My Authors
Read all threads
BLACK SEEDS
Siku zote tumekuwa tukiangazia filamu na tamthilia lakini leo nataka niangazie kitu tofauti kabisa kwa siku tatu mfululizo. Ili nyinyi wadau wetu tuwe pamoja siku zote na hili nitakalo liongelea leo ni muhimu sana ili tuendelee kuwa pamoja, nimesoma sana ili kuweza
kuandika uzi huu, mimi sio daktari nitakayoyaongea hapa ni kutokana na kusoma vitabu, vijaranda na vyanzo mbalimbali sio lazima ukubaliane nayo.
Leo tutaongelea mbegu za Habbat sauda wengine huziita black Cumin, au black seeds ambazo zinadaiwa kuongeza kinga mwili na kutibu
kutibu matatizo mbalimbali mwilini nimeliongelea hili katika kipindi hiki cha #StayHome #StaySafe ambapo kinga zetu za mwili zinatakiwa kuwa juu kupambana na COVID-19
Black seeds ni mmea ambao binadamu wamekuwa wanautumia kwa zaidi ya miaka 2000 iliyopita kutengenezea madawa
mbalimbali na pia uligundulika kupandwa kwenye kaburi (Tomb) la mfalme Tut.
Kihistoria Black seeds imekuwa ikitumika kwa kama matibabu ya maumivu ya kichwa (headache), meno, makamasi puani (nasal congestion) na minyoo ya tumboni (intestinal worms) pia ilitumika kutibu maambukizi
ya aina mbalimbali
Siku hizi Black seed hutumika kutibu njia ya chakula (degestive tract conditions) ikiwemo tumbo kujaa gesi, kuharisha (diarrhea) , kuhara damu (Dysentery), kuvimbiwa na shida ya kupata choo (Constipation and hemmorrhoids), Pia Black seeds kutibu mfumo
wa hewa (Respiratory Conditions) kwa magonjwa kama pumu (Asthma), mzingo (Allergies), Kikohozi (cough, Bronchitis, Emphysema) Mafua (flu, swine flu) na makamasi yanayoziba pua

Pia Black seeds ni nzuri sana kwa watu wenye matatizo ya shinikizo la damu (High blood pressure)
inashusa blood pressure, lakini sio nzuri kutumia kama wewe una shinikizo la damu la kushuka (Low blood pressure)
Inasemekana pia black seeds ina uwezo wa kushusha lehemu (Cholesterol levels) na kutibu baadhi ya saratani (cancer)
Na jambo muhimu hapa ni kuwa Black seeds
inapandisha haraka kinga za mwili (boosting Immune system) wanawake pia huweza kutumia black seeds kupanga uzazi na kuongeza uwingi wa maziwa kwa akina mama wanaonyonyesha
Watu wengine hupaka black seeds moja kwa sehemu yenye maumivu ya viungo (joint pain), maumivu ya kichwa na
matatizo ya ngozi, kwenye chakula black seeds hutumika kama kiungo
PUMU utafiti unasema kutumia black seeds kwa kuila inasaidia kukohoa, na ufanyaji kazi wa mapafu
Shinikizo la damu utafiti unasema kutumia black seeds kwa kuila mara mbili kwa siku kwa wiki 8 inaweza kusaidia
kushusha shinikizo la damu
Lehemu utafiti unasema kutumia mafuta black seeds kwa kuila mara mbili kwa siku kwa wiki 6 inaweza kupunguza lehemu isiyotakiwa mwilini (Bad low density lipoprotein) na kuiweka sawa sukari kwenye watu wenye matatizo ya kisukari pia inasaidia sana
kuondoa madhara wanayoyapata watu wanaoachana na matumizi ya madawa ya kuelevya (narcotic drug withdrawal) kutumia black seeds mara tatu kwa siku kwa siku 12 huweza kuondoa maudhi ya pembeni (side effects) ya (opiates withdrawal)
UVIMBE KWENYE KOO NA VIDONDA KOONI (Sore throat and Swollen tonsils) utafiti wa hivi karibuni umeshauri kutumia mchanganyiko wa chanca piedra (sijapata tafsiri ya Kiswahili aijuaye atauambie) na black seeds kwa kula kwa siku 7 inaweza kuondoa maumivu hayo
Matumizi ya black seeds
Kuna njia nyingi za kutumia black seeds mojawapo ambayo ni rahisi ni kuchanganya unga wa black seeds na Asali na kulamba itakusaidia sana kuongeza kinga za mwili ambazo tunazihitaji sana kwa muda huu.

Zinapatikana wapi black seeds: masokoni, maduka ya
dawa za kienyeji, maduka ya viuongo vya pilau

Angalizo:
1. Usitumike kwa akina mama wajawazito black seeds inazuia uterus contraction
2. Isitumike kwa watu wenye low blood pressure kwa maana itashusha zaidi blood pressure
3. Usitumie kama unatumia sedative vidonge vya usingizi kwa maana black seeds pia hondoa tatizo la kukosa usingizi na kukupa usingizi ukichanganya unaweza ukapata matatizo ya kulala sana kulikopitiliza
4. Usitumie kama unatumia vidonge vya kushusha pressure, pressure yako yaweza
pressure yako yaweza kushuka zaidi tumia kimoja kwa wakati mmoja
5. Black seeds huzuia damu kuganda mwilini ni kama vile mtu amezaye vidonge vya kuzuia damu kuganda kama Aspirin ukiwa unatumia Black seeds tafadhali usitumie vidonge vya aina yyt vinavyozuia damu kuganda maana
mchanganyiko unaweza ukauletea matatizo au usitumie black seeds hadi umalize dozi ya vidonge
6. Kama una kisukari tumia black seeds kwa uangalifu sana kwa maana inaweza kushusha sukari mwilini tumia ukiwa unapima sukari yako
7. Usitume au simama kutumia wiki mbili au tatu kabla ya kufanyiwa operesheni kwa maana black seeds inazuia damu kuganda, inapunguza sukari mwilini, na kuongeza kiwango cha usingizi kwa baadhi ya watu kwa ufupi black seeds inaweza ikaleta mwingiliano anesthesia wakati wa
operesheni na baada ya operesheni
8. Usitumie black seeds kama unatumia dawa za Kupunguza kinga za mwili (immunosuppressants) kama vile azathioprine(Imuran), basiliximab (simulect) na nyinginezo nyingi kwa sababu black seeds huongeza kinga za mwili kwa haraka sana
Dozi na uwingi wa black seeds kwenye matumizi na machanganyiko tafadhali muulize muuzaji atakupa kiwango na uwingi wa kutumia

NAPENDA KURUDIA MIMI SIO DAKTARI HAYA NILIYOANDIKA NI MAKUSANYO KUTOKA KWENYE MACHAPISHO MBALIMBALI
Vyanzo:
1. rxlist.com/body_vitamin_e…
Accessed on 18/05/2020 at 0949 hours
2. rxlist.com/black_seed/sup… accessed on 18/05/2020 at 0910 hours
3. en.m.wikipedia.org/wiki/Nigella_s… accessed on 17/05/2020 at 2030 hours
4. healthline.com/nutrition/kalo… accessed on 16/05/2020 at 1800 hours
5. medicalnewstoday.com/articles/322948 accessed on 17/05/2020 at 2010 hours
TAFADHALI RETWEET IWAFIKIE WENGI YAWEZA KUWASAIDIA WENGI HUWEZI JUA KUBONYEZA TU NENO RETWEET WAWEZA KUOKOA MAISHA YA WAPENDWA WENGI
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Cipherdot Series And Movies

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just two indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!