γ€€

Keep Current with Habibu B. Anga

Habibu B. Anga Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

PDF

Twitter may remove this content at anytime! Save it as PDF for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video
  1. Follow @ThreadReaderApp to mention us!

  2. From a Twitter thread mention us with a keyword "unroll"
@threadreaderapp unroll

Practice here first or read more on our help page!

More from @habibu_anga

17 Jul
π—‘π—”π—‘π—œ π—”π—Ÿπ—œπ— π—§π—˜π—žπ—” 𝗠𝗧𝗒𝗧𝗒 π—ͺ𝗔 π—₯π—”π—œπ—¦, π— π—”π—­π—œπ— π—•π—¨, 𝗠𝗒π—₯π—’π—šπ—’π—₯𝗒.?

FINALE

Naam, niwamalizie sasa hiki kisa. Kama haujasoma sehemu ya kwanza, angalia kwenye profile yangu juu kabisa pinned tweet.

Sasa,

Wale wakimbizi waliorejea SA, tokea hapa Morogoro... Image
wakaeleza namna ambavyo waliishi kambini Mazimbu na kijana anayeitwa Louis Mathakoe ambaye sasa hivi wanaonyeshwa picha kwamba identity halisi kijana huyo ni mtoto wa Rais Mbeki.

Wajumbe wa Tume ya TRC walivyo endelea kuhoji kuhusu nyendo za kijana Kwanda akiwa hapo Mazimbu..
Ndipo wakaelezwa nini kilimpata kijana Kwanda pale Mazimbu.

Wakimbizi hawa walieleza kwamba kijana huyo aliishi kambini Mazimbu kuanzia mwaka 1983 mpaka mwaka 1989.
Wakaeleza kwamba kuna siku kambini hapo walifika watu ambao waliwahisi kuwa ni maafisa wa vyombo vya ulinzi vya...
Read 25 tweets
15 Jul
π— π—§π—”π—‘π—­π—”π—‘π—œπ—” #1: π—π—”π—¦π—¨π—¦π—œ π—ͺ𝗔 π—žπ—¨π—žπ—’π——π—œ, π—¨π—π—”π—¦π—¨π—¦π—œ π—ͺ𝗔 π—•π—œπ—”π—¦π—›π—”π—₯𝗔

#7

Majukumu wakuu, mniwie radhi.

Tuendelee,

Mara ya mwisho nilisema, kuna Mtanzania ambaye mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu alidai kwamba alinyang'anywa passport na Idara ya Intelijensia Image
na kisha kupewa Hati ya Kusafiria ya nchi ya Afrika Kusini

Nikaeleza kwamba mtu huyu ambaye alikwenda Afrika Kusini kutafuta maisha mwanzoni mwa miaka ya tisini, mojawapo ya harakati zake kubwa za kwanza ni pale alipomshawishi Nelson Mandela na taasisi yake ya Mandela Foundation
kutuma ombi la kuandaa pambano la masumbwi la marudiano kati ya Evender Holyfield Vs Lennox Lewis yeye akiwa kama 'promota'.

Pia nikaeleza namna gani ambavyo kampuni ya Vodacom walimdondokea kumuomba awasaidie kuwatoa korokoroni wajumbe wao wa Bodi ya Wakurugenzi nchini Congo...
Read 19 tweets
11 Apr
MTANZANIA #1: JASUSI WA KUKODI, UJASUSI WA BIASHARA

Thread..

Si rahisi kuwa mahususi sana ni mwaka gani, lakini tunakadiria kwamba katikati ya miaka ya tisini hivi Mtanzania ambaye kwa sasa nimtaje kwa jina lake moja tu la Matiko aliondoka jiji Dar kwenda nchini Afrika Kusini
Kwa ajili ya kutafuta maisha. Lakini tofauti na Watanzania wengi wanaozamia SA ambako wakifika uanza kwa kufanya shughuli za hali ya chini, ilikuwa tofauti kabisa na bwana Matiko ambaye aliingia SA akiwa na mtaji wa kuridhisha kutokana na fedha ambazo alizipata toka kwenye mauzo
ya sehemu ya shamba lake la karibia Ekari 300 zilizoko kijiji cha Ghesaria Wilayani Serengeti.

