Mwaka juzi kwenye hafla ya mapokezi ya ndege kwenye nchi fulani hivi hapa Afrika Mashariki kuna incident ndogo tu ilitokea lakini wengi ikatufikirisha sana.
Dakika chache baada ya Rais wa...
nchi hiyo kumaliza kuongoza hafla hiyo ya mapokezi ya ndege akashuka jukwaani na akianza kuandoka.
Lakini kabla hajakwenda kupanda gari, kama ambavyo ilikuwa ada kwa Rais yule akaelekea upande waliokaa wananchi wake na ili awasalimie.
Na kusalimia huku akaanza jukwaa ambalo...
walikuwa wamekaa wageni VIP.
Wageni wale mashuhuri wakasimama na Rais akawa anapita akiwapa mkono.
Mojawapo ya wageni wale mashuhuri alikuwa ni mfanyabiashara maarufu sana mwenye asili ya kihindi.
Rais alipopita mbele yake, mfabiashara huyu akanyoosha mkono ili asalimiane na...
Rais. Ajabu ni kwamba moja ya walinzi wa Rais wa nchi hiyo akaudaka haraka mkono wa mfanyabiashara yule na kisha kuutupa pembeni kwa nguvu na hasira.
Lilikuwa ni tukio dogo sana na lililodumu kwa sekunde chache lakini lilikuwa linaleta maswali mengi sana.
Sababu hii haikuwa...
sehemu ya procedure/skills kwenye kumlinda Rais. Wengi waliona kama ni 'kibri' ama 'kujimwambafy' kwa mlinzi huyu.
Lakini pia inaakisi kiwango kisichomithirika cha nguvu ambayo walinzi wa marais kwenye nchi zetu wamejilimbikizia.
Nguvu ambayo hakuna mtu ama chombo chochote kwenye
nchi wanaweza kuidhibiti.
Huu ni mfano tu nimetoa kwenye nchi hiyo. Lakini kwa sasa hapa Afrika Mashariki na Kusini kumeibuka kama 'trend'. Trend ya walinzi wa viongozi wakuu wa nchi kujilimbikizia kiwango kikubwa sana cha ushawishi kuvuka hata muongozo wa mipaka ya kazi zao.
Na historia inatufundisha kwamba, mtu anapolimbikizia kiwango kikubwa hivi cha 'power' mara nyingi atatumia kwa manufaa yake binafsi, na mara nyingi atatumia kujilimbikizia mali na utajiri.
Nitoe mfano hai...
Hapa kusini mwa mpaka wetu wa nchi, tuna majirani zetu wa Malawi...
Hivi ninavyoandika kuna kesi ya utata sana inaendelea pale.
Serikali ya Malawi inamshitaki moja ya Mlinzi wa Rais anayeitwa Norman Chisale kwa makosa ya kutumia nafasi yake kujilimbikizia mali zenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 12 pamoja na magari ya kifahari yapatayo 78
Norman Chisale alikuwa Mlinzi wa Rais aliyemaliza muda wake Peter Mutharika
Huyu somo hakuwa Waziri, sio kingozi wa chama, sio kigogo serikalini, ni mlinzi tu wa Rais, sasa anawezaje kujilimbikizia mali kiwango kikubwa namna hii.
Kuna namna ambayo inatumika karibia walinzi wote
wa namna hii.
Kwanza wanajilimbikizia 'power' na kuhodhi access ya Rais.
Kwa mfano pale Malawi, Norman Chisale alijilimbikizia ushawishi kiasi kwamba ikafika mahala huwezi kuonana na Rais ofisini kwake bila yeye kutoa idhini.
Kwa taratibu za kiprotokali ruhusa ya kuonana na...
Rais inatolewa na Ikulu chini ofisi ya Katibu wa Rais.
Vyombo vya intelijensia vyaweza kutumika kufanya vetting za watu ambao wanafika kuonana na Rais.
Lakini Norman Chisale alijilimbikizia nguvu kiasi kwamba yeye pekee ndiye alikuwa anatoa ruhusa ya mwisho ya kuonana na Rais...
