My Authors
Read all threads
DILI FEKI SAFARI YA SIKU TATU NAIROBI
mwaka 2016 ndio mwaka ambao akili yangu ilikuwa na udhubutu mkubwa wa kuamua na kufanya mambo mengi hasa ya kibiashara, leo nitaeleza namna ambavyo niitiwa dili feki la kuuza used bottles Nairobi! Kama kawaida unapotafuta kitu internet ni..
ni lazima uanze kwa kugugo na kutafuta taarifa, basi rafiki yangu alikuwa anatafuta Package materials na aliniomba nimsaidia kutafuta kwa sababu nilifahamiana na watu Nairobi, basi nikaingia zangu kwenye internet na kuumpa jamaa mmoja Nairobi na tukaanza kuongea biashara hiyo
Jamaa mwenyewe mkikuyu anaitwa Kariuki, niliongea nae na nikampa mshikaji wangu number zake ili aweze kupata Package za products zake, basi jamaa wakaongea lkn hawakuweza kufanya biashara, basi mm na Kariuki tunaendelea kuwasiliana huku akiniuliza maswali mengi kuhusu tz .....
Aliniuliza sana kuhusu biashara na alionekana ana uzoefu mkubwa na mimi nikaona sio mtu kuacha kuwasiliana nae, basi jamaa akaniambia naweza kufanya nae biashara ya kumuuzia used bottles kwa ajili ya Recyling kwa sababu NRB hakuna na atakuwa ananunua kwa pesa nzuri ....
Alitaka colourless bottles za konyagi, savanah n.k baada ya kuelewana kuhusu bei niliona ni bonge la dili kwani nikiweza kupeleka gari moja ya tani 10 basi ningepata faida ya karibia 15mil na jamaa alitaka kuanzia tani 30 basi mchaga wa watu nikaona maisha si ndio haya sasa
Nikamwita mshikaji wangu nikamwelezea issue yenyewe akaniunga mkono, huku Kariuki akiwa anatuharikisha ya tupeleke mzgo mapema na tukivuka border tuu anatupa pesa yetu, basi tukaanza msako wa chupa kwenye vijiwe vyote vya morogoro, kama Mo twn, down town, nyumban park, uhuru n.k
Tukaanza kukusanya chupa za kutosha huku tukiwa na malengo makubwa sana na biashara ile, kwa hiyo tukapanga kufungua kampuni kabisa na kujikita kwenye hiyo issue, chupa tuliweza kuzipata kwa bei poa sana kitu ambacho kilitupa moyo zaidi wa kupiga kazi, huku jamaa akiendelea.....
akiendelea kutuharakisha, basi nikampigia kariuki simu na kumwambia mzgo uko tayari lakn tulitaka kuja Nairobi kuangalia mazingira ya biashara, huku nyuma tulikuwa tunatafuta kumzunguka mchizi kwa kuuliza sehem ambazo wananunua chupa Nairobi ili tukiipata tusimuuzie yeye..😃😃
kwa sababu tukiona kama jamaa ananunua kwa bei kubwa sana huenda yeye anapata sana faida, kwa hiyo tukapata number za mnunuzi mmoja na number za kiwanda cha chupa cha Central glass na tukapanga nao appointment tukifika nairobi huku tukiwa na mpango wa kuonana na Kariuki na...
na kusaini nae dili ya pesa ndefu basi tulikuwa na kigari chetu Corrolla , tukaanza safari jioni na tulifika arusha saa kumi asubh, tukatafuta parking na kusinzia kidogo kwenye gari tungoje asubh ili tudandie lift kwa washikaji wa Dolphin pale Mianzini tuanze kuitafuta NRB
Ilipofika saa 12 tuliiacha gar kwa jamaa angu na kuanza safari ya Nairobi, kipindi hicho Uhuru alisema ruksa kuingia Kenya ukiwa na National ID tuu na passport tulikuwa hatuna, basi tulipofika boda tukaenda Migration na vitambulisho vyetu, wakatuchomolea ikabidi sasa turudi mpaka
Longido kwenda kukata pass za muda, na mpaka saa saba tulikuwa tayari na pass zetu, tukabadili pesa na kuingia Kenya, kama saa 12 tunaingia NRB hatufahamiani na yoyote, tulipofika tukachukua taxi na kumwambia atupeleke hotel ya bei nafuu, basi nilishangaa yule taxi driver alipo..
