🚀Kumekuwa na P2E games nyingi zilizoundwa hivi karibuni. Nyingi zikiwa na mfumo wa card based na nyingine trading based.
Thetan Arena inatumia mfumo wa battles (yaani kupiganisha characters ndani ya game).
Battles hizi zinapigwa mtandaoni kati ya character wako na wa adui yako
🚀Characters wa Thetan Arena tunawaita Heroes. Heroes hawa utawapiganisha katika teams.
Na kwa ushindi unaopata utazawadiwa tokens za game hii ambazo kwa sasa token moja ina thamani ya $4.
🚀Kwa sasa game inaweza chezwa katika mifumo ya Battle Royale, Superstar, Deathmatch, na Tower Seige.
Kila mfumo una namna yake ya kucheza. Mifumo karibu yote inahusisha wewe kupigana dhidi ya timu pinzani na timu yako itashinda kwa kuwa timu ya mwisho kuwa hai.
🚀Mfano Tower Siege unaicheza kwa kulinda tower ya timu yako na wakati huo huo kuipiga tower ya wapinzani wenu.
Mtakapo fanikiwa kuangusha tower ya wapinzani mnaibuka washindi na kujishindia Tokens ambazo unaweza uza na kupata pesa.
🚀Heroes wana classes (aina) ndani ya game. Classes hizi ziko aina 3, Assassin, Marksman na Tank.
Assassins ni wale hujificha na wanaweza kusababisha damage kubwa kwa maadui.
Marksman ni wale ambao wanaweza mdhuru adui yako kutoka mbali.
🚀Tank hawa husababisha damage kubwa zaidi kuzidi wote na mara nyingi ndiyo huwa wanaongoza timu.
Nimechagua kuelezea Thetan Arena kwa sababu ni game unaweza anza kuicheza BURE. Yani wanakupa nafasi ya kufanya majaribio kabla hujaamua kuweka pesa yako ili upate nyingi zaidi.
🚀Utakapo jisajili kwenye game sasa hivi kwa mara ya kwanza utapewa kila hero mmoja BURE kwa kila class.
Huyu atakuwa mwenye uwezo mdogo na hatakushindia coins unazoweza uza na kupata pesa.
Kwa sababu huyu umepewa bure ili kufanyia mazoezi.
🚀Nilisema kwamba heroes wana classes 3. Kitu sikusema ni kwamba ndani ya class pia kuna level za hawa heroes.
Heroes hawa hata zawadi za ushindi pia wanatofautiana na gharama unayoweza mnunua pia wanatofautiana.
🚀Mfano tuchukulie class ya Assassin. Levels zake ni hizi
🚀Baada ya kuwa umeshafanya hayo yote, sasa ni muda wa kununua heroe wako kwenye market place ya @ThetanArena
Sasa kabla ya yote muone @MaujanjaCrypto atakuuzia hizo $BNB kisha utahamisha kutoka Binance kwenda Metamask Wallet.
🚀Utaconnect metamask wallet yako na account yako ya Thetan arena kule kwenye market place.
Network unayotakiwa kutumia pale ni Binance Smart Chain. Kuna vitu vya kuzingatia wakati unanunua hero wako.
1. Class ya hero unataka.
2. Level ya hero wako. Kumbuka ukubwa wa level ndiyo ubora wa hero wako. Kwa maana ya kwamba hero mwenye level kubwa ana rewards & bonus kubwa zaidi. Pia anaweza cheza battles nyingi zaidi kwa siku.
3. Battles ambazo tayari amecheza.
Unaweza ona hero anauzwa bei ndogo sana ukaswawishika kumnunua. Lakini akawa amemaliza nusu ya battles anatakiwa kucheza
Frame 1: Hero anauzwa $94 lakini ameshacheza battles 100 kati ya 259 anazotakiwa kucheza.
🚀Maana yake thamani yake itaisha mapema kwa kuwa kabakiza battles 139 tu.
Frame 2: Anauzwa $166 na ana battles 361, pia hajacheza battle yoyote bado.
Huyu ana nafasi ya kukupa faida kwa kuwa utamtumia muda mrefu zaidi.
🚀Najua utaogopa kuona $166 😂. Ukimtumia vizuri kwa hizo battle 361 na kushinda unaweza pata zaidi ya $1,000.
Pia hautapoteza hela yako yote, kwa sababu kwenye thetan arena hata ukipoteza mechi unapewa 1 THG kama zawaid ya kucheza game.
🚀Kwa maana hiyo una nafasi ya kurudisha pesa uliyoanzia au kupata zaidi, kulingana na thamani ya THG iko vipi muda huo.
Pia ukiona battles zinakushinda unaweza rudisha pesa yako kwa kumuuza hero wako.
Na hii ndiyo sababu nimechagua Thetan Arena kwa kuwa ni Win-Win game.
🚀Nimeandika uzi huu kwakuwa sikuweza elezea kwa undani ndani ya magazine ya @HabariTech 😁. Kule nimewapa mwanga wa uchumi mzima wa Play-To-Earn hapa sasa najazia nyama.
Uzuri wa hizi games sio lazima ucheze wewe mwenye. Wengine wanasema, "Mtu mzima hachezi games" 😂😂
🚀Sawa wewe huchezi basi mpe mwanao au mdogo wako anayependa games acheze.
Unajua nini?
Hautaita tena January Njaanuary 😉. Kwa kucheza hizi games mwanao anaweza kuanza jilipia ada yeye mwenyewe.
Haya naita Mafao ya Play-To-Earn. Chelewa Chelewa utakuta mwana si wako.
🚀Tunashukuru kwa sapoti yenu kusoma magazine ya @HabariTech mpaka sasa kwa magazine Toleo 3 tunawasomaji 260+.
📡Mara nyingi camera zilizofichwa huwa na lengo zuri la kudaka wezi au matukio ambayo yanaweza hatarisha usalama.
Na wakati mwingine camera hizi hufungwa kwa lengo la kutumika kudaka matukio ya faragha ili kusambaza kwa lengo la kumtia mtu aibu au kufanya blackmail.
📡Itakuwa vyema leo nikikujuza kuwa unaweza tumia smartphone yako kujua kama kuna camera zimefichwa katika chumba ulichopo.
MUHIMU: Njia hizi hazihusiana na kutambua camera ya Smartphone iliyofichwa.
📡Huenda tabia zetu na namna tunatumia hivi vifaa ikawa ni sababu ya hizi mashine kuharibika haraka
📡Hakuna kitu kinachodumu milele na hasa vifaa vya elektroniki. Watengenezaji wa vifaa hutengeneza vifaa wakiwa na malengo kwamba kwa matumizi sahihi hicho kifaa kitadumu kwa miaka kadhaa.
Muda huo huwa sahihi ukitumia ipasavyo kwa usahihi.