Kwanini pirates wanatumia torrents kusambaza na kupakua files zao?
Huduma nyingine za internet zinazoendana na torrents kwanini hazitumiki katika sharing ya pirated files?
Haya maswali yote yanapatiwa majibu kupitia Bittorrent protocol.
🎁Unapofungua browser ili kuperuzi mtandao, browser inatuma request kwenda kwenye server yenye IP address ya website unayotaka kuifikia.
Request hii inaenda kuiomba server ikupe HTML za hiyo website ili uweze kuiona na kufanya kitu unataka.
🎁Ombi lako likikubalika, kwamba server iko hewani na website unataka kuifikia ipo, jibu linarudi kwako kwa mfumo wa picha, video na maneno (Kama websites zinavyo onekana).
Hapa kila unapotafuta website au kwenda page mpya, browser yako inapakua hizi data kutoka kwenye server.
🎁Mtandao umeundwa na WWW.
Kila website unayoona mtandaoni ipo katika server moja au zaidi katika maeneo tofauti tofauti duniani.
Unapotaka kuifikia website kama habaritech.com request inatumwa kwa moja wapo ya server ndipo majibu yarudi kwako.
🎁Uhusiano huu unaitwa Client-Server Model.
Yani ni sawa na pale mtaani kwenu kuna duka 1 la mangi ila wateja wengi.
Mangi = Server
Wateja = Clients
Kwa maana hiyo client hautakuwa wewe pekee unayetuma request kwenye server.
Inawezekana clients 1000 mkatuma request kwa pamoja
🎁Itakuwaje sasa kama duka la mangi likafungwa?
Watu wote mtashindwa kupata mahitaji yenu kwa siku hiyo. Maana yake server inapoacha kufanya kazi, request zote kwenda kwenye server hazitajibiwa.
Client-Server ni uhusiano ambao uko centralized, na hii ndiyo moja ya hasara yake.
🎁Torrents
Torrents zinatumia BitTorrent protocol.
Hii ni Peer-2-Peer (P2P) protocol. Yaani mteja na mteja mnahudumiana wennyewe moja kwa moja.
Mama chausiku akihitaji mafuta ya kula anaenda kwa Mama Majuto. Hakuna haja ya duka la mangi.
🎁P2P protocol inaruhusu kila computer kwenye mtandao kuwasiliana zenyewe moja kwa moja.
Hapo nadhani umeona utofauti uliopo kati ya Client-Server Network na hii Peer-2-Peer Nerwork.
🎁Tunapopakua files kutoka torrent. Kwanza huwa tunapakua torrent file ambayo tunaenda itumia kwenye torrent client kama uTorrent (Micro Torrent).
Wengi huwa mnaita u-Torrent, ile sio U. ni herufi ya kigiriki yenye maana ya Micro.
🎁Torrent client ndiyo inaanza pakua file yetu tunayotaka kama vile movie ya Batman 2022.
Ile .torrent file ya Batman tuliyo ipakua imebeba Metadata kuhusu movie ya Batman na sio movie yenyewe.
Metadata na ni taarifa kuhusu data zenyewe kabisa (eg file size, structure ya file)
🎁Metadata ndani ya .torrent file pia inabeba tracker addresses.
Trackers ni server inayobeba orodha ya computer zote ambazo tayari zina movie yetu ya Batman.
Computer hizi tunaziita seeders.
Bila shaka mtumiaji wa torrents umeshakutana na huu msamiati wa seeders.
🎁Seeding ni kitendo knachotokea mara baada ya kumaliza kupakua movie yako kupitia torrent client.
Unapofanya seeding unaruhusu watu wengine (Leechers) kupakua vipande vya movie hiyo kutoka kwako.
Nitaelezea mbele kwanini nasema vipande.
🎁Kabla hatujafika mbali ieleweke kwamba kutumia torrents ni kinyume cha sheria, na baadhi ya nchi kama Germany wana sheria kali kupinga torrents.
Ukiwa Germany na PC yako ikagundulika inafanya torrent seeding, utawekwa chini ya ulinzi wa polisi mara moja.
🎁Sasa unapofungua ile .torrent file kwa torrent client, ile client ya uTorrent kwanza itafanya connection na trackers zote ili kuunganika na computer zenye hilo file unapakua.
Baada ya hapo uTorrent itapakua file hiyo moja kwa moja kutoka kwenye hizo PC (seeders) kuja kwako.