Ilifika kipindi Chisale alikuwa anazuia mpaka viongozi wa chama tawala cha DPP kumuona Rais akiwa Ikulu
Chisale akalimbikiza mamlaka kiasi kwamba akawa kama kivuli cha Rais
Kuna viongozi wa DPP walitaka mpaka kujiuzulu kwa kuchukzwa kwao na nguvu kubwa ambayo Chisale alikuwa nayo
Sasa, wakishajilimbikizia nguvu kubwa namna hii, hatua inayofuata ni kutumia ushawishi huo kuchuma mali.
Kwa mfano;
Marais huwa wanapokea "zawadi" nyingi toka kwa watu mbalimbali.
Ubaya baadhi ya "zawadi" hizi ni rahisi mno kuzi-trace. Kwa mfano magari.
Pale Malawi kipindi cha
Peter Mutharika, kwa mfano wewe ni mfanyabiashara mkubwa na unataka kumpa zawadi Rais kama vile gari
Ulikuwa unawasiliana na mlinzi wake Norman Chisale. Kisha hiyo gari inasajiliwa kwa jina lake (Chisale) alafu yeye anaenda kuripoti kwa Rais na kisha Rais anampa maelezo gari hiyo
iende wapi, au apewe ndugu yake yupi au kiongozi gani wa dini.
Chisale akawa anatumia mfumo huu huu pia kupokea "zawadi" zake binafsi.
Kwa mfano, ukitaka akupe ruhusa kuonana na Rais ikulu.. unampatia "zawadi" ya gari ya kifahari, kisha ndio anakupa appointment ya kumuona Rais..
Na magari haya akawa anayaweka kwenye kivuli kile kile kwamba ni "zawadi za Rais".
Mchezo huu ameufanya kwa muda mrefu kiasi kwamba mpaka mwaka jana anakamatwa, Norman Chisale alikutwa na magari ya kifahari yapatayo 78. Magari ya gharama ya juu kabisa kama vile Range Rovers, BMWs
Mercedez Benz, Jeep Wranglers n.k. jumla 78.
Kama hiyo haitoshi, Chisale alikuwa anatumia TIN namba ya Rais ambayo automatically ina msamaha wa kodi, akawa anaitumia kwa ajili ya kuagiza shehena za cement toka nje.
DPP wa Malawi amedai kwamba kati ya mwaka 2014 mpaka mwaka 2020
Chisale alikuwa ameagiza jumla ya mifuko milion 2 ya simenti ambayo ilikuwa inauzwa kwenye maduka aliyoingia nayo ubia ya wafanyabiashara wa bidhaa hiyo.
Lakini pia Chisale alikuwa anatumia nguvu yake ya kuwa karibu na Rais kulazimisha taasisi za umma kufanya warsha na huduma za
malazi kwenye hoteli zake zinazoitwa Zimatha Executive Hotels.
Ukitazama rekodi za kihasibu za serikali kati ya mwaka 2016 na 2020 utaona kuna mamia ya mamilioni ambayo serikali ilikuwa inalipa kwenda Zimatha Executive Hotels... hoteli ambazo alizijenga kwa hela za deals za ikulu
Mwaka jana Rais Lazarus Chakwera alipochukua nchi moja ya hatua ya kwanza aliyoichukua ilikuwa ni kuwashughulikia watu ambao walikuwa wanapambanuliwa kama ni "untouchable". Na mojawapo ya watu hao alikuwa ni huyu Norman Chisale.
Enzi za utawala wa Peter Mutharika, huyu Chisale..
alikuwa ndiye mtu wake wa mkono wa kuume
Kuna kipindi fulani mwaka 2017 baadhi ya maafisa wazalendo wa tasisi ya kupambana na rushwa ya Malawi wakaanza kuhoji juu ya utajiri wa kupindukia wa huyu mlinzi wa Rais.
