My Authors
Read all threads
Mwaka 1989 mwanaharakati na muhitimu wa Sheria kutoka Harvard Bryan Stevenson anasafiri kwenda Alabama akiwa na matumaini ya kuwasaidia watu wenye maisha ya chini ambao hawana kipato Cha kutosha kuweza kuafford huduma Bora za kisheria, uko anakutana na mwanadada Eva Ansley kwa
kwa pamoja wanatengeneza kitu kijulikanacho Kama Egual Justice Initiative. Baadae anasafiri na kwenda kukutana na mfungwa Walter "Johnny D" McMillian mfungwa Anae subiria hukumu ya kifo akiwa kahukumiwa kwa mauaji ya Ronda Morrison yaliyotokea mwaka 1986.

Bryan anapitia ushaidi
wa kesi hiyo na kugundua ushaidi mzima ulikuwa umeegemea kwenye shuhuda ya mtu mmoja Ralph Myers ambaye nae alifungwa kwa makosa ya uhalifu na alikubali kutoa ushaidi zidi ya Walter kwa makubaliano ya kupunguziwa kifungo chake. Hatua ya kwanza kumsaidia Walter, Bryan anaamua
kuomba msaada wa wakili wa serikali Tommy Chapman, lakini bila kuangalia notes za Bryan, Tommy anamtolea nje Bryan juu ya kesi hiyo.

Bryan anaamua kumuomba rafiki wa familia ya Walter, Darnell Houston kutoa ushaidi ambapo siku ya tukio Darnell na Myrers walikuwa pamoja na Wala
hawakuwepo eneo la tukio na hivyo kuleta utata kwenye ushaidi aliotoa Myrers mwanzo na hivyo kufanya kesi hiyo kutingishika kiushaidi. Baada ya Bryan kuwasilisha ushaidi wa Darnell's polisi walimgeuzia kibao na kumkamata kwa kosa la kudanganya chini ya kiapo (Perjury). Wakati
Bryan akipambana na kufanikiwa kuyafutilia mbali madai hayo, uku Darnell anapata vitisho vya usalama wake na kutakiwa kukataa kutoa ushaidi mahakamani, hivyo Bryan anaamua kumgeukia Myers mwenyewe.

Ambaye baadae anakubali kwamba ni kweli ushuuda wake ulikuwa ni wakupangwa baada
ya polisi kumtishia kumfunga na kuhakikisha anahukumiwa kuuawa kwa kiti Cha umeme. Bryan anafanikiwa kukataa rufaa zidi ya kesi ya Walter katika mahakama ndogo ya mji huo na kufanikiwa kumshawishi Myers kutoa ushuuda mpya. Lakini hakimu wa mahakama hiyo anakataa shauli la kesi
hiyo kusikilizwa upya.
Mwisho anaamua kupelekea rufaa yake katika Mahakama Kuu ya Alabama. Mahakama Kuu wanatengua hukumu ya mahakama ya mwanzo na kesi hiyo kusikilizwa upya. Bryan dokezo lake likiwa ni kesi hiyo kufutiliwa mbali kabisa, Anamfuata Tena wakili wa serikali
Chapman nyumbani kwake ambae kwa Mara nyingine Tena Anamtolea nje Bryan. Siku ya kusikilizwa kesi hiyo Bryan Ana wasilisha shauli lake na Chapman anakubali kujiunga nae na kufanya kazi pamoja, mwisho kesi hiyo inafutiliwa mbali na Walter anapata nafasi nyingine ya kujumuhika na
na familia yake akiwa mtu huru.

Bryan na Eva wameendelea kuyawekeza maisha yao katika kuipigani haki za watu wa chini. Walter aliendelea kuwa marafiki na Bryan mpaka mauti yalipomfika mwaka 2013. Upelelezi ulifanyika upya juu ya maauaji ya Morrison na kuonyesha Walter hakuwa
muhusika na inaaminika inawezekana ni mzungu ndiye aliye fanya tukio hilo. Mpaka Sasa kesi hiyo haijapatiwa uvumbuzi.

JUST MERCY ni movie iliyotoka December 25, 2019 ikikuletea uondo wa story hii ikiwa imechezwa na wakali Michael B Jordan (Bryan Stevenson) na Jamie Foxx
(Walter "Johnny D" McMillian) na Brie Larson ( Eva Ansley) na ni movie iliyo jizolea sifa kubwa Sana ikiwa imeisha kuwa nomited Mara 5 na kufanikiwa kujizolea tuzo 3.

Katika siku ya kwanza ya kutolewa movie hii katika theater kazaa iliingia kitita Cha dola $81,072 katika Jumba
nne tu za Filamu. Ikiwa imepewa rate ya 83% na mtandao wa Rotten Tomato na rate ya 7.3/10 kutoka ImDb.
Baadhi ya waigizaji wake hasa wale wakubwa wameisha tokea kwenye movie kadhaa za Marvel ikiwemo Michael B Jordan alietokea kwenye Black Panther kama Killmonger na Fantastic Four
Movie hii ipo cipherdot series and movies karibuni sana
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Cipherdot Series And Movies

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!