My Authors
Read all threads
JE WAZIJUA TUZO ZA FILAMU MBAYA DUNIANI
GOLDEN RASPBERRY AWARDS
Golden Raspberry Awards(Razzie) ni tuzo zinazotolewa kwa filamu ambazo hazikufanya vizuri sokoni au kuwa na kiwango cha chini sokoni au kuwa na mafanikio madogo, wapenzi wa Movies tulio wengi tunajua tuzo kubwa na
zinazoheshimika za ACADEMY AWARDS, Lakini tuzo za Razzie zimekuwepo kwa miaka 40 hadi hivi leo na zinaenda sambasamba kabisa na tuzo za Academy Awards

Sherehe ya kwanza ya kukabizi tuzo za Razzie ilifanyika rasmi mnamo march 1981 kwenye sebule ya bwana John
JB Wilson huko Hollywood kwa kuheshimu filamu mbaya za mwaka 1980.
Hizi tuzo zilianzaje? Bwana Wilson alikuwa na kawaida ya kufanya sherehe nyumbani kwake usiku wa siku ambayo sherehe za kutoa Tuzo za Academy ukiwa unaendelea, Mwaka 1981 wakati (53rd Academy awards) tuzo za mara
ya 53 zikiwa zinatolewa naye bwana Wilson kwa mara ya kwanza akawa anaendesha sherehe yake ya kuwatunuku tuzo wale waliofanya vibaya kwenye fani ya filamu kwa mwaka 1980, Bwana huyu aliwaalika marafiki mbalimbali ambao walijaa sebuleni kwake na kuwafanya wapige kura
ya kuchagua picha mbaya ya mwaka 1980 kati ya CAN'T STOP THE MUSIC na XANADU akagawa karatasi za kupigia kura kwa wageni wote waliohudhuria sherehe hiyo. Na baada ya zoezi hilo bwana Wilson alisimama kwenye mfano wa kijukwaa kidogo kijulikanacho kama Kinara kwa
Kiswahili fasaha (podium) kilichotengenezwa kutumia makaratasi magumu yanayofanana na mabox(cardboard), akafunga pamba kwenye mti na kuufanya mti huo ufanane na kinasa sauti (mic) ambacho akakifunga kwenye mti wa mfagio wa ndani, vitu hivyo vyote vilikuwa si halisia 'fake'
kuonyesha ufake wa swala nzima. Baada ya kusimama hapo na kuitangaza filamu ya "Can't Stop the Music" kuwa ni filamu ya kwanza kupata tuzo ya Razzie baada ya kuchaguliwa kuwa filamu mbaya ya mwaka kwa kura nyingi na wahudhuliaji wa sherehe hiyo. Sherehe hii ilifanikiwa
sana na wiki moja baadae tukio hilo liliandikwa na magazeti mengi na pia lilitajwa kwenye gazeti kubwa la Los Angeles Daily News likiwa na kichwa cha habari kilichosema "Chukua Bahasha hizi Tafadhali" inakadiriwa kufikia watu zaidi ya 40 walihudhuria sherehe hiyo
Sherehe ya pili ya tuzo Razzie ( 2nd Raspberry Awards) zilifana pia zikihudhuliwa wa wahudhuliaji zaidi 100 Wakati sherehe ya tatu ulihudhuriwa ma wageni zaidi ya 200, Huwezi kuamini kufikia mwaka wa nne wa sherehe hizi (4th Raspberry Awards) mashirika makubwa matatu ya
televisheni ikiwemo CCN ya rusha matangazo ya sherehe hizi. Mafanikio makubwa yalikuja tu walipogundua kuwa sio rahisi kubishana na Oscars usiku wa Oscars na hivyo kufanya sherehe usiku mmoja kabla ya usiku wa Oscar kwa maana usiku huo waandishi wa habari wanakuwa hawana
kazi hivyo ni rahisi kuhudhuria.

Raspberry Awards Organisation inakuwa na wanachama kutoka watengenezaji wa filamu na watoa maoni wa filamu duniani na wapenzi wa filamu ambao wote hupiga kura na kuchagua filamu mbaya kuliko zote za mwaka huo, wanachama(members) hutoka kwenye
majimbo yote 50 ya Amerika isipokuwa jimbo la Antaktiki (Antarctica), wahusika mbalimbali huja kupokea tuzo zao,
Baadhi ya waliopokea tuzo zao kwa ufupi
Tom Green( Worst Actor/Worst Director), Halle Berry na Sandra Bullock (Worst Actress), Michael, J. D Shapiro
(worst Screenplay), Paul Verhoeven( Worst Director), Mshindi wa mara 8 Oscar Awards Alan Menken, Dinesh D'souza, Fifty shades of grey mzalishaji (producer) Dana Brunetti, Michael De Lucana and Dwayne(the Rock) Johnson hawa wote waliweza kuja na kuchukua tuzo zao
Tuzo kati ya Razzie na Oscars
Washindi wa Picha nzuri na Mbaya kwa wakati mmoja,
Kuna baadhi ya washindani waliweza kupata tuzo ya filamu mbaya na tuzo ya filamu bora kwa wakati mmoja watu wote hawa walipata tuzo za Oscar na tuzo za Razzie kwa
usiku wa mwisho wa wiki hiyo hiyo akiwemo Alan Menken 1993, Brian Helgeland mwaka 1998, na Sandra Bullock 2020 hawa wote watatu walishinda kila tuzo kutoka kwenye filamu tofauti. Kuna waigizaji wawili walipendekezwa kama washindani wa kupata tuzo za kutoka kwenye Oscars na
Razzie kwa filamu hiyo hiyo moja. Ina maana kuna watu waliowaona hawakuwa vizuri kabisa katika uigizaji wao na wakati huo upande mwingine walionekana kuwa bora hawa ni James Coco (Only when I laugh)) na Amy Irving (Yentl), Wimbo wa Aerosmith uliojulikana kama " I don't Want to
Miss a Thing" kama nyimbo iliyotumika kwenye filamu ya Armageddon ya mwaka 1998 ilichaguliwa kama nyimbo bora na wakati huo huo ilichaguliwa kama nyimbo mbaya, hata wimbo wa Trisha Yearwood ulioitwa "How Do I Live" kwenye filamu ya Conair ya mwaka 1997
Na nyimbo ya Tony Bennett iliyojulikana kama " Life in a Looking Glass kwenye filamu ya That's Life ya mwaka 1986. zilionekana kuwa bora na kuwa mbaya kwa wakati mmoja

