➡️Saratani ya titi ni kati ya saratani zinazowaathiri zaidi wanawake. (Namba 2 chini ya saratani ya shingo ya kizazi)
➡️Mwaka 2020 Tanzania kulikuwa na wagonjwa wapya 3992 wa saratani ya matiti (hawa ni wale waliofika kwenye vituo vya Afya) wengi huchelewa tiba
Uelewa ni muhimu
➡️Kuwa na uelewa kuhusu mwili wako na kuweza kugundua mabadiriko ni moja ya njia bora ya kulinda afya yako.
➡️Hii ina umuhimu mkubwa hasa linapokuja suala la matiti kwa wanawake.
Kwa wastani mwanamke 1 kati ya 8 huwa na uwezekano wa kupata saratani ya matiti kwa maisha.
KUCHUNGUZA SARATANI YA MATITI
1⃣Kujichunguza mwenyewe mara kwa mara kwa mara.
2⃣Uchunguzi wa kitabibu wa matiti kila mwaka.
3⃣Wanawake wote wenye umri kuanzia miaka 21 wajichunguze matiti yao siku ya 5-7 baada ya kumaliza hedhi mbele ya kioo.
DALILI 1 - UGUMU KWENYE TITI
➡️Saratani huweza kuja kama eneo gumu kwenye ngozi ya titi.
➡️Lakini sio kila ngozi ngumu kwenye titi ni saratani, huweza kutokea hata wakati wa hedhi au kunyonyesha.
➡️Ni muhimu hali hii kwenye titi kuangaliwa na daktari ili kujihakikishia.
DALILI 2 - KISHIMO KWENYE TITI (Dimple)
➡️Uvimbe wa saratani huweza kuvuta ngozi na tishu za titi ndani na kusababisha kishimo.
➡️Kishimo ambacho hakiondoki huweza kuwa dalili ya uvimbe ndani za titi hivyo huitaji uchunguzi.
DALILI 3 - UKOKO KWENYE CHUCHU (Crusty)
➡️Hali ya ukoko kwenye chuchu mara nyingi huwa sio tatizo kubwa, vilevile huweza kuwa dalili ya ugonjwa wa Paget.
➡️Seli za saratani ya ziwa huweza kuishi katika chuchu na kusababisha hali ya ukoko hasa wekundu ambao hautoki.
DALILI 4 - WEKUNDU KATIKA ZIWA
➡️Wekundu na ziwa kupata joto mara nyingi ni dalili ya maambukizi kwenye ziwa (mastitis) hasa wanaonyonyesha.
➡️Lakini kama matibabu hayasaidii; wekundu kwenye maeneo ya ziwa huweza kuwa dalili ya aina ya saratani (inflammatory breast cancer).
DALILI 5 - CHUCHU KUTOA MAJIMAJI
➡️Chuchu zinapoanza kutoa majimaji yanayotoka katika kipindi usipotarajia mfano: Huna maambukizi, huna ujauzito wala hunyonyeshi ni muhimu hiyo hali ikaangaliwa na daktari.
DALILI 6 - KIDONDA/VIDONDA KWENYE TITI
➡️Saratani ya matiti huweza kusababisha kidonda kwenye titi.
➡️Mara nyingi kidonda hiki huambatana na uvimbe mgumu ndani ya titi.
➡️Kadri muda unavyokwenda kidonda hiki huweza kuanza kutoa harufu.
DALILI 7 - UVIMBE/KIVIMBE KWENYE TITI
➡️Uvimbe mlaini kwenye ziwa huweza sababishwa na changamoto mbalimbali ambazo sio saratani.
➡️Lakini uvimbe ambao ni mgumu, pia haujongei ndani ya ziwa huweza kuwa saratani.
Ni muhimu kila uvimbe kuangaliwa na daktari.
DALILI 8 - CHUCHU KUINGIA NDANI
➡️Mabadiriko kwenye umbo la chuchu kama chuchu kuingia dani huweza kuwa dalili ya saratani.
➡️Uvimbe wa saratani ukiwa unakua ndani ya titi huvuta chuchu kuelekea kwake.
DALILI 9 - MSHIPA MPYA UNAOKUA KWENYE TITI
➡️Mara nyingi mtu anaponenepa au kunyonyesha matiti hupata mishipa ya damu inayoonekana kwenye ngozi.
➡️Lakini katika hali ambayo ni nadra sana; mshipa mpya kwenye ngozi ya titi huweza kuwa dalili ya saratani ya titi.
