My Authors
Read all threads
THEY BOTH FELL IN LOVE WITH A VET ❤💊
So
kila mtu hujikuta katika mahusiano kwa namna ya tofauti.Usishangae sana ukiona mtu anatoka jela na mpenzi wa maisha yake. Au hata muharifu akatoka rumande na mpenzi wa maisha yake ambae mwanzo alikua askari wa hiko kituo

T H R E A D 👇
Ni katika pirika za kila siku ambapo mioyo miwili iliyoshibana huungana na kutengeneza kitu kimoja cha thamani sana (upendo).
Pirika za kila siku huleta watu pamoja na ule muingiliano wa baina ya watu ndio huongeza ukaribu na mwisho katika hayo mazingira watapatikana wapenzi ❤
Pirika na harakati za kila siku ziliniletea mtu wangu wa muhimu.

Story yangu inaanza wakati ule,nimetoka chuo nimechoka sana halafu jioni maana kile chuo wale wazee kukutoa saa moja jioni hawaoni soo😔
So ile nafika home hata kabla sijaamua nakula nin au naanza na kipi
Akaja mpangaji mwenzangu anasema alikuja mzee Jongo anaulizia kama kuna mwanafunzi anaesomea habari za tiba ya wanyama,tulivomwambia yupo akasema kama ukifika basi ukamuone kwake 🙄
Wazee huyu mzee Jongo ni captain wajeshi tabasamu lake ni adimu kama jua kuzama asubuhi🙌🏼
Jamaa mkubwa kiumbo amejazia kinoma anajumba lake pale mtaani na inasadikika aliwahi kamata mwizi kabla hata ya kumpiga yule mwizi ilibidi tuu aanze kulia 😂

Wadau wanasema anamtoto wa kike mmoja mzuri lakini mi hata sikua na muda na mtoto wa mjeda so hata nlikua sijawahi muona
Nlivopokea taarifa nkaona isiwe kesi ngoja niende yawezakua ni dili.Nlivogonga wakafungua nikamkuta mzee Jongo mwenyewe kavalia pensi la jeshi na T-shirt
Nkasalimia kwa adabu nlizofundishwa jandoni maana yule mzee hakuonekana kama matani ni msamiati kwenye kamusi yake ya maisha😁
Nikajitambulisha akasema yes ni kweli aliniulizia akadai binti yake mbwa wake tangia asubuhi hayuko sawa.
Picha linaanza mbwa anaitwa Roxie ni pet dog sio hawa mbwa koko wanaokimbizwa hadi na paka🤣
Jimbwa lina manyoya kama sufi meupe na mabaka ya kaki akasema mwanae alimtoa
Poland 🇵🇱 alivotoka kusoma. Nkaoneshwa mbwa mwenyewe kalegea huyo
Ile nkiwa nimeinama chini nkaona miguu kama inakuja mahali tulipokua.Guys ile miguu ni kama mikono kwa ile ngozi nyororo na kile kibangiri sijui ni kikuku kile , kucha rangi asili kisigino kipo kama kona ya mkate🙌🏼
Nkasema kimoyo " Mungu naomba hiki kikombe kama ikibidi kiniepuke maana hapa ni kwa mwanajeshi"😫

Akainama pia yule mrembo akasema anaitwa Melania ndo mwenye huyo mbwa na anampenda sana kwaio mimi kama daktari ananitegemea

Nkasema usijali.Bhana nlisema tuu maana wakati huo hata
Mambo ya tiba tulikua hatujafundishwa ndo kwanza basic science😬
Nkamwambia dada samahani nimeacha mlango wa chumba bila kufunga so nkaufunge then narejea.Akasema poa
Nkafika ghetto nkatafuta namba za mwanangu Tomas ye yupo mwaka wa mbele kwaio atakua anajua shida nini
Sitaki kupoteza point tatu mbele ya mrembo yule mwenye lips nene usawa wa mfuniko wa ndoo ndogo ya lita kumi ❤
Ikaita bhana nkamuuliza "Oi hivi kuna shida hapa street kuna mbwa kalegea macho yamemtoka sana na hana nguvu shida nini hii"

Eti jamaa anasema kama vipi aje yeye 🤣
Nkasema fala nielekeze tuu hukohuko usije huku.Maana nlijua akija atanyakua point zote, so akanambia huyo kaishiwa maji tuu mpe Normal Saline tuu(hii ni drip ya chumvi na maji kwa wale msiojua 😎)
Nkarudi pale chapu nkawaagiza wafate vifaa vinavohusika nikatundika drip kwa Roxie
Tukiwa tunasubiri kuona kama drip itafanya kazi nkabaki napiga story na Melania anasema anapenda mbwa sana so atanihitaji sana.