Wall Street, filamu ya mwaka 1987 ndo filamu pekee iliyojishindia tuzo zote mbili kwa wakati mmoja (Worst and
Best film) picha bora na picha mbaya ya mwaka

Tuzo kati ya Razzie and Golden Globe
Neil Diamond mshindi wa Razzie akiwa muigizaji mbaya(Worst Actor) wa mwaka 1980 Lakini alipendekezwa na Golden globe katika uhusika huo huo kama muigizaji
bora (Best Actor)

Cocktail ya mwaka 1988 ilijishidia tuzo ya Razzie (Worst Film) picha mbaya na mtiririko mbaya wa matukio (Screenplay) na wakati huo huo kujishindia Golden Globe for Best Original Song

Tuzo kati ya Razzie na Grammy
Nyimbo mbalimbali zilipata kuchaguliwa na tuzo za Razzie na wakati huo huo kuchaguliwa na tuzo za Grammy ikimaanisha zilikuwa mbaya na bora kwa wakati mmoja hapa ndo pale mwingine anaposema hii movie mbaya mwingine anasema bonge la movie. Nyimbo kama ya
madonna " Die Another Day" (Best Dance Recording), nyimbo ya Will Smith "Wild Wild West" (Best Rap Solo Performance) na nyinginezo nyingi.

Tuzo Kati ya Razzie na Suturn
Mwaka 1981 Stanley Kubrick alipendekezwa (nominated) kwenye tuzo zote za Razzie na Suturn, kwenye Razzie kama
Director mbovu (Worst Director) Wakati huohuo akapendekezwa na Suturn kama mungozaji bora (best Director) Katika tuzo za Suturn kwenye filamu moja hakika huwezi kuamini mambo haya. Pia mwaka 2002 Natalie Portman katika filamu ya "The Shinning" alipendekezwa
kama muhusika mkuu msaidizi mbovu! (Worst Supporting Actress) na wakati huo huo alipendekezwa na tuzo za Suturn Kama muigizaji msaidizi bora (Best Supporting Actress) kwenye uhusika mmoja na kwenye filamu hiyo hiyo moja

Tuzo Kati ya RAZZIE NA INTERNATIONAL
Mwaka 2017 Darren Aronofsky mungozaji (Director) wa filamu ya "Mother" alipendekezwa kama mungozaji mbovu (Worst Director) na tuzo za Razzie na kupendekezwa kuwa muongozaji bora katika tuzo za kimataifa International Awards

Mwaka 2018 katika filamu ya "The Mystery Comedy" ya
Holmes & Watson, filamu hii ilijishindia tuzo 4 katika tuzo 6 iliyopendekezwa nazo iliweza kujizolea, Worst picture, Worst Director, hii ilikuwa kwenye sherehe ya 39 ya Razzie na kushinda tuzo mbili za ALFS kwa waigizaji Steve Coogan na Noah Jupe
March, 15, 2020 sherehe za 40 za kuwatunuku tuzo washindi kutoka Razzie zilitakiwa kufanyika siku hiyo lakini kutokana na ugonjwa wa COVID-19 sherehe hii imeharishwa na tarehe ya kufanyika kwake haijatajwa.
Kwa mwaka 2019 zifuatazo ndizo filamu zilizopendekezwa
kuingia kwenye tuzo za Razzie au kwa kusema vinginevyo hizi zimeingia kwenye list ya filamu mbaya kwa mwaka 2019, "Cats", "Rambo Last Blood" A Medea Family funeral

Ni wangapi walikuwa wanafahamu uwepo wa tuzo hizi?
Missing some Tweet in this thread? You can try to force a refresh.

Enjoying this thread?

Keep Current with Cipherdot Series And Movies

Profile picture

Stay in touch and get notified when new unrolls are available from this author!

Read all threads

This Thread may be Removed Anytime!

Twitter may remove this content at anytime, convert it as a PDF, save and print for later use!

Try unrolling a thread yourself!

how to unroll video

1) Follow Thread Reader App on Twitter so you can easily mention us!

2) Go to a Twitter thread (series of Tweets by the same owner) and mention us with a keyword "unroll" @threadreaderapp unroll

You can practice here first or read more on our help page!

Follow Us on Twitter!

Did Thread Reader help you today?

Support us! We are indie developers!


This site is made by just three indie developers on a laptop doing marketing, support and development! Read more about the story.

Become a Premium Member ($3.00/month or $30.00/year) and get exclusive features!

Become Premium

Too expensive? Make a small donation by buying us coffee ($5) or help with server cost ($10)

Donate via Paypal Become our Patreon

Thank you for your support!