My Authors
Read all threads
SHE DESERVED LOVE BUT I DECIDED TO RESPECT HER,I WAS WRONG 💔

So guys,heshima na upendo ni vitu viwili ambavyo vinashabihiana.Kuna wakati utadhani unapendwa kumbe una heshimiwa na kuna wakati utaheshimiwa we ukadhani unapedwa
Nilishindwa kujua tofauti yake

T H R E A D 👇
This might be my first love story tangia nazaliwa, nilikua na umri mdogo sana lakini ilitosha kunifunza jinsi mapenzi yanavotawala kila rika. Ni zamani sana miaka ile shule ya msingi, shule zetu izi za kawaida so wale wa kupanda school bus inabidi mtuvumilie kidogo kuna vitu
nawezakua nataja humu mkahisi ni ushirikina 😂 but we enjoyed that life by the way.
Back in the days primary school nilikua na rafiki yangu wa kike ambae pia alikua ni jirani yangu pale nyumbani.Wote tulikua tunaishi Tabora na elimu yetu ya msingi tulisomea pale. Aliitwa Alice
She was full package of a friend, kila mahali nilikua nae kucheza pamoja, nikiagizwa tutaenda wote,mtaani mpaka shuleni.Alikua msafi sana kuanzia mavazi mpaka mwili. Upole wake ulitosha kabisa kumuondoa kwenye makosa hata yalofanywa na darasa zima.Alivutia sana japo kitaaluma
hakua anaweza saana. Mi usafi haikua kipaumbele changu nkioga nikivaa bukta yangu ya shati langu la mtumba jeupe na soksi za pundamilia nlikua naona nimemaliza yote zile shati za tomato kwangu ilikua anasa kubwa😂
But nlichojivunia mimi ni kuwa mzuri kwenye hisabati na sayansi
Kwaio wewe ukinizidi kwenye usafi mi kuna mahali utanihitaji tuu. Nliishi na Alice sana kuna kipindi akawa mpaka anakuja nyumbani weekend wanafua nguo na mama pamoja wakati mi niko room nafanya maswali kwenye vile vitabu vya JIPIME 😂
Ilifika hatua wakawa wanaitana Mkwe na mama
Mi sikua najali yote hayo nliona ni utani tuu. Kwenda shule bila hela ya pochopocho kwangu ilikua kawaida sana na sikuona soo, Alice alifanya kumudu kuninunulia bagia,kashata na kunikatia Barafu walau lile jua la saa nane lisiniumize koo 😁
Yalikua maisha flani mazuri na bila
Shaka siku za kufunga shule kwenye matokeo usipomtaja Noel ndani ya Top three basi ujue labda hakufanya mtihani,kwaio nikipewa zile daftari kama mshindi ilibidi nimgawane Alice maana ye namba zake zilikua za mbali kidogo yote hayo nilifanya kama kujali heshima anayonipa ❤
Sasa tulivofika darasa la tano kwenye darasa letu akahamia mtoto wa kike ambae alikuja kuwa gumzo la shule nzima.Kwanza yupo kama Muhindi aliyekosea masharti akajikuta ardhi ya Bongo kwa ule unywele na rangi ya mtume,urefu wa haja na macho mazuri mwembamba lakini akipita utageuka
Akajitambulisha darasani kwamba anaitwa Winnie kahamia pale baada ya baba yake kutoka Mbeya akahamishiwa kikazi pale manispaa.
Wazee sijui nlikuaje lakini nilihisi kuvutiwa na yule dada kama walivofanya wengine mule darasani.Nkajiapiza lazima nimpate na ikibidi "tufanye matusi"🤣
Sema nkawaza ivi ntamshinda Jackson alivo msafi na nadhifu, vipi kuhusu Musa bingwa wa kabumbu, au yule Emmanuel mtoto wa pastor anayekuja na hela kila siku shule.

