📡Mara nyingi camera zilizofichwa huwa na lengo zuri la kudaka wezi au matukio ambayo yanaweza hatarisha usalama.
Na wakati mwingine camera hizi hufungwa kwa lengo la kutumika kudaka matukio ya faragha ili kusambaza kwa lengo la kumtia mtu aibu au kufanya blackmail.
📡Itakuwa vyema leo nikikujuza kuwa unaweza tumia smartphone yako kujua kama kuna camera zimefichwa katika chumba ulichopo.
MUHIMU: Njia hizi hazihusiana na kutambua camera ya Smartphone iliyofichwa.
1. Chunguza vizuri mazingira ya chumba ulichopo.
Ukiingia ofisini/bank na sehemu nyingine za muhimu kama utatizama vizuri juu utaona camera zimefungwa.
Hata ATM kuna camera imefungwa inayorekodi matukio yote.
Kuna wakati camera za hivi ndizo hufungwa kwenye baadhi ya vyumba hotelini ili kunasa matukio yanayoendelea ndani ya vyumba.
Mara nyingi huwa ni kwa nia nzuri, ila si jambo sahihi kufunga camera ndani ya vyumba.
Kwahiyo unapoingia chumba cha wageni jitahidi kuchunguza vizuri, iwapo utaona camera yoyote.
Una mawili aidha uondoke usitumie hicho chumba au waambie wazime camera zao unataka privacy yako.
2. Tumia simu yako
Hapa kuna njia mbili.
Moja, Washa wifi ya simu yako acha ifanye network scanning kama dakika moja hivi. Kuna aina ya CCTV camera zinakuwa connected na internet.
Hizi ni zile unaweza ona zinarekodi nini kutoka mahali popote duniani.
Camera hizi huonekana hata kwenye Wi-Fi ya simu. Hivyo kwa kutumia wifi ya simu yako utaweza kujua kama kuna camera ndani ya chumba hicho.
Kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini
Mbili, Zima taa zote ndani ya hicho chumba kisha tumia camera ya simu yako (Ku)Scan chumba chote.
Iko hivi, Kuna camera ambazo hutoa infrared radiations kama ya remote za TV au decoder.
Ukilenga camera ya simu yako kwenye camera hizi kuna mwanga utatokea.
Ukiona mwanga wa hivyo sogea karibu uchunguze vizuri ni nini kinatoa mwanga huo. Mara nyingi huwa ni camera iliyofichwa.
Camera hizi hufichwa maeneo haya
.Fire detectors
.Vioo
.Makabati
.Mapambo
.Kona za chumba
.Feni
.Saa za ukutani
3. Chunguza vizuri vioo ndani ya chumba ulichopo
Kuna vioo aina mbili. Vya njia moja na njia mbili.
Kioo cha njia moja ni sawa na kila unatumia nyumbani kujiangalia asubuhi unapojiandaa kutoka.
Vioo vya hivi (kutegemeana na upana wa kioo) ukiweka kidole utaona kuna nafasi kati ya kidole chako na picha ya kidole kwenye kioo.
Kioo cha njia mbili, ni kile ambacho upande mmoja utaona reflection yako, lakini aliye upande wa pili anaona unafanya nini.
Kioo cha njia mbili ukiweka kidole utaona kinagusana moja kwa moja na kile kwenye kioo.
MUHIMU: Inategemeana sana na upana wa kioo.
Mtu aliyeko upande wa pili wa kioo cha njia mbili anaweza rekodi kila unachofanya bila wewe kumuona.
4. Mhoji vizuri mwenyeji wako
Hii ni haswa kwa wale wanaenda faragha kwa ajili ya mambo yao.
Iwapo huna imani na mwenzako, kabla hamjaanza mambo yenu basi tumia namna yote mshawishi simu zenu mziweka mahali pa wazi zionekane.
Pia usikubali ashike simu bila kujua nini anafanya. Itakusaidia kuepukana na aibu zisizo za lazima.
Hii yote ni kwa sababu faragha ni ya muhimu kwa kila mtu. Jali sana privacy yako itakulinda sana.
Usisahau kupakua magazine ya @HabariTech toleo 3 kujifunza mengi zaidi
📡Huenda tabia zetu na namna tunatumia hivi vifaa ikawa ni sababu ya hizi mashine kuharibika haraka
📡Hakuna kitu kinachodumu milele na hasa vifaa vya elektroniki. Watengenezaji wa vifaa hutengeneza vifaa wakiwa na malengo kwamba kwa matumizi sahihi hicho kifaa kitadumu kwa miaka kadhaa.
Muda huo huwa sahihi ukitumia ipasavyo kwa usahihi.