My Authors
Read all threads
MY THREE MONTHS EXPERIENCE OF DATING A SLAY QUEEN 💔 🙌🏼

So,siku zote uzuri wa mapenzi ni pale unapopendwa bila sababu, maana akikupenda kwa sababu fulani means sababu hiyo ikipotea hatokupenda tena,
Mpaka tunaachana sikuwahi kujua ni mtu wa aina gani.

T H R E A D 👇🏼
Ni vizuri mtu kuwa real ili upendwe au mtu akupende vile ulivo pasipo kuvaa uhusika wa mtu mwingine. Your are beautiful /handsome the way you're.
Nlikua naskiaga tuu slay Queens mpaka yalonikuta.Miezi mitatu tuu ilitosha kuona kama mwaka mzima umepita sasa kwa zile mikiki 🙌🏼
Ilikua Jumamosi narudi home kutoka Library nimepanda bajaji moja na mtoto mzuri.Kwa wingi wa mambo kichwani sikumzingatia kabisa hata alivovaa maana nlikuja kugundua alikua amevaa pensi ya jinsi na blauzi ya mabega wazi, wigi na kibegi kidogo wao wanaita "NaiNai" kipindi nashuka
Tulishuka kituo kimoja na yule dada nkatoa 1000/-nilipe nauli maana nauli kwa kawaida ni jero tuu.Nlivorudishiwa chenji yule dada alikua bado kama anatafuta hela kwenye begi lake mi nkaona hayanihusu niondoke.
Akaniita akaniomba kama sitojali nimlipie nauli 500/- kwamba..
Pesa yake alipoiweka haioni. Nkaona jero si kitu kwanza ningeishia kununua Mo Energy vile nlikua nimechoka 😂
Akanishukuru pale tukawa tunaongozana tuu mi sina story kwanza coursework zenyewe hazija kaa poa huko nianze kuongeza mzigo mwingine tena 😎
Tulivosogea kidogo mbele..
Binti yule akavunja ukimya kuniuliza ninakoelekea nkamjibu na yeye akasema anafata vitu kadhaa kwa shoga yake yupo mtaa ninao ishi ila yeye anakaa hostel.
Nkaona huu sio uhalisia wangu kupiga kimya mbele ya mtoto wa kike nkaanza kuchangamka kidogo nkamuuliza jina akasema
Ye anaitwa Nasra ila shoga zake wamezoea kumuita Nas. Nkamwambia mi naitwa Noel. Akang'aka eti "ooh nice name " nkatabasamu 😄nkamuuliza

Me; unatumia social network gani?

Her; sipendi twitter ni ya wazee, Facebook ni washamba,whats up natumia kidogo ila hasa natumia Insta
Akaitaja kwa kifupi ivoivo na akantajia handle yake ya insta woiii jina lina Queen nani sijui humo humo miss nani sijui🤣 mwisho wa thread ntalitaja watu wakaone

Tukabadilishana namba pale tulivofika junction kila mtu akaenda kivyake.
Imefika night mood ya kufanya shule ikaisha
Nkaona nimpumzikie mtoto Nasra maana kwa wakati huo nlikua single sasa nkaona nikijiweka hapa kwa muda sio mbaya.Bora hata nisingethubutu 😖
Nkamtumia meseji akareply chap ati nayeye alikua nawazo la kuntafuta wakati huo. Nkatabasamu nkiwaza uyu analeta drama uyu 😁
Tukapiga story mbili tatu anauliza nasoma course gani nkamtajia nkamuuliza akasema ya kwake atantajia muda mwingine🙄