Kuna afisa wa ngazi za juu wa "takukuru" alikuwa anaitwa Issa Njauju
akafungua faili na kuanza kumchunguza Chisale ili ajue source ya utajiri wake
Wiki moja baadae mwili wa Issa Njauju uliokotwa kando ya mto ukiwa umeoza na umekatwakatwa vipande vipande kama nyama ya kuku.
Ilikuwa ni mwiko kumgusa Norman Chisale.
Na huyu ndiye moja ya watu ambao
Rais Chakwera alianza nao kwenye kampeni yake ambayo aliipambanua kama kutokomeza ufisadi uliokithiri nchini Malawi.
Mwaka jana 2020 mwezi July, polisi wa Malawi wakamkata Norman Chisale na alikutwa na ukwasi mkubwa usiomithirika.
Akaunti zake za benki zilikuwa na mabilioni ya..
fedha. Alikuwa anamiliki majumba ya kifahari kwenye miji yote mikubwa ya Malawi
Magari ya kifahari yapatayo 78 Bandari kavu na mahoteli.
Mali zote hizo alizichuma kwa kufanya kazi tu ya kumlinda Rais ambayo alikuwa analipwa mshahara wa kwacha 25,000 (shilingi milioni 3) kwa mwezi
Mchezo huu wafanyika kwenye nchi nyingi hapa Afrika.
Tofauti ni kwamba pale Malawi, Rais wa chama kingine aliingia madaraka na akaamua kuwaanika watangulizi wake.
Siku moja na sisi upekuzi kama huu ukifanyika, tutashuhudia viroja vya karne.
Habib B. Anga
To Infinity and Beyond
β’ β’ β’
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
Tujadili kidogo Executive Protection.
Hapa chini nimeweka picha za inner cycle za ulinzi wa Rais JPM, Samia, Ndayishimiye (Burundi) na Mnangagwa (Zim).
Kwa kila Rais utaona 'First Ring' zao (hao walinzi wanaomzunguka Rais muda wote) lazima kuna afisa mmoja au wawili..
amebeba begi la mkononi
Umewahi kujiuliza hilo begi lina dhumuni gani.?
Hiyo picha hapo juu, JPM alikuwa chato na hapo alikuwa anakwenda kwenye kibanda cha simu kusajili line yake kwa alama ya vidole
Kwa hiyo hakuwa kwenye ziara au anakwenda kikaoni.. sasa hilo begi ni la nini?
Na si yeye tu.. siku ukibahatika kuwa mahala ambako Rais SSH yupo, tazama kwa makini wale walinzi wake, hasa ile 'first ring', wale walinzi wenye suti wanaomzunguka.. utaona vivyo hivyo pia, kuna maafisa wawili au watatu wana mabegi ya dizaini hii wamebeba mkononi.
Naam, niwamalizie sasa hiki kisa. Kama haujasoma sehemu ya kwanza, angalia kwenye profile yangu juu kabisa pinned tweet.
Sasa,
Wale wakimbizi waliorejea SA, tokea hapa Morogoro...
wakaeleza namna ambavyo waliishi kambini Mazimbu na kijana anayeitwa Louis Mathakoe ambaye sasa hivi wanaonyeshwa picha kwamba identity halisi kijana huyo ni mtoto wa Rais Mbeki.
Wajumbe wa Tume ya TRC walivyo endelea kuhoji kuhusu nyendo za kijana Kwanda akiwa hapo Mazimbu..
Ndipo wakaelezwa nini kilimpata kijana Kwanda pale Mazimbu.
Wakimbizi hawa walieleza kwamba kijana huyo aliishi kambini Mazimbu kuanzia mwaka 1983 mpaka mwaka 1989.
Wakaeleza kwamba kuna siku kambini hapo walifika watu ambao waliwahisi kuwa ni maafisa wa vyombo vya ulinzi vya...
Kuna masuala huwa yanakuwa salama yakiachwa bila kuzungumzwa. Sababu ukianza kuhoji kuhusu ukweli na undani wake, unajikuta unafungua mlango wa hatari ambazo pengine hauko tayari kuzikabili...
