My Authors
Read all threads
HII YA LEO ITAKUUMIZA SANA
INAHUSISHA MATUKIO, FILAMU NA TAMTHILIA ZILIZOFUTWA AU KUHAIRISHWA AU KUSIMAMISHWA KWA MUDA USIOJULIKANA KUTOKA NA CORONAVIRUS (COVID-19)
Kutoka na mlipuko wa coronavirus mambo mengi yamesimama na yataendelea kusimama hakika yatupasa kuchukua tahadhari
pasipo kudharau kwa ajili ya Afya zetu
Leo nakuletea uzi wa matukio(events) yaliyofutwa au kuahirishwa filamu ambazo zilitakiwa kutoka(released) tarehe zimesogezwa mbele filamu na Tamthilia ambazo zipo kwenye uzalishaji (filming and shooting) KUSIMAMISHWA kwa muda au hadi
itakapotangazwa tena , Tamthilia zinazoendelea kusimamishwa, upigaji na uaandaji wa filamu na tamthilia kwenye movie sets na studios kusimamishwa kwa muda usiojulikana, pamoja na yote wapenzi wa filamu na tamthilia tutaathirika sana kipindi hiki.
March 20
1. Filamu za "Sing-long-Event" , "Apollo 13" , "Romeo and Juliet" , "Braveheart" , "Chasing Whiskey" , "Children of the sea" , "Climate Hustle 2" , "Digimon Adventures: Last Evolution Kizuna" , "Dino Dana the Movie" , "Gladiator" na nyinginezo nyingi tarehe zake za
kutoka zimefutwa au kuahirishwa

2. Tuzo zitolewazo na Havana Film festival New York zilizotakiwa kufanyika tarehe 28/04/2010 hadi 5/05/2020 zimehairishwa mpaka itakapotangazwa

3 Utengenezaji wa filamu ya "Baz Luhrmann's Elvis Presley Biographical Drama" imesimamishwa baada ya
Mhusika Tom Hanks na mke wake Rita Wilson kugundulika kuwa na coronavirus

March 19
1. Tuzo za 47 za Annual Daytime Emmy Awards zilizotakiwa kufanyika tarhe 12 june mwaka huu zimehairishwa mpaka itakapotangazwa
2. Cannes Film Festival sherehe hii ilitegemewa kufanyika May 12
mpaka May 23 imeahirishwa hadi itakapotangazwa
3 Filamu ya "Minions: The Rise of Gru" ilitakiwa kutoka July 3 mwaka huu imehairishwa hadi itakapotangazwa
4. Tuzo za Webby Awards 2020 zimefutwa zilitegemewa kufanyika May 11, 2020 katika jiji la New York tuzo zitatolewa kupitia
Sherehe ya mtandaoni

March 18
1. Sherehe za 46 za Seattle International Film Festival zilizotakiwa kufanyika tarehe 14 May mpaka June 7 zimefutwa
2. Sherehe za Sarasota Film festival zilipangwa kufanyika Aprili 1-5 zimehairishwa
3.Lionsgate wamesogeza tarehe za kutoka kwa
filamu zifuatazo kwa muda usiojulikana
- "Spiral: From the Book of Saw" ilitakiwa itoke May 15, 2020
- "Run" ilitakiwa kutoka May 8, 2020
- "Antebellum" ilitakiwa kutoka Aprili 24, 2020
4. Sherehe za mwaka 2020 za Edinburgh Film Festival ambazo zimefanyika kwa miaka 77 hazijawahi
kuhairishwa mwaka huu zimehairishwa tarehe itatolewa baadae