Mi nina neno basi mkulungwa 😂kila kitu ni "Usijali" tukabadilishana contacts pale na bahati nzuri mbwa akapata nafuu nkataka kusepa mzee Jongo
Akanipa 20k nkawa navunga kama nataka sitaki zile wakati najua nisaa tatu usiku na ghetto friji linanizomea😁
Nkapokea asee nkapitia msosi nkaenda kula ghetto siku ikaisha. Kesho mchana nikiwa chuo nkamtext Melania akasema mbwa wake anaendelea poa na anacheza.
Nkasema ntapita
Kweli bhana ile nimepita yule mbwa kachangamka sana utafikir sio yule alietaka nionekane sijui kitu wakati legend 😄
Tukapiga story kadhaa na Melania akasema anaenda kumsaidia house girl kupika ili niondoke niko fresh so nibaki nacheza na yule mbwa Roxie.
Mbwa akaanza kunipenda
Anafurahi vile namchezea manyoya nkawa naenjoy pia mapicha kibao napiga nae.
Melania akaniita nkaenda kula then nkasepa ghetto.Daah nkaona kama ile roho yangu ya "if i die i die " inakuja inanambia nimjaribu mtoto wa mjeda weee nikaiambia mwana ukome nliyoyaona JKT yanatosha
Usiku bhana nkaona hapana ngoja nimtext by the way she was charming so i did enjoy that chatting. Ananipa mastory za Poland huko mi naona chenga Poland nye nye nye 😂
Nkasema ngoja nimuingizie mambo flani..Sasa ile natype akatuma "usiku mwema Doctor see u".
Duh poa bhana ikaisha
Kesho yake ikawa weekend nkaingia town nkachukua kilo moja ya nyama nkafika ghetto nkaichemsha nkapunguza kidogo kwenye chombo nimpelekee yule mbwa Roxie.
Woii mi sio fala kuna kitu nlikua nshakiwaza😂
Nkafika yule mbwa keshanizoea basi anafurahi nikampa msosi akaja Melania
Ananipongeza kwa moyo mzuri (deep down najua nimepunguza kama share yangu moja😭)

Bhana nkaanza kumchombeza pale pale kwao kwa mjeshi IF I DIE I DIE.
Nkasema
" Melania upo smart sana kuanzia nakufahamu mpaka leo hii nimegundua exposure na knowledge yako ni kubwa sana"
akasema nazingua 😁
Nkaendelea" sure,kuweza kuishi na mbwa asiyeweza kuongea na mkaelewana ni kipaji pia" akasema " hata wewe upo vizuri siunaona mbwa kakupenda"

Chiii nkaona Yes " So Melania ukiona mbwa kanipenda ivi jiulize nikipendana na mtu inakuaje " akauliza nachokaanisha
Nkasema " am proud of my true love, nikipenda napenda kweli na sichomoki kama nyama ya katikati ya mshikaki" akacheeka sana na meno yake meupe 😉❤

Siku ikapita bila kusema nachotaka bahati nzuri kesho yake asubuhi akantumia text anadai jioni anataka evening walk with me
Fresh jioni kavaa pensi yake na sandals na mbwa wake tukawa tunapita mtaani. Basi wana wa street wakawa wanatamani wawe mimi au yule mbwa😂
Nkanza kuleta zile mada asee demu kajawa maarifa sana nkaona nisipoteze muda mwisho ntakosa nkamchana. " Unajua Melania ifike mahali akili
..yangu ipumzike haiwezekani ikuwaze wewe kila saa, tunavotembea tunaendana mpaka vivuli vyetu ni mashahidi, sikia sauti ya upepo inavoimba nyimbo za mahaba kila tunakopita i think we can comnect ❤"
Weee akageuka kama haamini.Akasema Noe wewe ulikuja kama doctor saiv mapenzi
Na kazi vipi tena.Mi nkakaza " nafasi ya kazi naijua na yamapenzi naijua isitoshe mi nakupenda so najua jinsi ntajigawa kikazi,shule na wewe"
Hapo nlikua nimemnyanyua mbwa.Akanipokonya mbwa akarudi zake home nkabaki pale sielewi💔 😒
Nkaona nrudi tuu home nshaharibu kazi siku zenyewe za mitihani ya semester imekaribia halafu najiongezea stress 🚮
Sasa bhana nkawa kila night namsumbua kwa meseji naanza kama namuulizia habari za mbwa wake Roxie then nachomekea mambo yangu😁
Akantumia meseji " Noe ukiendelea hivi namwambia baba kila kitu unachofanya"
Duuh nkaona fresh ngoja ntulie.Sasa kila nkipita pale kwao namkuta mbwa yupo anacheza pale nje ananifata namshika manyoya anafurahi mno mpaka nkawa najiuliza mbwa kanipenda demu kakataa hii ni nyota gani
Ilivoisha UE nkawa sina ishu basi roho ya kukata tamaa mi sikua nayo nkawa nampandia hewani mara kwa mara
Nkamtumia Text ya mwisho " hey Melania i've been struggling for a long time but it won't work out, i wonder your dog fell in love with me why you?? Unacheza tuu na hisia
zangu muda mrefu sasa ni mwezi na nusu. So ukiwa ready utaniambia lakini sintokusumbua tena" 💔
Hakujibu text namimi nkapotezea maana kesho yake matokeo ya semester yametoka nimepata sapu moja hiyo ndo ikanifanya nisimuwaze tena😂😂
Siku mbili zikapita nkaona text yake " So Noe ndo umeamua kukaa kimya "
Nkajua tayarii ✌️..Nkamtext back akajibu we can connect and she felt the same way, and she loved me. I won love to both "she" and " her dog" japo kwa mbinde😁
#End
#MyMindSpeak
#NohTalk ☕️
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Noe_Wenc 💊

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!