🍿Kampuni nyingi na wanasheria duniani wamejaribu sana kuhakikisha website hii haipatikani mtandaoni bila mafanikio.
Kwa kuwa content zinazokuwepo huko hazikutakiwa kuwepo na mara nyingi zinawakosesha mauzo kwa kuwa ni usambazaji wa content usio sahihi.
🍿Kuna miaka ya nyuma waliwahi fanikiwa kuiondoa online. Bahati mbaya mafanikio yao hayakudumu kwa muda mrefu.
Saa chache baada ya kuondolewa online website ya Pirates bay ilirudi online. Hivyo wakaona wabadili namna ya mashambulizi yao.
🍿Walichokifanya ni kuwageukia waanzilishi wa website hii. Imani yao ikiwa ni kwamba kwa kuwaonda waanzilisha basi wataondoa huu mwiba kwao.
Waliweza kuwakamata na kuwahukumu na kila kosa la hakimiliki pamoja na kuwaweka jela, lakini Pirates Bay website bado iko hewani.
🍿Fredrik Neij, mmoja wa waanzilishi hakujutia kuwepo jela. Alisema kuwa haoni shida kuwepo jela ili mradi tu pirates bay iko hewani.
Pirates bay ilianzia wapi?
Kwanini wanashindwa kuizima?
Nini kimewakuta waanzilishi wake?
Leo tutajibu haya maswali.
🍿Kujua pirates bay imetokea wapi, inabidi turudi nyuma kugusia taasisi ya huko Sweden iitwayo PIRATBYRA, maana yake The Piracy Bureau.
Taasisi hii ilijikita katika kuhalalisha piracy kupitia connection za kisiasa, petitions na lobbying.
🍿Wafanyakazi wa taasisi hii waliamini kwamba taarifa ilitakiwa kusambazwa bure mtandaoni bila kifungo cha hakimiliki.
Kuna wengine walisema piracy ni nzuri kwa kuwa inasambaza softwares kwa mtu hata ambaye angeshindwa kulipia kuipata software hiyo.
🍿Ukifikiria ni kama wako sawa vile. Binafsi sidhani kama sofwares kama Windows au games kama GTA zingekuwa maarufu kama zilivyo sasa hivi.
Mara nyingi nimeona watu wakifanya piracy ya game kwa mara ya kwanza kisha baadae wanalipia baada ya kupata experience nzuri ya software,
🍿September 2003, Wafanyakazi 3 wa PIRATBYRA waliamua kuipeleka mbali zaidi.
Hawa walikuwa ni Peter Sunde, Gottfrid Svartholm na Fredrik Neij walianzisha file sharing website inayojulikana kwa jina la Pirates Bay.
🍿 Wazo lao lilitokana na Bittorrent iliyokuwepo hewani miaka ya nyuma kidogo kabla ya Pirates Bay.
Pirates Bay mwanzo iliendeshwa kupitia servers zilizokuwepo Mexico. Gottfrid aliwashawishi waajiri wake wenye servers mexico wamsaidia kwa kumpa server hizo.
🍿Muajiri huyo hakutaka website hii itumie server kwa muda mrefu, hivyo aliwaondoa baada ya muda mfupi.
Gottfrid aliona isiwe tabu, alihakikisha website inabaki hewani kwa kutumia laptop yake kama hosting server ya hii website.
🍿Hii ilikuwa ni laptop yenye uwezo wa Pentium 3 na RAM yenye 256 MB.
Japo laptop yake haikuwa na uwezo, kulikuwa na traffic kubwa ya watu waliotumia website ya Pirates bay ndani ya muda mfupi.
Hii ni kwa sababu. 2003 hakukuwa na file-sharing websites nyingi kama sasa hivi.
🍿Kufikiwa mwishoni mwa 2004, Pirates bay ilikuwa na watumiaji wapatao 1 million na jumla ya files 60,000 ndani yake.
Kufikia hapo, founders wa pirates bay walilazimika kuongeza servers ili kubeba idadi kubwa ya watumiaji waliyo nayo.
🍿2006, ndipo kila aina ya file mtandaoni ilikuwa shared ndani ya Pirates bay. Kuanzia picha, video mpaka games.
Wakati kampuni kama Mega walijaribu kupunguza ukali wa piracy kwenye huduma yao, Pirates hawakufanya hivyo.
🍿Polisi walivumilia mwanzoni, lakini baadae walishindwa baada ya malalamiko kuwa mengi.
Walilazimika kwenye kuvamia data center ya Pirates mnamo tarehe 31 May 2006.
Polisi 65 walivamia hiyo data center na kufanikiwa kuzima servers zote.
🍿Katika uvamizi huu, hakuna muanzilishi hata mmoja aliyetiwa mbaroni, lakini ujumbe wa polisi uliwafikia.
Hawakutakiwa kuanzisha tena website hii.
Ushahidi mnauona leo, jamaa hawakutii maagizo, walienda nunua servers mpya na kuweka data center eneo lisilojulikana huko Uholanzi
🍿Pirates bay ilirudi hewani ndani ya siku 3 toka server za mwanzo kuzimwa na polisi.