Akaniuliza exactly nakoishi nkamtajia mimi nkamuuliza hostel gani anaishi akanikwepa akaleta mada za mapenzi.Nkajua huyu mtu chenga nyingi asijue mi ndo kocha😁
Katika kupiga story kadhaa ye akaadha kama kujirahisha kwangu design kama anatengeneza mazingira ni shoot my shot 😀..Nikajitupia tuu baada ya kujua lengo lake nkamwambia
" Hey Nasra tumejuana leo lakini najihisi vingine ambavyo nahitaji tuu kukwambia kwa sasa kwa sababu lazma..
ntasema tuu hata siku za mbele, kiufupi nimetokea kuvutiwa na wewe and i hope we'll make a perfect combo,will you be my girlfriend? " hapa sasa ndo nkagundua ndio nlipoharibu maana eti kirahisi binti akakubali na yaliyofatia ndani ya miezi mitatu mpaka nkahisi kuna director nyuma
Yangu halafu nacheza movie bila kujijua😫🙌🏼
Bhana penzi lile la ghafla lilianza kwa bashasha zote ikafika time tunachat what's up na normal text mada mbili tofauti na zote zipo hot🤣
Hakuchukua muda sana bhana akaanza vioja.Kuna siku nipo nae Cafeteria tunakula nkaomba simu
yake nimpigie mtu.Sasa nkashangaa simu ina cover ya iPhone nkajua hii ni iPhone 8 kwa ukubwa ule lakini alivonipa naona zipo sehemu tatu za kubonyeza na iphone ina power button moja 😳 kumbe ni Tecno K7 🙌🏼
Nikaona anakosa kujiamini akasema kaweka ivo kwa muda coz iPhone ipo room
Nkapuuza tuu sikujali sana. Mind you mpaka muda huo detail nazojua kuhusu Nasra ni jina lake na namba za simu tuu vingine alinikwepa anadai atanambia next time😁
Sasa katika story nkamuuliza kama anapokea mkopo na bumu akasema eti yeye hasumbuki na hela za masimango kama izo
kwamba baba yake ni mmiliki wa kampuni moja pale Kigamboni na anamudu kila kitu.Nkasema Chiiii hizi hela zinazoweka watu mjini ye anaita za masimango 😂🤣
Siku zikakatika bado niko nae huyu dada ambae hakuchoka kunistaajabisha nikimkuta na shoga zake tunaongea pembeni mim na yeye
Yani hataki kabisa nizoeane na wenzie alihisi ntachukua detail zake labda😄
Nadhani sikua serious na yale mahusiano maana nlikua nayaacha yajipeleke nione mwisho wake utaishaje coz it was my new experience.
Siku moja nikapita kwa wahasibu pale administration kusaini bumu
Nikakutana nae nkamuuliza anafanya nini eti akasema amekuja kumsainia bumu rafiki yake. Mi hata sikuhoji sana japo kimoyomoyo nlikua nacheka kinoma maana bumu unasaini kwa fingerprint ambazo kila mtu duniani anayo yake peke ake sasa iyo kumsainia mwenzie vipi🤣🤣
Siku moja nkamualika ghetto maana tushakua wapenzi miezi miwili tayari so sio mbaya sana kuliko ile mmejuana wiki moja tuu "njoo ghetto" bro ukifanya ivo umefeli 😁
Akaja bhana yule binti mpaka ndani na macho yake ya kudadisi nlikua naskiliza nyimbo za Post Malone aksema eti
Hapendi nyimbo za ivo nkamuekea Shape of You ya Ed sheeran akaanza eti " oooh jamani huu wimbo unaskitisha sana " nkahisi simuelewi huyu manzi maana lyrics nzima ya wimbo naijua na sioni mahali pakusikitisha 😂😂
Nkajisemea "huyu dada ni fala kweli mbona ni wimbo mzuri tuu huu"
So tukala msosi pale ghetto tukapiga story mpaka zikaisha,kilichofata sijui but she was good on bed 😁
Jioni nkamuita boda akamrudisha hostel kwao.
Sasa bhana siku moja tukakutana campus akasema yupo na njaa nikamwambia achukue funguo akapike ghetto kuna kila kitu😎
Buana buana si akaenda ghetto nkamuelekeza atakapoacha funguo baada ya vyote.
Sasa ile narudi picha linaanza nakuta room zote zinawaka taa yangu tuu ndo haiwaki nkampigia simu Nasra
"hello mchumba mambo,ilipiga shoti humu ndani " akasema eti anahisi umeme uliisha maana hata
nywele zake hakuziset vizuri na ile drier 😳
Daah yani kumbe alifanya ghetto langu salon kabisa na kaja na lile drier kamaliza Unit 56 za umeme zilizobakia 😫
Nkapotezea nkafungua friji stock imepukutika kishenzi yani mahitaji ya wiki nlofanya imebaki stock ya kula kama siku tat
Nkaona nkimuuliza saivi ataona mwanaume nina gubu sana..Ilivofika jioni baada ya kuchat sana nkamchomekea izo story like " mtoto mzuri ulipika kweli wewe mbona hamna kilichopungua humu ndani ".
Akasema " hatukula sana japo nilienda na Fetty,Shadia na Sheyla" daah..
Wazee kumbe siku hiyo nilifuturisha 😭
Nkakausha bhana siku ziende.Sasa nkaona ijumaa moja nimtoe out kidogo mrembo maana tokea tunaanza sijawahi kumtoa nkamuuliza" Baby unaendaga wapi ukitoka out " eti akasema anaendaga KFC 😒 sasa nikicheki Morogoro hamna hata KFC daah wadada🙌🏼
Nkaona mambo yasiwe mengi nkamchukua mpaka uhuru park uzuri nlishaanza kumzoea kwaio kumchana makavu yasiyoumiza ilikua kawaida.
Tulivofika nkamwambia " mchumba hapa nina bajeti ya 40k ukiagiza zaidi ya hapa ni juu yako" akajichekesha tukaenda akaagiza Heineken kadhaa mi Castle
Ilikua siku poa uzuri wake alikua sio wakuboa maana maongezi yake ni story za instagram macerebrity tuu mi izo sio mambo yangu naona kama ananichanganya tuu😂
Bhana ikawa siku nimelala usingizi ukakata nkaona niwashe data tuu nione what's going on
Meseji kadhaa za whats up zikaingia na moja ilikua ya jamaa yangu Owen ye ni mtu wa Club sana.Alikua amentumia video clip flani inaonesha mtoto wa kike kalewa chakali amelala kwenye kochi ndani kama ya Club
Kuangalia vizuri ni Nasra asee sikuamini😳😫
Nkampigia simu that night
Simu inaita bila kupokelewa.Asubuhi akanicheki nikamtumia ile Clip eti akakataa kata kata sio yeye nikapanga tuonane aiseeee ileile nywele style alosuka ndo yeye kwenye video clip halafu nkambana akakubari eti alienda na shoga zake wakamuacha.
Sasa tulikua na jamaa yangu Owen
Huyu jamaa yuko real sana akaanza kumchana manzi palepale kwamba anamuona sana Club.
By the way vitu kama ivo sio vitu navyopenda na kumbe kuna mengi tuu binti alikua anafanya kimya bila mi kujua na hapo ikabidi niachane na Nasra.
Nlipata story baada ya kuwa na madeni mengi ya
Ya watu ilibdi aache chuo yule dada.Yupo kwao Dar.
#End
#MyMindSpeak
#NohTalk ☕️
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Noe_Wenc 💊

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!