🎁Seeders wataendelea kufanya upload ya file, endapo tu torrent client (uTorrent) yake inafanya kazi.
Akizima uTorrent yake, utaendelea kupakua kutoka kwa wengine.
Zoezi hili litashindika iwapo hakuna seeder hata mmoja wa hiyo file.
🎁Unapopakua torrent file, wewe unaitwa "Leecher".
Huu mtandao wa Seeders & Leechers unaitwa Torrent Swarm.
Unapofanya leeching haupakui file lote kutoka kwa seeder mmoja. File inakuwa katika vipande ndani ya PC tofauti tofauti.
Hivyo wewe unapakua kipande kwa kila seeder.
🎁Baada ya kumaliza kupakua hivi vipande ndipo, torrent client yako inachukua jukumu la kuviweka pamoja hivi vipande ili kuunda file zima kama inavyotakiwa.
Kwa kufanya hivi download speed inakuwa kubwa, kwa kuwa unachukua vipande vipande kutoka kwa watu wengi.
🎁 Ukimaliza kupakua file yako, unageuka kuwa seeder. Unaanza upload file ili watu wengine wapakue kutoka kwako.
Sio lazima uwe seeder. Unaweza zima seeding ya file ili kutoendelea tumia bando lako.
Ila huo ni ubinafsi 😁 Wewe umepakua kwetu bure, ila hutaki wenzako wapate.
🎁Nasema hivyo kwa sababu, kadiri seeder wanavyokuwa wengi ndivyo ambavyo download speed inaongezeka.
Kama bando ni ya mawazo, sio mbaya zima tu seeding.
👽Moja ya kikwazo kilisema, "Kuzuia zaidi ya nusu ya uagizaji wa Russia kuingiza teknolojia ya juu nchini mwao, Kuzuia Russia kupata pembejeo muhimu za kiteknolojia, Kudhoofisha msingi wao wa viwanda...
👽...na kudhoofisha matarajio ya kimkakati ya Russia ya kuwa na Ushawishi katika jukwaa la ulimwengu." -mwisho wa nukuu.
Inawezekana ilionekana ni kikwazo kikubwa kwa muda huo. Ila ni kidogo sana ukilinganisha na yaliyofata baada ya hapo.
Au wanavyofanya @CipherdotM na channel yao ya movies. Kwa wengine telegram ni sehemu ya kupakua miziki ya Spotify, YouTube au Apple Music bila kuwa na account katika platform hizo.
Na wengine wanatumia kupakua movies za Netflix ama Amazon Prime
Bahati mbaya channel & bots nyingi zinazotumia majina na content za kampuni kubwa huwa zinafungiwa na telegram kwa sababu ya ukiukaji wa hakimiliki (copyright infringement).
Telegram wapo kulinda maslahi yao na ya kampuni nyingine, hivyo ni lazima wafanye hivi.
Confidentiality, Integrity & Availability hizi ni kama muongozo wa usalama wa aina yoyote, ili kulinda taarifa zinazotunzwa au kutumwa dhidi ya mtu asiye husika.
Confidentiality, inahakikisha kwamba mtu asiyetakiwa kuwa na access hapati hiyo access. mfano account yako ya twitter inalindwa na password yako.
Password unayoijua wewe na kuiweka siri ndiyo confidentiality yenyewe. Maana yake ili mt apate access lazima umpe hiyo password.
Integrity, account yako ya twitter ikatokea imedukuliwa alafu tweets zikawa tofauti na tulivyokuzoea tutajua sio wewe.
Hapo integrity imepotea. Kwahiyo integrity ni ukweli na kuaminika kwa data. Mtu asiye ruhusiwa ku access system hatakiwi kuweza badili data ili integrity iwepo
📡Mara nyingi camera zilizofichwa huwa na lengo zuri la kudaka wezi au matukio ambayo yanaweza hatarisha usalama.
Na wakati mwingine camera hizi hufungwa kwa lengo la kutumika kudaka matukio ya faragha ili kusambaza kwa lengo la kumtia mtu aibu au kufanya blackmail.
📡Itakuwa vyema leo nikikujuza kuwa unaweza tumia smartphone yako kujua kama kuna camera zimefichwa katika chumba ulichopo.
MUHIMU: Njia hizi hazihusiana na kutambua camera ya Smartphone iliyofichwa.