Matiko akatumia mtaji huo akiwa hapo SA kuanzisha biashara ndogo ndogo
Moja ya biashara aliyoanzisha ambayo ilipanda mbegu ya kumbadilisha Matiko na kumfanya aingie kwenye ulimwengu wa
Read 25 tweets
5 Apr
Kuna uzi niliandika hapa Mwezi March kuhusu dhana nzima ya Ulinzi wa viongozi wa juu.
Nikasisitiza sana kwamba sula la ulinzi wao sio tu kulinda wasidhuriwe kimwili bali pia kulinda hadhi zao, heshima zao na siri zao.

Kitimbwi ambacho kimetokea leo cha Rais wa nchi

ThreadπŸ‘‡πŸ‘‡ Image
Kuteua na kufukuza Mkurugenzi wa TPDC ndani ya masaa machache kabisa... ni failure kubwa ya kitengo cha intelijensia ya nchi ambao wana jukumu la kulinda hadhi na heshima ya Rais.
Mtu yule aliyeteuliwa huku akionekana kwamba hana sifa kabisa ya kushika wadhifa ule, ina reflect..
ombwe la weledi ambalo linaikumba idara hii adhimu ya ujasusi.

Mhe. Rais @SuluhuSamia ambaye watu wametokea kuwa na imani naye sana, tukio la leo kwa kiwango fulani limetia doa hadhi yake na kuzua maswali mengi sana

Kwamba, kosa la dhahiri namna ile limetokeaje?
Intelijensia ya
Read 18 tweets
2 Apr
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

PART 5 (HITIMISHO)

Nikiwa nahitimisha ni vyema kusisitiza kwamba, kikosi hiki cha makomando wa Kenya ambacho kinaendeshwa kwa amri ya CIA na NIS (Idara ya Ujasusi Kenya) kwa sasa kimegawanywa kwenye vitengo viwili.. Image
Kitengo cha kwanza ndio ile Rendition Operations Team; hawa wanahusika sana kama target anatakiwa kukamatwa akiwa hai

Alafu siku hizi kuna RRT (Rapid Response Team) hawa wanatumika zaidi kama target anatakiwa kuwaneutralized (kuuwawa) au kuhusika kuokoa mateka kama watekaji wana
mafungamano na vikundi vya kigaidi na si lazima kuwakamata wakiwa hai.

Sasa nieleze baadhi ya Oparesheni ambazo makomando hawa wa Kenya na CIA wamewahi kuzifanya.

1. Kuuwawa kwa Sheikh Aboud Rogo

- Sheikh Aboud Rogo ni moja ya watu maarufu sana kwenye masuala ya dini kuwahi...
Read 25 tweets
1 Apr
ZIMWI TULIJUALO: USO KWA USO NA CIA NDANI YA AFRIKA MASHARIKI

PART 4

Ile taarifa ambayo Asad aliwapatia ilikuwa ya maana sana kwa CIA.

Mpaka muda huu ambapo Asad alikuwa anahojiwa (kumbuka hiyo ni mwaka Oct 2003) huyo "bwana somba" Odeh tayari alikuwa ameshakamatwa Image
na yuko gerezani Guatanamo Bay (alikamatwa tangu mwaka 1998).

Taarifa hii ya Asad iliwapa CIA kitu kimoja muhimu sana.. walithibitisha intelijensia yao kuhusu shirika la al-Haramain kutumiwa na al-Qaida kusambaza fedha ulimwenguni kwa watu wao.
Ushahidi huu ulitumiwa na Marekani
kushawishi Umoja wa Mataifa kulipiga marufuku shirika hilo na mpaka leo hii ninavyoandika shirika hilo ofisi zake zote ulimwenguni zimefungwa

Lakini hicho sicho ninachotaka kuandika
Ninachotaka kuandika ni namna ambavyo ile confirmation ya Asad iliwasaidia CIA kuanza kunusa kila
Read 16 tweets

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3/month or $30/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!

Follow Us on Twitter!

:(