March 17
1. Maukumbi yote ya kuonyeshea sinema ya Cinemark popote yalipo yamefungwa kwa muda usiojulikana
2. Sherehe za mwaka 2020 za Women+Film Festival zilitakiwa kufanyika Aprili 14-19 zimehairishwa hadi baadae
3. Sherehe za mwaka 2020 za Sonoma International Film zilizopangwa kufanyika Machi 25-29 zimehairishwa
4. Tamthilia ya "The painted Bird" iliyotegemea kuanza kuonyeshwa Aprili 17 imehairishwa hadi baadae msimu wa kiangazi
5. Disney wamehairisha tarehe za kutoka filamu zifuatazo
- "Black Widow" , "Woman in the Window" na "Personal History of David Copperfield"
Hadi hapo itakapotangazwa
6. Tuzo mashuhuri za BAFTA(Television Craft Awards and Television awards) za mwaka 2020 zilipangwa kufanyika Aprili 26 na May 17 na tukio la kutaja majina ya
ya waliopendekezwa (nominees) yaliyotakiwa kutajwa Alhamisi ya tarehe 26 Machi limehairishwa mpaka itakapotangazwa tena
7. Thailand nchi nzima wanafunga majumba yote ya sinema na ufungaji huu umeanza Machi 18 hadi Machi 31

8. Filamu ya AVATAR 2 iliyokuwa inatengenezwa na
James Cameron huko New Zealand Utengenezaji umesimama
9. Kwa kuanza tu majumba yote ya kuonyesha sinema ya Cineworld na Odeon yamefungwa na hivi karibuni majumba yote ya Sinema nchini Uingereza yatafungwa

March 16
1. "The Young and the Restless" na "The Bold" and the Beautiful
uzalishaji umesimama kwa wiki 2
2. All Alamo Drafthouse Cinema locations zimefungwa kwa muda usiojulikana
3. Msimu wa 4 wa Tamthilia ya FARGO uliotakiwa kwenda hewani Aprili 19 uzalishaji wake umesimamishwa, tarehe mpya itatolewa baadae
4. Hiki ni kichapo kwa wapenzi wa
S. W. A. T wakati Msimu wa tatu ukiwa unamaliziwa uzalishaji umesimama kwa muda usiojulikana
5. Sony wamesimamisha uzalishaji wa filamu ya UNCHARTED iliyotakiwa kuanza upigaji wa picha huko Berlin kwa wiki 6 haijulikani itaathiri vipi tarehe yake
ya kutoka Machi 25, 2021 hii filamu itakuwa imebeba wahusika kama Tom Holland, Mark Wahlberg na Antonio Banderas ikiongozwa na Ruben Fleischer
6. "On a Magical Night" filamu ya Christophe Honores iliyotakiwa kuanza kuonyeshwa kwenye makumbi ya sinema nchi Marekani kuanzia
Machi 27, 2020, imehairishwa kwa muda usiojulikana
7. MATRIX 4 Filamu ya Warner Bros uzalishaji wake umesimamishwa ambapo upigaji wa picha umehama kutoka San Francisco Amerika kwenda Berlin Ujerumani
8.Filamu ya FANTASTIC BEASTS ya Warner Bros iliyotakiwa kuanza utengenezaji wake
nchini Uingereza Machi 16, 2020 imehairishwa, na uzalishaji wa FILAMU YA BATMAN pia umesimamishwa,
9. Filamu ya "Midnight In The Switchgrass" uzalishaji wake umesima baada ya wiki moja tu kuanza uzalishaji, Sony pia wamesogeza mbele tarehe ya kutoka kwa filamu ya "THE CLIMB"
iliyotakiwa kutoka Machi 20, 2020
10. Uzalishaji wa filamu ya "Card Cutter" ambayo ilibakiza wiki moja kukamilika imesimamishwa baada ya Mhusika mmoja kukutwa na maambukizi ya coronavirus, huyu muigizaji alitoka Los Angeles na kwenda kuungana na wenzake kwenye movie set ya Biloxi
Missouri na kusababisha Movie set kufungwa na waigizaji na timu nzima kuondoka kutoka eneo hilo.
11. Tamthilia inayozalishwa na Amazon Studio ijulikanayo kama LOVE ISLANDS FRANCE imesimamishwa baada ya wiki 2 ya uzalishaji Episode ya kwanza ilitakiwa kutoka March 2, 2020
12. Uzalishaji wa tamthilia za PEAKY BLINDERS na LINE OF DUTY za BBC umehairishwa kwa muda usiojulikana
13. Maumivu mengine kwa wapenzi wa Tamthilia ya THE WITCHER msimu wake wa pili (season 2) umesimamishwa uzalishaji kwa wiki 2 huku wakisoma upepo wa huu ugonjwa
14. Nchi ya India imeanza kusimamisha uzalishaji wote wa filamu na tamthilia kuanzia Machi 19 hadi Machi 31, 2020 kufikia tarehe ya mwisho wazalishaji wote waliopo ndani ya nchi au nje ya nchi watapewa siku 3 kufunga virago vyao