DALILI 10 - TITI KUBADILIKA UMBO AU UKUBWA
➡️Kwa kawaida ujauzito, unyonyeshaji au hedhi huja na mabadiriko ya umbo/ukubwa wa maziwa.
➡️Lakini iwapo titi moja bila kutarajia linapovimba, kubadiri umbo au kuanguka ni dalili inayohitaji uchunguzi.
DALILI 11 - NGOZI YA TITI KUWA KAMA GANDA LA CHUNGWA
➡️Ngozi ya titi mara nyingi ni laini.
➡️Inapotokea ngozi ya titi kuanza kupata mwonekano kama ganda ya chungwa huweza kuwa dalili ya saratani hasa aina inayoitwa "inflammatory breast cancer".
MUHIMU
⚠️Iwapo utagundua au utaona badiriko lolote kwenye matiti/titi ni muhimu kutopuuzia.
✍️Nenda Hospitali
✅Daktari atachukua historia yako na kukupima pia kuna vipimo muhimu kwenye uchunguzi kama mammogram utafanyiwa.
Saratani ya matiti inatibika, chukua hatua mapema, itambue na wahi kupata ushauri wa kitaalamu.
• • •
Missing some Tweet in this thread? You can try to
force a refresh
#AfyaSwahili | MAMBO MUHIMU KUFAHAMU KUHUSU UGONJWA WA EBOLA.
--> Uzi huu ni muhimu kutokana na kuwepo kwa mlipuko wa Ebola katika nchi jirani na elimu ya msingi ni muhimu sana.
➡️Ebola ni ugonjwa unaotokana na maambukizi vya virusi.
➡️Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa ya mlipuko yajulikanayo kama homa za virusi ambazo huambatana kutokwa damu sehemu mbalimbali za mwili (Viral haemorrhagic fevers).
➡️Ebola ni ugonjwa hatari sana.
➡️Kwa wastani husababisha vifo kwa wastani wa nusu wa watu wote waliougua.
➡️Uwezo wa kusababisha vifo hutofautiana kati ya mlipuko na mlipuko kwa wastani vifo huwa 20% hadi 90% ya wagonjwa.
➡️Kisukari ni ugonjwa wa kudumu ambao hutokea pale kiwango cha sukari (glukosi) katika damu
kipo juu zaidi kutokana na kukosekana au mwili kushindwa kutumia homoni ya insulini
➡️Kiwango cha glukosi kikiwa juu kwa muda mrefu, husababisha madhara katika mwili
➡️Unapokula chakula, mfumo wako wa kumeng’enya hukichakata na kutengeneza glukosi.
➡️Glukosi inapoingia kwenye damu, husababisha kongosho lako kutoa homoni inayoitwa insulini.
➡️Insulini huzunguka mwilini na kuwezesha seli kupata glukosi ili kuitumia kuleta nguvu mwilini.
➡️Tatizo la dharura la kiafya ambalo ni moja ya magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo.
➡️Mitindo ya maisha na Lishe ni vitu vinavyochangia wagonjwa wanaopata stroke kuongezeka
➡️Kiharusi huacha ulemavu au kifo
➡️KIHARUSI hutokea pale seli za ubongo 🧠 zinapokufa kutokana kuziba au kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo hivyo kukosa hewa ya oksijeni na virutubisho.
➡️Kiharusi kikihusisha mshipa wa mkubwa wa damu kwa wastani mgonjwa hupoteza seli za ubongo (neuroni 1.9) kila dakika.
KUNA AINA KUU MBILI ZA KIHARUSIBrain
1️⃣Kiharusi kinachotokana na kuziba kwa mishipa ya damu ya damu ya ubongo
2️⃣Kiharusi kinachotokana na kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo
🗒️80% ya watu wanaopata kiharusi hutokana na kuziba kwa mishipa ya damu kwenye ubongo.
Matumizi holela ya dawa aina ya antibiotiki huchangia usugu wa dawa kutokea.
Bakteria wanapopata usugu husababisha
➡️Kutokupona ugonjwa hata baada ya kutumia antibiotiki ambazo zimekuwa zikitibu ugonjwa huo
➡️Kuongezeka kwa gharama za matibabu
➡️Kifo
Unatengeneza tatizo usugu wa dawa iwapo
➡️Humalizi dawa ulizoandikiwa na daktari
➡️Unatumia dawa zisizo na ubora/feki
➡️tumia dawa zilizoisha muda wake wa matumizi
➡️Unakula nyama, maziwa, mayai au damu yenye masalia ya antibiotiki kutoka kwa mifugo iliyotibiwa