Alipoanza kutukaribisha na alitupatia b'ness card yake na alitupeleka Green park hotel Thika road huku tukishangaa fly over za NRB na taa nyingi pamoja na Jam kubwa sana, tulipofika hoteln cha kwanza tuliulizia Wi-Fi 😃 kwani tulikuwa tumekaa muda mrefu bila kuwasiliana
Asubh ilipofika tulikuwa na appointment kule Central glass kwa hiyo tulipanda taxi tena mpaka pale kiwandani ambapo kwa karibu ndipo ulipo uwanja wa Nyayo, tulifika na kuongea na marketing officer na akatuambia kweli ananunua chupa lkn sio kwa bei kubwa na bei aliyotupa ilikuwa..
ndogo sana, basi ilipofika mchana ilikuwa ni muda wa kuonana na Kariuki lkn alikuwa hapokei simu kabisaa basi tukampigia supplier mwingine nae alikuwa karibu na alifika mara moja, tulikaa nae na alitueleza vzr kuhusu biashara ya Glass na pombe kwa kenya kwa upana sana bcoz yeye..
Alirithi biashara hiyo kutoka kwa baba yake hapo ndipo nilijua kuhusu tycoon wa biashara za vileo duniani akina ABinBev, namna EA breweries ilivyokufa na tz kupata hasara, na mambo mengine mengi lkn alitueleza kuwa biashara ya glass ina faida ndogo sana na yeye ndie supplier
Basi akatueleza kuwa NRB kuna matapeli wengi na huyu Kariuki ni tapeli alitaka tulete mzgo then asitulipe pesa na atukimbie, basi tulijaribu kuwasiliana nae tena lkn hakupokea simu, basi ikabidi tuanze kutafuta kazi ya kufanya kesho yake na turudi tz kwani biashara hakuna tena
Basi nikakumbuka kuna mshikaji mmoja mwitaliano nilikuwa naunua bidhaa kwake so ni vzr kwenye kumuona, tulifunga safari kesho yake hadi Thika na tulipofika alitupokea vzr na alitutembeza kiwandani kwake ambapo anatengeneza dripline na net za green house
Tulizunguka sana na kujifunza kutoka kwake kwani alikuwa kijana kama sisi na alipewa kazi ya kusimamia kiwanda hicho cha baba yake alichokianzisha miaka ya 1970 baada ya hapo tuliagana na jamaa na kusepa huku tukiwa na machungu ya kupoteza biashara ambayo tulikuwa na malengo nayo
Tulikaa Pale Thika mjini na mshikaji wangu huku tukitafakari tunakwenda kufanya nini na mzgo wa chupa tulioukusanya ambao ulifikia tani 12 hivi, basi tukaanza safari ya kurudi bongo huku tukitafuta plan B ya namna ya kuuza ule mzgo kwani tulikuwa tumeshatumia kama 1mil hivi
Tuliingia tz usiku kama saa tatu hivi pale Namanga na kuanza safari ya kuja Chuga ambapo tulifika kama saa sita hivi, tulilala na asubuhi tulianza safari ya kuja morogoro huku tukiwa na huzuni sana kwani tulikuwa tumeweka malengo makubwa sana kwenye ile business
Leo nitaishia hapa lakn hatukukata tamaa tulianza kutafuta soka na hapa ndani la chupa, thread ijayo nitaeleza zaidi kuhusu biashara ya used bottles.
MWISHO
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Eng Octavian Lasway

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!