👽Moja ya kikwazo kilisema, "Kuzuia zaidi ya nusu ya uagizaji wa Russia kuingiza teknolojia ya juu nchini mwao, Kuzuia Russia kupata pembejeo muhimu za kiteknolojia, Kudhoofisha msingi wao wa viwanda...
👽...na kudhoofisha matarajio ya kimkakati ya Russia ya kuwa na Ushawishi katika jukwaa la ulimwengu." -mwisho wa nukuu.
Inawezekana ilionekana ni kikwazo kikubwa kwa muda huo. Ila ni kidogo sana ukilinganisha na yaliyofata baada ya hapo.
👽Mambo yalizidi kuwa mabaya kwa Russia, baada ya mamilioni ya watu kuonyesha kutofurahishwa na anachokifanya Russia.
Serikali za dunia na kampuni binafsi zilichukizwa na kitendo hiki na walianza ichukulia Russia hatua.
👽Vikwazo vilivyotangazwa na serikali za dunia na hatua zilizochukuliwa na kampuni binafsi iwapo vitasimama, kuna uwezekano mkubwa uchumi wa Russia utayumba vibaya mno.
Upande wa Teknolojia hii hali itafanya Russia irudi nyuma zaidi ya miaka 10.
👽Russia anatumia teknolojia kupigana vita zake. Kuanzia Cyberattacks mpaka vifaa vya kivita anavyotumia kuharibu miundo mbinu ya mawasiliano huko Ukraine.
Vikwazo vya mwanzo vya US viligawanyika katika makundi mawili.
👽Moja, ilikuwa katika mali zilizo milikiwa na serikali. Kikwazo hiki kilizuia kuagiza vipuli vya vifaa vya kivita, hakuna user manual za vifaa kwenda Russia wala misaada ya kifedha inayohusu teknolojia ya vifaa vya vita.
👽Hii ina maana ya kwamba Russia hatakiwi kupokea tech yoyote iliyoundwa US bila kibali maalumu cha serikali.
Mbili, Watu wasio husika na jeshi kikwazo hiki kina maana hawataweza kupata vitu kama semi conductors, vifaa vya mawasiliano, huduma za usalama, avionics, sensors n.k.
👽EU, Korea Kusini na Japan pia waliweka vikwazo vinavyo endana na hivyo kwa namna yao.
Japo kwa nchi kama Korea Kusini hawakuweka vikwazo vigumu kwa kampuni zoa.
Samsung bado aliendelea kupeleka simu zake nchini Russia.
👽Waziri mkuu wa Italy pia alipendekeza bidhaa za starehe kama bidhaa za Gucci zisiwepo katika orodha ya vikwazo.
Mambo yalienda vizuri, lakini Russia alipozidisha uvamizi, mambo yalianza kubadilika.
👽Kampuni Binafsi kama Samsung na Prada wakaona ni bora wakafuata serikali za zilichofanya na kuacha kupeleka bidhaa zao nchini Russia.
Hata walionunua nishati kutoka Russia wakaona ni bora kuachana na zoezi hilo na kutafuta njia mbadala.
👽Kilichofuata ni kampuni za usafirishaji kuacha kutoa huduma yao Russia.
Hizi ni Maersk, FedEx na DHL.
Hii imepelekea kampuni za magari kama Ranault kushindwa endeleza huduma nchini Russia, hivyo kusimamisha utoaji huduma.
👽Orodha ya kampuni zinazoacha kutoa huduma kwa Russia inazidi kuongezeka.
Hata kampuni za ndege kama Airbus na Boeing wameacha kutoa huduma zao kwa Russia.
Kampuni hizi mbili wameacha kuuza ndege zao Russia, pia hawasafirishi tena vipuli kwenda Russia.
👽Kushindwa kupokea vipuli vya ndege pamoja na wataalamu na maelekezo ya matengenezo ya ndege kutafanya baadhi ya ndege kushindwa kuendelea na kazi ndani ya wiki chache.