Uvamizi wa polisi ulifanya Pirates Bay kuwa maarufu zaidi. Baada ya kurudi hewani idadi ya watumiaji wa Pirates bay iliongeza kwa kasi kubwa sana.
🍿Jambo hili lilishika sana vichwa vya habari na kupelekea watu wengi kuwa upande wa founders wa Pirates bay.
Mpaka mdukuzi mmoja aliamua kulipiza kisasi kwa kudua website ya polisi wa Sweden. Website hii iliporudi hewani, Website ya serikali ikaondolewa hewani na wadukuzi.
🍿Baada ya uvamizi wa Polisi, Pirates Bay ilipanda kuwa website ya 465 inayotumika zaidi duniani.
Baadhi ya wanasheria walihamia upande wa founders na kusema uvamizi ule wa Polisi haukuwa sahihi.
🍿Hii ni kwa sababu servers zile zilikuwa na website za biashara nyinginezo nje ya Pirates Bay.
Jambo lililopelekea hasara kubwa kwa biashara hizo. Pia Polisi hawakuwa na sababu ya msingi kufanya uvamizi huo.
🍿Wali ilaumu serikali ya Sweden kwa kufata matakwa ya siasa za serikali ya Marekani badala ya kufata sheria zao wenyewe.
Serikali ilikataa mashtaka haya vikali na kesi haikwenda popote ikaisha.
🍿Katika matumizi ya mtandao takribani kila mtumiaji wa mtandao hutumia pirated video, software, audio, picha n.k walau mara moja katika maisha yake.
Hivyo Pirates Bay kutopatikana haikutegemewa kwamba watu wangefurahia,...
🍿... badala yake serikali ya Sweden ilipata tabu kurudisha imani yake kwa watu wake.
Kuona hivyo serikali ikatambua kuwa kufanya uvamizi sio jambo sahihi kwao, hivyo njia iliyobaki ni kuwaondoa waanzilishi.
🍿17 April 2009, waanzilishi wa Pirates Bay pamoja na mtu aliyewapa server Carl Lundstrom walihukumiwa kwa kuwezesha ukiukaji wa hakimiliki na kila mmoja alihukumiwa mwaka 1 jela.
Pia walitakiwa kulipa faini ya $4.3 Million.
🍿Walikata rufaa kwamba serikali ya Sweden inaendeshwa na siasa za nje na sio sheria.
Rufaa yao ilikubalika na kila mmoja alipunguziwa muda wa kifungo chake, badala yake faini ikaongezeka kufikia $6.6 Million.
🍿Muda wa press conference baada ya hukumu Peter Sunde alishika bango lililosema, "Mnanidai $3.2 Million tu" na baadae kuongeza kusema, "Kiasi hiki ndicho serikali itapata, pia mimi sina hiyo pesa na hata ingekuwepo ni bora nichome moto kila nilicho nacho, nisiwape hata majivu."
🍿Carl na Peter hakugoma kuwekwa chini ya ulinzi, lakini haikuwa hivyo kwa Fredrik na Gottfrid.
Gottfrid alitoroka kwenda Cambodia nchi ambayo haina sera ya kusafirisha wahalifu kurudi Sweden.
🍿Japo, pamoja na kutokuwa na sera hii, Gottfrid alikamatwa na Polisi wa Cambodia mnamo 30 August 2012 na kusafirishwa kwenda Sweden.
Ilisemakane Sweden na Cambodia walikuwa na makubaliano nyuma ya pazia.
🍿Kwa kuwa siku chache baada ya hapo, Cambodia walipokea msaada wa $41.6 Mil kutoka Sweden.
Gottfrid aliongezwa kesi ya udukuzi na ulaghai ambayo iliongeza kifungo chake kufikia miaka 3.
Alitumikia kifungo chake kwa miaka yote 3.
🍿Fredrik aliweza kuwakimbia polisi kwa muda mrefu. Alitorokea kwenda Laos/Thailand.
Aliishi katika hizi nchi mbili na alivuka mipaka mara kwa mara.
November 2014 aliwekwa chini ya ulinzi siku moja akivuka mpaka kwenda nchi nyingine.
🍿Yeye pia alirudishwa nchini Sweden ili kutumikia kifungo chake. Alibahatika kwa kuwa kifungo chake hakikuwa cha muda mrefu.
Yeye alihukumiwa kifungo cha Miezi 10 tu.
Ikiwa founders wote wako jela, ilikuwa ni muda mzuri kwa polisi kuzima Pirates bay jumla.
🍿9 December 2014, Polisi walivamia server za pirates bay kwa mara nyingine tena na kuchukua servers zote pamoja na computer na vifaa vingine vyote.
Hii ilitakiwa kuwa mwisho wa Pirates Bay kwa kuwa waanzilisha hawakuwepo kuirudisha tena.