Nikasema potelea pwete sina hela sina kipaji,sio msafi lakini juhudi zangu hazitoniangusha mimi eboh😎
Mchana wake
Tukiwa njiani kurudi home mimi na Alice nkaanza kumuulizia habari za Winnie.Nkaona kama hajafurahia na ujio wa Winnie maana kama kapata mshindani.
Kiufupi mule darasani ilikua ukiwataja mabinti wazuri Alice huezi acha kumtaja. So sikutaka kumkera zaidi na zile story tukaendelea
Na safari yetu huku akinifundisha kusali Rosari binti huyu wa kikatoliki.
Nilifika home baada ya kula ugali mlenda na dagaa kwa mama Noel ikabidi nijifungie ndani peke angu namuwaza Winnie.Nkaamua nichane karatasi kwenye counter book ya brother ambae kwa wakati huo nikiwa std 5
Ye alikua form one.Nlichana ili niandike barua ya mapenzi nifikishe yangu ya rohoni kwa Winnie ( ila ulikuaga ufala nyiee🤣)
Nikaandika vizuri na michoro ya moyo yenye mshale katikati nikafata bahasha ya 50/- kwa baba Ayubu nikaeka mate nikaifungia barua "Kiss before Open"🙌🏼
Sasa nkaona mbona kama mapema.Nkasubiri kama siku tatu ivi, khee yule Winnie akaanza mazoea na Emmanuel ambae ye kwao hela zipo nkaona ntachelewa mwisho niibiwe 😁
Nkaichukua ile barua ambayo ilikua masaa yote kwenye kibegi changu alichonirithisha bro kwa masimango sana yule boya
Nkampa barua dogo Aron baada ya kumsaidia maswali ya kutafuta mzingo wa mche mstatiri uliofungwa pande zote.Nkamwambia akimuona Winnie ampatie maana dogo alikua std 4 sisi tupo 5. Mchana tuko na Alice nikamvuta dogo pembeni anipe feedback lakini Alice asisikie coz i respected her
dogo akasema mambo fresh.Sasa bhana kesho yake ilikua jumatano ya ukaguzi wa usafi na kutolewa mbele kisa uchafu mi nilishazoea. Kama kawaida Mwalimu Msigwa hata kabla ya kunifikia kwenye mstari ilibidi nijitoe mbele maana asingeamini kama leo nimekua msafi wakati siku zote sio
Tukiwa pale mbele watu wachache tuu maana wachafu wenzetu siku hiyo walitusaliti kabisa mpaka bwana Festo ambae hadi mimi nlimzidi usafi akawa kabaki eti ni msafi 😫
Akaja mwalimu mkuu anaongea kwa hasira sana kwamba vijana badala ya kusoma tunawaza mapenzi tuu.
Nkaona tayariii
Akaitoa ile barua yangu ya mapenzi akaniita mbele.Sasa yeye akawa ameangalia walipo darasa la tano halafu mi nikatokea walipo group la watu wachafu..Akasema " yani pamoja na uchafu wako unawaza mapenzi tena kwa mtoto wa mkurugenzi" 😳
Wazee hapo ndo nkajua kumbe Winnie sio poa
Nlizibuliwa fimbo nyingi mno na aibu za vicheko kejeli na kubezwa na walimu na wanafunzi pale. Alice aliona aibu mara mbili yangu akainamisha kichwa.
Baada ya lile tukio sikwenda darasani siku tatu nkabaki home najisomea tuu maana umbea ulifika kwa wazee uzuri walipotezea maana
Nliaminiwa sana pale nyumbani halafu brother alikua ananipa moyo sana anasema
" we mdogo wangu cheza na fursa tuu hata huyo Alice unayemuona kama rafiki tuu siku utajuta, soko linapungua hili shauri yako"
Kipindi chote iko Alice alikua anapita home kunijulia hali.Sasa nayeye
Alivoona kumbe nataka kuwa na Winnie ndipo akaanza kuonesha ishara za kunipenda ile kiukweli japo hasemi kitu mi nlimsoma ila nkachukulia poa tuu.
Baada ya aibu kuisha nikarudi darasani back bencher na wanangu nkiwa na muangalia Winnie bado najiapiza mpaka nikupate wew 💪
Akaja ticha wa hesabu akaweka swali la umbo gani sijui lile.Watu wote kimya kama dakika tano,nikaona ngoja sasa nimuoshee Winnie sialikua hanijui huyu.
Nkasogea ubaoni kutafuta eneo lililotiwa kivuri.Wazee nilisolve kama ten minutes nikapata 34.6 cm2. Mpigieni makofi watu wewee🤣
Winnie akaona kumbe mi sio fala baada ya muda akaanza kuleta ukaribu nkasema haya sindo mambo 😁
But ilikua ni mwiba wa koo kwa Alice maana kuna siku jioni nimeagizwa mafuta ya taa na mama nikakutana nae njiani akaniuliza kuhsu Winnie mi nkakataa. Akaniuliza kama nampeda yeye
Nkakosa jibu akanambia alishaongea na mama yangu kuwa mimi siku moja ntamuoa 🙄
Ila utoto 🙌🏼
Sikujali nkawa na Winnie mpaka tunafika la saba huku Alice analalamika tuu na kuntumia barua za kunisihi nimpende akasema bila hivo hatokuja kuolewa kama sio mimi 💔
Ikafika siku ya graduation bhana baada ya yote sikunakuaga na disco vumbi nikamfata Winnie wangu tucheze magoma ya kizamani yale.
Katikati ya kucheza nikamuona Alice kwa mbali ananiangaza amebeba box lenye urembo wa gift paper like kuna zawadi anataka kunipa.Tukagonganisha macho
Nikaona anatoa chozi maana nlikua nimemkumbatia Winnie
Akatoka nje mbio mi hata sikujali 💔. Kesho nikaenda kwao kumtembelea wala hakutoka nje.Zikapita siku tatu akamtuma barua mdogo wake.Ilikua barua ya malalamiko mno. Matokeo yakatoka kwa bahati nzuri mimi peke angu tuu
Ndio nilifaulia shule ya nje ya mkoa.Mbaya zaidi mzee akahamishwa kazi akaja mkoa huohuo ambao shule yangu ipo so possibility ya kuonana na Alice wala Winnie ikawa ngumu sana.
Nilipomaliza kidato cha nne nikaenda Tabora bhana.Nkafikia kwa rafiki yangu akanipa story kwamba yule
Yule manzi Winnie alipata mimba ya mwanajeshi akaacha shule.😫
Nikaenda kwa mama Alice akasema kuna barua yangu hapa aliiacha Alice.Kiufupi Alice aliandika maneno ya kuumiza sana na kipande cha barua kilikua ni "..nilikupenda haukujali wala kuthamini, nilijiapiza uwe mwanaume
wangu hapo baadae,sasa umenikataa nimeamua kuto kuolewa naenda tuu kumtumikia Mungu nakutakia maisha mema" 💔
Aisee nilishiwa nguvu kwenye magoti.Kumbe Alice ilibidi tuu aende kwenye Shirika moja linaitwa CNDK lipo Rombo Kilimanjaro akasomee usista.Nliumia sana
Nilipomaliza kidato cha sita nkaenda Rombo lakini nkaambiwa alikuwepo pale ila kahamishwa kituo kingine kipo Mwanza 💔..Bado sijakata tamaa ntamtafuta walau nimuombe radhi
#End
#MyMindSpeak
#NohTalk ☕️
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Noe_Wenc 💊

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!