Haya ni maoni yaliyotolewa na wataalamu kutoka Amadeus na Sabre.
👽Amadeus na Sabre ni kampuni zinazoongoza kwa kuuza tiketi za ndege dunia nzima.
Software za kampuni hizi zinatumika na kampuni za Russia kama Aeroflot zinatumia kuendesha biashara zao pamoja na kampuni za nje ambazo zinamiliki na...
👽...kukodisha takribani ndege 515 kati ya 980 zinazotumika na kampuni za ndege za Russia.
Kwa maana hiyo zaidi ya nusu ya ndege za abiria zilizopo Russia itatakiwa zirudi kwa wamiliki wake nje ya nchini kabla ya mwisho wa mwezi huu.
👽Upande wa magari na malori, karibu brand kubwa zote zinaacha kutoa huduma nchini Russia.
Kampuni kama Volvo, Mercedes, Volkswagen, Toyota, Renault na Ford zimeacha kuuza na kutoa huduma nchini Russia.
Pia wamefunga viwanda vyao nchini humo.
👽Ili ujue hii kitu inawaumiza kiasi gani Russia nikwambie hivi, "95%" ya vipuli vya magari nchini Russia vinaagizwa kutoka nje.
Bila kampuni ya usafirishaji kama Maersk, watengenezaji vipuli hawana budi ila kuacha kupela vipuli nchini Russia.
👽Upande wa consumer electronics, orodha hii ina kampuni kama Apple, Samsung, Dell na HP.
Katika biashara kubwa zinazotoa huduma kuna Microsoft, SAP na Oracle wameacha kutoa huduma mpaka za huduma kwa wateja.
👽Kampuni za malipo kama PayPal wameacha kabisa kutoa huduma yao nchini Russia, wakati huo huo Mastercard, Apple pay, Google pay na Visa wamepunguza huduma zao kwa kiasi kikubwa.
👽Mpaka sasa viwanda vingi nchini Russia vimeacha kufanya kazi. Waliobaki wanalazimika kubadili miundombinu ili kuendelea na kazi.
Kulingana na bloomberg, watu 3 milion wa Russia wanafanya kazi katika kampuni za nje au zinazoshirikiana na kampuni za nje kutoa huduma zao.
👽Kwa maana hiyo hawa watu 3 milion wapo katika hatari ya kupoteza kazi zao.
Hili jambo pia litaua biashara ndogo ndogo nchini humo.
Hii ni kwasababu hizi biashara aidha zinasambaza bidhaa zao kwa biashara kubwa au zinategemea bidhaa kutoka biashara kubwa za nje.
👽Hata kampuni zenye high-tech huko Russia zinategemea teknolojia ya nje.
Vitu kama roboti za viwandani kutoka Germany, Factory Automations kutoka US na Japan, hata kampuni za kuzalisha nishati za Russia zinategemea vifaa na software kutoka nje.
👽Swali ni je, hizi kampuni zitaweza kuendelea kufanya kazi?
Wakati haya yote yakiendelea, bado Russia wakapigwa tena na kitu kizito. Russia hatoweza kupokea kabisa Processor chip zenye ubora wa hali ya juu.
Walichobaki nacho ni consumer grade chip.
👽Intel & AMD walitangaza kuacha kupeleka Russia na Belarus processor za viwandani.
Zile zinazotumika kuendesha mitambo ya viwandani. Hizi ni pamoja na processor za servers na PC.
Hapa wanaguswa watu wa gaming PC, servers na supercomputers za Jeshi.
👽Nokia na Ericsson wameacha kuuza vifaa vya mtandao nchini Russia.
Huawei na ZTE bado hawajatoa tamko, lakini hawataweza kuuza vifaa vinavyotumia teknolojia zilizozuiliwa.
Vifaa hivi ni kama ASML machines havitatakiwa kuuzwa kwenda Russia.
👽Hii ina maana kwamba watoa huduma za mitandao ya simu watalazimika kubadili teknolojia waliyonayo na kuanza nunua teknolojia mpya kutoka China.