🍿Siku 4 baada ya Pirates Bay kuondolewa hewani, moja ya torrent website iliyoitwaji Isohunt walianzisha website yenye jina la oldpiratesbay.org
Website hii ilibeba content zote zilizokuwemo katika website ya zamani a Pirates Bay.
🍿Hapa ndipo mamaka husika walitambua kuwa huu mchezo ni mgumu kwao.
Walichoshindwa kuelewa ni kwamba Pirates Bay hawakai na files wao wenyewe.
Wanaunganisha computer (peers) duniani kwa kutumia links.
🍿Kinachotunza ndani ya Pirates Bay ni links za kuzifikia hizi content, content zenyewe zipo katika kifaa cha kila mtumiaji wa torrent.
Maana yake ni kwamba kila unapo pakua kitu kupitia torrent unatengeneza copy ya content hiyo kuja kwako (leeching).
🍿Unapofanya seeding unaruhusu watu wengine wapakue content hiyo kutoka kwako.
Hivyo ikitokea kwamba Website moja ya torrent imeondolewa, sio ngumu sana kuanzisha website nyingine na kurudishia content zote zilizokuwepo.
🍿Hii ndiyo sababu haiwezekani kuizima kabisa Pirates Bay kwa kuwa haiko sehemu moja.
Kuona hilo mamlaka husika wameona ni bora kufanya kazi na ISP ili kuzuia huduma za internet kwa watu wanaofanya Piracy.
Pamoja na jitihada hizi bado wanashindwa kudhibiti kabisa.
🍿ISP kuzuia huduma kwa watumiaji wa Pirating site kumepelekea Pirates kuanza tumia VPN.
Kuhusu waanzilishi, sasa hivi Peter alifungua kampuni inayotoa huduma zinazoendana na Patreon, kampuni hiyo inaitwa Flattr.
🍿Yenyewe inatoa misaada kwa websites badala ya creators kama ilivyo Patreon. Pia inatumika kuvumbua mambo ya rushwa kama ilivyo WikiLeaks.
Gottfrid na Fredrik wameamua kupotea hawajulikani walipo na watumia internet bila kujulikana.
Fredrik alipotoka jela alisema atarudi Laos.
🍿Hizi ndizo sababu Pirates bay haiwezi kuondolewa hewani na ndicho kilichowakuta waanzilishi wa Pirates Bay.
Kujua founders wa startups za Tanzania wamefanya nini usisahau kupakua magazine hii ya @HabariTech
👽Moja ya kikwazo kilisema, "Kuzuia zaidi ya nusu ya uagizaji wa Russia kuingiza teknolojia ya juu nchini mwao, Kuzuia Russia kupata pembejeo muhimu za kiteknolojia, Kudhoofisha msingi wao wa viwanda...
👽...na kudhoofisha matarajio ya kimkakati ya Russia ya kuwa na Ushawishi katika jukwaa la ulimwengu." -mwisho wa nukuu.
Inawezekana ilionekana ni kikwazo kikubwa kwa muda huo. Ila ni kidogo sana ukilinganisha na yaliyofata baada ya hapo.
Au wanavyofanya @CipherdotM na channel yao ya movies. Kwa wengine telegram ni sehemu ya kupakua miziki ya Spotify, YouTube au Apple Music bila kuwa na account katika platform hizo.
Na wengine wanatumia kupakua movies za Netflix ama Amazon Prime
Bahati mbaya channel & bots nyingi zinazotumia majina na content za kampuni kubwa huwa zinafungiwa na telegram kwa sababu ya ukiukaji wa hakimiliki (copyright infringement).
Telegram wapo kulinda maslahi yao na ya kampuni nyingine, hivyo ni lazima wafanye hivi.
Confidentiality, Integrity & Availability hizi ni kama muongozo wa usalama wa aina yoyote, ili kulinda taarifa zinazotunzwa au kutumwa dhidi ya mtu asiye husika.
Confidentiality, inahakikisha kwamba mtu asiyetakiwa kuwa na access hapati hiyo access. mfano account yako ya twitter inalindwa na password yako.
Password unayoijua wewe na kuiweka siri ndiyo confidentiality yenyewe. Maana yake ili mt apate access lazima umpe hiyo password.
Integrity, account yako ya twitter ikatokea imedukuliwa alafu tweets zikawa tofauti na tulivyokuzoea tutajua sio wewe.
Hapo integrity imepotea. Kwahiyo integrity ni ukweli na kuaminika kwa data. Mtu asiye ruhusiwa ku access system hatakiwi kuweza badili data ili integrity iwepo
📡Mara nyingi camera zilizofichwa huwa na lengo zuri la kudaka wezi au matukio ambayo yanaweza hatarisha usalama.
Na wakati mwingine camera hizi hufungwa kwa lengo la kutumika kudaka matukio ya faragha ili kusambaza kwa lengo la kumtia mtu aibu au kufanya blackmail.
📡Itakuwa vyema leo nikikujuza kuwa unaweza tumia smartphone yako kujua kama kuna camera zimefichwa katika chumba ulichopo.
MUHIMU: Njia hizi hazihusiana na kutambua camera ya Smartphone iliyofichwa.