March 15
1 Uzalishaji wa "Lords of Rings" uliokuwa
unafanyika New Zealand umesimamishwa kwa wiki 2
2 Tamthilia ya "The Handmaid's Tale" ambayo msimu wake wa nne ulikuwa unatengenezwa imesimamishwa mpaka hapo baadae
3. Netflix wamesimamisha uzalishaji wa filamu ya "Red Notice" ya Dwayne Johnson the Rock iliyoanza kuzalishwa
kuanzia Februari 2020
4. Filamu ya Sylvester Stallone SAMARITAN uzalishaji ulisimamishwa kwa wiki 2

March 14
1. Wafaransa wafunga makumbi yote ya sinema nchini
2. Tuzo za picha mbaya (Worst films) Razzie zimehairishwa kutokea Machi 14 kwa muda usiojulikana
3. Filamu ya Jurassic
World: Dominion utengenezaji wake umesimamishwa pia.

March 13
1. HBO wamesimamisha uzalishaji wa tamthilia muhula wa pili wa "The Righteous Gemstone" na kupeleka mbele msimu wa pili wa EUPHORIA na tamthilia ya SNOWPIERCER nayo imesimamishwa
2. Tamthilia ya "Atlanta" ikiwa inaingia msimu wake wa 3 imesimamishwa, SNOWFALL msimu wa nne umesimamishwa
3 Uzalishaji wa YOUNG SHELDON, BATWOMAN, THE BACHELORETTE na GOD FRIENDED ME umesimamishwa hadi itakapotangazwa apo baadae.
4. Disney wanasimamisha uzalishaji kwenye, "The Little Mermaid" , "Home Alone" , "Peter Pan & Wendy" , "Nightmare Alley" na "Shrunk"
5. Sony wamesimamisha uzalishaji wa NIGHTINGALE na THE WHEEL OF TIME tamthilia za kufikirika
March 12
1. Uzalishaji wa "Grace and Frankie" kutoka Netflix umehairishwa
2. Grey's Anatomy muhula wa 16 uzalishaji umesimama hadi itakapotangazwa tena baada ya wiki 2 kwa kuona hali ya Ugonjwa
3. Tamthilia zifuatazo uzalishaji wake umesima hadi itakapotangazwa tena
-"The Tonight Show" na Jimmy Fallon kama mhusika mkuu
- Late Night na Seth Meyers kama mhusika mkuu
-"The Wendy Williams Show" kabla ya hapo walitangaza kuwa haya maonyesho yangeendelea pasipo watazamaji lakini wameamua kusimamisha kabisa
4. Filamu ya iliyokuwa inasubiriwa sana ya MULAN ilivyotarajiwa kutoka Machi 26, 2020 uzinduzi umesogezwa mbele tarehe ya uzinduzi huo haijatangazwa
5. New Mutant iliyotakiwa itoke Aprili 3, 2020 na "Antlers" ilivyotarajiwa kutoka Aprili 17 kutoka 20th Century Studio tarehe hizo
zimefutwa na bado tarehe mpya hazijatangazwa.
5. IFC films wamasogeza mbele tarehe za kutoka filamu yao ya "The Truth" iliyotakiwa kutoka Machi 20, 2020
6. Filamu ya "The Artist's Wife" mhusika mkuu Bruce Dern na Lena Olin imehairishwa
ilitakiwa kutoka Aprili 3 haijulikani itatoka lini
7. Apple wamesimamisha uzalishaji wa morning Show muhula wa pili,
8. Paramount Pictures watachelewesha utokaji wa. Filamu ya vichekesho (comedy) ya "The Lovebirds" mhusika mkuu Kumail Nanjiani na Issa Rae, ilitakiwa Aprili 3
9. Kichapo kingine kwa wadau wa Movies ni hiki hapa universal Studios imesogeza filamu yake ya Fast and Furious sehemu ya 9 (F9) ilitakiwa kutoka May 22, 2020 sasa imepangwa kutoka Aprili 2, 2021 kama mwaka mzima mbele Hivi,hiki kitawaumiza wengi mimi mwenyewe nikiwa mmoja wapo
10. Universal Television itachelewesha kutoa miradi mitatu ya utengenezaji wa tamthilia kwa makampuni mbalimbali ya filamu
- " Little American" muhula wa 2 kwa ajili ya Apple TV+
- "Russian Doll" muhula wa 2 kwa ajili ya Netflix
- "Rutherford Falls" kwa ajili ya Peacock
11. Disney imefuta kapeti jekundu (red carpet) kwa ajili ya ufunguzi wa filamu ya MULAN kwa nchi za Ulaya
12. Paramount Pictures itachelewesha utokaji wa QUITE PLACE PART 2 ilitarajiwa kuzinduliwa Machi 18 haijulikani itazinduliwa lini
Tamthilia ya NBC, "Celebrity Race Across
The world uzalishaji wa msimu unaofuata umesimamishwa uliotakiwa kuanza Aprili 2020