Mojawapo ya masuala haya ni madhira ambayo yanafanywa na watu tuliowapa madaraka. Nyendo zao, na siri zao ni kana kwamba haupaswi kutamani kuzifahamu.
Lakini binadamu tumeumbwa na kiu ya kutaka kujua, na kiu hii ni kama upele, hauachi kuwasha mpaka uukune
Na pia historia ya nchi
zetu haiweze kukamilika kwa vizazi vinavyo kunufaika, kama kuna mawe tutayaacha yakiwa yamefunikwa.
Sasa,
Mojawapo ya skandali mbaya sana kwenye bara hili la Afrika, ni tukio la mtoto wa Rais ambaye alidhaniwa amefia mjini Lusaka, Zambia lakini baadae ikaja kuthibitika kwamba..
Mara ya mwisho nilisema, kuna Mtanzania ambaye mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu alidai kwamba alinyang'anywa passport na Idara ya Intelijensia
na kisha kupewa Hati ya Kusafiria ya nchi ya Afrika Kusini
Nikaeleza kwamba mtu huyu ambaye alikwenda Afrika Kusini kutafuta maisha mwanzoni mwa miaka ya tisini, mojawapo ya harakati zake kubwa za kwanza ni pale alipomshawishi Nelson Mandela na taasisi yake ya Mandela Foundation
kutuma ombi la kuandaa pambano la masumbwi la marudiano kati ya Evender Holyfield Vs Lennox Lewis yeye akiwa kama 'promota'.
Pia nikaeleza namna gani ambavyo kampuni ya Vodacom walimdondokea kumuomba awasaidie kuwatoa korokoroni wajumbe wao wa Bodi ya Wakurugenzi nchini Congo...
MTANZANIA #1: JASUSI WA KUKODI, UJASUSI WA BIASHARA
Thread..
Si rahisi kuwa mahususi sana ni mwaka gani, lakini tunakadiria kwamba katikati ya miaka ya tisini hivi Mtanzania ambaye kwa sasa nimtaje kwa jina lake moja tu la Matiko aliondoka jiji Dar kwenda nchini Afrika Kusini
Kwa ajili ya kutafuta maisha. Lakini tofauti na Watanzania wengi wanaozamia SA ambako wakifika uanza kwa kufanya shughuli za hali ya chini, ilikuwa tofauti kabisa na bwana Matiko ambaye aliingia SA akiwa na mtaji wa kuridhisha kutokana na fedha ambazo alizipata toka kwenye mauzo
ya sehemu ya shamba lake la karibia Ekari 300 zilizoko kijiji cha Ghesaria Wilayani Serengeti.
Matiko akatumia mtaji huo akiwa hapo SA kuanzisha biashara ndogo ndogo
Moja ya biashara aliyoanzisha ambayo ilipanda mbegu ya kumbadilisha Matiko na kumfanya aingie kwenye ulimwengu wa
Kuna uzi niliandika hapa Mwezi March kuhusu dhana nzima ya Ulinzi wa viongozi wa juu.
Nikasisitiza sana kwamba sula la ulinzi wao sio tu kulinda wasidhuriwe kimwili bali pia kulinda hadhi zao, heshima zao na siri zao.
Kitimbwi ambacho kimetokea leo cha Rais wa nchi
Threadππ
Kuteua na kufukuza Mkurugenzi wa TPDC ndani ya masaa machache kabisa... ni failure kubwa ya kitengo cha intelijensia ya nchi ambao wana jukumu la kulinda hadhi na heshima ya Rais.
Mtu yule aliyeteuliwa huku akionekana kwamba hana sifa kabisa ya kushika wadhifa ule, ina reflect..
ombwe la weledi ambalo linaikumba idara hii adhimu ya ujasusi.
Mhe. Rais @SuluhuSamia ambaye watu wametokea kuwa na imani naye sana, tukio la leo kwa kiwango fulani limetia doa hadhi yake na kuzua maswali mengi sana
Kwamba, kosa la dhahiri namna ile limetokeaje?
Intelijensia ya