Russia sio kati ya nchi zenye uhitaji mkubwa wa processor chip kwa kuwa wao hununua vifaa vilivyopo tayari kwa matumizi.
👽Hivyo watu wanaweza pata intel processor katika laptop za Huawei au Qualcomm chip katika simu za Xiaomi.
lakini kitu chochote complex zaidi ya hapo kama processor kwa ajili ya vifaa vya jeshi hawataweza kupata.
👽Maabara zenye ubora zaidi Russia wana uwezo wa kutengeze processor chip kufikia 65nm tu. Hizi ni processor ambazo hazina uwezo mkubwa.
Zinatumika kwa kazi ndogo ndogo kama card za bank na milango zinazotumia electronic chip.
👽Kampuni mbili kubwa zinazofanya Chip Design nchini Russia Baikal Electronics na MLICT wanawatumia TSMC kama kiwanda cha kufanya manufacturing.
TSMC pia wametangaza kuwa wanaacha kufanya kazi na Russia.
👽Baadhi ya drones za jeshi za Russia zilizokamatwa Ukraine zimegundulika kutumia teknolojia ya nje kwa kiasi kikubwa.
Vitu kama Camera, Sensors mpaka Motors.
Labda Russia wanaweza kwenda China kuanza tumia Teknolojia za huko.
👽Lakini hata hiyo pia itakuwa ngumu kwa kuwa kampuni kama SMIC ya china pia wanatumia teknolojia ya nje ya China kuunda baadhi ya vifaa vyao.
Hivyo nao wanaweza kusiti kwa kuogopa kufungiwa teknolojia hizo na kampuni za nje.
Ninachoona ni kwamba Putin hakujiandaa na vikwazo vya namna hii. Jambo hili litapelekea kuyumba sana kwa uchumi wa Russia.
Lakini ngoja tusubiri kuona nini kitafata baada ya vita kuisha.
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
Au wanavyofanya @CipherdotM na channel yao ya movies. Kwa wengine telegram ni sehemu ya kupakua miziki ya Spotify, YouTube au Apple Music bila kuwa na account katika platform hizo.
Na wengine wanatumia kupakua movies za Netflix ama Amazon Prime
Bahati mbaya channel & bots nyingi zinazotumia majina na content za kampuni kubwa huwa zinafungiwa na telegram kwa sababu ya ukiukaji wa hakimiliki (copyright infringement).
Telegram wapo kulinda maslahi yao na ya kampuni nyingine, hivyo ni lazima wafanye hivi.
Confidentiality, Integrity & Availability hizi ni kama muongozo wa usalama wa aina yoyote, ili kulinda taarifa zinazotunzwa au kutumwa dhidi ya mtu asiye husika.
Confidentiality, inahakikisha kwamba mtu asiyetakiwa kuwa na access hapati hiyo access. mfano account yako ya twitter inalindwa na password yako.
Password unayoijua wewe na kuiweka siri ndiyo confidentiality yenyewe. Maana yake ili mt apate access lazima umpe hiyo password.
Integrity, account yako ya twitter ikatokea imedukuliwa alafu tweets zikawa tofauti na tulivyokuzoea tutajua sio wewe.
Hapo integrity imepotea. Kwahiyo integrity ni ukweli na kuaminika kwa data. Mtu asiye ruhusiwa ku access system hatakiwi kuweza badili data ili integrity iwepo
📡Mara nyingi camera zilizofichwa huwa na lengo zuri la kudaka wezi au matukio ambayo yanaweza hatarisha usalama.
Na wakati mwingine camera hizi hufungwa kwa lengo la kutumika kudaka matukio ya faragha ili kusambaza kwa lengo la kumtia mtu aibu au kufanya blackmail.
📡Itakuwa vyema leo nikikujuza kuwa unaweza tumia smartphone yako kujua kama kuna camera zimefichwa katika chumba ulichopo.
MUHIMU: Njia hizi hazihusiana na kutambua camera ya Smartphone iliyofichwa.