March 11
1. Hulu wamefuta uzinduzi wa filamu yao ya "Little Fire Everywhere" kutokana na coronavirus iliyotakiwa kuzinduliwa Machi 12, 2020
2. Uzalishaji wa tamthilia ya RIVERDALE umesimamishwa baada ya mmoja waigizaji kukutana na mtu aliyekutwa kuwa na coronavirus Warner Bros wakafunga kambi
3. Uzalishaji wa tamthilia ya " Survivor muhula wa 41 umesimamishwa hadi labda mwishoni mwa mwezi May 2020 usimamishaji huo
usimamishaji huo utaathiri na uzalishaji wa muhula wa 42 uliokuwa unatarajia kuanza May 24, 2020
4. TWITTER na YOUTUBE wamefuta muhadhara (live) wa matangazo yao ya herufi mpya(fonts) na kufanya kwenye mitandao (najua nyinyi ni wadau wa Twitter ndo maana nimewaibia hiki kitu)
5. Disney wanasimamisha uzalishaji wa "Falcon" na "Winter soldiers" wakati huohuo HBO nao wamafuta uzinduzi wa filamu ya makala (Documentary) iitwayo "After Truth: Disinformation And The Cost of Fake News"
6. Sony wamesogeza tarehe ya kuzindua filamu ya vichekesho ya
Peter Rabbit 2" iliyotakiwa kutoka Aprili 3 na kupelekwa mbele miezi 5 kwa mpango huo itazinduliwa Agosti 7, 2020
7. MGM, Universal, and Bond Producer wamesogeza filamu ya James Bond ya NO TIME TO DIE mpaka November 12, 2020 kabla ya hapo filamu hii ilipangwa kuzinduliwa April 8,
8. Filamu ya MISSION IMPOSSIBLE iliyokuwa kwenye uzalishaji ilisimamishwa Februari 26, filamu hii inatengenezwa na Paramount Pictures ambapo uzalishaji ulikuwa unaendelea katika mji wa Venice, Italy ambako visa vya Coronavirus vimekuwa vikubwa.
Je tamthilia pendwa ya Money heist muhula wa nne unaijua Hatima yake?? Tufuate kwenye page yetu kupata taarifa @CipherdotSV @Cipherdotm
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Cipherdot Series And Movies

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!